PETE YA KIKE Sehemu Ya 20






"habari za kazi mume wangu"
Maimuna au maimati alimsalimia mume wake huku akimvua tai, mana suria yeye ndio wa kwanza kuingia kazini na ndio wa mwisho kutoka kazini, hatakiwi kuonwa na mtu yeyote yule ndani ya wiki hizi za karibuni,....basi suria alikwenda kuoga kisha akapata chai ili kusubiri chakula cha jioni, wakiwa wawili tu na mke wake,.... Sasa wakati surian kakaa kwenye sofa akipata chai, na mkewe akiwa jikoni anafanya mambo ya chakula cha jioni,.. Ghafla alianza kushikwa shikwa nyuma ya shingo yake....
"mke wangu acha utani... Hebu kapike mi nataka kulala"
Aliongea surian,... Lakini na huku jikoni, maimuna naye kuna kitu kahisi ndani ya nyumba yake,... Huku sebuleni, surian anazidi kushikwa na anaemshika yupo nyuma ya sofa, na kwakua suria anajua ni mke wake hivyo katulia na kusapoti kushika mkono wa huyo mwanamke ambaye anamshika,... Lakini surian kuangalia huo mkono, laaaaaaa haulaaaaaa

ENDELEA.........

Kabla ya siku hio nyakati za jioni katika himaya ya majini wema ndani ya bahari,.. Sio majini wote wa ndani ya bahari ni wema, wengine ni wabaya, ila kundi hili la akina shaimati na maimati, wao ni kundi la majini wema, ama wazuri, wasio na tabu na mtu,....

Sasa siku hio shaimati alikuwepo nje akiwa kama malikia wa eneo hilo baada ya murati Sabaha kukiuka masharti yalio wekwa dhidi ya binadamu na majini, sasa malikia wa majini katika himaya hio ni Murati shaimati (shamimu).... Sasa siku ya leo Aliweza kumkumbuka ndugu yake au jini mwenzie ambaye kwa sasa anakula raha ndani ya ndoa yake, na hayupo tena katika himaya hio, japo anaruhusiwa kwenda kusalimia....
"nimemmisi maimati wangu jamani"
Ilikuwa ni sauti ya shaimati akiwa chumbani kwake, na nyakati hizo zilikuwa ni za usiku wa saa sita, kulilindima baridi kwa kiasi fulani,...

"naweza kwenda hata kumuona angalau kwa macho tu"
Aliongea shaimati akiwa pekee hapo chumbani kwake, kwani hakua na mtu wa Kuzungumza naye,.... Haikupita hata dakika moja shaimati kapotea katika mazingira ya kutatanisha, kana kwamba kaelekea duniani kwa nduguye maimati,...

Kama kawaida yao au kanuni na masharti yao wao wenyewe kuja duniani kila saa nane za usiku, haijalishi unakwenda kwa ubaya ama kwa uzuri,.... Majini karibu wote wamepewa uwezo mkubwa, ingali wanatofautiana nyenzo kwa wale wazuri na wabaya,.... Shaimati hakuwa na muda wa kufikiri kuwa maimati anaishi wapi, kwani wao wana uwezo wa kunusana popote pale walipo, na mbaya zaidi nyumba ya maimuna au maimati haipo mbali sana na bahari ambayo wao hutokea, hivyo ilikuwa ni rahisi sana kwa shaimati kujua wanapo ishi....

Ikiwa ni saa nane usiku shaimati akiwa nje ya jengo la ndugu yake ambaye ni maimuna,....

Na wakati huo huo maimuna alikuwa akipata raha zake toka kwa mume wake,.... Na mbaya zaidi naye kagundua kuwa shaimati yupo nje ya jengo hilo ambalo yeye yupo kwa ndani na wakati huo alikuwa katika hali ya kufanya mapenzi na mume wake ambaye ni surian....

Sasa maimati kumbe anapenda sana ndugu yake au jini mwenzake aje kuolewa, mana mpaka sasa hajui hata raha ya mapenzi ipoje,... Sasa maimuna akaanza kulia milio ya msisimuo ambayo inaweza kumfanya shaimati kuyatamani maisha ya ndoa, hivyo maimuna akazidisha milio ya kimapenzi kwa makusudi ilo shaimati asikie naye aitamani ndoa ili wote wawe wamesha olewa, mana kule ujinini sio wengi ambao wana asili mbili, na shaimati na maimati ni majini walio shibana...

Kweli zile sauti taamu ziliweza kupenya kwenye masikio ya shaimati, hivyo akajikuta anaanza kutega sikio ili kusikia ni utamu wa aina gani ambao ndugu yake huupata kila usiku wa saa nane,... Sasa shaimati alikuwa akihisi baridi, lakini ghafla akaanza kuhisi joto, kana kwamba sauti tu inampa joto, je kama angelikuwa shughulini ingelikuwaje,.. Na wakati huo maimuna anazidi kulia milio ile ya hatari hatari, yaani ile ya kumtoa nyoka pangoni... Shaimati alipotea pale nje haikujulikana kaelekea wapi,

Kesho yake asubuhi sana nyakati za saa 12 na nusu, surian ndio wakati wake wa kutoka nyumbani ikiwa anamaliziwa kufungwa tai na mke wake, na siku hio mke hakuwa tayari kwenda kazini,... Na surian anawahi kazini ili asionwe na wafanyakazi wake kwani kuna masharti kawekewa na mke wake,...

Ilipofika nyakati za macha shaimati aliingia ndani kwa maimuna, alimkuta anasoma kitabu cha dini, mana hana pakwenda kwa nyakati hizo,
"heeeeee shamimuuuuu... Karibu"
Maimuna alimkaribisha mwenzie kwa furaha na kujifanya jana hakumhisi kuja kwake,... Sasa kila mmoja anajua kuwa usiku wa jana hakujulikana, hivyo ndivyo ilivyo kwa majini, huyu kajua kuna jini mwenzie nje, lakini yule wa nje hajui kama kajulikana ndani, na yule wandani kajua kuwa kuna jini nje lakini hajui kama kajulikana kule ndani.... Hivyo ndivyo ilivyo kwa majini,

"ahsante, heeeeee munaa umenenepa jamani"
Aliongea shaimati kama kumsifia maimuna kwani ilionekana hali ya mwili wake kuwa mkubwa kiasi fulani,
"mambo ya ndoa hayo"
"mmmmhhh kwa unavyo yasifia mhhh"
"sasa nisi yasifie kwanini? Mana nipo ndani ya ndoa, na nimejua utamu wake na raha zake..."
"mmmhhh hongera yako mwenzangu"
"haya niambie, hawajambo huko kwetu"
Shaimati aliuliza hali ya ujinini kuwa hawajambo
"aahh nadhani wote wamekumisi sana, ila mimi nimetoka kwa kutoroka ujue"
"weeeeee, sasa wairati sarika akijua itakuwaje shaimati? Hebu nenda bwana"
Maimuna alimtaka jini mwenzie aweze kurudi ujinini kwani alitumia njia ya kutoroka usiku ule,
"nitakwenda,.. Lakini nami nimejikuta nayatamani maisha ya duniani"
"sawa lakini unatakiwa upewe ruksa ya kuja kuishi duniani"
Aliongea maimuna huku shamimu akiwa hatamani kurudi ujinini....
"Kiukweli shamimu nahisi upo huru huku duniani, Kiukweli nayatamani maisha yako ambayo unaishi...."
Aliongea shamimu huku akiangaza macho huku na kule na kuiona picha ya surian iliopo ukutani
"waooo shem wangu huyu"
Aliongea shamimu huku akiisogelea ile picha na kuishika shika, kitu ambacho maimuna hakukipenda, kwasababu alihisi shamimu angemtamani mume wake,...
"shamimu? Naomba utoke tafadhali"
Aliongea maimuna huku akiwa kakasirika kwa kitendo cha shamimu kuipapasa picha ya surian kimahaba
"unanifukuza nyumbani kwako"
"sina maana hio, ila kuna hisia za ujinga mbele ya uso wako"
Aliongea maimuna huku shamimu akijibu
"ni kweli, sikua nikitamani mwanaume kamwe... Lakini sauti za jana, zimenifanya nami nivute hisia kali na kujiuliza ni raha gani ambazo unazipata usiku wa saa nane..."
Aliongea shamimu ambaye ni jini mwenzie na maimuna, na wote binadamu kwa majini... Yaani wana asili mbili...
"ni sawa, lakini jaribu kutafuta wako"
Aliongea maimuna jambo ambalo limemchekesha sana shamimu huku akisema
"kwani wewe huyu ni wako"
"una maana gani"
"mchumba wa mtu huyu... Hapa umempokonya mwanamke mwenzio tunda lake... Sasa limekuwa lako, wakati ulilichuma kwenye mti wa watu"
Aliongea shamimu huku maimuna akiwa hataki kuyajali maneno yake
"ok sawa, hata mimi nililijua hilo... We nenda nyumbani kwetu... Na pia nisingetamani kukuona kwa wakati mwingine"
Maimuna aliamua kama ni mbwai iwe mbwai, lakini sio kwenye swala la mume....
"sawa, nakwenda, lakini kaa ukijua kua, mti wenye matunda ndio hupigwa mawe"
Aliongea shamimu kisha akapotea katika mazingira ya kutatanisha, kana kwamba tayari wamesha anza ugomvi kati ya wawili hawa kisa ni mwanaume mmoja tu,.....

Sasa ilipofika nyakati za jioni, surian akiwa kaketi katika sofa akipata chai safi kabisa.... Na wakati huo katoka kuoga, lakini katika kidole chake hakukua na pete,... Ghafla shamimu alitokea nyuma ya surian na kuanza kumshika shingoni, tena ile kimahaba.. Surian kwa akili yake alijua ni mke wake, mana wanaishi wawili tu na yeye hana nguvu au uwezo wa kujua kuwa kuna jini mwingine kaja... Sasa surian akawa anaushika ule mkono kwa nia ya kusapoti mshiko mshiko wa mkewe,.. Japo alikuwa akimharakisha akapike kwani anataka kulala... Na wakati huo kule jikoni, maimuna naye keshajua kuwa shamimu yupo mdani, sasa hakutaka kutoka mapema ili ajue shamimu kampenda mume wake kweli au alitania... Hivyo akachelewa kutoka na kubaki kuchungulia kwenye upenyo wa mlango,... Aliweza kuona jinsi surian anavyo shikwa shikwa kimahaba na wakati huo suria anajua ni mkewe kwakua yupo nyuma ya mgongo wake

Lakini surian kuangalia huo mkono, laaaaaaa haulaaaaaa, kumbe hakuwa mkewe... Na aliujua vyema na kukumbuka, siku ile ya Kwanza kupelekwa ujinini alishikwa mkono na huu mkono, hivyo alipo uona tu akastuka na kuamka... Alikuwa ni shamimu,.. Na pale pale maimuna akatokea
"shaimati, hivi ni tabia gani umeanza... Mbona asili yetu hatupo hivyo ndugu yangu"
Aliongea maimuna tena kwa upole wa hali ya juu...
"yaani kitendo cha kumshika mumeo, joto nililo pata... Sijawahi kulipata toka kuzaliwa kwangu.... Ila narudia tena MTI WENYE MATUNDA NDIO WENYE KUPIGWA MAWE... Nakwenda, lakini jua kuwa umedungua tunda la mtu, hivyi sio lako"
Aliongea shamimu kisha huyoo akapotea,... Maimuna alikasirika sana kwa kitendo ambacho shamimu kakifanya,
"surian mume wangu, kwanini hujavaa pete yako...."
Muna alilia na mume wake kwanini hakuvaa pete ambayo kapewa, mana kama surian angelikuwa na pete basi shamimu asingeliweza kumsogelea kamwe,...
"samahani mke wangu,... Nami nilijua ni wewe ndio upo nyuma yangu na ndio mana nikawa nimetulia... Basi nakwenda kuvaa"
Aliongea surian kisha akaingia chumbani na kuivaa PETE YA KIKE, ambayo ndio msaada wake juu ya viumbe vibaya na hata vizuri,.. Kwani shamimu ni kiumbe mzuri lakini amekuwa na tamaa ya mapenzi ingali mwanzo hakuwa hivyo.... Ila jambo hilo analijutia sana maimuna kwa kuongeza milio ya mahaba ilio mfanya shamimu kupata hamu

Kesho yake, kama kawaida surian akiwa kazini ikiwa ni mida ya saa nne za asubuhi,... Kwa ukawaida hatakiwi kutoka ofisini hapo mpaka siku 17 ziishe ndipo anaruhusiwa kuonwa na wafanyakazi wake... Leo mkewe kaja kazini hivyo ndie mwenye kutembelea wafanyakazi kiwandani,.. Wafanyakazi wenyewe wanabaki mdomo wazi kwani maimuna ni mzuri mithili ya malaika, hata wanawake wenzie walikuwa wakimshangaa mwanamke huyo ambaye ndio mke wa boss wao...

Tukija huku ICC ambako ndipo faima anapo fanyia kazi kwa kufanya mauzo ya nguo za Kiislamu,... Baada ya kufanya biashara na wateja alio kua nao, sasa katulia huku akiwa anafungua simu yake,... Kuna namba ya simu alikuwa akiitafuta na kuipata
"RIKI, hivi utakuwa mkweli kwangu... Kiukweli naogopa kuumizwa katika mapenzi,.. Sihitaji pesa zako wala uzuri wako.. Nahitaji mapenzi ya kweli ila nahitaji ubadilike"
Aliongea faima bada ya kuiona namba ya Riki ambaye ni mwanaume aliotokea kumpenda sana hivyo hapo kaitafuta namba ili aweze kumpigia simu amkubalie....

Lakini kabla hajapiga, alifungua upande wa picha, zake na kuangalia picha ambazo alipiga akiwa na surian,.. Kitendo ambacho kilimtoa machozi kwa mara nyingine tena, hivyo inaonekana anamkubalia tariki ili ampunguzie tu mawazo, ila aliopo moyoni ni surian japo anasikia kafariki dunia....
"mwaahhh,.. Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi, sitokaa kukusahau surian wangu... Nakupenda kuliko hata ninavyo jipenda... Sijakusaliti, ila nakwenda kumpata mwenzangu atakaye nipotezea mawazo yangu... Nakupenda sana mume wangu, japo nasiki umefariki dunia... Mungu akulaze mahali pema peponi... Amen"

Aliongea faima baada ya kuangalia picha ambayo walipiga pamoja,... Faima aliweka simu sikioni, alimpigia tariki ili amkubalie ombi lake,... Na simu ilianza kuita.... Ilipokelewa
"hallow Riki Asalam Aleykh"
"waaleykh msalam, vipi hali"
"salama tu"
"haya niambie bibie, nina furaha sana kuiona simu yako nyakati hizi"
"ndio... Vipi upo bize sana"
"hapana, hapana, hapana,... Sipo bize.. Nipo ofisini hapa kuna baadhi ya documents nazi saini"
"basi nitakwambia baadae Ukimaliza"
"nooooo niambie sasa hivi.... Usiutese moyo wangu kwa madakika machache yajayo"
Aliongea tariki na kujifanya mtu wa busara na mwenye pesa....

Lakini sasa faima kabla hajaongea, alishangaa kusikia sauti ya kike hapo nje ikisema kuwa....
"surian wako yupo hai"
Faima alikata simu haraka ili kuangalia hapo nje ni nani kataamka maneno hayo,...
"waaaaaaoooooo.... Dada shamimu, ulienda wapi"
Ikumbukwe kuwa shamimu na faima walijengaga urafiki wakati ule walipokuja kutafuta MWANAUME MSAFI, na faima alitoboa siri ya yeye na surian kuwa wao hawajawahi kufanya mapenzi, ndipo shamimu akaanza kumfuatilia mchumba wa faima kwasababu ndio aina ya mwanaume waliokuja kumtafuta, hivyo faima anatakiwa kumlaumu shamimu mana shamimu ndio kasababisha surian kwenda ujinini
"mbona nipo jamani fey"
"hapana bwana dada,... Karibu miezi mitatu minne hivi sijakuona"
"aahh si unajua mambo ya kazi fey"
"ni kweli,... Haya niambie dada shuu"
"nipo... Mbona kama ulikuwa unalia"
"we acha tu dada shuu,... Ni mwezi wa tatu kama sio wa nne, surian wangu sijamuona, naumia sana..."
Aliongea faima huku akilia na kumuegemea shamimu....
"mbona surian yupo na hata jana nilimuona"
Shamimu katumbua jipu lililoiva....
"unasemaje dada shuu"
"surian wako jana nilimuona... Na jinsi ya kumpata ni rahisi sana... Ila unatakiwa kuwa mpole, mvumilivu, mnyenyekevu, na mwenye utulivu..."
"sawa dada shuu... Nipo tayari kutii vigezo vyote,.. Hebu niambie... Nampataje na yupo wapi kwasasa"
Faima aliuliza kwa umakini huku akiwa katoa macho
"unaijua kampuni mpya inayotengeneza nguo za dini hapa mkoani Tanga"
"ndio.... Si hii inayo itwa MICCO"
"yeeees.... Mmiliki wa kampuni hio ni surian na mke wake"
Faima kashtuka kwa kusikia neno SURIAN NA MKE WAKE
"hivi umesema surian peke yake au surian na mke wake"






No comments: