HADITHI: RED BIKINI SEHEMU YA TISA(09).





ILIPOISHIA👉🏽 watu wote walijikuta wakikutana ndani ya varangati la fumanizi. ENDELEA👇🏽

"Daaddy!?" Edwin aliita huku akiwa kama haamini kwa anachokiona mbele ya macho yake.

Watu wote kwanza wakatulia na kila mmoja akijiangalia na kumuangalia aliyekuwa mpenzi wake. Hakuna aliyeamini kwenye macho yake kwa maana kama mchanganyiko basi ulikuwa mchanganyiko wa maana.

Edwin yuko na Lecho ambaye ni demu wa Sudi, Sudi nayeye alikuwa na Jesca lakini kasheshe yake ni kwa Lecho kwanini alale na Jesca?. Irene nayeye anamsala wa kulala na baba wa Edwin na mbaya zaidi Edwin ni mpenzi wake, maana yake hapo baba na mwana wamejikuta wakichangia mwanamke mmoja.

"Edwin!!?" Mr Dango alijikuta akimuita mwanae huku akifunga taulo lake vizuri. Kila mtu alibaki akishangaa na aliyekuwa kwenye mshangao mkali ni Irene baada ya kugundua Mr Dango ni baba wa Edwin.

"Wewe malaya kumbe unanizunguuka kwa kulala na rafiki yangu." Sudi aliongea kwa gadhabu huku akitaka kumvamia Lecho lakini baadhi ya watu waliokuja kuamua wakamuwahi kumzuia.

"Malaya mwenyewe mwenda wazimu mkubwa wewe unafanya nini sasa?" Lecho nayeye akapandisha hasira huku akibwatuka kwa sauti ya juu.

"Daddy! Unafanya nini sasa?" Edwin alizungumza huku akiwa kama anataka kulia.
"Edwin mwanangu?"
"Don't say anything, huna la kujitetea maana kila kitu kiko hadharani." Huku akimuangalia Irene kwa jicho baya.

"Mmmh! Umefurahi sasa?" Edwin alimuuliza Irene.
"Edwin please!"
"Acha kujifanya mnyenyekevu." Huku akimsukuma Irene na kurudi chumbani.

Lecho alipotaka kurudi chumbani alipoingia Edwin lakini alizuiliwa na Sudi.
"Unaenda wapi sasa?" Huku akimshika mkono.
"Kwani unataka nini?" Lecho aliuliza.
"Usiniulize kama hivyo." Huku akimvuta.

"Hebu muachie kwanza huyo Dada." Jesca aliingilia kati huku akimvuta Sudi na muda huo huo Lecho akapata upenyo wa kuingia chumbani kwao na kuufunga mlango kwa funguo, akimuacha Sudi akishikwa na hasira.

"Hebu rudi chumbani." Jesca alimtahadharisha Sudi huku Irene akitoka chumbani na mkononi akiwa ameshika simu ya Sudi.

Irene alimkabizi simu sambamba na chaji Sudi bila kuzungumza chochote kisha akarudi chumbani kwenda kuyamaliza na Mr Dango.

**********
"Aibu gani hii sasa?" Edwin aliuliza huku akiwa amejiinamia kitandani.
"Hupaswi kuwa hivyo maana haya ni mambo ya kawaida." Lecho alimpoza Edwin.

"Haiwezekani Irene afanye huu ujinga, hadi baba yangu?" Huku akianza kulia na kumlalia Lecho kifuani.
"Shiiiii! Pole mpenzi!" Huku akimkumbatia na kumbembeleza bila kujua nayeye anamsala kwa Sudi.

**********
"Inamaana ulishindwa kujizuia? Mbona wanaume mnakuwa hamridhiki?" Jesca alimuuliza Sudi aliyekuwa amasimama dirishani huku akionekana mwenye jazba sana.
"Wewe ulitaka labda nifanye nini?"
"Ufanye nini kivipi? Ulishindwa kukataa mpaka mkaanza kufanya uchafu mule mule chumbani? Sasa si bora hata mngetoka na mgeenda vyoo vya nje?" Jesca aliongea kwa sauti ya juu.
"Ok! Sawa nimekuelewa, next time nitafanya hivyo, asante kwa ushauli wako." Huku akivaa nguo zake.

"Unataka kwenda wapi sasa?" Jesca alimuuliza Sudi huku akisimama mbele yake.
"Siwezi kuendelea kukaa hapa tena." Huku akivaa raba zake miguuni.

Hakutaka hata kubishana sana Sudi alichomoka kwa kasi na kuondoka zake anakokujua yeye, akimuacha Jesca ndani ya mshangao.

**********
"Hupaswi kunilalamikia." Irene alifoka huku akivaa nguo zake kwa hasira.
"Yani kosa ufanye wewe halafu bado ujifanye umechukia." Mr Dango aliuliza huku akimuangalia Irene.
"Sina muda huo tena wa kuzungumzia yaliyotokea." Huku akiondoka zake.

"Kaa na mwanao kwanza myamalize." Kisha akaubamiza mlango.
"Shiiit!" Mr Dango aliongea huku akiutupa mto sakafuni.

**********
Nje ya lodge ya one night alionekana Sudi akitafuta usafiri na kwa bahati nzuri aliiona taksi moja ikirandaranda mitaa ile, bila kuvunga akaipungia mkono na ikaanza kusogea.

Yani ukifata jina la One night lodge ilisadifu kabisa mambo yaliyotokea mule ndani, usiku mmoja tu mambo yakawa yamesha malizika tena hata usiku wenyewe ukawa haujaisha kabisa.

Sudi aliingia ndani ya taksi na kufunga mlango lakini kabla taksi haijaondoka mlango ulifunguliwa na Irene akaingia utazani kana kwamba alikuwa na Sudi.

Sudi akabaki anamshangaa tu Irene na kumruhusu dereva aondoe gari.
"Tunaweza kuondoka."

"Unafanya nini sasa?" Sudi aliuliza.
"Usiongee chochote." Huku akimkumbatia na kumbusu mdomoni.

"Mnaelekea wapi bosi?" Dereva aliuliza.
"Tupeleke lodge yoyote iliyokuwa safi." Sudi alizungumza huku akiwa amemkumbatia Irene.

**********
Nyumbani kwa madam Happy, alionekana Farida akiwa nje ya nyumba karibu kabisa na geti.

Katika kibanda cha mlinzi wa lile geti zilisikika sauti za kimahaba za mwanadada Farida akinung'unika huku yule mlinzi akijilia tunda kwa raha zake.

"Taratibu baba mbona leo mimi wako jamani." Alisikika Farida akimsihi huku akiwa ameshika ukuta na kujiachia kwa kumuachia mlinzi msambwanda aliyekuwa akijipakulia atakavyo.

Farida hakuwa na jinsi kwa maana asingempa mlinzi utamu uwenda siri yao ingevuja, basi akaamua kutokuwa mchoyo wa burudani akaamua kummegea kautamu na mlinzi wa watu apate kujiburudisha.

Sekeseke lilikuwa balaaa kwa maana hata mlinzi hakuwa haba kwenye kale kamchezo, mshike mshike uliendelea mahala pale mpaka walipomaliza mtanange wao huku kila mmoja akijikuta akifurahia ule mchezo.

Kwa upande wake Farida alijkuta akiburudika zaidi ya ile mikuno ya baba mwenye nyumba, mlinzi alikuwa yuko vizuri mara dufu.

**********
"Inamaana huna mawazo yoyote juu ya hili lililotokea?" Sudi alimuuliza Irene.
"Kwanini nisiwaze? Wakati Edwin ameshagundua kila kitu." Huku akikaa kitandani.
"Sasa tunafanya nini?" Sudi aliuliza.
"Hata sielewi." Huku akijilaza kitandani.

"Hakuna cha kufanya zaidi ya kulala tu, kesho itakapofika ndipo tutakapojua." Huku akivua viatu vyake na kupanda kitandani.
Walibaki wakiangaliana bila kuzungumza chochote kwa maana hata tamaa ya kufanya mapenzi hakuwa nayo.

**********
"Sasa tutafanya nini?" Lecho aliuliza.
"Hakuna cha kufanya zaidi ya kutuliza akili." Huku akimkumbatia na kulala naye kitandani huku wakitandikana mabusu.

ITAENDELEA



No comments: