KUSIMAMA KWENYE UHALISIA WAKO NI MOJA YA NJIA KUU KUULINDA UHUSIANO NA NDOA YAKO.
Watu wengi wamekuwa wakianza vizuri kwenye MAHUSIANO na NDOA zao kwa kusimamia nafasi zao kama inavyotakiwa, Lakini cha ajabu kadiri siku zinavyokwenda na mwenza wake kuona usalama wa mahala alipo ndipo huanza kujisahau na kuacha mwenendo ule ulio mvutia mwenza wake.
Laiti kama Mwanaume angesimama kwenye MAJUKUMU YAKE KAMA BABA siamini kama kuna Mwanamke angejaribu kuona alipo sio sehemu salama, Vivyo hivyo kwa WANAWAKE kama wangesimama vyema kwenye nafasi zao kama MAMA wala sioni mwanaume ambaye angefanya yasiyompendeza mke.
Imekuwa kilio kila mwenye MAHUSIANO analia na kujutia, Kila mwenye NDOA anatamani KUONDOKA Yaani hakuna mahala utakimbilia ukapate nafuu, Ambao hawajaoa WANAKWEPA KUOA lakini pia walioko kwenye NDOA nao kwa namna ambavyo wanapitia magumu wanawatamani walioko kwenye MAHUSIANO.
Kwa sasa huwezi kutafuta MTU AMBAYE yeye ndoa ama mahusiano yake yako imara japo awe MSHAURI wako maana lugha inayotumika kwenye MAHUSIANO na kwenye NDOA ni moja kwamba KWA SASA HAKUNA UPENDO😭😭😭
Wazazi nao pamoja na ukomavu wao ki FIKRA lakini unakuta wapo wanaoachana na tayari wana wajukuu hivyo HAKUNA PA KUKIMBILIA😭😭😭
kila mmoja na kilio chake, Mwenye mlevi anaona nafuu ya Mwenye mzinzi wakati huo huo Mwenye mzinzi anatamani bora angekuwa na mlevi😅😅😅
Na ukiangalia tatizo ni dogo sana;
▪WATU KUTOSIMAMA KWENYE UHALISIA WAO WA AWALI.
Kwani Unafikiri mtu akijua una wenge atakupaje MOYO WAKE? Sana sana atakuwepo kwa sababu zake wala PENZI lenu haliwezi kuibeba TASWIRA ya kudumu, Yaani ni KUDINYANA na kila mmoja arudi kwao, Kwa hakika hakuna mbadala wa kuimarisha MAHUSIANO NA NDOA kama wahusika hawawezi kwenda kwenye UHALISIA WA ENEO ALILOPO vinginevyo hivyo vilio na majuto yatakuwa ndiyo sehemu ya MAISHA YENU.
Kutupiana majukumu huko ndiko yalianzia madhaifu ya DHARAU na mwisho kabisa ni UANGAMIVU WA PENZI kama ulijua huwezi kuwa BABA kumbe kipi kilikuingiza kutaka MKE? Ungebakia MWANAUME ukapambana na WANAWAKE ili mkapeana adabu, Wewe ukimwaga MBOGA mwenzio anamwaga UGALI😅😅😅
Rejea kwenye misingi na uhalisia alio uona mwenza wako hata akatamani na kuwa na shauku ya kuwa nawe, Usijidanganye kwa kuwa MNAISHI PAMOJA hilo ni jambo dogo sana ikiwa MAPENZI YAKIISHA.
Fikiria zaidi kuwa sehemu ya UHALISIA WAKO ili kumjenga mwenza wako kisaikolojia kwamba UNAMPENDA kinyume chake UTAJUTIA KUMKOSA KWA UFALA WAKO
No comments: