Mwanamke Akikupenda Utaona Vitu Hivi 10.



Ishara za mwanamke anaekupenda,lakini siyo kwamba ishara hizi zote anaweza kuwanazo msichana mmoja,ila kila mmoja kwa ishara zake
Hatua hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda,wasichana wanatofautiana ila wengi wao wana-share ishara tofauti.

1.Mnapoongea:

Sikiliza sauti yake,kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini.
anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.
Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia.
Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea,
ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu.

2.Anapenda hugs na kukushika:
Unapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako,au unapokutana naye
anaweza kuhug.

3.Ajali za kijitakia

anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia,au anakukumbatia.
anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike,atajitahidi usigundue
mbinu zake kwa kupotezea “Ooh i’m sorry i didn’t mean it”


4. Anaibia kukuchunguza:
Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia,ukigeuka anajifanya yuko busy na mambo
yake kumbe anakuchunguza taratibu

5. Wangalie marafiki zake.

Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga,hata kama mmeenda out pamoja na marafiki
zake utakuta yupo karibu na wewe,akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu
waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta,ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake
kuhusu wewe.

6. Anapenda umjali.
Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie,mfano mmeenda mahali kukawa na baridi
hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako,hata kama kuna watu
hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.

7. Hawezi kuzuia tabasamu.
Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee,hata kama kuna kitu kimemwudhi
atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.

8. Ishara za mwili.

Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini.
kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani,utamwona anashtuka gafla.

9. Anafurahishwa na vituko vyako.

Huwezi ukamboa,hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.

10.Anakujali:
Anakuwa anakujali,mfano akiona umeumia labda umejigonga,yupo radhi akuhudumie.
unapokuwa naye anaweza kuuliza…”unahitaji chochote?….unaweza ukasema “nina kiu ngoja ninunue maji”
utamsikia “nina maji,kunywa haya yangu kwanza”.basi ujue kwamba anakujali.




No comments: