NDOA NI SAFARI NGUMU SANA MTANGULIZENI MUNGU MTAFIKA SALAMA

Image may contain: 1 person
ivyo hivyo ndoa isiyo na ulinzi wa Mungu huishia pabaya.
Safari yeyote huwa kufika salama sio mazoea bali ni kwa neema ya Mungu hivyo ni vema kufanya sala na maombi kabla ya kuianza safari vivyo hivyo kabla ya kuianza ndoa yenu ni vema kila mmoja wenu kwa nafasi yake (mme na mke) kumuomba Mungu awalinde, awatie moyo, awape uvumilivu, awape moyo wa hekima, busara, upole, nidhamu, uaminifu, unyenyekevu, heshima, shukrani, upendo, umoja, ushirikiano, heshima na utii.

Safari yeyote isiyoambatana na uwepo wa Mungu huwa haikawii kupata ajali maana shetani hupata nafasi katika safari hiyo na kusababisha ajali kama ilivyo kawaida yake. Vivyo hivyo katika safari yenu ya ndoa ni vema kujikabidhi kwa Mungu awaepushie kila baya, mkosi, laana na hila zote za wanadamu au shetani zitakozosimama kujaribu kuwatenganisha zishindwe.
Mojawapo ya vikwazo na changamoto kuu za safari ya ndoa ni usaliti, maneno ya wachochezi, ndugu, marafiki na majirani, kukengeuka kitabia kwa watoto, mme au mke, dhiki, kufilisika, ajali, ulemavu, magonjwa, madeni, skendo na hata vifo. Hakika yahitaji neema ya Mungu pekee na maombi kuzikabili changamoto hizo iwapo zikijitokeza katika ndoa la sivyo ndoa lazima itavunjika tu maana kiukweli kwa hali ya kawaida kibinadamu ni ngumu kuzimudu.
hakika nakuombea Mwenyezi Mungu ailinde ndoa yako dhidi ya hila na vikwazo vyote, kama unakubaliana nami TYPE AMEN kisha SHARE post hii na marafiki zako
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda




No comments: