Vyakula 10 Bora ambavyo Mama mjamzito Anastahili kula

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini. Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku. Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora.
Hivi ndivyo vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kula;

1. Jamii Kunde 
Mbegu za kunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini. Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini. Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya,Peas,Karanga, Alfa alfa,Mikunde, maharage.
2.Mayai 
Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi ya magonjwa mbali mbali.

3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa 
Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi na siagi. Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli, Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo.
4. Viazi tamu 
Viazi vitamu vina vitamini A ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto,ngozi na mifupa
5. Nyama
Nyama ya kuku au ngombe huwa na protini nyingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne

6. Nafaka na vyakula vya Wanga 
Vyakula hivi huipa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto tumboni.Vyakula hivi ni kama mahindi,mtama ,mihogo,vyakula vya ngano kama mkate n.k.
 7. Avocado 
Ni matunda ambayo yana mafuta mengi maarufu kama fatty acid. Avocado inasaidia katika ukuaji wa ubongo,ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni.
8 .Mboga za majani 
Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha. Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia.
9. Mafuta ya samaki 
Mafuta ya maini ya samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto.
10.Maji 
Maji ni muhimu kwa mwili kwa sababu inasaidia kwenye mmenyenyo na unyonywaji chakula na pia husaidia kuzia choo ngumu Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI)




No comments: