Wachumba wagundua ni ndugu na dada siku chache kabla ya harusi yao


- Rose Wanjiku na John Njoroge (sio majina yao halisi) walianza uhusiano wa kimapenzi wakifanya biashara yao ya kuuza viatu

- Hat hivyo wawili hao walilazimika kuukatiza uhusiano wao walipowatembelea wazazi ambao waliwaarifu kwamba walikuwa ndugu na dada

- Babake Njoroge alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mamake Wanjiku na kupelekea kuzaliwa kwake

Rose Wanjiku na mpenzi wake John Njoroge (sio majina yao halisi) walikuwa wamechumbiana kwa muda mrefu na ndiposa wakaamua wakati ulikuwa umewadia kwao kuoana.

Njoroge aliamua kumpeleka mpenzi wake kwa wazazi wake ila mambo yaligeuka baada ya wazazi wao kuwaagiza kufutilia mbali uhusiano wao kwa kuwa walikuwa ni ndugu na dada.


Mwanadada huyu aligundua mchumba wake alikuwa ni ndugu yake. Picha: Kameme TV.
Wakizungumza na runinga ya Kameme, wapenzi hao walielezea machungu waliyohisi walipolazimika kutengana baada kugundua walikuwa na baba mmoja.

"Baada ya kumpeleka kwa wazazi wangu niliarifiwa kwamba babangu alihusiana kimapenzi na mwanamke mwingine na kupelekea kuzaliwa kwa mpenzi wangu, hivyo nilikuwa ndugu yake mkubwa," Njoroge aliimulia.

Ujumbe huo uliwavunja mioyo kwani walikuwa wamechumbiana kwa muda mrefu baada ya Njoroge kukutana na mwanadada huyo akifanya biashara yake ya kuuza viatu.


Jamaa huyu alikutana na mchumba wake akifanya biashara yake ya kuuza viatu. Picha: Kameme TV.
Wazazi wao waliwalazimu kutengana mara moja kwa kuwa katika mila ya Kiafrika si sawa kwa ndugu na dada kuoana na pia maandiko ya Biblia hayaruhusu.

"Nashindwa kuanza uhusiano mwingine wa mapenzi kwani bado nahofia huenda tena nikajikuta nachumbiana na jamaa wa familia yangu," Wanjiku alisema.

Suala hizi nzito liliwaacha watazamaji na masuali mengi ya kwamba ni nani haswa anapaswa kulaumiwa.

Hata hivyo mchungaji mmoja wa kanisa la AIC Rungiri aliiambia televisheni hiyo kwamba wa kulaumiwa ni wazazi kwani hawafanyi maandalizi ya familia kukutana angalu mara moja ili kujuana.

"Ni jukumu la wazazi kuhakikisha wanao wanakutana na kujuana. Wanapaswa kuandaa mikutano ya familia angalau mara moja kwa mwaka," mchungaji huyo alisema.




No comments: