FAHAMU MAMBO AMBAYO MWANAMKE HAWEZI KUMWAMBIA MWANAUME

Kwa wasomaji wa safu hii, kwa hakika wamekuwa mashahidi kuwa uhusiano wao na wenzi wao umekuwa imara sana.
Nachukua nafasi hii kuwashukuru wote ambao huwasiliana nami moja kwa moja kwa njia mbalimbali; wengine wakinipongeza kwa kazi hii huku wengine wakiomba ushauri kuhusu mambo mbalimbali ya uhusiano wao.
Tuendelee na mada yetu. Katika mapenzi, kila mmoja huwa na hisia zake moyoni, kwa bahati mbaya hisia hizo haziwezi kuonekana kwa macho na ni vigumu sana mtu kutoa hisia zake za siri.
Mara nyingi imekuwa ikitokea wapenzi kuzungumza kwa vitendo zaidi kuonesha kilichopo moyoni mwake.
Wachache walio katika uhusiano wameweza kung’amua siri iliyopo moyoni mwa mwandani wake, kwa wanaoshindwa hubaki wakifanya mambo ndivyo sivyo bila kujua wanawaudhi wapenzi wao kwa namna moja ama nyingine.
Leo nitazungumza zaidi na wanaume kuhusu siri hizo. Umeshawahi
kujiuliza, kila unayomfanyia mpenzi wako anayafurahia au yanamboa?
Linaweza kuwa swali gumu sana kwako, lakini leo nimekuletea siri nzito
usizozijua, walizonazo wanawake mioyoni mwao juu ya wapenzi wao.
Inawezekana huzijui, hii ni nafasi yako ya pekee kuzifahamu, kujifunza
na kuchukua hatua.
Kuzifahamu kutakusaidia sana maana kwa bahati mbaya wengi hawapo tayari kueleza kuhusu siri hizo.
NI NINI?
Kabla ya kuanza kuainisha siri walizonazo wanawake wengi mioyoni mwao juu ya wapenzi wao, ni vizuri kwanza nikaelezea maana halisi ya siri za moyoni.
Hizi ni siri za ndani, ambazo mhusika hushindwa kuzitoa kwa
hofu ya kuachwa na mpenzi wake. Hapa namaanisha kwamba hata kama kuna kitu utakachomfanyia na hakipendi, huwa vigumu sana kwake kukueleza wazi na badala yake hubaki akiumia, akisubiri muujiza wa mabadiliko yako!
Wakati mwingine huamua kukueleza kwa ishara ambazo wanaume waerevu huelewa na kuweka mambo sawa, lakini wale wasio na uelewa bapa hubaki wakivurunda kila siku katika uhusiano wao.
Hii ni mada muhimu sana katika maisha ya wapenzi, ila kumbuka
inakuhusu sana wewe mwanaume unayesoma na kukuweka sawa hata wewe mwanamke unayeteseka na siri hizo.
Baada ya kuona siri hizi ni vizuri ukamchunguza mpenzi wako na mwisho wa siku ufanye mabadiliko katika penzi lako ili kila mmoja afurahie kuwa na mwenzake.
Sasa tuanze kuziona siri hizo.
KUHUSU UAMINIFU!
Kwa mtazamo wa kawaida unaweza usione kama hii ni siri, lakini
tunapozungumzia uhusiano hili ni siri nzito kwa mwanamke! Wengi
wanafikiri kuishia kumwambia mpenzi wako unampenda pekee inatosha kumfanya aamini kila unachokifanya.
Hili halina ukweli hata kidogo, mwanamke anapenda uwe mwaminifu katika kiwango cha mwisho kwake, hataki kuwa na mashaka na wewe katika kila unachokifanya.
Anatamani kuwa salama hata utakapokuwa mbali naye kwa sababu za kikazi au mambo mengine. Ili uaminifu huu ambao mwanamke anauhitaji kwako uwepo, lazima uwe na penzi la dhati kwake, uwe huna ‘kimeo’ chochote nje.
Kwa maana hiyo, wakati mwingine mpenzi wako atakuwa huru na simu yako.
UKIMYAHii ni siri nyingine iliyojificha mioyoni mwa wanawake wengi, inawezekana kabisa hujawahi kumfikisha kileleni tangu mlipoanza uhusiano wenu, lakini hawezi kukuambia.
Anabaki kimya tu. Anajitahidi kukufanyia vitu fulani vya hapa na pale ili ugundue kuwa unachokifanya hakipendi, lakini kwa sababu wewe unajifikiria peke yako inakuwa vigumu kugundua moja kwa moja kwamba mpenzi wako hajafurahishwa na wewe faragha.
Tatizo kubwa katika hili ni kwamba, wanawake wengi huonyesha kufurahia sana wanapokuwa faragha na wapenzi wao kwa nia ya kukufanya usijisikie vibaya, uone kwamba kazi unaiweza, lakini moyoni mwake anaumia na anawaza kutafuta mwingine atakayeweza kumkata kiu yake ipasavyo.
Inawezekana akawa anakupenda kuliko kawaida, lakini kwa kosa hili ni
rahisi sana kutafuta mwanaume mwingine ambaye hata kama hatampenda, lakini awe na uwezo wa kumfurahisha ipasavyo faragha.


No comments: