FANYA HAYA KWA MPENZI WAKO NA MTADUMU KATIKA MAHUSIANO









1. KUWA NA MUONEKANO CHANYA (POSITIVE IMAGE) KWA MPENZI WAKO.
Ukiwa Ni Mtu Wa Kuangalia Mabaya/Kasoro Sana Kwa Mpenzi Wako Kuliko Mazuri Yake Hautakuja Kukaa Kwenye Relationship Kwa Muda Mrefu Hata Siku Moja…Utaendelea Kubadilisha Wanaume/Wanawake Kila Siku Na Mwisho Wa Siku Utajiona Huna Bahati Kwenye Mapenzi Na Wakati Unayeyaharibu Mapenzi Yako Ni Wewe Mwenyewe…Hakuna Asiye Na Kasoro (Ukiwemo Wewe Mwenyewe). Kwa Hiyo Muonyeshe Mpenzi Wako Mapenzi Bora Na Umrekebishe Pale Anapokosea Bila Kuwa Na Lawama Mara Kwa Mara, Kuna Makosa Mengine Ni Madogo Sana Na Unaweza Kuyarekebisha Kwa Kukaa Chini Na Mpenzi Wako Mkayamaliza Kwa Dakika 5 Tu Lakini Wengine Huwa Issue Kubwa Kwao Na Kusababisha Mwisho Mbaya.
2. SAMEHE NA KUSAHAU.
Unapomsamehe mpenzi wako kwa kosa lolote alilokosa basi hakikisha umemsamehe kiukweli na ujitahidi kusahau kosa alilotenda itasaidia uwe na amani ya moyo zaidi kuliko kumsamehe kwa usoni tu lakini moyoni ukawa na Donge bado, hii hupelekea kupunguza mapenzi kwa kiasi Fulani kwake na kujikosesha furaha ya mapenzi.Anapokosea siku nyingine usimkumbushe kosa lake la nyuma kwa sababu itamfanya ajione mwenye huzuni na ajione kuwa hakusamehewa.
3. MPE NAFASI/UHURU MPENZI WAKO.
Mnapokuwa kwenye mahusiano jitahidini kwa hali na mali kupeana nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa yale ya kitaaluma zaidi na kimaisha.anapokwambia yupo kwenye kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na umpe support ya kutosha kwenye kazi zake au biashara zake au hata masomo yake.usipende sana kulalamika pale anapochelewa kurudi kazini au kutoka kwenye biashara zake bali mpokee kwa upole na baada ya kupumzika ndipo muulize kwa upole na kimahaba zaidi kwanini siku hizi anachelewa sana kurudi au kwenye biashara zake au shuleni tofauti na zamani.Hii itajenga zaidi kuliko kubomoa kwa kulalamika na kupayuka mbele yake na huku yeye akiwa hata hajapumzika na itamfanya siku nyingine aione nyumba chungu kitu ambacho si kizuri kwenu wote wawili.
4. KUWA MBUNIFU KWENYE MAPENZI.
Napozungumzia ubunifu hapa nakuwa simaanishi kwenye upande mmoja tu wa kwenye yale mambo yetu ya chumbani, hapana. Hapa namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ndani na nje ya nyumba, jitahidi mara kwa mara kubuni vitu vipya vitakavyofanya azidi kukupenda na kukuona kama mpya kwake kila siku. Kama amezoea kupata zawadi za aina Fulani kutoka kwako basi jitahidi siku moja kumbadilishia zawadi kutegemea na unavyomfahamu mpenzi wako anapenda nini na nini. Hakuna anayemjua mpenzi wako zaidi kuliko wewe kwa hiyo lazima ujue ukifanya nini kwake na kwa wakati gani atafurahia na kujivunia kuwa nawe.
5. WHAT GOES AROUND COMES AROUND.
Unapokuwa kwenye mapenzi hakikisha kwa khali yoyote humfanyi mpenzi wako awe na huzuni kila mara. Hapa ninamaanisha kuwa USIPENDE KUMFANYIA KITU UNACHOONA AKIKUFANYIA WEWE UTAKOSA FURAHA. Hakuna kitu kibaya kwenye mapenzi kama kukosa mapenzi uliyoyategemea kutoka kwa mpenzi wako. Kama unaona mpenzi wako aki-cheat utaumia sana basi hata yeye siku uki-cheat ataumia tena inawezekana kuliko wewe utakavyoumia. Usimfanyie kitu amabacho wewe hupendi kufanyiwa hata siku moja.
6. MFANYE AJIVUNIE KUWA NAWE.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku unamfanya mpenzi wako ajivunie kuwa nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa kukuchagua wewe miongoni mwa wote aliowaona. Usijidanganye hata siku moja kuwa kwa kumpata tu na kwa yeye kukupenda basi hajaona mwingine wa kuweza kuwa naye. Wapo wengi sana anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua wewe katika hao wote, kwa hiyo usimfanye aanze kuwafikiria wale wengine wanaomfuatilia kila siku na kumsumbua.Ukianza kumwacha aanze kuwafikiria wengine aidha kwa wewe kuwa unamkosesha amani ya mapenzi kila mara au kwa mengine mabaya ndani ya mapenzi basi ipo siku utaishia pabaya.


No comments: