SHOGA,MPE MUMEO KIAMSHIO NI MUHIMU

MWANAUME ANAAMSHWAJE?
Ikifika alfajiri mwanamke kuwa wa kwanza kuamka kitandani, baada ya hapo fanya uchokozi wako kwa kumwamsha taratibu. Tena huo ndiyo muda wako wa kutumia utaalamu wako wote kuhakikisha anakuwa tayari kwa kupokea kiamshio kutoka kwako.
Endapo atapata kiamshio na umempa inavyotakiwa, utakuwa umefanikiwa kumfanya aamke akiwa amechangamka sawia na mawazo yake yote yatakuwa kwenye kazi.
Baada ya hapo, mpeleke bafuni akaoge, akitoka huko akute umeshamwandalia kifungua kinywa kizuri. Hakikisha kina mvuto ambacho anakipenda. Huo ni ushindi shoga.
Atakapotoka kwenda kazini, mawazo yake yote hujikita nyumbani. Aende nje kutafuta nini ikiwa raha zote anakutana nazo nyumbani? Shoga yangu, wengi wanasalitiwa kwa sababu ya kujisahau.
KWA WAVIVU
Kwa wale mnaoendekeza kazi za ofisini kama kigezo cha kuchoka, huo ni uvivu, itakula kwenu. Eti unaamka alfajiri unawahi kazini je mumeo akitoka nje na kwenda kutafuta huduma mbalimbali utaweza kufanya hizo kazi kweli au ndiyo utalia na kusema umerogwa na vimada usipendwe?
Wanawake wenzangu tuache visingizio kama wewe unafanya kazi kumbuka mume ndiyo kitu cha kwanza kwani umewaacha hata wazazi wako kwa ajili yake, kwa nini usimtimizie haki zake kwa kufuata mienendo iliyo sahihi? Kama una kazi za mbali au muhimu na yeye muweke kwenye ratiba ili usiharibikiwe upande mmoja.
Mume hapatikani popote bibi, si rahisi kihivyo. Kazi zinatafutwa hata kwa kuhonga na utapata, lakini ndoa utamuhonga nani? Je, utafanya nini ili kumpata yuleyule uliyefunga naye ndoa? Badilikeni mashosti ili kujenga nyumba ikae salama.
Mwisho nikukumbushe kuwa karibu na mumeo usiku wote. Mnapokaa sebuleni, talii kiwiliwili chake kama mpiga gitaa, hapo utamsababishia kukitamani kitanda, hivyo kulala mapema. Mkiwa kitandani mapema, itawarahisishia kufanya shughuli zenu mapema ili asubuhi mkiamka, muendelee na kazi za ujenzi wa taifa.


No comments: