UNAKOSEA WAPI.....KWANINI MAPENZI YAKUUMIZE
Kwa nini mapenzi yakuumize? Unakosea wapi, kwanini ukataliwe kila mara? Haya ni baadhi ya maswali ya kujiuliza kuhusu mateso ya mapenzi.
Kamwe katika maisha yako usiruhusu mapenzi yakutese, najua yawezekana kila mpenzi unayempata haudumu naye, wewe ni mtu wa kuumia na kulia kila siku, hujawahi kufurahia maisha ya mahusiano hata siku moja, jipange upya.
Thamini na jali zaidi maisha yako kwanza, fikiria kipi ni bora kati ya mapenzi na maisha yako, ni kipi kilitangulia? Kama maisha ndiyo yalitangulia kwanini usijijenge kwanza kimaisha ndipo mengine yafuate?
Hata kama unateswa na mtu unayempenda kwa dhati, hata kama ni mzuri kushinda malaika, kwani bila yeye maisha hayaendi? Si kweli na kama unaweza kuishi bila yeye kwanini akutese namna hiyo?
Hakuna kitu kinachouma kama mapenzi endapo utakosea kanauni zake, ukaruhusu moyo wote kuelekea huko, hakika yatakutesa.
Yawezekana hadi sasa bado kuna mtu anakusumbua, umejaribu kumbembeleza lakini hataki kukubaliana na wewe, umejaribu kumuonesha upendo wako wote ila halitambui hilo huyo hakufai.
Mapenzi hayapo ili yatutese, badala yake mapenzi yapo kwa ajili ya kutupa faraja maishani mwetu.
Muondoe kabisa akilini mwako mtu wa aina hiyo, kwani atakufanya uyaone maisha kwa mtazamo hasi jambo ambalo siyo zuri. Bado unanafasi ya kuweka upya.

No comments: