RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU 03

MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)

SEHEMU YA 3

 “wanakuita kipenzi cha warembo?” Haiba hakuruhusu hilo lipite akiwa kimya.
   “ndio jina langu la utani. Maana warembo wanapenda sana kuangalia filamu. Na mimi nafanya biashara ya vitu wanavyovipenda.” akili ya uokozi ilinipa jibu kali lililommaliza Haiba na kufanya atabasamu.

   Tulitembea kwa mwendo wa dakika kumi na kufika nje ya geti moja wapo.
   “hapa ndio nyumbani kwetu, mbali eeh?” Haiba aliniuliza baada ya kufika. Niliangalia saa yangu na kumtazama.
   “sio mbali kwa mwendo wa kiume. Kwakua wewe unatembea taratibu ndio maana unapaona mbali.” nilimpatia majibu hayo na kumfanya atabasamu.

   Alibonyeza kengele na kuniangalia. Alinipa ishara ya kuniaga na mlango ukafunguliwa akaingia ndani. Nilitazama jengo hilo, halikua kwenye hadhi ya chini. Hivyo nilipata tafsiri kua Haiba anaishi maisha mazuri japo si ya juu sana.
   “kwanza kidato cha pili tu kumiliki laptop ni wazi nilitakiwa kukuta jumba kama hili. Sasa mbona amechelewa kupata laki na ishirini tu?” nilijiuliza hayo wakati naelekea kituo cha daladala.
   Ilinibidi niende kwa Killer muda huo ili mradi aweze kutoa majibu.Kwakua alishanipanga kabisa kua niweke cha juu kama ganji, illinibi niongezee shilingi elfu kumi kutoka kwenye pesa zangu na kumpatia Killer laki moja na thelathini.
   “sio mbaya, ila ungemwambia laki na hamsini ili tupate kumi na tano kila mmoja.” Killer aliongea hayo bila kujua mwenzake kwenye kazi hiyo sijaingiza kitu chochote. Zaidi ni mimi ndio nimeongezea, tena nimeongezea bila muhusika kujua kama nimeongezea pesa kwenye matengenezo ya Laptop yake.
“nije saa ngapi?” nilimuuliza Killer baada ya kumkabidhi pesa hizo.
“naenda sasa hivi kariakoo. Ukija usiku kila kitu safi.” 
Nilimuamini Killer. Maana mara nyingi alikua mkweli kwangu na hakunificha kitu hata kama kitakua cha aibu.

   Basi nikaondoka na kurudi ofisini kuendelea na kazi. Siku hiyo nilifunga ofisi saa tatu usiku. Nilienda moja kwa moja mpaka ofisini kwa Killer na kumkuta.

   Kila kitu kilikua kipo sawa. Maana nilimkuta akirejesha mafaili ya Haiba kwenye Laptop yake. Nilijikuta nimetabasamu baada ya Laptop hiyo kutengemaa.

   Ilinilazimu kuchukua usafiri wa pikipiki mpaka nyumbani. Nilifanya hivyo kwa hofu ya kutembea usiku na kifaa cha watu.

   Kipindi hicho hata sikua na elimu ya kujua ukubwa wa computer. Niliamini ukubwa wa kifaa cha kuhifadhia kumbukumbu na diski ngumu ndio ukubwa wa mashine. Hivyo habari zingine sikua na elimu navyo. Hivyo nilijua tu kua laptop hiyo ni kubwa kwakua ilikua na vitu hivyo vyenye ukubwa kuliko computer ya ofisini yangu.

   Nililala nayo kitandani na kuifunika shuka. Sikutaka ipotee hata kama tungeli vamiwa na wezi hapo nyumbani siku hiyo.

   Asubuhi palipo pambazuka nilienda nayo ofisini na kusubiri mida ifike ili mwenye mali aweze kufika. Ilipofika saa kumi, nilimuona Haiba akiwa ofisini na sare zake za shule. Ndipo niligundua kua anasoma shule ya sekondari Loyola. Hiyo shule ni moja ya shule za kulipia ambazo licha ya pesa tu, pia lazima akili yako iwe inapiga kazi sana ndio uruhusiwe kusoma hapo. Ukiwa goigoi basi huendelei. Maana wao mitihani ya kurudia ni kila kidato. Na kama umetoka shule za serikali pindi uliposoma shule ya msingi, unalazimika utumie mwaka mzima kusoma maandalizi ya kuingia kidato cha kwanza. Ujifue kwanza lugha ya kiingereza ndio uende nao sawa.
   “kumbe kana mbongo eeh...” nilijiongelea mwenyewe na kumkaribisha huku nimetabasamu. Hata yeye  mwenyewe alinirejeshea tabasamu. Maana alijua mambo mazuri.

   Nilimuwashia Laptop yake na kumpatia. Hakika niliiona furaha yake juu ya laptop hiyo.
   “leo sikai sana. Ila nitafurahi ukinipa ofa ya juisi ya embe.” maneno ya Haiba yalipenya vizuri kwenye masikio yangu na kwenda kuchukua juisi mbili na kurudi kukaa naye.

   Siku aliyosema hakai sana, ndio siku aliyoondoka saa moja na nusu usiku. Ofisini kwangu alifika rafiki yangu aliyekua anaitwa Athumani. Nilimuachia ofisi na mimi nikamsindikiza Haiba mpaka karibu na kwao kisha tukaagana.

   Niliamini kua urafiki wetu hauwezi kukatishwa baada ya kupona kwa Laptop yake. Ndivyo ilivyokua kwa msichana huyo. Nyimbo nyingi zilizotoka nilikua nazipata kiurahisi kutoka kwa rafiki yangu Shabani Tagalile. Huyo ni rafiki yangu ambaye ana marafiki wengi kariakoo. Hivyo wimbo ukitoka leo hata zile ambazo zillikua zimevuja tu nilikua nazipatika na  kumtaarifu. Kuna  nyimbo zingine hua ananitajia ambazo sijawahi kuzisikiliza. Ila nikitafuta kwa jina alilonitajia basi niliweza kuzipata.

   Kitu ambacho Haiba alikua haruhusiwi kumiliki nyumbani kwao ilikua ni simu. Hivyo mawasiliano kwetu ilikua mpaka tukutane. Mitandao ya kijamii ilikuwepo, ila simu yangu haikua na uwezo wa kuingia. Kwa sababu ya kutaka ufahari, Nakumbuka nilijikwinya na kutoa laki moja na tisini na kununua simu ya kwanza yenye uwezo wa kuingia kwenye internet. 
   “Hivi Molito upo facebook?” hilo ni swali la kwanza kuulizwa baada ya kumuonyesha rafiki yangu Haiba simu yangu niliyoinunua. Kiukweli ushamba uliendelea kunitafuna. Nilikua nausikia mtandao huo ila sikua nafahamu chochote. Kwakua nilishamzoea, nilimuambia ukweli kama sina akaunti huko.
   “weka email yako.” 
Yaani Haiba siku hiyo alizidi kuniumbua. Nitafanyaje sasa na mambo ya email nipo nayo kushoto. Baada ya kumuambia kua hata hiyo sina pia. Akaweka kifaa cha kunasiamawimbi ya mtandao  kwenye laptop yake na kuingia mtandao uliondikwa yahoo!
   “jina lako nani. La kwanza na la mwisho.” Haiba aliniuliza na kunitazama kuashiria kua alikua akivihitaji kwa ajili ya kuandika kwenye ufunguzi wa email hiyo.
   “Hussein Molito.” nilimtajia jina hilo na kumfanya ashangae na kunitazama.
   “kumbe Molito ni jina lako halisi?” swali hilo nilishakumbana nalo mara nyingi. Maana jina langu halijakaa kibantu.
   “ni jina langu hasa, tena Molito nilipewa mimi kama kumbukumbu kwa ajili ya babu yangu.” niliongea hayo na kumfanya Haiba atabasamu na kuandika majina hayo.
“email yako itakua husseinmolito@yahoo.co.uk... Au imekaaje hiyo kwako?” Haiba aliuliza na kunifanya nitabsamu. Sikua na la kupinga kwa kitu alichokipenda rafiki yangu huyo.
Nilimtajia nano siri ili aweze kunifungulia akaunti kwenye mtandao huo.
   “facebook utakua unaitwa Hussein De Molito.” alinijulisha hayo na kuniambia kama nina picha kwenye computer yangu. Nilimuonyesha na akachagua picha moja iliyomvutia na kuiweka  kwenye sehemu iliyomuomba picha.
   “hapa utatafura rafiki zako. Ukijaza shule yako basi wale wote uliosoma nao utawaona na hapa ndipo pakuomba urafiki. Mtu akikutajia jina analilotumia huku facebook basi unalitafuta kwa kuandika jina lake hapa. Ngoja nikuombe urafiki ili uone jinsi ya kukubali pia.” nilipatiwa elimu ya kutosha na binti huyo na kunifanya niwe natabasamu. Maana tayari niliona urahisi wa kuutumia mtandao huo.
   “Haibery Slim” niliona jina hilo likijitokeza na kialama chekundu juu kikiandika namba moja. Hapo ndipo aliponiambia nibonyeze sehemu iliyoandikwa kiingereza ‘confirm friend request’ nilitabasamu tu kuona neno ‘Haib’ ambalo kwa upeo wangu haraka tu nikatambua lilikua linamaanisha Haiba. Pia nilifahamu kuwa hilo neno ‘slim’ lilikua linamaanisha umbo lake kutokana na wembamba wake.. Nikatamani kujua hizo herufi ‘ery’ zinamaana gani.
   “baba yangu anaitwa Zubery, hivyo nimechanganya herufi zetu hapo na nikapata neno Haibery. Na slim ni huu umodo wangu.” alijibu vizuri kabisa na kumfanya nimsifie.

   Usiku wa deni hauchelewi kukucha, kufumba na kufumbua matokeo ya kidato cha nne yakatangazwa.
   “Molito nitajie namba yako ya mtihani na namba ya shule.” Haiba alikua wa kwanza kuniuliza aliposikia tu matokeo yametoka. Maana alifika ofisini kwangu na laptop yake kwa minajili ya kuangalia matokeo yangu pamoja. Sikuweza kumzuia ili moyo ulikua unadunda balaa. Kishingo upande nilimpatia japokua sikutamani ajue. Maana ingekua aibu kwangu kama ningeanguka mitihani hiyo.
   “waooooh! Hongera sana. Umepata daraja la pili tena alama ya kwanza kabisa” maneno ya Haiba yalinifanya ninanyuke na kufurahi. Nilifurahi sana na Haiba akashiriki furaha yangu na kunikumbatia.
   Furaha ya kufaulu ilikua kubwa kiasi cha kumbatio hilo kuliona la kawaida wakati sikuwahi kupewa hiyo nafasi hata siku moja.
   “sasa unakaribia kwenda shule, na ofisi yako je?” Haiba aliniuliza baada ya kupongezana.
   “hii sio ofisi yangu, mimi nilikua mfanyakazi tu ya kujishikiza wakati nasubiri matokeo.” maneno hayo yalimfurahisha Haiba na kugundua kua shuleni nilikua nasoma na si kucheza.

   Nilipangiwa shule nje ya mkoa wa Dar-es-salaam. Hivyo huo ukawa ukuta wetu mimi na Haiba. Kuonana kwetu ikawa adimu sana. Maana kuna wakati nilipokua nimerudi likizo yeye alikua ameenda Tanga kusalimia ndugu na jamaa.

   Nakumbuka nilipomaliza kidato cha sita. Nilirudi nikiwa nimeshakua na sasa nilikua na wazo la kumuambia Haiba kua namuhitaji kama mpenzi wangu. Maana kwa kipindi chote moyoni mwangu hakuchuja. Na umbali wetu ulinifanya nimkumbuke sana. Hiyo ilitosha kabisa kuniambia kua nilikua nampenda sana Haiba kuliko msichana yeyote.

   Ilikua mwezi wa pili, hivyo hata Haiba alishafaulu na kuendelea na masomo ya kidato cha Tano hapo hapo Loyola. Alifaulu Daraja la kwanza ya 9. Niufaulu mkubwa sana na alistahili pongezi. Nilimnunulia zawadi kwa ajili ya kumkabidhi. Nilimjulisha kupitia mtandao facebook.
Alinipa namba zake za simu. Baada ya kumaliza kidato cha nne kumbe aliruhusiwa kutumia simu. 

   Nilimpigia kwa mara ya kwanza ili nipate kuisikia sauti yake. Maana niliikumbuka kwa kitambo sijapatapo kuisikia.

   Sauti yake ilikua ni ileile. Sauti teke ya mtoto mdogo na kicheko cha kasuku alichojaaliwa msichana huyo.
   “Natamani kukuona Haiba.. Maana kimasihara mwaka mzima hatujaonana.” 
Hicho ndicho kitu nilichomsisitizia Haiba baada ya kuwasiliana naye.
   “wewe tu, panga basi jumapili ni wapi tuonane.” jibu lake lilinifanya nitabasamu tu. Maana lilijipa tumaini kua huenda hata yeye ananihitaji, sema ananisubiri niongee.
   “tukutane Best Bite basi mida ya chakula cha mchana. Kisha kama kubadilisha kiwanja tutajua huko huko.” nilichagua hapo na kusikiliza jibu lake.
   “sawa, saa sita tukijaaliwa nitakua hapo.” Haiba alinipa jibu hilo na kunifanya niongee mambo mengine hasa nikimuhadithia vile nilivyokua najisikia iwapo nirudipo Dar na kumkosa.

   Kwakua siku hiyo ilikua siku ya Ijumaa, basi jumamosi nilitoka na fedha kiasi na kwenda kununua zawadi. Nilinunua ua zuri na saa iliyonivutia. Ilinigharimu laki moja na hamsini kununa vitu hivyo. Sikujali, kwakua mtu niliyekua nampelekea alikua na thamani sana kwenye moyo wangu.
Nilitafuta viwalo vizuri ili ning’ae kidogo. Nilifanikiwa kupata nguo zilizonivutia na kurudi nyumbani.

Siku ya Jumapili nilizinyoosha pasi nguo zangu na mida ya saa nne nikatoka.
Saa tano nikawa nimeshafika eneo husika. Nakaagiza juisi na kuchezea simu yangu ili kumsubiri mwanamke aliziteka hisia zangu toka namuona siku ya kwanza .

   ‘Saa sita na robo’ ubongo wangu ulinisomea saa haraka baada ya macho yangu kutazama eneo la saa ya simu simu yangu. 
   ‘labda kuna foleni, tulia Molito’ ubongo wangu ulinielekeza na mimi nikaupuuzia moyo uliokosa subira na kutaka kupiga simu kuulizia amefika wapi.

   Dakika zilikimbia kama kuna mtu alikua anazikimbiza. Hatimaye adhana ya adhuhuri ikaadhiniwa. Nikasubiri mpaka saa mshale wa dakika ulipofika kwenye tatu na kuniambia kua muda huo ulikua saa saba na robo. Hapo sasa ndipo nilipochukua simu yangu na kutafuta namba yake ili nimpigie. Kabla sijabonyeza kitufe cha kupigia simu, nilimuona akiingia na kuanza kutafuta ni wapi nilipo.

   Niliweza kumuona na kupunguza wasiwasi nilikua nao Basi nikatabasamu baada ya kumuona. 
   “waaoooh!” niliongea hivyo na kusimama ili kutengeneza nafasi ya kukumbatiwa na Haiba. Kweli nilifanikiwa na kukumbatiwa na msichana huyo. Niseme tu ukweli kutoka moyoni, nilisisimkwa mwili wote baada ya kutua kwenye kumbatio la msichana huyo. Haiba alikua mdada. Sasa maziwa yake hayakua yakutokeza kama vile awali. Alikua na ziwa zuri na nguo aliyovaa iliweza kunijulisha alikua na ziwa kama kifuu cha nazi. Na yalikua yamesimama dede. Kwa mwili wake wa sasa alikua na haki ya kubadili jina kule facebook. Hakua Slim tena. Alinenepa kiasi ila alivutia kwa muonekano. Hata sura ilionyesha wazi kua Haiba ameshakua. Ila kikubwa ni uzuri wake kuongezeka maradufu.

   Macho yake yalitua kwenye ua lililokua mbele yangu. Niliona kabisa akilifurahia.
   “hilo ua kwa ajili yangu eeh!” aliuliza, nami nikaona ni muda sahihi wa kumkabidhi zawadi zake.
    Nilimuomba mkono na kumvalisha saa ya thamani. Hakika kwa muonekano wake tu, bila kuuliza bei, ila alifahamu kua nilijikaza mwanaume na kutoa noti kadhaa ili kuipata saa hiyo. Hata ua pia halikua ua la mafungu.
   Alishukuru na kunizawadia kumbatio lingine. Hakika nilifurahi sana.
   “Naomba chips kuku. Na juisi halisi ya embe.” Haiba aliagiza alipoulizwa na muhudumu. Nami nikampa ishara oda hiyo ailete mara mbili.
   “umependeza sana Haiba.” nilimpa sifa zake mtoto mzuri.
   “Ahsante.. Hata wewe. Umependeza sana. Umekua mkaka na muonekano wako upo vizuri, nimependa kiduku chako na kidevu chako. You are so handsome Molito” 
doh! Kwa sifa hizo nilihisi kuganda. Maana kama nimeweza kumvutia, hata kile nilichopanga kumuambia siku hiyo kinaweza kufanikiwa kiurahisi. Nilijipa moyo kwanza.

   Baada ya kusifiana hapa na pale, ndipo tulipofanikiwa kumaliza chakula.
“ni sehemu gani tulivu ungependa twende?” niliuliza swali hilo na kumuangalia Haiba aliyekua anafuta mdomo wake.
   “leo ni siku yangu eeeh... Haiba Day!” swali hilo lilikua jibu tosha kwake.
“twende Mlimani City tukale ice cream kisha twende kunduchi beach.” Haiba alitoa maelekezo hayo. Na mimi nilikua nimejipanga vya kutosha. Nilivunja kibubu ili nisiadhirike kwa mtoto huyo niliyekua namuelewa vibaya mno.

   Basi ukawa ni mwendo wa kuwaneemesha madareva taksi tu popote pale tuendapo. Tulifika Mlimani City na kula Ice cream pamoja. Wakati huo nilifanikiwa kuiona simu ya Haiba, ilikua simu ya gharama kuliko simu yangu mpya niliyoibadilisha. Nilishuhudia akipiga picha tukiwa pamoja kwenye tukio hilo na mpaka tulipoenda Kunduchi Beach alikua anachukua matukio tukiwa pamoja. Hakika niliiona furaha yake kwa kila kitu nilichomfanyia. Nami kama mfanyaji nilifarijika kwakua lengo lilikua limetimia kama lilivyokusudiwa.

   Basi gazi lilipoingia, aliniambia kua ameridhika na sisi ni vyema tuondoke. Maana nyumbani kwao hua anafokewa kama ikifika saa tatu usiku na bado hajarudi nyumbani.

   Na mimi niliona huo ndio muda muafaka wa kuongea kilichopo moyoni mwangu. Maana ni kitendo cha muda mfupi sana kuongea japo kinahitaji ujasiri na nafasi pia ya kuzielezea hisia zako kwa mtu husika. Hasa ambaye haonyeshi kukukubali kama mpenzi.

   Nilimuomba tuongee na kuniruhusu, kwenye hoteli hiyo kulikua na sehemu tulivu sana. Hivyo tulifika hapo na kukaa karibu kabisa.
   “kwanza natanguliza msamaha kwa hiki nitakachoongea kwako kama kitakukwaza.” nilifungua maongezi hayo na kuzidisha umakini kwa Haiba na kumfanya atulie na kuniazima masikio yake ili yapate kusikia mpaka mihemo yangu wakati naongea.
  “toka siku ya kwanza nilipokuona, nilivutiwa na wewe. Nikakupenda pia. Na nilishindwa kusema kutokana na kidato ulichopo. Ila kwa sasa nimeona ni bora niweke wazi hisia zangu kwako ili na wewe uweze kutambua kilichopo moyoni mwangu. Nakupenda sana Haiba, kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu kabisa.” niliongea hayo na kumuona kabisa Haiba akihema. Ile mihemo ilinitafsiria kua kila nilichokiongea amekisikia vizuri.
   “nakuhitaji kwenye maisha yangu kama mke wangu hapo baadae. Umenivutia na nitafurahi kama ukinipokea kama mpenzi wako kabisa.” Niliongeza na kumfanya Haiba apoe. Maneno yote yalipotea. Ujanja wote ukawa mfukoni. Nadhani hakutegemea kama ningeweza kuongea hayo.
   “nipo tayari kukusubiri umalize shule na ndio tuanze rasmi mahusiano yetu. Ila nihakikishie tu kama utakua na mimi kwenye maisha yako. Nakuapia kwa Mungu wangu muumba wa ardhi na mbingu, nakupenda sana Haiba. Sijawahi kupenda kama hivi hapo awali. Na wala upendo wangu haujawahi kupungua toka nilipoanza kukupenda. Naomba unipokee kwa uzima na maradhi.. Ushujaa na udhaifu wangu. Naomba uwe furaha yangu ya pili baada ya mama yangu.” nilizidi kuongeza kila ambacho moyo wangu umepata ujasiri wa kusema. Hakika maneno yangu yalimgusa. Yalimchoma na kubaki akiniangalia. Nilimshika, nikamuona kabisa akitetemeka, Hana kauli.
   “Haiba, upo tayari kuwa na mimi?” hilo lilikua swali la mwisho. Swali ambalo ni lazima alijibu. Maana maelezo ya mwanzo alikua akiyasikiliza tu. Aliniangalia kwa aibu. Kisha akaongea kwa sauti ndogo lakini iliyopenya mpaka kwenye ngoma za masikio yangu.
   “nipe muda, nitakujibu Molito.” aliongea hayo na kunyanyuka. Niliweza kuiona hofu aiyokua nayo. Nilimsogelea na kusimama nae kwa usawa. Niliuinua uso wake ili apate kunitazama. Niliyaona machozi yake na kuyafuta kwa kiganja changu. ndipo aliponishika mabega na kunikumbatia.

   Nilijipa jibu mwenyewe kua tayari nimeshapendwa hata kabla mwenyewe hajaenda kujifikiria. 

  Baada ya kutoka kwenye kumbatio hilo,tuliondoka hapo na kurudi nyumbani. Nilihesabu kiasi kichobaki katika fungu nililotenga kwa ajili yake. Ilibaki shilingi elfu sabini. Nilitabasamu na kumkabidhi shilingi elfu thelathini. Alizikataa na baada ya kumlazimisha sana akazipokea na kuniaga.

   Nilirudi nyumbani nikiwa nimesuuzika roho, nafsi na mwili. Maana lile dukuduku lilikua limenikaba kwa kipindi kirefu niliweza kulitoa. Nlijipongeza mwenyewe kwa ujuasiri na u’Shah Rukh Khan wangu kumbe ulikua bado upo kwenye damu.

   Zilipita siku tatu bila kumtafuta Haiba. Sikufanya makusudi, ila nilikua nahofia kuonekana namyima nafasi ya kujifikiria.

   Siku ya ijumaa saa nne na nusu usiku, simu iliita na kuangalia jina, niliona jina la Haiba. Niliipokea haraka simu hiyo ili nipate kumsikiliza.
   “Molito, umelala?” lilikua swali nililokumbana nalo baada tu a kuipokea simu hiyo.
“hapana, niambie Haiba.” Nilijibu na kumfanya Haiba aendelee kuongea.
“nimeamua nikupigie muda huu ili niweze kukupa jibu lako.”
Maneno ya Haiba yalinifanya nikae vizuri ili niweze kusikia ni majibu yapi aliyotaka kuniambia usiku huo.
                           ***************  
   02/01/2018 ndiyo tarehe niliyopanda ndege kwa mara ya kwanza. Ilikua ni safari ndefu ambayo niliishia kuandika kwenye vitabu vyangu. Eeeh, ni vitabu. Kwani baada ya kusubiri matokeo yangu ya kidato cha sita. Nilikua nimeanguka vibaya. Na mimi sikutaka kusomea uaskari wala ualimu. Maana ndicho kitu pekee nilichotakiwa kufanya kama sitaki kurudia mtihani. 

   Maisha ya shule yalinichosha. Ndipo nikaamua kurejea kipaji changu ambacho nilikitelekeza toka mwaka 2008. Kipaji cha uandishi wa Riwaya.

   Niwarudishe nyuma kidogo. Kipindi naanza kuandika riwaya baada ya maisha ya shule kuishia njiani, nilianza kuandika rasmi kupitia mtandao wa kijamii wa facebook. Ilikua mwaka 2013 mwishoni. Hiyo ni baada ya kukaribishwa kwa mikono miwili kwenye kundi la mwandishi mwenzangu Frank Masai. Kundi hilo liliitwa Tungo za kusisimua. Hakika nilikutana na waandishi wengi. Hawakua wanaandika ili wapate pesa, bali kuonesha vipaji vyao. Hata mimi nakaanza kuandika huko na mwaka 2014 nikaanza kuwa maarufu. Nikafungua ukurasa huko facebook na kuandika jina la Tungo Za Hussein O. Molito. Mwaka huo huo nikafanya mapinduzi kwa kufungua na magroup Whatsapp na kuanza kuuza hadithi zangu. Ndipo hapo rawaya zikageuka kuwa ajira kwangu.
   Tarehe hiyo nilikua ndani ya ndege naelekea nchini Marekani kupokea tuzo yangu ya mwandishi bora Afrika ilioandaliwa na kampuni ya SWTL inayo jishughulisha na maswala ya lugha yenye makazi yake nchini Marekani. Hivyo mie kutangazwa kuwa Mtanzania wa pili kuchukua tuzo hizo toka kuanzishwa kwake baada tuzo ya kwanza kuchukua ndugu yangu Hussein Issa Tuwa.
   Ni vitu vingi sana vilipita katikati hapo, vya kufurahisha na kuhuzunisha. Ila katika kitu ambacho siwezi kusahau ni vile nilivyompoteza mwanamke niliyempenda kwenye maisha yangu, HAIBA. 
   Siku aliyonipigia simu na kuhitaji kunipa majibu yangu, ndiyo siku ya mwisho kuongea naye na siku ya mwisho kuonana naye. Sikujua kama alikufa au bado yupo hai, maana ni muda mrefu sasa umeshapita. 

   Katika mipango ya maisha nilijaribu kutafuta mbadala wa Haiba. Niliishia kupata mtoto, lakini sikupata msichana aliyeweza kuziteka hisia zangu kama Haiba. 

   Nakumbuka siku hiyo nilikua naamini kila kitu kimeenda sawa. Mpaka Haiba kuamua kunipigia simu usiku ni wazi kua ameshindwa kuvumilia na alikua anahitaji kuniambia vile alivyokua anajisikia juu yangu. Kumbe ilikua tofauti kabisa.
   “Molito, ni ukweli usiofichika kua hata mimi nina hisia za mapenzi juu yako. Nilikupenda na ulikua moja ya furaha yangu. Ila kuna kitu nilishindwa kukuambia palepale, nilihofia utajisikia vibaya. Ila nasikitika kukuambia kua siwezi kuwa na wewe kimapenzi. Hata kwa urafiki wa kawaida pia. Maana mpenzi wangu kaziona picha zetu na amekasirika sana. Nampenda sana na kurudi kwako kumenifanya nishindwe kuamua. Ila siwezi kuwa na mahusiano na watu wawili wakati nina moyo mmoja. Nimekaa, nimfikiria, nimeona bora niwe na huyu kwakua nampenda zaidi yako. Hivyo naomba usinichukie. Unaweza tu kuendelea na maisha yako Molito.” baada ya kuongea hayo hakunipa nafasi ya kujibu wala kujitetea. Akakata simu. Nilipopiga kwa mara nyingine haikupokelewa. Nilipopiga tena simu haikupatikana. Kuashiria kua imezimwa. 

   Hakika iliniuma sana. Nilipungua mwili kwa mawazo. Ilinichukua muda mrefu sana kukubali kua mahusiano yangu na Haiba yalikua yamefikia kikomo.

   Basi, Nikawasili nchini Marekani na kupokelewa na wenyeji wangu. Nikapelekwa hotelini ambapo niliambiwa nitakaa hapo kwa siku moja. Maana siku inayofuata ndiyo siku ya utoaji wa tuzo rasmi kabisa.

   Nikiwa kwenye chumba hicho. Niliendelea kupiga picha na kutuma kwenye mitandao yangu ya kijamii. Nilifanya hivyo kwa safari nzima. Maana picha ni moja ya ugonjwa wangu ambao sikutaka kujua tiba yake. 

Baada ya  kufungua pazia, nilikutana na kioo kilichoniwezesha kuona mandhari mbalimbali ya nchini humo. 
   Nilipochungulia chini, niliweza kuona bwawa la kuogelea. Nilitamani sana. Maana hata kuogelea napenda pia.

   Nilibadili nguo na kushuka chini. Niliogelea na baadhi ya watoto wazuri wa kimarekani. Nilipiga picha na wamerakani hao ambao hawakunibagua. Nahisi ni kulingana na hadhi ya hoteli hiyo au muonekano wangu ulikua umeikimbia Afrika. 
ITAENDELEA.........RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU

MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)

SIMU: 0718 97 56 59

ITAENDELEA.........

  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO

No comments: