RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU 04
RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU
MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)
SEHEMU YA 4
Nilibadili nguo na kushuka chini. Niliogelea na baadhi ya watoto wazuri wa kimarekani. Nilipiga picha na wamerakani hao ambao hawakunibagua. Nahisi ni kulingana na hadhi ya hoteli hiyo au muonekano wangu ulikua umeikimbia Afrika.
Siku iliyofuata nilienda kufanya manunuzi mbalimbali. Ikiwemo nguo na vitu ambavyo vitanifanya niwe na kumbukumbu navyo pindi nikumbukapo siku niliyoenda nchini Marekani kwa mara ya kwanza.
Maana baada ya kupokea tuzo tu, sitopata muda wa kuzurula tena nchini humo, nitarudi nchini Tanzani alfajiri inayofuata.
Wakati nipo kwenye duka kubwa nafanya manunuzi ya hiki na kile,
Hamadi!
Niliweza kumuona msichana anayefanana sana na Haiba.
Ni miaka mitano imepita hatujaonana, lakini sura yake iliniganda ubongoni. Niliacha kufanya nilichokua nakifanya muda huo na kutoka nje kumfuatilia msichana huyo.
Kadri nilivyozidi kumkaribia,ndipo fikra zangu zilivyozidi kuniambia kua ni sahihi kabisa nikiwazacho. Msichana huyo ni Haiba mwenyewe. Kuanzia tembea yake hadi muonekano wake wa nyuma.
Baada ya kuona natembea umbali mrefu na msichana huyo anazidi kukata mitaa, niliamua kupaza sauti yangu juu na kulitaja jina lake.
“Haibaaaa!”
Muito huo uliweza kumfanya ageuke nyuma na kumtazama mtu amuitae. Sikuamini macho yangu baada ya kumuona Haiba ananiangalia kama vile ndiyo mara yake ya kwanza kuniona au alikua hajui ni nani aliyemuita.
Nilimshuhudia akinipuuzia na kuvuka barabara na kuingia kwenye mgahawa mmoja uliokua pembeni kidogo ya barabara hiyo.
“ina maana amenisahau kiasi cha kutonifahamu mimi ni nani?... kwa miaka mitano tu?” nilijiuliza kwanza kisha na mimi nikavuka barabara na kwenda kwenye mgahawa huo na kukaa kwenye kiti cha mbele yake kutoka kwenye kiti alichokaa yeye.
“mambo.”
nilimsalimia kwa lugha ya kiswahili. Alishtuka kidogo baada ya kunisikia nimeongea lugha hiyo na kumfanya aachie tabasamu.
“na wewe ni Mtanzania eeh?”
swali hilo lilinifanya nichanganyikiwe hasa. Eeh, nilichanganikiwa kwakua haiwezekani aniulize swali hilo kama ndiyo mara ya kwanza tunaonana. Yaani anaigiza kua hanifahamu kabisa. Hakika aliniduwaza na kunifanya ile hamu ya kumuona ianze kupungua taratibu. Maana hata mimi sikua Molito wa miaka mitano wakati huo. Nilikua Molito ambaye amepanda ndege na hapo tunapoongea ni nchini Marekani. Hivyo kunifanya hanijui kulinifanya nishikwe na hasira. Sema nilijikaza ili niweze kuona misho wa mchezo huo utakua vipi.
“Ni Mtanzania halisi kabisa, Naitwa Molito.”
nilijitambulisha tena ili kama ananifananisha kwakua tumekutana kwenye nchi ambayo alifikiri siwezi kufika, Basi aweze kujua kua kila akionacho mbele yake ni sahihi na si ndoto tena za Bulicheka.
“waoooh... Nimefurahi kukufuahamu. Wewe umelijuaje jina langu?” Haiba aliniuliza swali hilo lililonifanya niachie tabasamu. Maana nilihisi kabisa alikua ananizingua na hakua ‘Serious’ hata kidogo.
“Haiba, acha masihara mama. Ina maana hunijui kabisa?” Niliamua kumuuliza kabla hasira hazijanijaa na kuamua kuondoka eneo hilo. Maana katika maisha yangu hua sipendi dharau.
“sikukumbuki... Hata sijui mara ya mwisho nimekuona wapi.”
Haiba alijibu huku akiwa haonyeshi tabasamu ili niweze kuamini kile ambacho alikua ananiambia muda huo.
Ilinishangaza sana.
“mbona sijabadilika chochote? Ina maana nimekua na muonekano mwengine kabisa tofauti na ule wa awali mpaka asinikumbuke tena? Muonekano sawa, jina je?” Niliongea na nafsi yangu huku macho yangu yakipata kummtazama Haiba ambaye hakunijali zaidi ya kuendelea kupiga fundo kinywaji alicholetewa.
“Basi sawa, tutaonana tena Mungu akipenda.”
Ilinibidi niongee hivyo. Maana kila sekunde iliyokua inazidi kusogea ndipo nilipopata hasira juu yake.
Muonekano wangu na maamuzi yangu yalimfanya Haiba aone kabisa kua nimekwazika. Hivyo nilivyonyanyuka na kuanza kuondoka, na yeye alinyanyuka na kunifuata .
“samahani kaka yangu. Naomba nijulishe umenifahamu vipi. Maana kiukweli kabisa sina kumbukumbu yoyote na wewe. Ila nimejisikia vibaya tu kushindwa kukutambua ili hali wewe unanifahamu.” Haiba aliongea maneno hayo na kunifanya nisimame na kumgeukia.
“hivi humkumbuki Molito. Yule mvulana aliiyekua anafanya kazi ya kukodisha CD, mtu aliyekutengenezea laptop yako baada ya kufa kioo.... Hivi ni kweli hukumbuki chochote kuhusu mimi?” Niliuliza kwa hamaki kidogo. Nilimuona msichana huyo akiwa mnyonge na kunitazama huku akijaribu kuvuta kumbukumbu zake.
“kiukweli sikukumbuki Molito.... Ila kuna sababu pia ya kutokukumbuka pia.... Hivyo naomba usinichukie.” Haiba aliongea maneno hayo na kunifanya nitamani kuijua hiyo sababu ni ipi na inahusiana vipi na kujifanya amenisahau.
“sio kwamba sikukumbuki wewe tu. Sikumbuki vitu vingi kwenye maisha yangu. Sikumbuki hata siku yangu ya kuzaliwa. Kumbukumbu zangu zimepotea toka siku niliyopata ajali... Hivyo nimepoteza uwezo wa kukumbuka vitu vyote vilivyopita.”
Majibu yake yalinifanya nishtuke sana. Maaana uso wake ulikua unamaanisha kile alichokua anakiongea.
“Mungu wangu... Ajali ya nini?” niliuliza kwa mshangao.
“nilipata ajali ya gari. Ni mimi pekee niliyepona kwenye ajali hiyo. Kwa taarifa za daktari wangu....wazazi wangu na ndugu zangu wawili walipoteza maisha hapo hapo. Nilikaa kwenye coma kwa miezi kadhaa... Na baada ya kurejewa na fahamu shida ikaanza kwenye uwezo wa kukumbuka. Natambua vitu ila sina uwezo wa kukumbuka vitu vilivyotokea nyuma yangu. Hivyo kumbukumbu zangu zitarejea taratibu kwa maelezo ya Daktari wangu.”
Hakika majibu ya Haiba yalizipooza hasira zangu na nafsi yangu kutawaliwa na huzuni kwa muda huo huo. Sikua nafahamu yote hayo, hivyo nikajikuta na mimi nakua mpole na kumsogelea karibu zaidi. Nilimkumbatia na Haiba akalipokea kumbatio langu.
“tunaweza kurudi ndani tukaongea kidogo?” ilinibidi nimuulize. Maana maelezo yake yalinisisimua na nilikua nayahitaji sana kwa ajili ya kazi yangu. Maana kisa chake nilitamani kuja kukiandika siku moja.
“sawa.”
Haiba alijibu na kufanya kile kitendo alichokiitikia, aligeuza njia na mimi nikamfuata na kuingia tena kwenye mgahawa huo.
“japo sijafanikiwa kukukumbuka.. Ila tunaweza kuwa marafiki tena kwa mara nyingine.” Haiba alifungua maongezi na kunifanya nitabasamu.
Maana mpaka hapo, nilikiri kua kweli nilishasahaulika na mrembo huyo. Japo si kwa matakwa yake, ni ajali ndo imesababisha. Hata hivyo nilimshukuru Mungu sikuona madhara yoyote mwilini mwake zaidi ya kupoteza kumbukumbu tu. Ilimradi ni mzima wa afya, na daktari amesema kua kumbukumbuu zake zitarudi, basi sikua na jambo lengine zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote.
Nilimpa mkono kuashiria kua nimekubali kuanza upya urafiki wetu.
“usiku wa leo napokea tuzo ya uandishi bora wa riwaya barani Afrika... Baada ya hapo, alfajiri na mapema ndege itakua inanisubiri kwa ajili ya safari yangu ya kurudi nyumbani kwetu nchini Tanzania.”
Niliamua kuongea maneno hayo na kumtazama usoni mrembo huyo. Dhumuni langu nilitaka ajue kua huenda urafiki wetu ukadumu kwa muda mfupi tu baada ya kujuana naye.
“hongera jamani kwa ushindi ulioupata.... Kumbe nina rafiki ambaye anafanya kazi ninayoipenda? Mimi napenda sana kusoma vitabu. Hasa vitabu vya riwaya za mapenzi na kijasusi. Natamani kusoma hiyo hadithi iliyokufanya ukashinda tuzo hiyo uliokuja kuichukua huku Marekani.”
Maneno ya Haiba yalinifanya nitabasamu na kumtazama usoni. Hakika niliweza kuibashiri furaha yake aliyokua nayo.
“bado sijakichapisha nakala ngumu. Ila naamini nikishachukua pesa za ushindi nitafanya hivyo. Ukibahatika basi utakipata kama vitauzwa hadi huku Marekani.” Nilimjibu hivyo na kufungua zipu ya begi langu na kutoa kipeperushi kilichokua kinaonyesha mahala ambapo tuzo hizo zitatolewa na kumkabidhi.
“hicho kitabu kinaitwaje?” Haiba aliniuliza wakati anapokea kile kipeperushi nilichompatia.
“SIKU 71.”
Nilimtajia jina la kitabu kilichoshinda tuzo na kumfanya afurahi.
“jina lake tu linatamanisha kujua kilichomo ndani. Hakika natamani kukisoma. Nikishindwa kukipata kwa nakala ngumu, Nitumie hata kwa email yangu mpya nilyofungua hivi karibuni.” Haiba aliongea maneno hayo na kunifanya nimzawadie tabasamu.
Hakika uzuri wa Haiba uliongezeka. Si ule wakitoto kama hapo awali. Hivi sasa alikatika hasa na nyonga zake zilitanuka. Kifua chake kilibetuka bila kushikiliwa na sidiria. Hivyo nilipata majibu kua bado hajazaa. Au kama kazaa, basi hajanyonyesha.
Niliyatoa mawazo yaliyoanza kuniingia baada ya kumuangala kwa muda mrembo aliyezitesa hisia zangu toka nilipomuona kwa mara ya kwanza.
Niliamini kua mlango wa mapenzi yangu kwake umeshafungwa. Maana mara ya mwisho aliniambia ana mtu wake na wanapendana sana. Na hivi sasa nimemkuta nchini Marekani. Huenda huyo mtu wake anaishi naye huku.
Mbaya zaidi ni vile hakumbuki chochote kuhusu mimi. Na mimi nimebakisha masaa kadhaa tu kuiaga Ardhi ya Marekani. Nilitikisa kichwa na kuyarudisha mawazo yangu kwenye kile kipeperushi nilichomkabidhi.
“nitafurahi kama nikikuona kwa sherehe hiyo.... Nafiri tiketi bado zinauzwa mpaka muda huu.” niliongea maneno hayo na kumuangalia Haiba usoni.
“nashukuru.... Ngoja ninunua tiketi online. Maana naona wameweka chaguo hilo pia.”
Haiba aliongea maneno hayo na kuchukua simu yake na kuanza kunakili namba zilizoandikwa kwenye kipeperushi hicho.
Baada ya muda aliniangalia na kutabsamu.
“nimefanikiwa kupata tiketi.... Hivyo nitakuwepo Molito.”
Maneno ya Haiba yalinifanya niwe na furaha.
Tuliagana na kila mmoja akashika njia yake. Mimi nilirudi kuendelea na manunuzi yangu na kurejea tena Hotelini kusubiri kufuatwa kama walivyo niahidi waandaaji wa tuzo hizo.
Masaa yalienda kwa kasi sana na hatimaye kiza kikatanda. Ilipotima saa tatu kamili, nilifuatwa Hotelini hapo na kupanda kwenye gari la kifahari. Kisha nikapelekwa kwenye ukumbi huo maridhawa.
Nilikutana na washindi mbalimbali wa riwaya na waandaaji wa filamu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
Maana tuzo hizo zilikua na vipengele vingi sana. Sio sisi tu waandishi wa hadithi, bali hata waongozaji wa filamu na wale waigizaji pia.
Katika vipengele vyote hivyo, ni mimi pekee ndiye niliyeiwakilisha nchi yangu ya Tanzania. Hakika nilijihisi ufahari kuibeba bendera hiyo kwa mikono yangu.
Kwakua lilikua ni jambo la heshima kwangu na kwa nchi yangu pia, na nilifahamu kua jambo hilo litasambaa kila mahali kupitia televisheni na mitandao, basi na mimi sikufanya ajizi kwenye upande wa mavazi. Nilivalia suti yangu safi ya rangi ya blue bahari yenye ufito mweusi uliozunguka shingoni mpaka kwenye usawa wa vifungo.
Ndani nilivalia neck pool na cheni ndogo iliyonifanya hata mimi mwenyewe kukiri kuwa nilikua nimependeza sana.
Muda ulipofika, tulikaa kwenye nafasi zetu na burudani zikaanza rasmi. Waimbaji waalikwa walianza kutumbuiza na baadae mshereheshaji alishika kipaza sauti na kuanza kuita watu watakaohusika na utoaji wa tuzo hizo.
“Mshindi wa kwanza wa Tuzo za waandishi wa Riwaya Afrika mwaka 2017/2018 ni .... Hussein Omary Molito.”
Zilisikika shangwe kutoka kila sehemu. Nami nilinyanuka na kuwapungia watu mkono na kwenda kuipokea tuzo yangu.
Niligeuka kuwatazama watu waliohudhuria na wanaonishangilia. Macho yangu yaliweza kumuona mtoto mrembo Haiba akiwa ni mmoja wapo.
Hakika nilifurahi. Maana hakunidanganya pindi aliponiahidi kua atakuja kwenye sherehe hizo za upokeaji wa tuzo.
Kwa kawaida kila anayepokea tuzo hizo anapewa nafasi ya kuongea mawili matatu. Hivyo nami nikasogea kwenye kipaza sauti ili niongee vile ninavyojisikia furaha kuipokea tuzo hiyo.
“Tanzania..oyeeeeeeee. Hakika shukurani za pekee zimuendee Muumba wangu kwa kunijaalia kipaji. Hakika si kwa ujanja wangu bali ni kwa neema zake jalia. Pili napenda kumshukuru Bibi yangu na dada yangu Fatuma. Hao watu ndio shabiki zangu wa kwanza kabisa kusema naweza na kunipa mawazo yao na kunifanya leo hii nimechagua fani ya uandishi kuwa fani yangu namba moja. Mama yangu Mungu akupe maisha marefu. Hakika najivunia kuwa na mama shabiki wa kile ninachokifanya. Na wote mlionipigia kura, nawapenda sana.”
Niliongea maneno hayo na makofi yakaripuka na shangwe kutoka kila sehemu. Macho yangu yakamtazama tena Haiba wangu. Dah! mtoto alikua anashangilia balaa. Nilitamani hata kumtaja. Ila hakua wangu na sikujua alikuja na nani. Huenda ningemuharibia. Hivyo kukaa kwangu kimya kuliokoa mengi kwa mawazo yangu.
Baada ya tukio hilo nilirejea kwenye nafasi yangu. Na baada ya kuisha kwa sherehe hizo. Nilienda kupiga picha na watu mbalimbali waliotaka kupata kumbukumbu na mimi. Na baadae nikafanikiwa kukutana na Haiba kwa mara nyingine na kupiga nye picha kadhaa.
“nimefurahi sana kukuona Haiba katika tukio hili adhimu kwangu.” niliongea maneno hayo ili kuweka hisia zangu wazi kwa msichana huyo apate kufahamu vile nilivyojisikia kwa kufika kwake.
Kauli yangu ilimfanya aone aibu kidogo na kuachia tabsamu. Hakika lilikua tabsamu lile lile la miaka nane iliyopita wakati tunakutana kwa mara ya kwanza. Ila ndiyo hivyo tu, mimi nakumbuka kila kitu ila mwenzang hakuna anachokikumbuka.
“hongera sana Molito kwa Tuzo.” Haiba aliongea maneno hayo na kuishika tuzo hiyo. Alisoma jina na kuniangalia.
“ Halafu sikudhani kama jina lako la mwanzo ni Hussein.”
maneno hayo yalinifanya na mimi nitabasamu.
“bila shaka ulidhani Molito ni jina la kubuni pia na si jina langu halisi.” nami nilijaribu kuingia kwenye mawazo yake ili nione kama nipo sahihi kwa kile alichokua anakiwaza toka tunaonana ile mchana.
“haswaaa... Maana halijakaa kibantu kama wewe ulivyojitambulisha na bendera uliyokuja nayo huku. Kuna watu kadhaa kutokea nchini Hispania ndio wanaitwa majina kama hayo. Milner, Molito na Milito.” Haiba aliendelea kulidadavua jina langu na kunifanya nitabasamu huku nikipata muda wa kumuangalia usoni. Hakika uzuri wa Haiba hauongopi. Licha ya kupita miaka mitano toka anipe majibu magumu yaliyo uadhibu moyo wangu kisawasawa, ila uteke wa sura yake ulibaki vile vile. Kilichoongezeka ni umbo tu na maziwa. Tena vimemfanya kila kilichokua kimejificha kwa ajili ya mwili wa utoto vitokee. Maana Haiba alijaaliwa shepu ya glasi ya kunywea mvinyo wa kigiriki.
“Molito ni jina la ukoo wangu kabisa. Hivyo wazazi wangu wakaniita tena jina hilo nami nimeamua kulibeba jina hilo mgongoni na kulipeleka kimataifa. Na najivunia kulitumia pia.” niliweka wazi hisia zangu kwenye jina langu na kumfanya Haiba acheke.
“kwa hiyo asubuhi ya leo unarudi Tanzania?” Haiba aliniuliza ili kuhakikisha kile kitu nilichomwambia mchana.
“ni alfajiri..ndege inaondoka saa kumi kamili. Hivyo nina masaa matatu tu yamebaki kabla ya kuiaga ardhi ya Marekani.”
Nilimjibu hivyo na kumfanya Haiba atabasamu.
“basi nipe namba zako ambazo unatumia whatsapp ili tuweze kuwasiliana kirahisi zaidi.”
Haiba alichukua simu yake na kunikabidhi baada ya kuitoa nywila. Nami niliichukua na kuandika namba zangu kwa usahihi kisha nikamrejeshea simu yake nikiwa nimeandika jina langu kwa herufi kubwa. ‘MOLITO’
“naomba nikuache. Maana hata mimi naishi mbali kidogo na mji huu. Ni mwendo wa dakika arobaini kwa Treni. Nimekuja hapa kama ambavyo nimekuahidi kua nitafika bila kukosa. Halafu kesho asubuhi na mapema natakiwa kuripoti ofisini. Hivyo nikutakie safari njema Molito. Nitakutafuta asubuhi au usiku huu huu pindi nitakapofika tu nyumbani. Usisahau kunitumia picha zetu pia” Haiba aliongea maneno hayo na kuondoka.
Nilishusha pumzi na kuendelea kumtupia macho binti huyo ambaye mwendo wake kama samaki atingishapo mkia wake. Nilitikisa kichwa changu na kutoka nje. Nilikuta kuna gari inanisubiri na kunirudisha Hotelini.
Japo nilirejeshwa Hotelini, lakini haikumaanisha nilitakiwa kulala. Maana yalisalia masaa mwili tu kabla ya kwenda uwanja wa ndege. Nilimuomba muhudumu anipige picha kadhaa kwa simu yangu nikiwa nimejifanya nimelala huku tuzo yangu ikiwa pembeni.
Hilo pozi nilikua nalitamani sana toka nilipokua naandika riwaya. Kwa Tanzania hua tunaliita pozi la taifa.
Basi baada ya kupigwa picha kadhaa. Kama ada yangu wala sikusubiri papambazuke, Nilipost kwenye mitandao yangu yote ya kijamii ninayoitumia na baadhi ya watu waliokua hewani muda huo walianza kubonyeza like kuashiria kua wameipenda hiyo picha na kutuma maoni yao kwangu yaliyojaa pongezi. Wengi wao walichukua picha zangu na kuanza kuisambaza na wengine kuipost kwenye mitandao yao mbalimbali.
Nilikumbuka maneno ya Haiba kua huenda akanitafuta akifika nyumbani. Niliwasha data ili nitumiwapo ujumbe niweze kuuona kwa haraka. Lakini sikupata ujumbe mpya wenye utambulisho wake mpaka naondoka hotelini hapo.
Safari ya kurudi nchini kwangu ilikua nzuri sana. Nashukuru Mungu tukio hilo la kuchukua Tuzo yangu ilichukuliwa kwa uzito mkubwa kiasi kwamba nilipofika tu uwanja wa ndege, nilipokelewa na waandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali licha ya ndugu zangu kufika uwanja wa ndege wa Mwalimu nyerere kunipokea kwa furaha.
Nilipokua chumbani kwangu. Niliwasha data na kujibu jumbe mbalimbali za watu wa kawaida na waandishi wenzangu waliokua wananipongeza. Nilifurahi sana kwakweli. Ila kidogo nilipata kunyong’onyea kwakua tu mpaka muda huo sikupata ujumbe wowote kutoka kwa Haiba.
Niliingia kwenye website ya waandaaji wa Tuzo. Niliweza kuona picha zetu mbalimbali. Na nilipoona zile picha tulizopiga mimi na Haiba, nilianza kuzipakua hizo kwanza kabla ya picha zote. Hakika zilikua picha nzuri sana.
“kumbe nilimshika kiuno...huyu mtoto, kiukweli kabisa. Bado nampnda hadi leo hii.” Niljisemea mwenyewe baada ya kuangalia picha hiyo kwa dakika zaidi ya kumi.
Kufumba na kufumbua, miezi miwili ikapita. Hakika iliniuma sana. Kuna wakati hua najihisi huzuni . Maana kwa kipindi chote hicho, Haiba hakunitafuta kwa njia yoyote ile toka nilipompatia namba yangu ya simu.
ITAENDELEA...............RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU
MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)
SIMU: 0718 97 56 59

ITAENDELEA...............
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: