RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU 09
RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU
MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)
SEHEMU 9
Niliamini juhudi zao za kutafuta muuaji wa Farahani zitafeli kwa Haiba ndio maana natoa ushirikiano mpaka mwisho ili hata wakishindwa kumnasa Haiba wasinigande mimi tena. Maana sina watu wengine ambao nina ukaribu nao huko Marekani zaidi yake.
“Molito.... Naomba nikuambie ukweli wa moyo wangu kabisa ili uniambie utanisaidia vipi tatizo langu.” Haiba aliongea maneno hayo baada ya kusikilizwa na muhudumu.
“kuwa huru kuongea chochote kile Haiba. Nakupenda na nipo tayari kukusaidia kama nitaweza kufanya hivyo.” nilimtoa wasiwasi Haiba na kumfanya ainamishe kichwa chini kisha akanitazama kwa mara nyingine.
“kwanza naomba unisamehe kwa kukuongopea.” Haiba aliongea maneno hayo na kuniangalia machoni.
“kipi hicho ulichoniongopea?” nilimuuliza na kukaa vizuri.
“toka siku ya kwanza kuonana na wewe huku Marekani, nilikua nikikuaminisha kua mimi nilipata ajali na kupoteza kumbukumbu zangu. iIa ukweli ni kwamba sikupata ajali na ninakumbuka kila kitu.”
Haiba aliongea maneno hayo na kunifanya nipigwe na bumbuwazi. Maana sikudhani kama hila zote alizokua ananifanyia alikua na kumbukumbu zake na alikua ananifahamu fika mimi ni nani kwake. Kwakua nilikua nina kazi nyingine ya ziada ya kuwasaidia polisi, niliweza kujizuia ile hali ya hasira ya kudanganywa na kubaki namtazama tu.
“ndio maana nikaamua kutanguliza kukuomba radhi kwanza kwakua nilikua nafahamu nitakukwaza. Kwa sasa nimefungua moyo wangu kwako na nimeamua kukupenda kwa dhati kabisa. Ila mwenzako nipo kwenye matatizo makubwa na nahitaji zaidi masaada wako ili niweze kufika nyumbani kwetu Tanzania.” Haiba aliongea maneno hayo na kunifanya nishushe pumzi ndefu.
“nakusikiliza.”
Kauli hiyo nilisiindikiza kwa kumkazia macho kisawasawa na kumfanya Haiba anitazame na kuinamisha kichwa chini.
“toka tulipoongea kwenye simu ile mara ya mwisho.... Nilikaa kwa muda wa miezi sita na ndipo nikaolewa na yule mpenzi wangu niliyekuambia kua nampenda kuliko wewe. Molito, Najutia maamuzi yangu ya kuolewa na mtu ambae sikua najua nia na madhumuni yake kwangu .... Hakika ameyabadili maisha yangu na kuvuruga mwenendo wake mzima..” Haiba aliongea maneno hayo na muda huo huo akaanza kulia.
Nilichukua jukumu la kumbembeleza na baada ya kurejea katika hali ya kawaida. Ndipo aliponihadithia mkasa mzima uliomkuta.
***************
Sherehe na shamrashamra zilitanda kila mahali. Wazazi wangu walifurahi sana baada ya mtoto wao kujitunza hadi kufikia kuolewa.
Baada harusi kuisha, tuliondoka nyumbani kwenda kuanza maisha mapya na mume wangu ambaye alikua anaishi magomeni.
Hakika mwanzoni mapenzi yetu yalikua matamu mfano hakuna. Nitake nini mimi nisiletewe. Hadi ikafikia wakati nikaanza kunenepa na kujisikia furaha ya kuwa na mume bora kama yeye.
Miezi ilienda na hatimae nilishika ujauzito. Ila kwa bahati mbaya mimba hiyo ilitoka ikiwa na miezi minne. Ndipo daktari aliposema kua nahitaji utulivu wa kutosha na ikiwezekana nisifanye kazi kabisa pindi nitakapopata ujauzito mwengine.
Tulikaa kwa muda wa miezi sita mengine, ndipo niliposhika tena ujauzito. Kiukweli mume wangu alijitahidi sana kuuliinda huo ujauzito ili mradi tuweze kupata mtoto. Maana kiu yetu kubwa ilikua ni kupata mtoto mapema.
Baada ya mimba kufikisha miezi sita, ndipo nilipopokea taarifa zilizonishtua sana. Taarifa ya ajali mbaya ya gari ambayo ilikua inaendeshwa na baba yangu.
Kwenye gari hiyo ya familia, hakuna hata mtu mmoja aliyepona. Hivyo nilipoteza familia yangu yote.
Kwa mshtuko wa tukio hilo, nilipoteza na kiumbe kilichopo tumboni. Hakika ni pigo ambalo siwezi kulisahau kwenye maisha yangu.
Nilikabidhiwa mali zote kama mtoto pekee niliyebaki. Nami nikamteua mume wangu mpenzi kuwa msimamizi wa mali zetu. Maana nilijua yeye ndiye familia yangu iliyobaki wa kufa na kuzikana. Kumbe hio lilikua kosa kubwa sana kwenye maisha yangu.
Mume wangu alinishauri tuuze mali zilizoachwa na wazazi wangu waliotangulia mbele za haki kwakua kuna mradi alikua anahitaji kuuanzisha kwa manufaa ya kizazi chetu.
nilikubali na nikatia sahihi ya kuuzwa kila kitu nilichomiliki, tukapata pesa nyingi sana.
Ndipo siku moja nilipokua natoka sokoni, niliweza kuwaona watu wakiwa nje wananisubiri. Maana mlango niliufunga wakati natoka. Mume wangu alikua safarini yapata mwezi mmoja.
Wale watu walijitambulisha kama wamiliki halali wa nyumba ile na kila kitu kilichokua ndani. Nilihisi wamechanganyikiwa. iIa waliponionyesha hati miliki ya nyumba ile, nilichoka.
Nilihisi huenda Mume wangu alirogwa au alilazimishwa kusaini ile hati. Nilichukua simu yangu na kumpigia. Lakini simu yake haikupatikana. Ndipo dalali aliponieleza maneno yaliozidi kunishangaza.
“mama, mume wako kwa sasa yupo Marekani. Na yeye ndiye aliyetuagiza tukumalizie kiasi kilichobaki ili uweze kutoka kwenye nyumba hiii uende kupanga. Yeye atarudi baada ya mwezi mmoja.”
Yule dalali alinipatia pesa. Nilizihesabu, zilikua kiasi cha shilingi milioni moja na nusu.
Kwakua mume wangu alikua hapatikani kwenye simu, niliwaomba wanipe wiki mbili ili niweze kutafuta nyumba ya kuishi na kuhama kwenye nyumba hiyo.
Walinikubalia na kuondoka. Hakika nilikua naona kama ni ndoto vile. Hatimaye wiki mbili zikapita na wenye nyumba wakafika.
Sina budi, niliamua kuwapisha kwenye nyumba hiyo na kuanza maisha mapya. Nilichukua chumba cha hotel kwanza wakati natafuta chumba cha kuishi na kununua vitu vya ndani.
Miezi mitatu baadae ile pesa iliisha, na ndipo ugumu wa maisha ukaniembelea. Mali zangu zote nilitapeliwa na mume wangu niliyempenda na kumuamini.
Nilianza kuishi maisha ya shida wakati sikuzoea shida, nilianza kuishi maisha ya kuwa na wanaume wengi ili niweze kujikimu kimaisha.
Roho iliniuma sana naniliamini ipo siku nitakuja kuzirejesha mali zangu kwa njia yoyote ile.
Siku zilisonga mbele, ndipo nilipokuja kuona kwenye mtandao picha za mume wangu msaliti akiwa kwenye suti na mwanamke wa kimarekani akiwa kwenye shela wakesheherekea harusi yao. Ni dhahiri alikua haniwazi tena na wala hajali mimi nitaishi maisha gani baada ya yeye kunidhulumu mali zangu na kutokomea ughaiuni. Hiyo ndio sababu iliyomfanya aoe kabisa mke mwengine. Tena si kuoa tu, bali amekua mfanya biashara mkubwa tu huko Marekani na anatambulika kabisa baada ya kuweka hisa kadhaa kwenye mashirika mbalimbali.
Taarifa nilizozipata ni kwamba, huyo mwanamke aliyemuoa naye kwao ni matajiri. Ila hata hivyo pesa zao zingine wamezipata baada ya kudhukumu mali zangu na za kampuni aliyokua anafanya kazi hapo awali. Hapo ndipo nilipopata hasira ya kisasi na kunifanya niwe nalia kila siku.
Kuna siku nilikua nataka kujiua kwa kujitumbukiza kwenye maji ya kina kirefu baada ya maisha kunipiga fimbo huku nikiwa sina msaada wowote. Maana kila aliyenisogelea alikua anataka kunitumia kwa shida zake za kimwili tu na si kunisaidia kunitoa kwenye dimbwi la mawazo nililoangukia. Ndipo mama mmoja wa makamo aliponiokoa kwa kunizua nisifanye hivyo.
Ni raia wa Marekani. Hivyo baada ya kufanikiwa kunizuia, alitaka kujia kwanini nilitaka kuhatarisha maisha yangu. Nilimuelezea kisa na mkasa. Akaniambia kujiua sio suluhu ya tatizo langu. Ila nahitaji kulipa kisasi ili niwe na amani.
Yule mama alinisaidia na kunipeleka nyumbani kwake. Alinipatia fedha za kutafuta passport nikafanikiwa kuipata. Baada ya hapo yule mama akaniambia atanisaidia kwa hali na mali mpaka nifanikiwe kuzipata mali zangu au kulipiza kisasi kwa mwanaume huyo aliyeniharibia maisha yangu.
Baada ya kukamilisha taratibu zote, Nilisafiri naye kutoka Tanzania hadi nchini Marekani na kwenda kuishi naye Philadelphia kwenye ile nyumba uliyonikuta.
Niliishi pale kwa muda wa mwezi mmoja na ndipo siku moja aliponipeleka kwenye moja ya sehemu zake anazofania kazi.
Hakika nilipigwa na butwaa baada ya kuona sehemu hiyo ina silaha nyingi sana huku kuna baadhi ya watu wake kwa waume wakizitumia silaha hizo kulengea shabaha.
“mimi si mtu wa kawaida kama muonekano wangu ulivyo. Mimi ni Mafia. Hua sina huruma na washenzi washenzi kama huyo mvulana aliyekua mume wako. Hivyo unatakiwa ujifunze kutumia hizi silaha kwa ajili tu ya kufanya kazi zangu na kazi zako hapo baadaye ya kuzikomboa mali zako na kumkomesha huyo mume wako.” yule mama aliongea kauli hiyo iliyonifanya nibaki kimya tu nikimtazama.
Siku zilipita na mimi nikawa najifunza taratibu. Na baadaye nikaweza kutumia silaha hizo. Nilifahamu jinsi ya kuzibomoa na kuziunda tena. Ndipo nilipoingia kazini rasmi kumsaidia mama huyo mlezi wetu kazi zake za uporaji kwa kutumia silaha za moto.
Kwakua wasichana tulikua watatu pakee kwenye kundi letu. Yule mama alitubatiza jina na kutuita Tai watatu.
Hakika tulifana kazi nyingi na yule mama alitulipa vizuri huku akituhakikishia ulinzi madhubuti kutokana na uimara wa watu wake wa kazi.
Njia pekee aliyotuambia kua itatufanya tuishi bila kukamatwa ni kuwa mbali na watu wengine tofauti na sisi wenyewe. Yaani tusijenge urafiki na watu wengine. Na hata tukihitaji kuwa na mahusiano ya kimapenzi basi tuchague wanaume wa pale pale kambini.
Kwangu mimi sikua na shida ya mwanaume kwakua nilikua nimeshaumizwa. Nilikua na shida ya kulipiza kisasi tu. Tena huyo mwanaume alivyozidi kufanikiwa na kutangazwa ndipo nilipozidi kupandwa na hasira.
Niliambiwa na mama nisiwa na haraka naye. Nahitajika kukomaa roho ili nisiwe na huruma kabisa. Aliniambia nikae kwa muda wa miaka mitatu ndipo nifanye maamumuzi ya kulipiza kisasi.
Mwaka jana, yule mama aliugua na miezi sita baadae akafariki. Hivyo tukabaki tunajiendesha wenyewe na ujambazi ukawa ndio kazi yetu.
Kama alivyosema mama pindi aliponipangia muda wa kuiva kiroho mbaya na kuwa tayari kulipiza kisasi ni miaka mitatu, kadrii muda ulivozidi kwenda ndipo huruma ikawa inazidi kupotea kwenye moyo wangu. Maana mpaka muda huo sikuona ajabu kufanya kitu chochote, wakati wowote na kwa mtu yeote. Maana kama kuua tu nillishaua sana. Na ikafikia kipindi niliua hadi watoto wadogo pindi wazazi wao wanapokua wabishi kutoa pesa.
Siku moja baada ya kutoka kufanya tukio,ndipo uliponiona na kunifuata. Nilikukumbuka ila sikutaka unizoee kwakua mimi si Haiba wako wa kule Tanzania. Nilikua Haiba mwengine ambaye angeweza kuyateketeza maisha yako pindi tu ungeweza kuaona mauaji niliyoafanya siku hiyo.
Ndio sababu ya kunifanya nijifanye nimekusahau huku upande mwengine roho ikaniuma kwanini sikukuchagua wewe uliyeonyesha kunipenda toka ukiwa huna kitu mpaka ulipofanikiwa.
Nilipoiona familia yako, roho iliniuma sana. Nilitamani hata mie ningekua na familia yangu na kuishi kwa upendo kuliko haya maisha mengine ya kimafia niliyochaguliwa kuishi na mume wangu wa zamani.
Siku tuliyo panga kufanya mauaji kwa mfanyabiashara Farahan ambaye ndiye alikua mume wangu aliyenidhulumu mali, tuliweza kumuona akiwa na wewe kule hotelini. Ndipo tuliposhauriana sisi Tai watatu kua tukufuatilie ili tuone ukaribu wenu upoje. Ndipo tulipoweza kupajua ni wapi anapoishi na familia yake yote tukaweza kuiona. Hasira iliyonishika nilitamani kuwaua wote kuanzia yeye,mke wake, hadi kizazi chake. Lakini roho nyingine iliniambia kua kwa sasa nahitaji kumuua yeye tu ili niwe na amani. Kama ni pesa ninazo na ninao uwezo wa kupora na kufanikiwa kuzipita pesa kama zake kwa masaa matatu tu. Ila yeye mwenyewe ndiye hastahili kuwa hai.
Siku uliyoondoka, ndiyo siku tuliyovamia nyumbani kwake na kumfunga kitambaa mke wake. Tulimpiga sindano ya usingizi na ndipo tulipomshurutisha Farhani aeleze pesa zake zipo wapi.
Akatupa na namba ya siri ya kadi ya benki na kadi yenyewe. Alituomba tuchukue mali zote ila tumuachie uhai wake na familia yake.
Nilijitoa kitambaa kilichoziba uso wangu, li aweze kuniona. Alishtuka sana, hakuamini kama Haiba yule mpole asiyeweza kuongea. Haiba aliyempenda kwa dhati na kumnyanyasa atakavyo akiishia kulia tu ndiye huyo aliyekua mbele yake aliyeshika bastola kwa nia ya kuyaondoa maisha yake.
Alipiga magoti na kuniomba msamaha. Watoto wake walikua wamewekwa chini ya ulinzi wakilia tu. Huku yule mtoto mdogo akilia bila kuelewa kitu chochote kilichokua kinaendelea muda huo.
Sauti za watoto wake hazikunifanya nishindwe kufyatua risasi na kumuua Farhani.
Hivyo nilikua nimeiva na kufikia kiwango ambacho sikua na huruma hata kidogo.
Kazi iliyonileta Marekani nimeimaliza na fukuto la kutafutwa kwa wauaji linaendelea kila kona. Sina wasiwasi wa kukamatwa, ila kuja kwako naamini nitaondoka salama huku Marekani na naweza kusahau kila kitu na kuwa mtu mwema tena.
Maana ile amani niliyokua naitaka nimeipata. Ingawaje kwa sasa nina hofu tena. Hofu iliyotengenezwa na penzi nililokatazwa kushiriki na mama.
Japo tayari una mtu mwengine, ila naamini mimi nilikua wa kwanza na utanipenda tu zaidi ya mwanzo. Ndio maana nikakwambia naomba unisaidie.
**************
Hadithi ya Haiba ilinisisimua mwili kwelikweli. Hakika niliona kabisa kua alikua kwenye mateso makubwa. Ila kilicho nisononesha ni kwamba mimi sio msaada wake tena. Bali nilikua kwenye hatua za kumkamatisha. Niliumia sana moyoni lakini sikua na jinsi.
“pole sana Haiba kwa yaliyokukuta. Nina imani nitakua mwema kwako na sitakupotezea furaha yako kama huyo mume wako wa zamani... Farahani.”niliongea maneno hayo na kumfanya Haiba atabasamu.
Aliangaza kulia na kushoto. Hakukua na mtu karibu yetu. Wahudumu walikua mbali kidogo na mahala ambapo siye tumekaa. Alitazama dirishani, hakukua na mtu anayepita. Maana pale tulipokaa palikua karibu na kioo kikubwa kilichotenganisha watu wapitao nje na siye tuliopo ndani.
Aliingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa bastola ndogo. Nilipatwa na mshtuko baada ya kuona ameielekezea kwangu.
“pole kwa kujiingiza kwenye mikono yangu Molito. Nimeshajua wewe ni nani na hivi sasa unajua kila kitu kuhusu mimi. Hustahili kubaki hai.”
haiba aliongea maneno hayo na kunifanya nianze kutetemeka.
“lakini....”
Niliitaka nijitetee, nilikatishwa kauli na Haiba.
“nyamaza.... Hiki ni kitu gani?” Haiba aliuliza na kukitoa kifaa cha kurekodia kilichopo kwenye ukingo wa shati langu.
“wewe ni mtu hatari sana. Toka mwanzo nilikushtukia ila sikua makini. Sasa tutasafiri wote au tutakufa wote. Ila huwezi kunichoma halafu ukaondoka kwenye nchi hii salama.” Haiba aliongea kauli hiyo baada ya kukichukua kile kifaa na kukivunja.
“tuondoke.”
Alichukua gazeti na kufunika mkono wake ulioshika bastola na kuniamuru niongoze njiakutoka nje.
Alichukua usafiri wa kukodi na kutupeleka hadi nyumbani kwake.
Tulitumia masaa takribani manne kwa usafiri huo na kunigharimu pesa nyingi za kumlipa dereva huyo. Kwakua sikutembea na pesa cash, Ilinibidi niende kutoa pesa kwenye kadi yangu na kumlipa dereva huyo pesa yake.
Tulifika ndani na kufungua mlango. Humo ndani kulikua kimya sana. Aliniamuru nikae kwenye kiti kisha na yeye akachukua pingu na kunifunga kwenye kiti hicho.
“tutakaa hapa mpaka muda wa kuondoka. Endapo tutavamiwa na askari basi ujue na wewe ndio mwisho wa uhai wako.” Haiba aliongea maneno hayo na kunifanya niwe mpole ili asibadili maamuzi na kuniua muda huo.
Kuna kifaa kimoja kiichokua ndani kidogo ya kufungo changu cha shati hakuweza kukiona. Hiko kifaa kilikua na uwezo wa kutambua popote niendapo. Hivyo nusu saa baadae tulishtushwa na sauti iliyotoka kwenye kipaza sauti.
“Haiba tunakuomba umuachie huru huyo kijana na wewe utoke nje na ujisalimishe.”
Sauti hiyo ilimfanya Haiba achukue bastola yake na kuchungulia kwenye dirisha na kuwaona askari waliozunguka jengo hilo.
“nilikuambia kua iwapo tutavamiwa na askari kabla muda wa kuondoka kufika nitautoa uhai wako.... Swali swala yako ya mwisho kabla sijachukua maamuzi niliyoamua kuyafana muda huu kwenye mwili kwako.” Haiba aliongea na kuninyooshea bastola na kuniweka kwenye usawa wa paji langu la uso.
“Tunawaomba mtoke ndani wenyewe kabla nguvu ya dola haijaanza kutumika.” sauti nyingine ya kipaza ilitushtua na kumfanya Haiba achanganyikiwe.
“Kwa heri Molito.”
Haiba aliongea kauli hiyo na kuona kabisa anataka kubonyeza kifyatulio cha bastola ili aweze kuusambaratisha ubongo wangu. Nilifumba macho kujaribu kukwepa kuliona tukio hilo linalotokea kwenye uso wangu.
Ndipo risasi ilipopenya kwa ustadi mkubwa na kuupiga mkono wa Haiba uliomfanya aachie bastola yake na kuanguka chini.
Muda huo huo askari waliingia ndani ya jengo hilo na kumuweka Haiba chini ya ulinzi.
Alice alifika na kuchukua kitu mfano wa kipini na kufungua ile pingu niliyofungwa kwenye kiti.
Haiba alinitazama kwa jicho kali la lawama juu yangu. Hata mimi nilijisikia vibaya sana kwa kuona mwanamke nimpendaye akiishia jela kwa kesi ya mauaji.
“pole sana Molito. Cha msingi umshukuru Mungu wako kwa kuweza kuipenyesha risasi yangu vyema na kufanikiwa kukuokoa. Maana kivyovyote vile Haiba alidhamiria kukuua.” Alice aliongea maneno yalionifanya niweze kumjua ni nani aliyefanya shambulio hilo la mwisho kwa Haiba na kuokoa maisha yangu.
“Ahsante sana Alice.” Nilimshukuru na kumfana Alice anikonyeze huku akitabsaamu.
Tulitoka nje na kuweza kuwaona wale rafiki zake Haiba pamoja na mabwana zao wakiwa chini ya ulinzi. Wote walionekana kunyong’onyea kama ishara ya kukosa msaada.
Baada ya kukamilika kwa kukamatwa watu waliohusika na mauji ya Farahani. Niliruhusiwa rasmi kuendelea na shughulii zangu ama kuondoka nchini humo.
Kiukweli sikuweza kuondoka. Niliomba ruhusa ya kwenda kumuona Haiba na kuongea nae.
“kila kitu kina mwisho. Naamini kile kilichokufanya ujitoe kafara umeshakitimiza. Hata mimi sikuamini kama wewe unaweza kuhusika mpaka siku ya mwisho uliponihadithia. Nilikua chini ya ulinzi toka awali na njia pekee ya kujinasua ni kutafuta muuaji halisi wa Farahani. Nimeumia sana baada ya kugundua muuaji mwenyewe ni wewe kipenzi changu. kukupoteza Haiba.” niliongea maneno hayo huku moyo wangu ukimaanisha nikisemacho. Hakika kitendo cha kukamatwa kwa Haiba tena kupitia mgongo wangu mimi, kumeniumiza sana.
Siku iliyofuata Haiba na wenzake walipelekwa mahakamani na kusomewa mashitaka ishirini na mbili ya mauaji na unyang’anyi. Hivyo kesi kuhairishwa baada ya watuhumiwa wote kukana mashtaka hayo.
Niliamua kubaki nchini Marekani mpaka tarehe tajwa ya watuhumiwa hao kurudi mahakamani.
Siku hiyo kulikua na ushahidi wa kutosha. Hali iliyowafanya washindwe kuruka na kuhukumiwa kwenda jela miaka thelathini kila mmoja.
Niliweza kumshuhudia Haiba wangu akilia baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka hiyo jela. Hakika hata mimi ilinichoma lakini sikua na jinsi. Maana kwa kesi iliyokua inamkabili, nilijua atahuumiwa kwenda jela maisha yake yote .
Niliamua kurudi nyumbani Tanzania kimya kimya bila kumtaarifu mtu yeyote. Nilifika saa tano usiku na kuchukua usafiri wa kukodi hadi nyumbani kwangu.
Nilifunguliwa na mlinzi wa getini na kuingia ndani. Kwa ukimya uliopo, nilijua wazi kua mke wangu ameshalala muda huo.
Niliangalia saa iliyokua mkononi mwangu. Niliona muda muda ulikua umeyoyoma sana. Ilikaribia saa sita na nusu. Nilichukua simu yangu na kumpigia mpenzi wangu.
“mume wangu!”
niliweza kuuhisi mshtuko mkubwa baada ya mke wangu kupokea simu yangu. Ilikua ni matarajio yangu tukio hilo kutokea kutokana na kutowasiliana naye muda mrefu sana. Kipindi chote nilichokua kwenye matatizo basi nilisitisha mawasilino yake kwangu.
Hivyo kumpigia tena kwa namba ya nyumbani,ilimfanya apatwe na mshtuko.
“nipo nje mke wangu..njoo unifungulie mlango.” baada ya kumaliza kuongea sentensi hiyo. Niliweza kuzihisi hatua za haraka zikikimbilia mlango na kuufungua.
Nilipokelewa kwa kumbatio mwanana na mabusu maridhawa na kunifanya na mimi nilipize.
Nilipokelewa mzigo na kusindikizwa chumbani kama sipajui vile.
Nilichojolewa nguo na kwenda bafuni kuupooza joto mwili na maji yaliyo kati na kati, si baridi wala ya moto na baada ya hapo tukatoka hadi kwenye meza ya chakula.
Japokua hakukua na hesabu yangu hapo nyumbani siku hiyo, ila kulikua na chakula cha kutosha hata kama ningeenda na wageni wengine wawili.
Baada ya kupata chakula nikarudishwa chumbani na kupewa pole za safari. Niliamua kuficha yaliyonisibu huko kutokana na uzito wake.
Ila nilimwambia tu wale wazungu walikua matapeli. Hivyo nilisumbuana nao sana mahakamani na nilizuiwa kutoka huko wala kuwasilina na simu nje ya mipaka ya Marekani.
Nilipewa pole kwa majanga yaliyonikuta. Ndipo nilipomuona mtoto akisaula nguo na kubaki na nguo za ndani laini.
Ule usemi kua wanaume watachoka vitu vyote lakini sio tendo. Ulijidhihirisha siku hiyo. Maana hata sijui uchovu wa safari ulipokimbilia. Na kwakua ni muda mrefu umepita sikupata chakula cha nafsi na roho. Basi nilikula mpaka nikavimbiwa.
Asubuhi palipo pambazuka. Niliamka na kwenda kujimwagia maji. baada ya hapo nilitoka nje ya chumba kuelekea sebuleni.
“babaaaaaaa!”
Nilishtushwa na sauti ya mwanangu mpendwa. Alinikimbilia na kunikumbatia.
Nilikumbuka nilimletea zawadi kadhaa kutoka nchini Marekani. Hivyo sikutaka furaha ya kuniona ipoe. Nilimuambia mke wangu alete begi nililobeba vitu vyake tu na kumkabidhi yale maroboti na kuiona kabisa furaha yake ikizidi maradufu.
Mchana wa siku hiyo, niljikuta nina hamu tu ya kutembelea maeneo ya Kigogo nilipokua nafanya kazi ya kukodisha DVD miaka kadhaa iliyopita.
Nilitumia gari yangu yenye vioo vyenye giza kali na kupita maeneo hayo.Hakukua na mabadiliko makubwa sana. Hivyo mitaa yote niliona inafanana tu na ile mitaa ya miaka tisa iliyopita.
Niliweza kuiona ile fremu yangu ikiwa na maandishi yale yale niliyoaandika mimi kipindi kile nilipopewa oda na bosi wangu Al - hadad.
Nilipitiliza hadi nyumbani kwa kina Haiba. Niliweza kuiangalia nyumba hiyo kwa muda mrefu kidogo. Hakika kuna kitu kilikuja kunichoma na kunifanya nianze kutokwa na machonzi kutokana na uchungu nilioupata. Niliamua kuondoka na kurudi zangu nyumbani. Hakika mzimu wa Haiba uligoma kabisa kunitoka kichwani mwangu.
ITAENDELEA....................RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU
MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)
SIMU: 0718 97 56 59

ITAENDELEA....................
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: