RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU 10 (Mwisho)






RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU

MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)


SEHEMU YA 10 (na ya MWISHO)

    Nilipitiliza hadi nyumbani kwa kina Haiba. Niliweza kuiangalia nyumba hiyo kwa muda mrefu kidogo. Hakika kuna kitu kilikuja kunichoma na kunifanya nianze kutokwa na machonzi kutokana na uchungu nilioupata. Niliamua kuondoka na kurudi zangu nyumbani. Hakika mzimu wa Haiba uligoma kabisa kunitoka kichwani mwangu.

   Kwakua watu walikua na kiu ya kusoma riwaya zangu baada ya ukimya wangu wa muda mrefu, Niliona sio mbaya kuandika hadithi fupi  kuhusu maisha yangu mimi na kipenzi changu Haiba. Riwaya ambayo naamini mwisho wake hakuna atakaye utarajia kama Haiba atakuja kuwa kiumbe mwengine kabisa kwa upole wake aliokuanao awali wakati nakutana naye.

  Mwisho wa siku ndio hivyo. Ameingia kwenye kina kirefu cha penzi kilichomfanya abadili mfumo wake wa maisha kutoka kua mtu mwema mpaka muuaji wa kutupwa asiye na huruma hata chembe. Amefanikiwa kulipiza kisasi kwa mtu aliyemfanyia ubaya na yeye hivi sasa anatumikia adhabu kali nchini Marekani kwa makosa yake ya mauaji aliyoyafanya nchini humo.

   Hakikua kitabu kirefu kama vile ninavyo viandika kutokana na ufinyu wa hadithi yenyewe na vile tulipotezana muda mrefu. Ila niliamini kwakua kina ukweli wa maisha yangu halisi ndani yake, basi Watu watakipokea na watavutiwa nacho kama si kuhuzunika pamoja na mimi muhusika mkuu wa hadithi hiyo.

   Nilikichapisha kitabu hicho na kukiingiza sokoni kwa bei rahisi kabisa. Niliweka bei ambayo naamini kila mpenda kusoma basi hatojifikiria mara mbili kukinunua kitabu hicho.

   Kwakua nilikua na pesa za kutosha na jina pia, hivyo haikua kazi kubwa kukichapisha na kupata mawakala wa kunisambazia kazi yangu hapa nchini na nje ya nchi pia.

   Tenda nyingine kutoka kwa wasambazaji wa nchini Marekani ilinifikia. Nilisafri hadi nchini Marekani baada ya kuhitajika kwenda kufanya mahojiano na kituo kikubwa cha televisheni.
Baada ya mahojiano hayo. Nilipata muda wa kukinadi kitabu changu. 
Hata humo napo mauzo yalienda vizuri sana.

   Kiukweli nisingeweza kurudi nyumbani bila kwenda gerezani kumtembelea Haiba. Nilifanya hivyo na ndipo nikapata habari zilizo nihuzunisha sana.
   “kwa sasa ni mgonjwa sana. Yupo hospitalini anapatiwa matibabu.”
Majibu hayo yalinifanyaa niombe ridhaa ya kwenda kumuona. Baada ya kufuata taratibu zote niliruhusiwa kwenda kumuona Haiba wangu.

Dah!
   hakika nilistaajabu sana nilipomuona. Hakua haiba yule Kisura niliyezuzuka naye. Alikua amekonda sana na mwene rangi ya manjano isiyopendeza kabisa.
Mikono yake iliyokonda ilikua kwenye adha isiyosimulika. Mkono wake kushoto ulikua ukipokea dripu ya maji na mkono wake wa kulia ulikua kwenye pingu iliyofungwa kwenye kitanda hicho huku askari wawili wakimlinda kwa silaha za moto.

   Nilifika na kulitaja jina lake. Aligeuka na kuniona. Kwa mara ya kwanza niliweza kuona tabasamu lake.

   Nadhani alifurahi baada ya kuniona nimefika hospitali kumjulia hali baada ya kupotezana nae kwa muda mrefu.

   Nilihisi  bado ana kinyongo na mimi. Nilipatwa na shauku ya kumuomba msamaha kwa yote yaliyotokea hadi kukamatwa kwake.
   “haiba...” nilitaka kuongea, lakini alinikata kauli.
   “umetoa ... Kitabu... Kipya?” Aliniuliza swali hilo kwa tabu sana.
Nami harakaharaka nilitoa kitabu kilichokua na sura zetu kwenye jalada na kumuonyesha.

   Alishangaa sana kuona kitabu hicho kikiwa na picha mojawapo kati ya zile tulizopiga siku ya utoaji tuzo. Hakika hiyo picha ilituonyesha tukiwa tumekumbatiana huku wote wawili tukiwa tumejawa furaha sana. Mbunifu wa jalada Frank Mansai aliifanya kazi yake sawasawa kulifanya jalada la kitabu hicho kuvutia sana.

   “nisomee ....hi...ki kit.....tabu.”  Haiba aliongea, Nami bila hiyana nilikifungua kitabu hicho na kuanza kusoma ukurasa wa kwanza mpaka wa pale tulipoonana mara ya kwanza nchini Marekani.
“basi...”
Haiba alinizuia kukisoma kitabu hicho na kuanza kulia. Alianza kukohoa sana hadi daktari akafika na kuniamuru nitoke nje. Nlijikuta na mimi nikianza kulia kwenye benchi. 

   Kiukweli nilisoma kwa hisia na kila nisomapo nilikua nakumbuka hatua zetu tulizopitia. Hali iliyonifanya nizidi kulia kila mara.

   Hali ya Haiba ilizidi kuwa mbaya na kushuhudia akitolewa kwenye kile chumba na kupelekwakwenye chumba cha wagonjwa mahututi.Huko nilizuiwa kwenda na kushauriwa nisubiri nje.

   Nilikaa hapo kwa masaa matatu zaidi. Ndipo nilishuhudia madaktari wakitoka huku nyuso zao zikionyesha hazina furaha. 
  
   Dakika moja baadae nikaona kitanda kinavutwa huku muhusika akiwa amefunikwa shuka la kijani. Akili ilinituma niwahi na kuwaomba wale manesi wanaovuta hiko kitanda nifunue ili nione mtu aliyefunikwa. 

   Kabla sijaruhusiwa kufunua. Haraka nilifunua na kukutana na kile nilichokua nakihisi.
Ulikua ni mwili wa Haiba. Ubaridi wa ngozi yake niliyoishika ilikua ni tafsiri tosha kua hayupo hai tena. Niliishiwa nguvu na kukaa chini huku mmachozi akinibubujika.
   “leo ndio mwisho wa kumuona Haiba wangu?”
Nilijiuliza na jibu lilikua kwenye kile kitanda kilichokua kinapelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
Illinibidi nikubali matokeo. Na njia pekee iliyobakia ni kuomba ridhaa ya kwenda kuzika. 
Baada ya kufuata taratibu zote. Niliruhusiwa kupewa maiti na kurudi nayo nchini Tanzania.
Kilikua kitendo cha ajabu kutokea na waandishi wa habari waliozipata taarifa kua narudi na Maiti nchini, walifika nakutaka kunihoji. Lakini sikua tayari kuongea kwa kipindi hiko.

   Hata familia yangu ilishtuka sana baada ya kuona nimechukua jukumu la kusafiri na maiti kutoka nchini Marekani na kuja kuizika huku kwetu na wakati si mmoja wa familia yetu. 

   Hakika niliweza kuwaeleza kisa na mkasa kilichotokea. Mama yangu alikua mtu wa kwanza kunielewa. Ndipo baba na ndugu zangu wengine wakashauri msiba ufanyike nyumbani kwetu Kinyamwezi.

Mpenzi wangu hakua na lakuongea zaidi ya kukubali maandiko yatimie. 
   “Kila mtu ana haki ya kuzikwa kistaarabu na si kutupwa na askari wa jiji.”
Hayo yalikua maneno yake ya kishujaa yaliyonifanya niamini kua kweli hivi sasa mpenzi wangu amekua.

   Hakika msiba huo ni moja ya misiba iliyoniuma sana na kulia waziwazi kama mtoto. 
Mbele ya familia yangu msiba ulionekana kabisa kunigusa kuliko misiba yote iliyotokea.

   Baada ya siku tatu. Ndipo nilipoweza kuita waandishi wa habari na kuwaelezea mkasa mzima.
   “kile kitabu cha MOLITO ‘penzi langu linavuja damu.’ Ni hadithi ya kweli isiyo na chembe ya uongo hata kidogo. Na iliishia huyo msichana Haiba akiwa gerezani baada ya kufanya mauaji ya aliyekua mume wake na watu wengine alipokua kwenye kazi yake haramu ya kutumia silaha za moto. Sasa hili ndio hitimisho lake. Msichana niliyemzika kwa uchungu ndio Haiba wangu wa kwenye kitabu. Ndiye huyo niliyempenda sana. Na kwa sasa ameshatoweka kwenye uso wa dunia. Ndio maana nikaipigania maiti yake kwa gaharama kubwa ili nipewe niizike mwenyewe na si kuzikwa kwa kutupwa na askari wa Kimarekani. Hivyo kufanikiwa kwangu kueleweka na familia yangu hasa mchumba wangu. Nasema wazi kua kuanzia sasa nimehamishia upendo wangu niliokua nampenda haiba kwake yeye. Nitampenda Daima na tukijaaliwa mwezi ujao nitafunga naye ndoa.”

   Nilimaliza mkutano wangu. Kwa maelezo hayo hakika hakukua na swali zaidi ya kupewa pole nyingi na hongera kwa maamuzi yangu mazito niliyoyachukua na kufanikiwa. 

   Hadithi yangu na Haiba ikafanya manunuzi ya kitabu hicho yaibuke upya na kulazimika kukitoa tena kitu hicho nikiwa nimemalizia kisa kamili kuanzia mwanzo nilipokutana na Haiba hadi kifo chake. 
             ****************MWISHO**************


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: