Umuhimu wa kujua kundi la damu la Mchumba wako
MISS Ruvuma 2006 ambaye pia ni msanii wa fi lamu na muziki, Isabela Mpanda au Bella, aliwahi kukaririwa akisema kila ‘anapotega’ ili apate mimba kupitia kwa mchumba wake wa zamani, Karama Bakari ‘Luteni Karama’ zinatoka, kitendo ambacho alisema kinamkosesha amani.
Bella mwenye watoto wawili wakubwa alisema alihangaika kuhakikisha anazaa na mpenzi wake huyo ambaye inasemekana alioa mke mwingine baadaye, lakini ndoto zake zikawa zinayeyuka kutokana na mimba kuharibika.
“Yaani watu wanahisi sipendi kumzalia Karama lakini ukweli hawaujui, mimba zimekuwa zikiharibika lakini naamini siku moja ndoto yangu itatimia,” alisema Bella. Je, ni wangapi ambao mimba zimekuwa zikiharibika mara kwa mara kama ilivyomtokea Bella? Je, sababu inaweza kuwa nini? Ukisoma makala haya hadi mwisho, utagundua kwamba pengine tatizo la Bella linatokana na damu yake kutoendana na ya aliyekuwa mchumba wake zama hizo.
Kutopima makundi ya damu Kuna vitu vingi vya kuzingatia unapomchagua mtu kuwa mwenza wa maisha kuchungazana tabia, dini, shughuli zinazoingiza kipato, ukoo anaotoka mchumba na hata kupima damu kwa ajili ya kuangalia suala zima la virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi (VVU) na magonjwa mengine ya zinaa.
Hata hivyo, jambo moja muhimu ambalo limekuwa likisahaulika ni wanandoa kuangalia makundi ya damu zao kama yanaendana na ndio msingi wa makala haya. Jambo hili halizingatiwi lakini utofauti wa makundi ya damu inaweza kusababisha matatizo kwenye ndoa hususani wakati wa ujauzito yanayomweka mtoto ambaye hajazaliwa mimba yake kuharibika au kufariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa makala haya, daktari bingwa na mhamasishaji wa damu salama wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, John Bigambalaye, anasema utofauti wa makundi ya damu kati ya wanandoa ni chanzo kimojawapo cha wanawake wengi kutopata mimba au mimba kuharibika. Ni kwa mantiki hiyo, anashauri kwamba mbali na wachumba kupima HIV, wahakikishe wanaangalia pia makundi yao ya damu kabla ya kufunga ndoa.
Anasema mwili wa binadamu umeundwa kwa chembechembe za damu na kwamba kila mwanadamu ana kundi lake la damu ambapo kuna makundi makuu manne ya damu duniani. Anasema kila mmoja wetu ana kundi mojawapo katika haya manne. Ambayo ni kundi A, kundi B, kundi AB na kundi O. Kadhalika anasema kila kundi la damu hapo juu lina rhesus factor ambayo inaweza kuwa chanya (+) au hasi (-).
Anasema kwamba kila mtu anarithi kundi la damu kutoka kwa wazazi wake. Kushindwa kupata mtoto Anasema kama mwanamke mwenye rhesus factor hasi (negative) ataoana na mwanaume mwenye rhesus factor chanya (positive), na kisha akapata mimba na mtoto akarithi rhesus factor kutoka kwa baba ambayo ni positive, kuna uwezekano wa mama kukomea kuzaa mtoto mmoja tu maisha yake yote.
Anasema hata huyo mmoja anaweza kumpoteza pia wakati wa kujifungua kwa sababu hasi na chanya hukutana kwenye damu na kwamba hasi na chanya zikikutana huleta madhara makubwa kwa hiyo hili tatizo linatakiwa kutatuliwa kabla ya kuingia katika mahusiano.
“Ili kupata mtoto kundi la damu la mwanamume linapaswa kuwa sawa na kundi la damu la mwanamke. Kama mwanaume ana kundi la damu A+ (chanya) basi mke wake pia awe na kundi lolote la damu ambalo ni chanya bila kujalisha ni A, B, O au vyovyote, hali kadhalika kama mwanaume ana kundi la damu hasi (negative) basi na mwanamke anapaswa kuwa na kundi lolote la damu ambalo ni hasi (negative),” anasema.
Anafafanua kwamba iwapo mwanaume ana kundi la damu chanya na mwanamke ana kundi la damu hasi, damu ya baba ndio inayoingia kwa mama kwa kuwa mama damu yake ipo huru kupokea na hivyo damu ya baba isipoendana na damu ya mama inakuwa kama kitu kigeni kimeingia ndani ya mwili wa mwanamke hivyo kutengeneza kinga mwili dhidi ya kitu hicho ‘kigeni’.
“Hii ndio unakuta kila mara mwanamke anabeba mimba miezi kadhaa inaharibika, kila akibeba inaharibika, hapo ujue kunatokea kutoingiliana kati ya rhesus factor (Rh) ya mama na ya mtoto, wakati mama ana hasi kichanga kina chanya.
“Ikiwa damu ya kichanga ni Rh chanya, ikivuja na kukutana na mzunguko wa uzazi wa mama ambao ni Rh hasi, seli za kichanga zitatambulika kama za kigeni matokeo yake mama atatengeneza kinga mwili inayoitwa Rh immunoglobulin G. Kingamwili zitapita kwenye mfuko wa uzazi na kushambulia seli nyekundu za damu za kichanga kilichopo tumboni, na seli nyekundu zikiharibika mtoto atapata ugonjwa wa manjano,” anasema.
Anasema iwapo mtoto akifanikiwa kukua akiwa tumboni, anaweza kupoteza maisha wakati wa kuzaliwa kwa sababu ya damu yake kutoendana na ya mama. Matibabu ya kurekebisha hali Anasema endapo mjamzito atahisi kitu na ataenda hospitali, ikabainika kuwa tatizo ni kundi la damu baina yake na mumewe, Dk Bigambalaye anasema kuna kipimo kiitwacho ‘cums test’ atafanyiwa na ikigundulika tatizo ni hilo atachomwa sindano inayoitwa ‘Anti – D gama’ ili kumlinda mtoto.
“Kabla ya hicho kipimo kufanyika na tatizo kujulikana wengi hupoteza ujauzito mara nyingi mimba ikiwa na miezi miwili, mitatu na kipimo hiki hakipo hospitali zote. Lakini tatizo lingine ni ufahamu wa mtu kutambua kwamba tatizo lake linaweza kuwa makundi ya damu kutoendana na hivyo kwenda hospitalini kupima.
Dk Bigambalaye anakiri kwamba kuna matabibu (clinical officers) ambao hawajui vyema hili tatizo lakini anashauri madaktari kujiongeza kila wakati kwani taaluma ya udaktari inahitaji kusoma kila siku.
Miezi sita baada ya kusafishwa Anasema pale mwanamke anaposafishwa kizazi, anatakiwa akae miezi sita ndio abebe tena ujauzito, lakini wengi hawazingatii hilo kwa maana kwamba akikaa sawa hata kabla hajafikisha miezi sita anabeba tena mimba.
Dk Bigambalaye anasema ukishasafishwa mzunguko wa damu unabadilika na kwamba hali hii pia imekuwa ikichangia mimba kuharibika na hasa kama mhusika damu yake haiendani na mumewe. Kuhusu kuchomwa sindano ya kukinga mtoto dhidi ya tatizo la utofauti wa makundi ya damu ya baba na mama, Dk Bigambalaye anasema sindano hiyo huchomwa mama anapokuwa mjamzito na siyo kabla ya hajapata mimba.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: