Asilimia 26.5 wanawake hufanya mapenzi kinyume na maumbile




Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mfumo wa uzazi unaharibika
Watafiti wanabainisha kuwa kitendo hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzazi, kina athari kubwa mno kwa mwanadamu, mojawapo ni ikiwemo uwezekano mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu hivyo.
Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alitoa ripoti hiyo hivi karibuni hapa jijini Dar Es Salaam.
Mremi akiwa na jopo la watafiti kutoka NIMR anasema kuwa wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi na Kuogopa kupata Mimba.
 Vilevile alizitaja sababu nyingine za wanawake kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
Sampuli za utafiti
Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha.
 Mremi anasema “Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani
Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo.
Imani potofu kwa wanaume
Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi kwa haraka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote.
Katika utafiti huo, wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile, licha ya kwamba ni jambo linalokatazwa na dini zote.
Tanga yaongoza
“Tanga ndiyo kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo” anasema Mremi
Fikra za kulinda ubikira
Ilibainika kuwa wasichana wengine walikiri kufanya hivyo kwa ajili ya kulinda ubikira wao na baadhi ni mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
Dk Mremi amekaririwa akisema “ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa baa, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani. Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo”.
Wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo hilo.
Dk Eliza Shayo, ambaye pia alishiriki katika utafiti huo anasema sababu ya kufanya utafiti huo ilikuwa ni kuangalia visababishi vya kusambaa kwa Ukimwi. 


“Lakini pia tuliweza kujua tatizo la  kufanya mapenzi kwa njia hiyo lina ukubwa kiasi gani” anasema
Dk Shayo pia anasema utafiti huo uliangalia iwapo wanaofanya vitendo hivyo hutumia kondom au la. Wengi walionekana kutotumia kondom wakifikiri hawawezi kupata virusi vya Ukimwi, imani ambayo sio sahihi.
Ni changamoto
Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Kusini mwa Afrika, (GEMSAT) Dominica Haule anasema utafiti huu ni changamoto kwa  serikali, watunga sera na vyombo vya sheria.
“Ni wakati muafaka wa kujadiliana nini kifanyike kupunguza tatizo hili. Hii ni hatari na haikubaliki,” anasema Haule
Anasema wadau wa afya hawana budi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu na kuweka wazi madhara ya vitendo hivyo.
Mhadhiri wa Masuala ya Saikolojia, Dk Kitila Mkumbo anasema suala hilo linaweza kuwa na athari kiafya.
“Kisaikolojia, kama wao wawili wamekubalina sawa, lakini kiafya lina athari kubwa,” anasema
Dk Mkumbo anasema ufanyaji wa mapenzi upo wa aina nyingi wengine hufanyia mdomoni, inategemea na makubaliano, lakini kiafya inaweza kuwa na athari.
Dk Meshack Shimwela, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Ndani ya Mwili kutoka hospitali ya Amana anasema mwanamke ambaye hufanya mapenzi kinyume na maumbile huathirika na kuacha kufurahia tendo hilo kwa njia ya kawaida.
“Lakini pia, wengi hujihisi kama wamelaaniwa na wanakosa kujiamini” anasema na kuongeza kuwa hata kama anaweza kufanya kwa mkumbo, baadae hujutia hasa anapojikuta anapata athari kubwa za kiafya kuliko furaha.
 Dk Shimwela anasema kitendo hicho  husababisha bakteria wasiohitajika kuingia katika sehemu ya haja kubwa na kuleta  uambukizo.
“Eneo la haja kubwa limeumbwa kutoa na si kuingiza. Hivyo kitendo hicho husababisha uharibifu na kulegea kwa misuli” anasema
 Anasema maradhi mengine ambayo hujitokeza katika sehemu ya haja kubwa pindi mtu anapofanya mapenzi kwa njia hiyo  hayana tiba.
Anaongeza kuwa wanawake hupata madhara wakati wa kujifungua na hatari ya kupata maambukizi ya VVU ni kubwa zaidi.
Hatari kuu
Jarida la  Havard la  afya ya Wanawake (Havard Women Health Watch) linaeleza kuwa ufanyaji wa mapenzi kwa njia ya haja kubwa ni chanzo kikuu cha maradhi ya kuambukiza ukiwemo Ukimwi.Hii ina maana kuwa watu ambao wanafanya vitendo hivyo wana athari kubwa za kupata virusi vya .
Kwanini ni hatari?
Tishu zilizo katika njia ya haja kubwa ni laini na hazina maji maji, hivyo huchanika kwa urahisi wakati wa tendo na kuingiza vijidudu.
 Utafiti kama huu ulifanywa nchini Marekani mwaka 2005 na kituo cha Kudhibiti Maradhi ya Kuambukiza (CDCP).
 Katika utafiti  huo asilimia  40 ya wanaume na 35 ya wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 25 na 44 walikiri kufanya tendo hilo kinyume na maumbile.
Wanatumia matambala kuziba kinyesi
Kuna athari kubwa za kufanya kitendo hicho, baadhi ya watu hujikuta wakivaa matambaza ili kuzuia kinyesi kisitoke kwa vile mfumo wa haja kubwa huwa umelegezwa.
Profesa wa Chuo Kikuu cha tiba cha Colombia, Judy Kuriansky anasema “Inashangaza kuona watu wanafanya mapenzi kwa njia hiyo wakidhani wanajikinga na Ukimwi, huko ni kujidanganya, ukweli ni kuwa njia hiyo ndio inayoweza kumfanya mtu kupata virusi kwa 



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: