:NAITAFUTA FURAHA YANGU 11 (MUENDELEZO)
Story :NAITAFUTA FURAHA YANGU
---sehemu ya 11---
Tulipo ishia jana,pale bibie suhaila alivyoota ndoto kama ya juma ya tukio ambalo lilitokea miez ya nyuma ya kuuliwa kwa bwana ally na mke wake rahma.
Suhaila alizinduka kwenye ile njozi alipiga kelele na kusema hapanaa hapana mimi sijaua ,
Adinani akawasha taa na kuuliza suhaila ni kitu gani kimekupata mbona unapiga kelele?
Suhaila alivyomwona adinani alitoa mikono kwenye masikio akawa amekodoa macho.adinani alivyomtizama aliona suhailah ametoa sana jasho alimuuliza kuna joto sana?
Suhailah alishusha pumzi na kusema "samahani kwa kukushitua ila nina tatizo ambalo limekuwa likinisumbua mara kwa mara ,huwa naota ndoto mbaya ila usijali.
Adinani alimletea suhaila maji ya kunywa ,kisha bibie suhaila alipokea wakati huo saa tisa usiku ,alikunywa maji alivyomaliza ,adinani alimwambia haya inuka ukalale kwenye kile chumba nimekutamdikia
Suhaila alishika kichwa chake alikuwa akishisi maumivu makali maana jana alilia sana.
Adinani alimuuliza uko sawa?,suhaila alishusha pumzi na kujibu niko poa ?adinani aliuliza tena kulikoni mbona jana ukawa kwenye ile hali.
Suahaila aliitizama nyumba ya akina adinani kwa muda kisha alimwangalia adinani kwa macho yaliyojaa uoga "suhaila alimwambia adinani sorry(samahani) kwa kilichotokea jana ,maana jana nilijihisi kurukwa na akili
Adinani alitabasamu kisha akamwambia jana ulitokea wapi na kwanini ulikuwa watembea peku peku?
Suhaila alijibu"nilitokea airpot mpenzi wangu niliyemwamini sana alikuwa mtanzania ila anafanya kazi dubai ni mfanya biashara ,toka majuzi nilikuwa namwona yupo na mwanamke mwengine ,kila nikumuuliza huyu mwanamke ni nani ,mpenzi wangu hakunijibu chochote alichokuwa ananifanyia ni vitendo tu ,alikuwa akimchumu huyo mwanamke kisha ananiangalia haniongeleshi chochote ,
Kama unakumbuka siku ile ulivyoniokoa nilivyokuwa nakimbizwa na wale vibaka ,yeye ndio alikuwa chanzo nilimkuta pale amempakata mwanamke nikimuuliza kwa nini unanifanyia hivi
Huwa anakaa kimya au ananijibu "kama kusoma hujui inamana picha huoni.
Basi nilikereka na kuanza kulia ,ni kweli nampenda huyo mwanaume ,vile vile jana kaniita airpot nilivyoenda aliniaga na kuniambia tusijuane yeye ameshapata mwanamke wanae endana hivyo anaenda dubai mahali waliko wazazi wake anaenda kumtambulisha huko.
Hapo ndio akili ziliniruka nikavua viatu nikavitupa nikaanza kulia na kutupa mkoba wangu ulikuwa na simu ,pesa hata sikujal vyote nimetupa.
Adinani alimwangalia sana suhaila akamwambia pole kwa yaliyokukuta "adinani alichukua kikombe cha chai na kumwambia suhaila nadhani wakiona hichi kikombe cha chai ,kwa upande wangu nakiona kizuri kuliko vyombo vyote hapa ndani ,sisi ni wa hali ya chini sana kwahio hichi kikombe ni kizuri kupita vyombo vyote hapa kwenye nyumba yetu .
Vile vile hichi kikombe kwa watu wengine wakikiona wanaona ni kibaya mno wanaweza kukitupa maana wanaona ni kibaya na hakistahili kukaa kwenye kabati la kwenye nyumba yake.
Hivyo mtu akiwa na kikombe kama hichi anaweza kukifanyia kitu chochote ,anaweza kukivunja ama kukitupa ,
Vile vile kwa upande wangu hichi kikombe ni mhimu sana kikivunjika naweza nikalia na kukosa raha.
Adinani alikirudisha kikombe kwenye beseni kisha akakaa na kutulia,suhaila aliyatafakari mafumbo aliyoongea adinani hakuelewa hata kidogo ,alijaribu kufikiria ila hakuelewa.
Suhaila aliita "adinaniii maneno uliyoongea yana maana gani?,mbona mimi sijaelewa?.adinani alimjibu "maana yake ni hivi kikombe ni mwanamke ,jinsi kikombe changu kilivyo nimekichukulia tabaka la watu wa hali ya chini ,
Mimi nakitunza hichi kikombe sababu nakipenda ila kuna watu hichi hichi kimombe hawawezi kuweka kwenye kabati la vyombo.
Kabati ni moyo wa mwanaume ama mwanamke anae penda ,hawezi kukuweka moyoni sababu huendani na thamnani ya nyumba yake ,thamani ya moyo wake ndio maana anaweza kukivunja kikombe ama kukitupa
Sasa wewe alikivunja kikombe ndio maana alikuambia anaenda kumtambulisba mchumba kwa wazazi wake ,akakuacha wewe ambae mmedumu kwenye mahusiano yenu kwa kipindi kirefu.
Pole ni hivyo tu suhaila ,ila hata mimi usiniulize maswali mengi sijawahi kuingia kwenye ndoa ila kwa ufahamu wangu nimekujibu.
Suhailah alimwangalia adinani ,mbona ni rika lake mbona anamafumbo magumu kiasi hichi.adinani alimwambia usiwaze sana wala usijidharau hufai kwa wanaume ,wapo wanakitafuta kikombe hicho na hawakipati.
Basi suhaila aliwaza mambo mengi jinsi alivyikutana na adinani hadi kamleta nyumbani.kufikia saa kumi na moja ,suhaila na adinani walipitiwa na usingizi maana wote walikesha wamekaa sebuleni.
Palipambazuka kama kawaida kunguru wa dar wao wakinusa harufu ya ukoko ,shombo la samaki basi wanawahi mahali yaliko tupwa asububi kunguru walidamkia kwenye ndoo ambayo adinani huwa wanatupa uchachafu usiku wake adinani alitupa chakula ambacho kililetwa na mtu kisha akawapatia nusra na mudrick wale.
Ni kweli kile chakula kiliwekewa sumu kali ,kila kunguru aliokula kile chakula hakuchukua dakika tato ,anadondoma chini ,hadi adinani kuja kuamka saa moja ,kunguru ishirini walikuwa wamedondoka chini wengine wamekufa kabisa.
Adinani aliangalia ni nini kimesababisha hadi kunguru kufa alivyoangalia alikuta kile chakula alichokitupa kilikuwa na sumu.
.majirani waliamka na kuangalia ni kitu gani kimetokea mbona kunguru wanaelea hewani wengine wamedondoma wengine wamekufa.watu walijaa kwa akina adinani wakijiuliza nani aliwema sumu kwenye chakula.,adinani hakuwaeleza kuwa chakula kuna mtu ambae hawajamtambua kawawekea wadogo zake alitaka kuwaua.
Adinani alikumbuka pia ,kuna siku aliwawekea chakula wadogo zake alivyorudi alikuta nyau wamekufa baada ya kula kile chakula na kiliwekewa simu.
Adinani alianza kuwaza ni nani anataka kuwaua wadogo zake ni swali ambalo lilimsumbua sana kichwani.juma nae kama alivyoambiwa na kelvin tayari amewapa watoto chakula chenye sumu hivyo wakila tu kesho tunawazika.
Basi juma aliamka mapema na kuwahi kwa akina adinani lengo lake ni umbea kwenda kuhakikisha ni kweli watoto wamekufa?
Alivyofika karibu na nyumba ya akina adinani aliona watu wangi wamekusanyika ,juma alitabasamu na kusema tayari wamekufa naona watu wamejaa.
Juma aliwaza nitaenda kwa style gani kwenye huo msiba,juma pasina kupata ukweli alianza kupiga ukunga jamana wamekufaaa ,kwanini wamekufa watoto hawa jamani alilia huku akikimbia mahali wamesimama watu ,
Kila mtu aligeuka baada ya kusikia kilio cha juma ,watu walijiuliza mbona analia nani kafa.juma alifika kwenye umati wa watu ambao walikuwa wakishangaa kunguru wamefika ,juma alizidi kujichanganya nani kawaua watoto wa mare....
Juma hakumalizia gafla aliacha kulia kwa unafiki alishangaa watu wote wapo kimya wanamwangalia yeye tu analia.
Juma alivyoangaza macho aliona chini kunguru wengi wamekufa ,alishituka baada ya kuwaona mudrick na nusra wapo wamesimama wanaangalia kunguru walio kufa.akakumbuka maneno ya kelvini"hao watoto kesho ukiamka ukazike tu maana nimewawekea sumu kali.
Inawezekana vipi watoto hawajafa wako wazima ,kunguru tu ndio wamekufa.
Watu walimuuliza juma "unalia nini mbona tunasikia unasema watoto wamekufa wa mare... malizia basi hatuja kuelewa
Juma alishituka alibabaika na kufuta machozi yake ya umbea na unafiki alisema jamani watoto wapuuzi nimekutana na watoto njiani wakaniambia eti watoto wa rafiki yangu ally wamefariki nimepata hofu sana.
Adinani alimwangaliajuma kwa umakini ,kisha adinani akajiuliza "nitapata wapi uthibitisho kuwa juma umemuua baba yangu.
Basi watu walimcheka na kumwambia hakika juma hio kichwa yako inaenda resi sana.juma alipata aibu na kubaki amesimama simama huku akiwaangalia mudrick na nusra wapo wazima.
Watu walianza kutawanyika wengine wakienda makazin maana tayari pashakucha.juma katika pitisha pitisha macho aliweza kumwona suhailah amesimama mlangoni tena yupo karibu na shangazi ambae ni kipofu.
Juma alishituka na kuficha sura yake na koti kisha akaanza kuondoka ,alijisemea inamana huyu binti amekuwa mkubwa hivi.kwa nini amefika kwa adinani ,mungu wangu hii si inakuwa hatari zaidi.
Juma alianza kukumbuka jinsi alivyowaua wazazi wa suhaila
Juma alitikisa kichwa hapana labda sio yeye.
Kabla juma hajapiga hatua kuna gari kali ya bei mbaya ilifunga breki mbele yake mlango ukafunguliwa ,
Wakati huo juma amekodoa macho huku akitetemeka
Je nini kitaendelea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: