NAITAFUTA FURAHA YANGU 12






Story;NAITAFUTA FURAHA YANGU


---sehemu ya 12----
   Tulipo ishia jana, Juma alishituka na kuficha sura yake na koti kisha akaanza kuondoka ,alijisemea inamana huyu binti amekuwa mkubwa hivi.inamana nae hakufa? Au nimemfananisha.

Juma alianza kukumbuka jinsi alivyowaua wazazi wa suhaila 
Juma alitikisa kichwa hapana labda sio yeye.
Kabla juma hajapiga hatua kuna gari kali ya bei mbaya ilifunga breki mbele yake mlango ukafunguliwa ,
Wakati huo juma amekodoa macho huku akitetemeka.

Alishuka bibie zumra ,kwanza aliita suhaila upo salama?,zumra alikimbia na kumkumbatia rafiki yake suhaila  na kumuuliza ulikuwa wapi na imekuwane ukawa kwa huyu kijana,
Basi juma alijikaza aliondoka eneo lile huku akijiuliza maswali mengi ,haka kabinti kamekua inamana bado kananikumbuka sura yangu ,

Mmmh hapana hanikumbuka nahisi ashasahau basi juma aliondoma ana hofu na tukio ambalo alilifanya miaka kumi na nane iliyopita nyuma.alikumbuka maneno ya baba yake suahaila
"Mimi umeniua kwa sasa wewe bado kijana ,chukua mali zote mwache mwanangu ,mama yake si umemuua nae ,basi mwache huyo mtoto hata kama atateseka sana ila awe haiii..
Pale pale baba suhaila alifunga macho na kupoteza maisha.
Juma amekumbuka lile  tumio basi akatikisa kichwa na kusema hapana hapana.
Alikodi piki piki na safari yake kuelekea gongo la mboto ili akakutane na rafiki yake kelvin.

Basi zumra baada ya kukutana na rafiki yake alimwangalia sana ,alikuta macho yamevimba alivyomtizama chini amevaa ndala tofauti. Adinani aliwakaribisha karibuni mzungumze kwanza.

Zumra aliuliza umenipigia simu umetumia simu ya nani na simu yako iko wapi?,suhaila alimwangalia zumra alimwamba samahani nisamehe simu yangu nilivyovurugwa na mpenzi wangu nilitupa ,viatu nikatupa nikabaki kama nilivyo.nilitembea kutoka airpot hadi hapa tabata nikakutana na  huyu adinani tena kaniokoa isingekuwa yeye basi leo hii ungesikia habari nyingine ,

Zumra aliogopa na kuuliza "ni mapenzi tu yamekuvuruga hadi utake kujiua?"suhaila alijibu ndio yalitaka kuniua ila hasira ni mbaya nimeamin nisamehe sana zumra.

Kaka naomba utupeleke shuleni tayari tushavaa nguo,nusra alimwambia kaka yake,adinani aliwaambia haya nawapeleka ,mudriki naomba utandike mkeka hapo chini ili mnywe chai mpate kwenda shule.
 Basi walitandika mkeka chini ,adinaani alitoa vikombe sita  vya chai kisha akatoa na sinia aliweka silesi za mikate kisha chai akamimina kwenye vikombe alivyomaliza aliwakaribisha ,zumra,suhaila nawao wajumuike wapate kunywa chai.

Zumra ni mtoto wa kitajiri mno anayo pesa za baba yake ,gari anayotembelea ni ya ghali sana,zumra alimtizama adinani ,akawatizama akina nusra kicha akatizama mkeka chai na mkate ambao upo kwenye sinia.
Kwa upande wake ilikuwa ni jambo geni maana yeye ashazoea kupata vitu vya kitajiri ,mara nusra alikimbia na kwenda kumwamusha shangazi yake ambae ni kipofu alimshika mkono na kumwongoza hadi sebuleni "haya shangazi kaa hapa vizuri ee.
Shangazi alikaa 
Yote hayo yanayofanywa na nusra katoto kadogo yaani zumra alishangaa ,
Maana yeye hadi alivyokuwa  umri wake hawezi kufanya hivyo kwao kuna wadada wakazi watatu ,

Adinani aliwakaribisha maana huo ndio uwezo wake ,hana pesa ya kuwapatia chai inayoendana na wadhifa wao basi aliwatengea chai ya kimasikini sikini.
Suhaila hayo mazingira kwake si mageni alikaa chini na kumshika zumra kisha akamvuta nae akae kwenye mkeka.

Zumra alikuwa amevaa suruali nyeupe halafu mkeka ulikuwa na vumbi inamana akikaa hio suruali inachafuka.nusra alisema anti mwenye nywele ndefu subiri usikae kwanza nikuletee kitenge ukalie.

Nusra masikini alienda kwenye sanduku la nguo la marehemu mama yake alitoa kitenge kisafi alirudi na kumtandikia zumra juu ya mkeka na kumwambia haya anti kaaa.

Zumra mwenyewe alibaki ameshangaa mbona haka katoto kadogo kana akili hivi basi walianza kunywa chai.
Ile chai ilikuwa ya moto mno .
Nusra aliita kaka chai ya moto naomba unipozee "adinani alikuwa anamkorogea shangazi chai baada ya kuongeza sukari alimjibu nusra kachukue ile bakuli pale nje utie maji halafu uweke chai yako ipoe.
Zumra aligeuka alimwona nusra anamwaga mapovu ambayo yalikuwa kwenye ile bakuli ,kisha alienda kwenye kindoo cha maji alichota maji masafi alirudi na kukaa kisha akaiweka  chai yake ipoe pamoja na ya mudrick

Zumra alitizama lile bakuli ambao wamepozea chai ndio  mudrick alikuwa anafua soksi halafu watoto wameweka chai,kwa zumra kwake aliona kinyaa kutokana hajazoea maisha ya kimasikin

Walianza kunywa chai ,kwa bahati mbaya kikombe cha zumra kilikuwa kimepasuka kidogo basi kikawa kinamwaga  chai kidogo kidogo.zumra alichukua slesi moja ya mkate alianza kula ,

Asikuambie mtu chakula cha watu wengi kinanoga ,zumra aliweka ushua pemeni alikula silesi tano za mkate yaani alisikia poa sana ,alitizama jinsi nusra anamjali shangazi yake ambae ni kipofu ,mara anamsaidia kumpa mkate.

Zumra akajifunza jambo ,kumbe watoto wote wa kitajiri hawana upendo wala hawafurahii maisha kama maisha ya kimasikini
Yaani zumra toka alivyozaliwa hadi anakuwa hajawai kula chakula kwenye sinia moja.
Walikunywa chai basi adinani alikuwa anawaangalia zumra na suhaila maana wao ni watoto wakitajiri lakin leo wamekaa kwenye mkeka wakanywa chai tena kwenye vikombe  vya plastiki vingine vimepasuka vingine vinamsinzi kidogo wakala.

Walivyomaliza suhaila aliuliza zumra hauna elfu mbili hapo wakaongeze mikate mbona mitamu hivi kweli sijawahi kula kama leo nimekula silesi tano ,zumra nae amevutiwa maisha ya namna hio alimpa adinani elfu mbili na kumwomba aongeze mkate.

Duka halikuwa mbali ,adinani aliongeza mkate mwingine wakala wote yaani wakashiba na furaha juu ,suhaila akaanza kusahau kuachwa na mpenzi wake,
Walivyomaliza nusra alisema haya kaka naomba utusindikize shuleni 

Adinani aliwaambia haya nawasindikiza ,zumra alishangaa kuona nusra ana miaka mitatu anavaa viatu mwenyewe ,akakumbuka maisha yake alianza kuvaa nguo mwenyewe ana miaka kumi na mbili.kwa zumra aliona mambo mageni mno

Adinani aliwaomba "suhaila ,zumra naomba mnisubiri niwapeleke shule wadogo zangu hapo tu tabata shule.zumra alitabasamu alisema
"Adinani hapana wacha niwapeleke na gari mwenyewe leo shuleni
"Adinani alisema hapana unamaliza mafuta sisi tunatembea tu haraka haraka.

Zumra alimshika mkono nusra "aliita nusra leo nawapelema mimi shuleni aliwatoa nje akafungua milango ya gari kisha akawapandisha.adinani ,suhaila na shangazi ndio walibaki nyumbani.

Zumra aliweza kuwafikisha shuleni ,kwanza gari yake ilivyoingia shuleni ,walimu waliacha shughuli zao walijua huenda mkuu wa mkoa ama afisa elimu amewasili kwenye shule yao.

Wanafunzi walikuwa paredi ndipo gari ilipaki maeneo hayo ,zumra alishuka akawafungulia akina nusra na mudrick milango ya gari.
 Nusra ,na mudrick walishuka kila mwanafunzi walishangaa ,zumra aliwakumbatia na kuwaambia masomo mema.

"Anti bye bye baadae si utakuja kutuchukua tena ee anti tuahidi kama utakuja ni maneno aliyoongea nusra ,bibie zumra aliwatizama wale watoto na kuona wamefurahi hakupenda wakose furaha kwa siku hio

Aliwaambia ndio nitakuja kuwachukua kisha akawapungia mkono ,walimu walishangaa hawa watoto wamempata nani huyu mwenye gari nzuri na binti wa kisasa binti wa kitajiri

Wanafunzi walianza kuzungumza yaani  hawa mayatima leo wamepata lifti wanachekelea sana.basi na wao walijiunga kwenye mstari 

Zumra alirudi kwa adinani ndipo alikuta adinani nae anajiandaa aende kwenye kibarua chake,suhaila aliuliza "adinani unaenda wapi sasa hivi?,adinani aliwaza hana hata senti tano mfukoni aliwajibu naenda kwenye kibarua changu.

Zumra alimwambia sawa haina shida na huyu shangazi yako anabaki na nani?,adinani aliwajibu "atabaki tu hapa nyumbani kulinda nyumba maana siwezi kukaa nyumbani lazima nikatafute vibarua ili maisha yaende.
Zumra alitaka kusema basi kaa nyumbani nitakupa pesa ,alitaka kuongea akashidwa na kusema"adinani  unaweza kutuamini tuondoke na shangazi yako halafu baadae tumtamrejeshe?,maana huyu nikipofu halafu kwa umri wake anaweza akapitiwa na vijana wenye njaa kali wakambaka  tu.

Adinani aliwaza ,kisha akawaambia sawa ili mrufudishe mapema ili akina nusra wakitoka shuleni waje kukaa nae.suhaila aliitikia sawa ,walimchukua shangazi wakampakia kwenye gari ,kisha wakaondoka nae huku adinani ane alifunga nyumba 
Adinani hakuwa na nauli alianza mchaka mchaka alikimbia hadi matumbi kwenye kibarua cha kusomba tofali.

Juma na kundi lake hawakuridhika kwanini nusra na mudrick hawajala chakula ,kile walichokiwekea sumu.
Walienda hadi nyumba ya adinani na hapakuwa na mtu waligonga palikuwa kimya

Lakin mama joy alivyosikia mlango unagongwa alisogea na kubaini ni akina nani wanagonga alisogea hadi karibu ndipo alisikia daniel akiongea kwa sauti ya chini akimwambia kelvin

"Sikia hawa watoto wakirudi tuwatie kwenyd roba tunawasukumiza matambara mdomoni kisha tunaenda kutupa mbali.mama joy kusikia vile aliogopa bahati mbaya mama joy anasumbuliwaga na kikohozi ,akiwa anasikiliza njama wanao panga akina kelvini gafla kikohozi kilikamata mama joy.
Akajikuta akikohoa kwa nguvu koho !!!!

Daniel aliuliza nani katusikiliza kamata huyo ,mama hata  hakusogeza mguuu alishangaa amedakwa mkono aliangalia ni nani kamshika alivyoinua macho alikutana na sura ya danile

Mama akakumbuka danile alishawai kumwambia umbea umbea wa kufuata yasio kuhusu nitakukata shingo sasa mama kasikia kwa masikio yake wanapanga kuwakamata akina nusra

Je nini kitaendelea?


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: