NAITAFUTA FURAHA YANGU 13 & 14





Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU

--sehemu ya 13-&14--
     Tulipo ishia jana, Mama akakumbuka danile alishawai kumwambia umbea umbea wa kufuata yasio kuhusu nitakukata shingo sasa mama kasikia kwa masikio yake wanapanga kuwakamata akina nusra

Daniel alimuuliza mama joy kwa ukali unafanya nini?,mama akiwa anatetemeka alimjibu nilikuwa napita na hii njia ndio nimefika sasa hivi nashangaa unanikaba kwani kuna tatizo gani.?

Daniel alimwangalia sana mama joy ,kisha akamwambia haya pita nenda ulikokuwa waenda ,ila kama umesikia mazungumzo yetu pia ole wako tufel  dili letu hapo ndio utajua mimi ni nani.
 Mama joy aliachwa akawaza ,sana akaona si vyema kuwaacha watoto waangamie ,mama joy alijitolea alienda hadi maeneo ya tabata shule kwenda kuwasubiri   akina mudrick wakitoka shule awachukue na kuwapeleka  hata kwa rafiki zake wasirudi nyumbani maana amewasikia akina daniel kwa masikio yake mawil wanapanga kuwateka watoto na kuwafungia kwenye roba kisha akawatupe.

Tukirudi shulen akina nusra waliruhusiwa ,wanafunzi wanzao waliwazingira na kuwaambia "we nusra na kaka yako mudrick nyie kwanza masikin hamna hata pesa ya kununua lamba lamba ,ona sisi tumenunua,halafu asubuhi mlihurumiwa sijui na nani huyo akawapa lifti ya gari na kuwaleta shuleni basi mnajiona wajanja ,nyie mayatima tu.ni maneno ya wanafunzi wenzao walikiwa wamewaandama na kuwacheka wakati ule.

Mudrick huwa hapendi kuambiwa yatima ,alimtizama mwanafunzi aliyewaambia wao ni mayatima alimpiga ngumi ya tumbo puuuu!yule mwanafunzi akainama kwa maumivu ,kisha mudrick akamsukuma akadondoka chini,
Nusra alikaa chini na kuchotea mchanga kwenye siketi yake alikinga kisha alitaka kumwagia yasin ambae amewaambia wao ni yatima ,kabla hajamwagia ule mchanga machoni.

Sauti ilisikika "nusraa acha usifanye hivyo,nusra aligeuka na kutizama ni nani anamwita aliona zumra amesimama kwenye gari yake,nusra aliita anti ,lakin kuna mwanafunzi mwingine alitoa penseli yake mfukoni kisha akataka kumkita nusra kichwani ,kaka yake aliwahi na kumsukuma nusra kisha wakadondoka basi mudrick alichomwa mgongoni,bahati nzuri mudrick alikuwa kavalia begi la shule hivyo hakuumizwa.

 Zumra alifika na kumuuliza kwanini mnapigana?,nusra alimshika mkono zumra na kumwambia anti akina yasini wanatuambia sisi mayatima ,ndio maana kaka amewapiga.zumra alishusha pumzi na kuwaambia okay msijali nimekuja kuwachukua twendeni nyumbani ,aliwapakiza kwenye gari safari moja kwa moja hadi nyulumbani.

Zumra anafika nyumbani aliona mwanaume mmoja akiwa amefunika uso wake na kofia kubwa amezunguka nyuma ya nyumba,zumra alikanyaga breck na kurudisha gari nyuma hakuwafikisha nyumbani aliwachukua akina nusra na kuwapeleka sinza kwenye nyumba  yake anayo kaa.
Nusra aliuliza "anti huku ni wapi mbona nyumba kubwa hivi?,
Zumra alitabasamu na kuwaambia tuingie ndani shangazi yenu yupo huku,
Nusra aliingia ndani  alishangaa kumkuta shangazi ameogeshwa amepakwa mafuta amevalishwa nguo safi ,ukiambiwa huyu ni kipofu huwezi kuamini
Nusra kumwona shangazi yake alimkimbilia na kumkumbatia ,haa shangazi umependeza nani emekununulia nguo ?atakuwa ni kaka ee.

Shangazi alimshika nusra kichwani alimpapasa nyele na kumwambia"pole na masomo nusra ,hizi nguo nimevalishwa na huyo anti aliyekuja kuwachukua nyumbani.
Wakati huo zumra alimwita mfanya kazi wake wa ndani awaletee chakula akina nusra 
Chakula kilipakuliwa mezani ,kisha zumra aliwachukua ili wakale.
Nusra kufika mezani ,aliuliza ",anti hapa kwenu hamna mkeka?,mimi siwezi kula nikiwa nimekaa kwenye kiti nishazoea mkeka.

Zumra alimwangalia nusra alimwambia usijali haya nakuletea ,alichukua kapeti  la manyoya akamtandikia chini kisha akamuwekea chakula ,nusra alianza kula,wali alipiga kijiko cha kwanza ,alisema"shangazi njoo tule wote,

Shangazi akawaambia kuleni mie nishakula ,basi walipata chakula safi ,baada ya kushiba ,zumra alimwambia mfanya kazi wake awaogeshe kisha akatoka na kuwanunulia nguo zingine
Aliwanunulia nguo za shule akawanunulia ,na kuvaa nyumbani

Alirudi nyumbani watoto walivalishwa nguo kisha wakawekewa move za katuni hakika watoto walifurahi na kumpenda zumra ,
Tukirudi kwa akina daniel waliwasubiri akina nusra lakin hawakutokea hadi wakaondoka pasina kufanikisha .

Mida ya saa tisa siku hio adinani alirudi nyumbani mapema akiwa amenunua unga wa dona kilo mbili ,alifika na kukuta nyumba imefugwa.adinani aliondoka na kwenda kwa mama joy maana huyo ndio kampa jukumu la kuwaangalia akina nusra  hasa akiwa nyumbani.lakin alifika kwa mama joy hakuwakuta alimkuta mama joy amejiinamia tu.
Shikamoo mama joy ,adinani alisalimia 
"Marhaba mwanangu "nae alijibu

Akina nusra na mwenzake wameenda wapi?,mama alimwangalia adinani akiwa na simanzi ,alianza kuongea kwa hisia huku akionekana mwenye hofu aliita "adinani ,maisha yenu yaonesha yapo hatihani si dhani kama kweli wadogo zako wapo salama,nimesikia kwa masikio yangu kuna watu walikuja na kuwatafuta hapo kwenu akina mudrick na wakazungumza wakiwapata wanawatia kwenye gunia na kwenda kuwatupa mbali.
Nimejitahidi hadi kwenda shuleni ili nikawachukue akina adinani sikuwaona sijui wametekwa au laaa.

Kwa kweli ile taarifa ilimshitua adinani,kwanza aliwaza watakuwa wapi au watakuwa kwa mama micki ,adinani aliamua kumpigia mama mick ,nae alipokea simu
Haloo adinani uko salama?
Niko salama mama vip akina nusra na shangazi yao wapo huko?,
Upande wa pili"hapana hawajaja wadogo zako kwani vipi hawapo nyumbani
Ndio hawapo"adinani alijibu na kukata simu.

Adinani akiwa na mawazo huku akiwaza kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa kupotea kwa wadogo zake mara mlio wa simu ulisikika kwenye simu yake.
Adinani aliifungua ile sms "adinani niko na wadogo zako na tuko njiani tuna kuja ni mimi zumra"
Hapo ndipo adinani alishusha pumzi na kusema asante mungu ,kisha alimwangalia mama joy na kumwambia "kuna wadada flani waliwachukua akina nusra hivyo wanawaleta nyumbani kwahio wapo salama.

Adinani alimjulisha na mama mick kuwa aache wasi wasi wadogo zake ashajua waliko ,adinani alienda nyumbani na kuwasha jiko ,alichukua sufuria kubwa kidogo alisonga ugali mkubwa alivyomaliza alienda kwa wauza samaki ,adinani alinunua dagaa mchele(uono). Alirudi nyumbani na kukata kata nyanya ,hoho ma karoti aliziunga zile dagaa maji akatia na maji basi mchuzi maji ndii umejaa kwenye kisafuria.

Adinani ile anamaliza kupika alishangaa kuona gari aina ya super costemar (,haice ndogo) malngo ulifunguliwa wakwanza alikuwa suhaila kushuka ,alishuka pia dada mmoja mwenye asili ya ushombe shombe ,akashuka zumra kisha nusra na mudrick wakashuka ,vile vile na shangazi adinani alibaki kushangaa.

Wote walikuja wakiwa wamependeza harufu nzuri za pafyumu ,kaka kakaa nikuambie kitu "leo tumeenda kwa anti huyu mwenye nywele ndefu ,tumeangalia tv yaani nimeangalia katuni linamkimbiza mwenzake nimecheka ,halafu tumekula ice cream kaka,ni maneno aliyoongea nusra pindi alipomwona kaka yake.

Adinani alishangaa wadogo zake na shangazi wamenunuliwa nguo mpya ,viatu yaani watoto wamependeza ,alimwangalia shangazi ambae ni kipofu kavalishwa miwani yaani huwezi amini kama ni kipofu.
Basi walisalimiana suhaila aliita adinani"yaani tuna kama mwaka hatujala ugali plz tunaomba utupikie ugali kama hutojali.

Lile swali lilimfanya adinani achungulie sebuleni ambako ametandika mkeka wake kama kawaida ameweka ugali  kwenye sinia kisha amefunika na sufuria alilopikia.
Adinani akiwaangalia akina zumra hawaendani kabisa na mazingira anayo ishi adinani 

Adinani alijisemea moyoni "haya ndio maisha yangu ,huu ndio uwezo wangu aliwaambia karibuni ugali nishapika tena mkubwa naomba tuingie tukale.
Waliingia wote ,kuna mdada ambae wamekuja nae,ki ukweli yule dada nae anaonekana hajawahi kukaa maisha ya uswazi ama maisha ya kimasikini ,kwanza alifika mlangoni aligusa mlango na kidole akasema"zumra hapana mimi siingii kuna vumbi kwenye hii nyumba hivyo mtanikuta kwenye gari.

Suhaila alimshika mkono na kumwambia "unasemeaje wewe alimshika na kumwingiza ndani ,alishangaa akina nusra wanavua viatu na kukaa kwenye mkeka ,vile vile zumra nae akakaa kwenye mkeka ,alimwangalia suhaila 
Akamwambia "siwezi kukaa kwenye mkeka mchafu namna hii plz naomba mniache,
Suhaila aliita "neeema plz sit down(kaa chini).alimvuta na kukaa chini

Adinani alifunua sufuria kitu kikaonekana ugali wa dona tena mgumu ,ukiwa wa moto wa wastani harufu ya ugali safi ulio iva adinani akawaambia "karibuni tule.
Waoooo suhaila alifurahi na kunawa wa kwanza huku akionekana mwenye hamu ya kula ugali huo
Suhaila aliwauliza wenzake "mshawahi kula ugali wa dona tena kwenye sinia?,sasa ngoja muone jinsi unavyokuwa mtamu.
Neema alionesha sura ya mtu mwenye kinyaa ,alimwambia suhaila stop hii ni nini gundi ama kitu gani.

Kabla hawajaanza kula sauti kwa nje ilisikika ikisema "adinani toka haraka nimekufatuta sana leo ndio mwisho 
Adinani alishituka baada ya kuisikia ile sauti aliifahamu na kufanya asimame kwa hofu huku ameshikilia tonge la ugali mkononi

JE NINI KITAENDELEA? 
**************
---sehemu ya 14---
    Tulipo ishia jana, Kabla hawajaanza kula sauti kwa nje ilisikika ikisema "adinani toka haraka nimekufatuta sana leo ndio mwisho 
Adinani alishituka baada ya kuisikia ile sauti aliifahamu na kufanya asimame kwa hofu huku ameshikilia tonge la ugali mkononi....SONGA NAYO.........

Mara mlango ukapigwa teke ,nusra aliuliza nani wewe ?mara alitokea rafiki yake mick akiwa amebeba tikiti pamoja na ndizi mbivu ,mick alisimama mlangoni,
Adinani alivyomwona rafiki yake mick ikabidi acheka na kukaa chini.kisha akamtizama neema ambae kajificha mgongoni mwa suhaila ,yaani aliogopa jinsi mick alivyopiga mlango teke.

Mick tabia gani hizo kushituana ndugu yangu karibu tujumuike chakula bana,adinani alimwambia rafiki yake ,wakati huo mick amesimama tu mlangoni ameshangaa kuona adinani amepata ugeni ,yaani watoto wa kitajiri wamemtembelea tena wamekaa kwenye mkeka.

Mick aliingia kisha akakaa pembeni aliwaambia kuleni kwanza ngoja mie nikate tikiti mkimaliza kula mtashushia na tunda kidogo basi bibie suhaila alitoa nyama za kuchoma alikuwa amezifunga kwenye foil kisha akaweka chini kwenye mkeka walianza kula ugali ,nyama pamoja na dagaa mchele.
Zumra alikula ugali ,neema yeye hakula alisema hawezi kula kwa adinani maana kwa upande wake aliona mazingira machafu hajazoea kukaa sehemu zenye vumbi.

Suhaila aliita "adinani usijisikie vibaya huyu rafiki yetu neema ndivyo alivyo amelelewa mazingira ya ulaya hivyo hapa kwako anaona hapastahili  kukaa.
Adinani alijisikia vibaya ,aliitizama nyumba ya kwao ambao ilikuwa imejaa baibui ,yeye hanaga muda wa kufanya usafi ,maana akiamukaga yeye ni kutafuta vibarua ili aweze kupata chakula cha wadogo zake.
Anti naomba nyama nzuri" ni maneno aliyoongea nusra akimwambia zumra ,basi zumra alifanya hivyo ,huku mudrick nae alimtafutia shangazi yake ambae ni kipofu nae alimpa nyama.
Yale mazingira ya kula wengi wamekaa eneo moja zumra aliyapenda na kutamani kila siku awe anafanya hivo.

Walimaliza kula kisha wakapewa tikiti na mick nao walikula,basi walishiba vizuri hadi zumra alishidwa kuinuka peke yake hadi akanyanyuliwa na suhaila,wakati huo neema yeye aliondoka na kwenda kukaa kwenye gari.

Baada ya kumaliza kula ,nusra alimwambia zumra"anti kwetu kuna panya huwa wanakatiza sana sebuleni wanakimbia hao?
Zumra aliuliza kwa mshangao panya ,sijawahi kuwaona live nawaonaga kwenye vitabu na tv tu.
Ha ha ha nusra alicheka na kumwambia anti we muongo panya hujawahi kuwaona kweli.

Ni kweli zumra mazingira anayoishi hajawahi kuona panya kwa macho kutokana na nyumba zao huwa zinapigwa dawa mara kwa mara zakufukuza wadudu ,hivyo panya hajawahi kumwona

Wakiwa wamsimama mara panya alitokea kwenye chumba alikiwa amekimbia alienda mahali wamesimama akina zumra ,basi nusra alipaza sauti anti ona panya huyo ,ki ukweli suhaila na zumra wanaogopa panya mno ,suhaila alipanda juu ya meza huku mudrick akicheka na nusra bibie zumra alikuwa amesimama karibu na adinani alimrukia adinani na kumganda ,adinani alimshika mtoto wa kike amemushikilia mabegani nae alimshikilia ili asidondoke.

Zumra alificha uso wake kifuani kwa adinani ,huku amefumba macho ,zilipita dakika mbili ameng'ang'ania kwa adinani ,basi walimcheka ndipo adinani alimshusha chini ,zumra akawa ana wasi wasi walitoka na kwenda kukaa kwenye gari.

Wakiwa kwenye gari zumra alipigiwa simu ,nae aliipokea 
Haloo baba 
"Salama uko wapi nakutafuta njoo nyumbani kuna mgeni amekuja kwa ajili yako "baba alimwambia mwanae
Zumra alifumba macho na kujibu nakuja kisha akakata simu.

Zumra aliwaaga adinani ,nusra ,mudrick na shangazi yao kisha wao waliondoka walimwahidi adinani kesho watarudi maana wamependa sana kula pamoja pia wanapata furaha hasa wakiwa wote,adinani aliwaambia hamna shida karibuni

Akina zumra wakiwa njiani kuelekea nyumbani ,suhaila aliuliza "ulijisikiaje ulivyo mpandia adinani na kuficha uso wako kwenye kifua chake,zumra alikumbushwa lile tukio alitabasamu tu na kuonesha mwenye furaha akamwambia bana usiniulize chechote mie nilikuwa naogopa panya imetokea nimemrukia hata sikujua.
Neema nae aliongea "kwahio baba yako amekuita unaenda kukutana na yule mwanaume aliyekufutia?

Zumra alipiga usukani kwa mikono kisha"akamwambia neema hebu niache sitaki kuongelea habari hizo ,basi kwenye gari walikaa kimya "zumra alianza kukumbuka maneno ya baba yake"mwanangu nimekutafutia mwanaume lazima akuoe na akija plz mwanangu usinitie aibu uongee nae vizuri .
Yale maneno yanamkosesha sana raha zumra

Tukirudi kwa akina adinani baada ya zumra na wenzake kuondoka basi mick aliuliza "adinani rafiki yangu imekuwaje umepata ugeni wawatoto wazuri mmepika ugali dagaa safi tu na wanakula.
Adinani lile swali lilimfanya ashushe pumzi kisha akamwangalia mick,aliutizama mkeke ambao walikuwa wameukalia na kupata chakula kwa pamoja.
Ujue mick watoto wa kitajiri huwa baadhi yao kuna kitu wanapenda ,hawa tumezoeana muda mfupi lakin wamekuwa wanapenda kula vyakula vyetu vya hali ya chini ,japo mara ya kwanza walikuwa wanaogopa lakin inaonesha hawa mabinti

Wanapenda kuishi maisha ya kawaida hawapendi kuishi maisha ya kitajiri ndio maana umewakuta wanakula ugali mgumu na dagaa maji freshi tu.japo kwangu naona aibu ila sina namna wanachokikuta ndio hicho hicho tunakula

Ha ha ha mick alicheka na kusema hapo nimeipenda rafiki yangu lakin yule dada aliyekupandia alivyokuwa anaogopa panya aisee kala ugali yaani ukiambia ni mtoto wa kitajiri na anaendesha gari kali basi unaweza ukabisha hadi kesh
Ha ha we umeanza uchokozi halafu ujue ulinishitua mick umekuja na sauti ambayo sijaizoe hebu niambie ulikuwa unamaanisha kusema nini kusema adinani leo ndio mwisho wako.

Ha ha mick alicheka na kumpiga Adinani mgongoni na kumwambia hujui tumefunga shule sasa ndio mwisho wa kwenda shule na hapa tunaanza kupiga misele wote.
Aah kumbe mwezi wa kumi nambili ushafika ok poa ndugu umekuwa mtu wa ngapi maana daah mie ndio shule basi.
Aah bana nimechukua nafasi yako ambao ulikuwa unaishikaga wewe

Adinani aliuliza umekuwa wa kwanza ee ,mick alijibu ndio ,adinani alifurahi kuona rafiki yake kushika nafasi ya kwanza vile vile aliumia maana yeye ndio alikuwa anaongoza kila mtihani.,adinani akajikuta anawakumbuka wazazi na kujisemea moyoni mama umeondoka na ndoto zangu za kusoma mmeondoka nazo .

Tayari ishatimia saa moja usiku ndipo adinani alitoka na rafiki yake ili amsindikize mick amtoe hadi barabarani kisha mick aende nyumbani kwao.
Walivyosindikizana aliwaacha mudrick na nusra wakiwa wanajifunza kuchora pale pale sebule huku shangazi alikuwa chumbani kalala.

Adinani alivyomsimdikiza tu rafiki yake,hazikulita dakika mbili umeme ulizimika gafla kwenye nyumba yao tu.nusra na mudrick walikuwa wanasoma kupitia mwanga wa taa ,sasa umeme umezimika gafla.
Nusra alitoka nje ili kuangalia kama umeme umekatika kote,lakini ilikuwa siku mbaya kwa upande wao ,katoto kadogo kalikabwa na kusukumiziwa matambara mdomoni yaani nusra hakutoa hata sauti ,kisha katoto kalipigwa mtama kalidondoka kifudi fudi na kufanya kachunike kwenye paji la uso ,puani na mdomoni damu ilitoka lakin alikuwa amezamishiwa matambara mdomoni

Mtu ambaa alikuwa amefunika uso wake na kofia alimkanyaga nusra shigoni kisha akamfunga mikono kwa nyuma.akamfunga na miguu
Mudric k nae alitoka aliita nusraaa uko...hakumalizia kumbe kulikuwa na mtu mwingine amejibanza karibu na mlangoni alifanya kuuziba mdomo wa mudrick akamzamishia matambara 
Akampiga mtama nayeye alikunja mikono ya mudrick kwa nyuma kisha akaifunga
Hakuishia hapo aliukanyaha mguu wa mudrick wa kulia kitu kilisikika kooooh!
Mguu ukavunjika lakini huyo mtu hakuwa na chembe ya huruma alimshika adinani kisha akatoa gunia kubwa la mfuko waliwaingiza kisha wakalifunga hilo gunia.

Mudrick na mdogo wake nusra wakawa wanafurukuta ndani ya gunia ,wanalia ila sauti hazitoki kutokana na kuzibwa na matambara mdomoni ,
Wakati huo mudrick amevunjwa mguu na wamefugwa kwenye roba.
Sauti ilisikika tu ikisema kelvini beba hawa watoto kwenye roba tuondoke ,

Je nini kitaendelea?


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: