NAITAFUTA FUFAHA YANGU 15






Story :NAITAFUTA FUFAHA YANGU


----sehemu ya 15
  Tulipo ishia jana, Mudrick na mdogo wake nusra wakawa wanafurukuta ndani ya gunia ,wanalia ila sauti hazitoki kutokana na kuzibwa na matambara mdomoni ,
Wakati huo mudrick amevunjwa mguu na wamefugwa kwenye roba.
Sauti ilisikika kelvini beba tuondoke

Daniel alitoka kwenye ile nyumba ,alionekana yeye ndie aliingilia dirishani na kwenda kukata umeme kwenye main switch kisha  kelvin na kijana mwingine wao walijificha mlangoni hivyo nusra na mudrick walivyotoka kuangalia kama umeme kwa nyumba za majirani hujakatika ndio wakaweza kukamatwa.

Piki piki ilikuja na kupakia gunia ambalo wamefugwa akina mudrick.piki piki iliwasha ,jinsi walivyofugwa ilikuwa ni ngumu sana mgongo wa mudrick ulikuwa umegusa chuma endapo piki piki itapita kwenye mabonde basi mudrick anaweza kuvunjika mgongo wakati huo tayari mguu umevunjika.
Piki piki ilianza safari ya kwenda kuwatupa hawa watoto kutokana na roba kuwa zito na lamefugwa basi nusra walianza kukosa hewa huku miili yao kuanza kulegea taratibu wakati huo piki piki ipo kwenye mwendo.

Adinani baada ya kumsindikiza rafiki yake alirudi nyumbani  ,anaingia anakuta nyumba ipo kimya ,adinani aliita ,nusraaa!!!
Mudrick!!! Hapakuwa na mtu shangazi aliitika na kusema "kwani hao watoto hawapo?
Adinani alijibu ndio hawapo halafu mbona umeme hamna wakati nimeweka sio muda wa elfu mbili ina maana umeisha?
Adinani akaenda kwenye mita namba kuangalia alikuta uniti zipo alirudi ndani upesi na kwenda kuangalia kwenye main switch alikuta imezimwa ipo off.
Adinani aliwasha ndipo umeme ukawaka aliangalia dirisha alikuta lipo wazi.

Adinani akajua hapa hamna usalama "adinani alichukua simu yake na kumpigia zumra ,haikupita dakika moja simu ikapokeleea
Haloo adinani zumra aliongea 
Zumra akina nusra siwaoni nyumbani sijui wameenda wapi halafu hapa nyumabani mazingira nimeyakuta yako tofauti.
Zumra aliuliza nini?,wakati huo walikuwa wapo kwenye foleni tayari washafika tabata ya relin sehemu moja kuna roud about.
Kutokana na foleni 
Zumra alivyopata hizo taarifa alizunguka ile raund  abauti gafla gari yake ikagongwa na piki piki kwa mbele.
Ile piki piki ikadondoka
Aliyekuwa anaendesha nae alidondoka na mzigo wake ambao alikuwa amefunga kwa nyuma ,aliinuka upesi ili aiwashe piki piki 
Ile piki piki ikagoma kuwaka.

Yule dereva hakujali piki piki aliufungua mzigo wake ambao ilikuwa roba ili aubebe wakati huo zumra ,suhaila baada ya gari yao kugongwa kwa mbele walishuka maana taa ya mbele iligongwa 

Walikuta yule mtu anauweka mzigo wake begani ili aondoke ,zumra anamazoezi mno aliruka na kukanyaga piki piki ya yule kijana kisha akampiga teke la kifuani yule mtu akamwambia unaenda wapi wakati umeharibu gari yangu.
Yule mtu alipepesuka na kuachia roba lake.
Lile gunia lilidondoka wakati huo watu washajaa. Baada tu yakusikia ajali.

Yule jamaa kuona vile alikimbia na kuondoka ,gafla sauti ya mtoto ilisikika kwa mbali ikiita kakaaa, kakaaa
Kila mtu aligeuka na kuuliza mtoto wa nani anaita kaka
Kutokana na giza huku taa za gari kumlika 
Neema alisema jamani nasikia sauti ya mtoto kwenye hili roba.
Ile roba ikafunguliwa ,walishangaa kukuta watoto wawili wamefungiwa humo.

Zumra aliwasha taa ya simu ile anamulika alikutana na sura ya nusra akiwa ametapakaa damu usoni,walimtoa mtoto wa pili ambae ni mudrick masikini alikuwa kimya ,uso hautamaniki kwa damu.
Walivyowafungua kamba walishangaa kuona mguu wa mudrick umevunjika ,zumra aliita nusraaa nusraaaa  kumbe nusra nae alikata moto  akapoteza fahamu kabisa.
Suhaila ,neema na zumra wakabaki kuangaliana.
Umati wawati walijaa na kushangaa ukatili wa watoto wadogo kufugwa kwenye gunia.
Wakati askari wa usalama bara barani nae alishuhudia ndipo alitoa amri hao watoto wawahishwe hospitali upesi sana.

Zumra na wenzake waliwapakia akina nursa kwenye gari yao maana hali zao ni mbaya kutokana na lile gunia kudondoka ,yaani watoto walipigiza vichwa vyao kwenye lami.

Watoto walipelekwa moja kwa moja mhimbili maana hospitali zingine walishidwa kuwapokea kutokana na hali zao mbaya.ile piki piki iliyowagonga ilikamatwa na kupelekwa kituoni huku aliyehusika na tukio alikimbia.
Zumra alimpa ujumbe adinani" watoto tumewapata kimungu mungu ila wanahali mbaya alimwomba awahi mhimbili .
Adinani alimchukua shangazi yake ambae haoni na kumpeleka kwa mama mick alifika na kuwaomba alale hapo yeye anaenda muhimbili kuwaona wadogo zake wamepata dharura ya gafla

Mick aliuliza "adinani usinitanie bana si nimeondoka sasa hivi nimewaacha wanajifunza kuchora sugura muda si mrefu iweje uniambie wako mhimbili.
Adinani akiwa anatiririsha machozi alimwambia ",mick hata mimi hainiingii akilini ila twende tukajiomee wenyewe.

Waliondoka hadi mhimbili wanafika wanaambiwa wasubiri maana wadogo zake wanahali mbaya, hasa  mudrick inaonesha kichwa kimeumia mno hivyo anatakiwa afanyiwe upasuaji ili kutoa damu isigusane na ubongo
Nusra alionekana kukosa pumzi vile vile alivyopigiza kichwa kwenye lami ndio kilipelekea kupoteza fahamu ,pia alionekana kuvimba lipsi ,amechumbuka puani na kwenye paji la uso.

Adinani alikabidhiwa roba ambalo wadogo zake walikuwa wamefungiwa ndani ,adinani macho yake yakiwa yamejaa machozi aliyapangusa na kutizama na kuona damu nyingi zilizomwagika

Dokta aliomba upesi kaka yake apimwe ,kama damu zitaendana ili mudrick aongezewe laa sivyo anapoteza maisha.
Adinani alipima kilo alikuwa na kilo chache mno'kilo 49 hivyo ni hatari kutolewa damu hata yeye anaweza kupoteza maisha lakin damu zake na mdogo wake zilikuwa zina landana.

Kutokana na adinani kula chakula kidogo ,vile vile anashinda kwenye kaz ,hivyo mwili wake ulikuwa hauna afya nzuri kutokana na kukosa muda wa kupumzika.
Dokta alimwambia hapana kilo zako hatuwezi kutoa damu maa a hata wewe unaweza kupoteza maisha.

Adinani aliomba awaone wadogo zake ,kwa mara ya mwisho ili atolewe yeye damu hata nikifa basi nitakufa bila kinyongo ila wadogo zangu wapone,
Dokta alimruhusu adinani akaingia kwenye chumba ambako wapo wadogo zake hakuweza hata kutembea alilia na kujutia kuwapoteza wazazi ,wamemwachia kazi nzito mno.
Alitizama nusra ambae hajazinduka ,akamwangalia mudrick ambae anahitajika kufanyiwa upasuaji kichwani adinani akakumbuka na  tukio lake ambae alikatwaga shingo na msumeno.

Adinani alitoka na kumwomba dokta amfunyie upasuaji mdogo wake ili aokoe maisha yake ,adinani  adinani alipewa fomu akajaza kuwa anakubali afanyiwe upasuaji

Yeye nae alipelekwa chumba maalumu akatolewe damu ,adinani alimwomba dokta kama hatojali ,damu yake itolewe yote ,wadogo zake wawekewe hata yeye akifa sawa ila wadogo zangu wapone.
Dokta akimwangalia adinani akaishia kutikisa kichwa na kuonekanika anaumia wadogo zake kuwa katika hali ile.

Adinani alitolewa damu hadi akawa anajisikia kizungu zungu ,kutokana na damu zake kuwa chache ,kusimama hawezi nae ikabidi alazwe maana hali yake nae ikawa mbaya.

Hadi saa nane usiku ndipo nusra alizinduka "wakati huo mudrick amefanyiwa upasuaji na ameshatundikiwa dripu ya maji na damu.nusra alivyofumbua macho cha kwanza aliongea ",danieĺ niue mimi mwache kaka yangu mudrick ,daniel nifunge mimi mwache  mudrick.

Dokta walishangaa na kuuliza daniel ni nani?,nusra akiwa hajielewi alizidi kuongea"daniel wewe ni mbaya sana nifunge kamba mimi mwache mudrick.
Dokta alisikiliza kisha alimwita polisi nae alisikiliza  walienda kwa adinani ambae nae alionekana mwili wake kukosa nguvu walimuuliza unamjua daniel?

Adinani alifumba macho na kuwaambia namjua ila kwa sasa si zungumzi chochote najisikia kulala ,moyo unanienda mbio
Wakati huo zumra na wanzake wao walienda nyumbani huku wakimwacha mick awaangalie watoto pamoja na kaka yake.

Asubuhi panakucha polisi walifika hospitali ya mhimbili kwa ajili ya kumhoji adinani kama anawajua hao watu ,vile vile na piki piki ambayo wameikamata.
Unamjua daniel maana mdogo wako alivyozinduka anamtaja daniel 
Adinani alitiririsha machozi na kusema namjua kwa sura ila kwasasa sijui anakokaa ,
Sawa pia kuna piki piki tumeikamata yenye namba...alimtajia 
Kitenda cha askari kutaja zile namba adinani alishituka mno .hizo namba bado anazikumbuka ndio za piki piki yake ambae aliibiwa na akina kelvin

Yaani hadi sasa haijabadilishwa plot namba,adinani akiwa na hali mbaya aliwaeleza hio piki piki ni yakwake na ashaibiwa nae tayari ashailipaga kituo cha polisi na hana deni
Vile vile hio piki piki nilipewa mkataba na juma.

Unapajua kwa juma?,adinani alijibu ndio napajua,basi polisi waliwaacha wapumizike wakiwa sawa wataanza upelelezi

Tukirudi kwa kundi la juma walikutana maeneo ya kinyereze ",",unauhakika hao watoto wamekufa,ilikuwaje usababishe ajali ugonge gari ya watu halafu kibaya zaidi piki piki umeiacha ,hebu niambie kelvin akili zako ziko sawa?
Kelvin aliwaza na kusema sikuwa na namna mtoto mmoja sijui alitoa vipi matambara mdomoni na ndio aliita kaka watu wote wakasanukia dili.
Juma aliinamisha kichwa chini na kusema kwa sasa tumelikoroga wenyewe tusipo angalia tutalia na kusaga meno ,ikijulikanika tu tumekwisha ,
Daniel fanya kitu kimoja ile nyumba ya kijana leo kapige moto usiku wa manene ,ili tukifanya hivyo tuwavufuge wasiweze kufuatilia hili la kupatikana kwa watoto kufungiwa kwenye toba

Daniel alikohoa kidogo na kusema usijali nitaenda  kuiteketeza na moto leo usiku.
Tukirudi hospitali ,nusra ndio alirejewa na fahamu na kuomba akamwone kaka yake ,nesi alimchukua hadi chumba aliko lazwa adinani maana toka alivyotolewa damu hakuweza hata kutembea mwili wake ulikosa nguvu,
Nusra alifika na kukuta kaka yake amefungwa dripu anaongezewa damu pamoja na maji ,maana nae ilibidi aongezewe damu laa sivyo angekufa
Nusra alimuuliza nesi ",mbona kaka mmemfungia mirija hii ya juice ambayo inafanana kama ya mama joy anavyotengeneza juice ya embe kwanini mmemfunga na hilo chupa la maji?

Nesi alimwangalia na kumwambia anaumwa hapo anaongezewa maji",nusra alimwangalia nesi na kumuuliza ,",inamana kaka anaumwa hadi hawezi kunywa maji na mdomo?,
Nesi aliona nusra anauliza maswali magumu alimtoa na kumpeleka chumba cha mudrick 
Ile wanafika wodi aliyoko mudrick waliona dokta anaenda upesi huku amebeba vifaa,

Yule dokta anafika mlangoni alikutana na dokta mwingine mwenye simanzi na majonsi ,alimwambia dokta ushachelewa huyu mtoto tayari
Wakati huo akina zumra na suhaila na wao ndio wanafika walisikia kisha waliuliza kwa pamoja ,mudrick amefariki?

JE NINI KITAENDELEA?
"


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: