NAITAFUTA FURAHA YANGU 16
Story;NAITAFUTA FURAHA YANGU
-----sehemu ya 16----
Tulipo ishia jana, Yule dokta anafika mlangoni alikutana na dokta mwingine mwenye simanzi na majonsi ,alimwambia dokta ushachelewa huyu mtoto tayari
Wakati huo akina zumra na suhaila na wao ndio wanafika walisikia kisha waliuliza kwa pamoja ,mudrick amefariki?.
Dokta alishika upara wake na kusema ,kazi ya mungu haina makosa ,kisha akaondoka lakin dokta mwingine aliwaangalia akina zumra na suhailah aliona wanatiririsha machozi ,hakutaka kuamin kweli mudrick amefariki alienda wodi ya adinani alibeba vifaa vya kushitua mapigo ya moyo.
Aligusa mikono ya mudrick ya baridi halafu alikuwa tayari ashafunikwa shuka hadi usoni
Dokta alifunua alikutwa kweli sura ya mudrick imebadilika ukimwangalia ni kama wa blue flani
Dokta alijaribu kushitua mapigo ya moyo ya mudrick ,alishangaa kwa mbali mudrick anashituka.dokta alishangaa ,alirudia tena kushitua mapigo ya moyo kumbe mtoto bado mapigo yake yalikuwa yanadunda kwa mbali
Wakati huo zumra na mwenzake walienda chumba cha adinani ambako nae alikuwa bado katundikiwa dripu za kuongeza damu,suhaila alikuwa wakwanza alikuta adinani yuko na mdogo wake nusra ,na nusra ndio alikuwa anamtoa matongo tongo kaka yake usoni huku akiongea
"Kaka yaani huku sijui umepapendea nini watu wengi ,mi nataka turudi nyumbani huku kila mtu analala kitanda chake ,mie nataka nikalale na shangazi yangu ,maana shangazi huwa ananikumbatia na kunifunika sasa huku nafunikwa na watu ambao siwajui.
Adinani alimshika mdogo wake ambae hajui kama yupo hospitalin na wamelazwa yeye anajua wapo wamelala kwa watu ,alimwambia hapa tunasubiri mudrick aamke ndio twende nyu...
Hakumalizia adinani alimkuta suhaila amesimama mlangoni akitiririsha machozi,mara zumra nae alikuja akiwa analia ,alishidwa kujizuia alimwegemea suhaila zumra alilia kwa nguvu.
Nusra aliwaangalia na kuwaambia "anti zumra mwenye nywele ndefu kuna mtu amewapiga?,mbona mnalia nyote?,au mama yenu amewachapa?,
Suhaila alishidwa kujizuia alimwambia "adinani mdogo wako mudrick amefariki
Adinani aliinuka upesi wakati huo ashachomoa dripu ,kitendo cha kuinuka upesi ,adinani toka ametolewa damu amekuwa akijisikia kizungu zungu ,hivyo alivyosimama aliyumba na kuwadondokea akina zumra.
Zumra yupo chini adinani yupo juu yake adinani analia ,zumra nae analia,
Suhaila aliwainua lakin pale pale adinani akili ziliruka kabisa .alitoka nje ya hospitali akiita mama na baba yaani alisahau kabisa kama ameambiwa mdogo wake amefariki.
Wakati suhaila anakimbia ili kumrudisha adinani ambae alikuwa analia na kuita baba na mama kwa nguvu,zumra aligeuka na kuona madaktari wanaingia wodi ya mudrick wakiwa wamebeba vifaa.
Zumra alimuuliza dokta ,mbona mnaingia kwenye hio wodi kuna nini?,dokta akajibu yule mtoto bado hajafa na mapigo ya moyo yameanza kurudi taratibu zumra alifuta machozi na kusema mungu msaidie huyu mtoto apone.
Wakati huo manesi walimkamata adinani ambae amechizika baada ya kupokea taarifa mdogo wake amekufa,walimrudisha kwenye wodi na kumchoma sindano ya usingizi
Hazikupita dakika kadhaa adinani alipitiwa na usingizi ,hadi mida ya saa saba mchana mudrick akawa anahema vizuri ila macho bado hajafungua wala kuongea huku kaka yake nae amelala baada ya kudungwa sindano.
Suhaila na zumra walimchukua nusra na kwenda kumtafutia chakula wakiwa wanakula nusra alianza kueleza maana nusra hakupoteza kumbu kumbu yeyote",
Anti ,mlivyoondoka nyie kaka nae alimsindikiza mudrick umeme wa nyumba yetu ukakatika
Nilitoka nje kuangalia kwa akina kasimu kama umeme upo nikashangaa nafunikwa mdomo ,halafu nikapigwa mguu nikadondoka vibaya anti ,nikaumia uso si unanona vidonda vyangu ee hivyo usiniwekee chili kwenye chipsi yangu weka tomato tu.
Basi suhaila alimwekea tomato kwenye chipsi ambayo wamemnunulia ili ale, nusra akaendelea kueleza "kuna piki piki ilikuwa inapita hapo kwenye hio njia inayoenda kwa mama joi ilimulika vizuri nilivyoangalia nikaona alikuwa daniel ambaye alikuwa anakaa kwetu pale.alikuwa mwenyewe kabisa.
Basi akanifunga miguu na mikono akaniingiza kwenye roba kisha mudrick nae wakamuweka walitufunga kwenye piki piki
Uso wangu ulikuwa karibu na mikono ya mudrick basi tukiwa kwenye piki piki huku tumefugwa roba kaka mudrick akiwa anahema huku mikono yake inajoto kali alinipapasa uso ,
Ndipo alikutana na mdomo wangu unamatambara pale pale kaka akanitolea hayo matambara kwa mikono yake nae sijui alikiwa amefugwa kama mimi hivyo sikuona
Ndio maana mimi niliweza kuita kakaa sababu mdomo wangu haukuwa na matambara
Hapo akina zumra ndio wakaelewa hawa watoto walikuwa wametekwa ,suhaila aliuliza
Nusra bibie ulivyokuwa kwenye gunia ilikuwaje ?,
Nusra aliinuka na kuziba pua yake na mdomo kisha akasema nilikuwa nakosa hewa ya kuhema.
Zumra na suhaila waliwaonea huruma sana akina nusra mateso waliyopata ni historia katika maisha yao.
Walimaliza kula kisha wakachukua chakula cha adinani walimpelekea walikuta tayari ashaamka adinani alikula ,siku hio zumra na sauhaila walishinda hospitalini hadi usiku.
Tukirudi nyumba anayokaa adinani kundi la juma lilitumwa likachome nyumba ya adinani maana wameshidwa kuimiliki ,na wanahisi huenda sasa wale watoto washaanza kuwahisi kuwa wao ndio chanzo cha wazazi wao kufa ,hivyo wanaona heri kuichoma ile nyumba ili kuwafukuza kabisa eneo hilo.
Usiku wa manena ,siku hio daniel kama kawaida yake alibeba dumu la petrol na bomba akiwa amefunika uso wake alitoboa dirisha kisha akaingiza mpira na kuanza kumwagia petroli ndani ili awashe moto ,
Kwa bahati mbaya pasina kujua ndani ya hio nyumba ,mick alienda kulala ili kuilinda nyumba ya rafiki yake.
Mick akiwa amelala alishangaa kuona miguu yake inamwagiwa kitu cha baridi ,mick alihisi ni maji ,lakini alianza kuisikia harufu ya petrol,micka alishituka pembeni palikuwa na ndoo ya maji ,basi aliitenga ndoo ya maji upesi
Nje wakati daniel anamwaga ile petrol haikumwagikia chini bali ilimwagikia kwenye ndoo yenye maji.
Daniel alimaliza kumwaga alipiga njiti ya kiberiti kisha akairusha kwenye hilo tobo la kwenye dirisha ,mick akiwa ndani aliidaka na kuizima ile njiti kabla haijagusana na petrol,
Daniel alivyofanya hivyo hakusubiri aliwasha piki piki na kuondoka eneo hilo huku akijua kazi ashamaliza kama alivyofanyaga kwenye duka la baba yake adinani.
Aliondoka moja kwa moja hadi kwa juma.
Alifika na kuipaki ile piki piki ,alimkuta juma na kelvin wakinywa pombe ndani ya nyumba ya juma.
Daniel alifika akiwa anajitapa ,alianza kuongea "wale watoto basi kwa sasa itakuwa ni mwisho wa habari yao ,nimeshachoma nyumba ,juma aliuliza unauhakika moto umewaka au unasema tu kwa kuwa nimelipa pesa.
Ha ha daniel alicheka huku akimimina bia kwenye glass na kusema kwani kwenye duka la ally nilifanyeje si nilifanya kama leo ,we kesho ukaangalie tu jinsi nyumba ilivyoungua.
Hatimae palikucha asubuhi kabisa keherehere juma alifika eneo lile mapema akiwa anachekelea na kuamini hio nyumba imeteketea cha ajabu anafika eneo lile anakuta nyumba ipo vile vile ,tena walikuwa wapo na daniel.
Kuna mtu alikuwa amekaa choo cha jirani akiwa na kamera yake safi alitegesha vizuri na kuweka tageti ya kurekodi.
Juma aliuliza "we daniel si uliniambia umemaliza kila kitu ,sasa imekuwaje mbona nyumba ipo vile vile ,daniel alijibu kwa sauti ya chini wakiwa wamesimama karibu na choo cha jirani yake adinani.,
Twende ukaone mahali nimetoboa na kumwaga petroli tena nilipiga na njiti kabisa huenda njiti imezimika.
Walizunguka kwenye nyumba ya adinani na kuchunguza waliamini ni asubuhi hamna mtu aliyewaona.
Kwenye choo cha jirani kuna mtu aliendelea kuwapiga picha ,daniel na juma,yule mtu ambae alikuwa amevalia juba na kufunika uso wote ,alikuwa kavalia kiislamu juu mpaka chini alitoka chooni kisha akapishana na akina juma,aliwatizama tu huyo mwanamke ndio ambae alikuwa anawapiga picha pasina juma na daniel kuwajua.
Juma waliwasha piki piki na kuondoka.tukirudi hospitali asubuhi kabisa mudrick alifunua macho yake ,akiwa haongei chochote ,siku hio mama mick aliwahi kufika hospitalini ili kuwaangalia wanaendeleaje.
Mama aliruhusiwa akaingia kwenye chumba cha mudrick akiwa ameongozana na nusra.
Nusra alifika na kukuta mguu wa mudrick umefugwa gamba jeupe na gumu (p.o.p).
Nusra alimwangalia mudrick kichwani na kuona bandeji sehemu ambako amefanyiwa upasuaji
"Nusra alikaa chini na kutiririsha machozi alisogea hadi amelala mudrick kitandani "aliushika mkono wa mudrick akaanza kuongea "aliita mudrick inamana kwa sasa hutaweza kucheza na mimi,shuleni hutaenda tena ,umevunjika mguu,utakuwa wakulala tu.
Mudrick uliniahidi utahakikisha na kuwa na furaha ,shuleni naonewa kila siku ,nani atanisaidia "nusra alilia mno.
Mudrick alimwangalia tu nusra pasina kufanya chochote.
Mama.mick nae aliumia ,yaani watoto walikuwa kwa upendo sasa mmoja kavunjika mguu na mwingine mzima.
Nusra akiwa analia alitoka ndani ya wodi akiwa anakimbia kwa maumivu ya mwenzake kuvunjika mguuu
JE NINI KITAENDELEA?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: