NAITAFUTA FURAHA YANGU 17





Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU


____sehemu ya  17_____
       Tulipo ishia jana,ni pale nusra na mama mick walivyoingia wodi ya mudrick ili kwenda kuona hali yake ,nusra alianza kuongea maneno yaliyojaa majonzi,nusra alilia mno.
Mudrick alimwangalia tu nusra pasina kufanya chochote.
Mama.mick nae aliumia ,yaani watoto walikuwa kwa upendo sasa mmoja kavunjika mguu na mwingine mzima.
Nusra  akiwa analia alitoka ndani ya wodi akiwa anakimbia kwa maumivu ya mwenzake kuvunjika mguuu.

Ile anatoka alikutana na adinani ambae nae afya yake kwa sasa ilikuwa njema walitoka na kwenda wote tena kwa mudrick ,lakin nusra alifumba macho hakutaka kuona mguu wa mudrick uliovunjika maana anaumia mno.

Nusra kwanini ,unafumba macho"hiiiii hiii sitaki kuona mguu wa mudrick kaka ,nusra alijibu kwa sauti iliyoambatana na kilio,basi muda wao walipiwa ni mdogonwalimwona mudrick ,ambae kwa sasa  hali yake yatia matumani ukimwangalia ,anafumbua macho vile vile kuongea anaweza ila sauti ipo kwa mbali mno.

Tukirudi maeneo ya sinza ndipo mick aliitwa na akina zumra pamoja na suhaila ,mick aliweza kwenda hakukataa wito maana aliona rafiki yake anaurafiki pia na hao wadada.mick alishangaa jumba wanaloishi wale wadada lilikuwa lakifahari sana ,mick aliamin wazazi wa akina zumra basi wanayo pesa.

Mick akiwa anashangaa ndipo bint mmoja aliingia  akiwa amevaa ushungi ,baibui kubwa yaani alikuwa anaonekanika macho tu.
Alifika sebuleni aliweka kamera yake kubwa mezani na kuvua nikabu yake ,hapo ndio mick alishangaa kumwona suhaila.

Khaa suhaila.wewe ndio ulikuwa umevaa kama nikabu hii ,mie nikajua labda mama yako niko nahangaika kukusalimia shikamooo
"Marhabaaa suahaila aliitikia na kufanya wote wacheke.mara zumra nae alikuja sebuleni kisha akauliza " ehe suahaila umeweza kupiga picha au kuwaona hao watu?

Suhaila aliishika kamera kisha akatoa flsha ambae anaitumia,alichukua laptop kisha akaweka ,aliwaambia haya mtangalie mick ukiwajua hawa watu uniambie maana nimewakuta kwenye nyumba ya akina adinani wakizungumza utumbo ,tena kuna clips zingine nimewarekodi

Zumra aliuliza "usiku ilikuwaje wamwagie petrol kwenye nyumba ya watu ,ndio walikuwa wanataka kuichoma ama?,mick alijibu ndio walitaka kuichoma,zumra aliendelea kuuliza " kwani adinani ana ugomvi gani na hao watu hadi watake Kumchomea nyumba jamani.

"Mick alianza kuwapa story njinsi ilivyo" toka wazazi wake walivyopataga ajali na kufariki ,ndipo adinani na wadogo zake walianza kuishi maisha ya tabu sana "nakumbuka kuna siku adinani wakati anafanya kazi ya uboda boda alikujaga na hati ya nyumba yao na kuniambia nikae nayo ,maana kuna watu wanaitafuta hio hati ,kisha akaniambia anahisi wanataka kumnyang'anya ile nyumba.
Vile vile ,kuna siku tena adinani alikujaga kulala kwetu siku nilivyomuuliza kulikoni " aliniambia amewasikia kwa masikio yake mawili "juma na daniel wanazungumza wao ndio waliwaua wazazi wake ,kwahio mie nahisi atakuwa huyo juma na daniel ndio wanataka kuchoma hio nyumba.
Zumra alitikisa kichwa kuashiria ameelewa mchezo wanao mchezea adinani ,yaani hadi wanataka kuwaua.

Suhaila alianza kufungua picha kwenye laptop alizopiga huku akimwonesha mick kama anawajua hao watu.
Alianza picha ya juma aliuliza " mick unamfahamu huyu mtu ?
Juma alijibu ndio namfahamu anaitwa juma na ndio alikuwaga rafiki mkubwa wa baba yake adinani lakin baada ya baba adinani kufariki ,akabadilika na kujitenga kabisa na akina adinani

Suhaila akaendelea kuonesha picha nyingine ilikuwa ya daniel ,umeiona hii picha?,ndio namjua ,huyu anaitwa daniel alikuwa mpagaji kwenye nyumba ya adinani.

Zumra aliwambia "mick asante kwa kutuambia ,sasa hawa watu tutawanasa tutawafuatilia pasina  wao kujua halafu kitakacho wakuta watajuta.
Suahaila alimwambia zumra " ni kweli daniel ndio alitaka kuwaua akina nusra ,maana nusra alivyozinduka hospitali alitaja daniel usimuue mudrick.
Okay tujiandae tukawaone hospitali tujue wanaendelea ,basi walitoka nakwenda hospitali waliwaangalia na kuwapelekea chakula.

Mara zumra alipigiwa simu na baba yake ,akiitwa nyumbani ,zumra hakubisha alienda moja kwa moja hadi masaki ndiko anakoishi baba yake,alifika na kuingia ndani
Zumra kufika ndani alimkuta baba amekaa na kijana ambae zumra anamjua.
Baba aliita "mwanangu njoo ongea na mwenzako amekuja kukuona ,

Zumra alijisemea moyoni " baba kwanini unanifanyia hivi?,zumra alitoka hadi sebuleni alimsalimia yule kijana mwenye asili ya uarabu uliochanganyika na uswahili "baba alianza kuongea " mwanangu kama nilivyokuambia mchumba niliokutafutia ndio huyu hapa anaitwa "mohamedi ,baba ake ni mtu anaemiliki kampuni kubwa kubwa pia kwao wanaishi dubai ,kama nilivyokueleza mwanangu sitaki uje uishi maisha ya tabu ndio maana nimekutafutia mchumba kwakuwa ushamaliza masomo yako ,basi kwa sasa ni muda mwafaka wa kujuana na huyu mchumba.
Zumra alichofanya ,alimsalimia mohamedi kisha akamwambia baba siko tayari kuolewa na huyo mtu ,si chaguo langu mimi nina uhuru wa kuchagua mme ninaye mpenda mimi ,halafu baba pesa unayo kuna haja gani ya kutafuta mwanaume ambae kwao wanamiliki makampuni.
Zumra aliondoka na kuingia chumbani kwake.

Mzee alimtizama mohamedi ambae ni mtoto wa rafiki yake na waliahidiana mtoto wako akikua ataolewa na mtoto wake.mzee aliwaza na kumwambia " mohamedi usijali nitamshawishi mtoto wangu naimani atakubali ila nadhani umemwona ,kijana alitikisa kichwa na kujibu
"Nimemwona pia nimempenda na naomba pia utumie kila njia akubali ili nimuoe na tutimize ahadi zenu .
Mohamed nae aliaga na kuondoka.

Maeneo ya kinyerezi ndipo juma ,daniel na kelvin ,walipanga mbinu za kwenda kuichoma ile nyumba " halafu leo mchana nimeshinda maeneo hayo ,sijaona wale watoto au walishafariki maana hata kwenye vyombo vya habari sijawasikia wakitangazwa.
Juma aliwaangalia kelvin na daniel ,kisha akaongea "hivi mshawahi kuwaza itakuweje endapo tukajulikana unahisi ni kitu gani kitatokea ,daniel alicheka na kusema haiwezekana ,wale watoto wadogo  watatukamataje na akili zetu zote.

Juma alitikisa kichwa na kusema hio nyumba iteketee leo lazima na si hiyari ,wakati huo hospitalin hali ya mudrick ilianza kuwa poa baada ya kufanyiwa upasuaji kichwani pia mguu wake uliovunjika nao ulifugwa ,alianza kuongea kidogo kidogo.

Usiku uliwadia ,huku suahila pamoja na zumra walitafuta vijana watatu na kuwapa kazi ya kwenda kulinda nyumba ya akina adinani ili kama akina juma watasubutu kufanya hivyo waweze kuwanasa na hapo ndio itakuwa mwisho wake.

Mida ya saa mbili usiku ,suhaila alikawa amejipumzisha kwenye sofa ndipo usingizi ulimpitia analianza kuota ndoto mbaya.
Alianza kuota tukio ambalo lishawahi. kutokea  akiwa mdogo wa miaka mitatu " watu walivamia chumba chake usiku na kuvunja mlango ,walimvalisha mfuko usoni asiwese kushuhudia ndipo sebuleni baba na mama yake walitekwa na majambazi.

Mama alipigwa risasi ya kichwani ,pale pale akapoteza maisha ,baba alipigwa risasi ya kifuani karibu na moyo ,alipigwa mguuni alipigwa na begani.baba alidondoka chini akiwa hajielewi.
Baba akiwa anasikia maumivu makalina alisema "mimi wakufa moyo wanienda mbio kila kitu chukueni ila binti yangu suhaila bado ni mdogo naomba mwacheni akiwa salama ,mali zote chukueni msituue familia nzima

Suhaila alishuhudia baba yake akipigwa risasi ya kichwa ,pale pale suhaila akatamka " nendeni kwenye chumba cha baba kile kule ,chini ya kitanda kuna sanduku kubwa lenye pesa ,mkachukue msimuue baba yangu.
Wale wavamizi ama majambazi walikuwa na uchu wa pesa walimwacha suhaila na kukimbia kiliko chumba cha baba yake ,pale pale suhaila alipata mwanya na kukimbia wakati anafika mlangoni alipishana na mlinzi akiingia na kuchukua lile sanduku la pesa.

Alikuwa amevalia nguo za kawaida ,ile akiwa anakimbia alidondosha kofia ambayo alikuwa ameficha uso.wakati huo suhaila amejificha kwenye maua aliweza kuifahamu.

Ilikuwa sura ya mlinzi wao ambae alikuwa akilinda getini,na ndio mlinzi aliwaambia majambazi tokeni ,twendeni tukimbie kabla polisi hawajafika.
Jambazi mmoja alimulika mlinzi wao taa usoni ,suhaila akiwa amejificha alishuhudia alikuwa ni juma ambae alikuwa analinda nyumba yao.
Pale pale suhaila alizinduka kwenye ndoto akiwa amejiegesha kwenye sofa ,moyo wa suhaila ulienda mbio ,aliweza kuitambua sura ya mtu aliyehusika na kifo cha wazazi wake ni  juma
Pia juma huyo huyo ndio anataka kuchoma nyumba ya akina adinani

Je nini kitaendelea?


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: