NAITAFUTA FURAHA YANGU 18
Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
----sehemu ya 18----
Tulipo ishia jana kwenye ndoto aliyoota bibie suhaila ni tukio ambalo linamuumizaga sana, Ilikuwa sura ya mlinzi wao ambae alikwa akilinda getini,na ndio mlinzi aliwaambia majambazi tokeni ,twendeni tukimbie kabla polisi hawajafika.
Jambazi mmoja alimulika mlinzi wao taa usoni ,suhaila akiwa amejificha alishuhudia alikuwa ni juma ambae alikuwa analinda nyumba yao.
Pale pale suhaila alizinduka kwenye ndoto akiwa amejiegesha kwenye sofa ,moyo wa suhaila ulienda mbio ,aliweza kuitambua sura ya mtu aliyehusika na kifo cha wazazi wake ni ya juma
Pia juma huyo huyo ndio anataka kuchoma nyumba ya akina adinani.
Suhaila aliinuka na kujihisi mpweke kwenye huu ulimwengu alinyanyuka na kwenda kitandani ambako alianza kukumbuka ,baada ya wale.wezi kukimbia yeye alirudi ndani na kukuta baba na mama washafariki ,alilia sana ndiposiku hio suhaila aliondokaga nyumbani na wala hakurudi tena.
Suhaila kumbu kumbu zake za udogoni bado anazo ,alitaka kumjibu juma wewe si ndo umetoka na sanduku la pesa za baba na kuwambia wauaji waondoke polis wanakuja ,kila akitaka kumwambia suhaila anahisi mdomo mzito.
Suhaila hakusema chochote,
Juma alizidi kujifanya nae amepigwa mno ,ndipo majirani na polisi waliweza kufika eneo lile, juma ni mjomba wake kabisa na ndio alipewa kazi ya kulinda nyumba na baba yake,maana ndie alikuwa kaka yake mama.
Suhaila akashusha pumzi na kujiesemea ,juma ,jumaa ulinifanya nikateseka miaka kumi na mbili yote ,yaani shulee sijasoma nimekuja kujifunzia ukubwani ,kwanini juma wewe ni katili namna hii."suhaila aliendelea kukumbuka ,baada ya polisi kufika nyumbani kwao waliwachukua mama na baba kwenda kuwafanyia uchunguzi ,baada ya hapo walirejeshwa na kuzikwa ,wauaji hawakujulikana hadi leo hata jeshi la polisi waliipotezea hio kesi.
Mwaka mmoja ulipita baada ya wazazi suhaila kufariki ndipo juma ambae aliishi kwenye ile nyumba ,aliamua kuiuza ile nyumba .tena hakumwambia hata suhaila ,.japonalikuwa akimwona suhaila akikatiza mitaani hakumpa.hata mia ya kununua andazi.baada ya muda suhaila alirudi nyumbani na alikaa siku tatu ndipo baada ya hapo
"Mtoto alishangaa usiku gari inaingia na vitu ,aliyenunuua alikuja kuahamia na alimkuta amelala ndipo aliwauliza ninyi ni akina nani?,alikuwa mzee mwenye mvi za wastani alimjibu "we mtoto hii nyumba tumeinunua na tumeuziwa na juma ,ambae ndiye mmiliki wa hii nyumba na juma ashaondoka ,hapa umebaki wewe sasa hatutaki kujua tunaomba utoke.
Suhaila alijikuta hasira zimamjaa kichwani alikuwa ameshikilia glass ya maji aliitupa na kupasuka yote sababu ya hasira.toka siku hio juma hakurudi tena ,nyumba aliuza nyumba pesa akabeba na wazazi wake amewaua ,hapo ndipo suahila alianza kupitia mateso tena akiwa na miaka minne.
Suhaila aliacha kukumbuka hayo matukio aliingia bafuni na kuoga huku kuonekana ana hasira ,aliita jumaaaa ,wewe si mjomba wangu wangu nimesema na sasa nishakugundua wewe ndio umewaua wazazi wangu hakika nisikukamate.
Basi muda ulisogea hatimae saa nane usiku ilitimia ,mji ukiwa umetulia ,mingurumo ya magari makubwa yakinguruma taratibu ,taa za majumbani zimemulika ipasavyo,
Kelvin akiwa ameongozana na daniel waliweza kufika nyumba ya adinani walizunguka nyuma ya nyumba ndipo walianza kumimina petrol tena kwenye tundu ambalo walitoboa ,wakiwa wanafanya hivyo ,kelvin alimwambia daniel ,ujue sisi tumekuwa wapumbavu sana ,jana si umejaribu kuichoma hii nyumba imeshindikanika ,sasa na leo tunakuja ,je kama watu wametushitukia si wanaweza kutukamata tu .
Daniel alimwambia we kelvin nae sijui ukoje ,aliongea huku anatafuna pili pili kichaa ,alimwambia piga kimya hapa hamna wa kutukamata kabla hajamazila walishangaa kuona watu watatu wamewazingira.
Daniel aliweka dumu chini la petrol ,waliulizwa ninyi ndo mnataka kuchoma hii nyumba ee ,kelvin alitoa nondo ili awapasue wale vijana watatu kabla hajafanya hivyo kijana mmoja aliruka na kudunda kwenye ukuta alimkereza ngumu ya sikion tu taratibu kelvin alishuka taratibu na nondo yake kisha akawa chini.
Daniel kuona vile akajua hapa wamekwisha ,aliwatemea wale vijana pili pili machoni ambayo alikuwa anaitafuna.pale ndio aliwapoteza ile wanafumba macho kwa uchungu wa kuwashwa na pili pili ,danile alikimbia na kumwacha kelvin amezimishwa.
Wale vijana baada ya muda walinawa uso zao kisha walipiga simu polisi ,na hapo kelvin alikuja kubebwa na kwenda kuzindukia kituo cha polisi.
Wale vijana waliopewa kazi na zumra walimweleza wamemkamata mmoja na mwingine kawakimbia ila huyu mmoja yupo polisi ,zumra aliwaambia kazi nzuri sana hivyo kesho atawasili kituo cha polis mapema ili kumhoji huyo kijana.
Upande wa pili daniel alirudi kwa juma akiwa anahema ,alimkuta juma yuko na mke wake ,mke wa juma hakupenda kabisa kuona kitendo anachofanya mmewe hivyo alikuwa anatafuta upenyo wa kutoroka ikiwezekana aachane na juma maana juma ni muuaji na katili mwenye kuzulumu mali za watu.
Kitendo cha daniel kurudi huku anahema ,juma alimwambia mke wake hebu toka nje nizungumze na daniel hapo ndio alimpa nafasi mke wake kutoroka mke wa juma alikimbia na kuapa hatorudiana na muuaji maana muda wowote anaweza kumwacha,.
Vip daniel mbona umerudi unahema sana ,juma aliuliza
"Juma nikuambie tu kwa sasa tuwe makin ,tulijua nyumba ya adinani haina mlinzi tunaenda kama twaenda chooni kumbe sio kuna vijana watatu wameweza kutukuta tunamwaga petrol ili tuchome ile nyumba ki ukweli wapo vizur mmoja aliweza kumzimisha kelvin kwahio kelvin amekamatwa mie nimewatemea pili pili nikakimbia.
Juma aliinuka na kupiga meza kwa nguvu ,alianza kuzunguka zunguka ,nyie sasa hivi mnanizunguka labda mbona pesa nawapa kila siku nawaambia ueni hao watoto lakin sasa hali ndio imefikia hivi ,unadhani itakuweje tukigundulika halafu yule kelvin anapenda pesa akiambiwa tunakupa kiasi kadhaa cha pesa mtaje anaekutuma kazi anatutaja mbona.
Daniel aliwaza na kusema ,tumtafute mama mick yule aliyemlipia piki piki tumuue kabisaa maana huenda yeye ameweka walinzi kwenye nyumba ya adinani halafu yeye anaonekanika yupo karibu na adinani.
Juma alisema wazo zuri ,tafuta huyo mama mick ua kabisa maana wanatufanya tunaishi roho juu.
Asubuhi pana pambazuka zumra alienda hospitali na kumchukua adinani pamoja na nusra ili waende kituoni maana kuna mhalifu mmoja wamemkamata.
Suahaila akiwa kwenye gari alikuwa anapekua picha kwenye kamera yake ,kuna tukio ambalo ashawai kuota ,ajali ya piki piki ambayo ilitokeaga maeneo ya tabata relini miezi kumi na moja iliyopita na ndio ambao ilipelekea vifo vya bwana ally na mkewe rahama ,waliweza kupoteza maisha baada ya kugongwa na gari.
Siku hio suhailah alikuwa kwenye sheli hio na alikuwa anaweka mafuta saa nane usiku ,alikuwa ametokea airpot kumpeleka zumra ,gari iliisha mafuta maeneo ya tabata relini ndipo aliingia kuweka mafuta ,
Gafla akiwa amesimama nje ya gari yake akisubiri mafuta ya wekwe alisikia kishindo cha kugongwa kwa piki piki.
Suahaila aligeuka wakati huo alikuwa ameshikilia kamera akiangalia picha ambazo wamepiga na zumra wakati wanaagana uwanja wa ndege.
Alipiga gari picha ambalo liliigonga ile piki piki ,alishuhudia likirudi nyuma kisha likawarudia wale watu na kuwagonga tena ,
Alishuka dereva aliangalia aliyewagonga ,kisha aligeuka na kutizama kama kuna watu bahati mbaya aligeukia upande aliko suhaila ,pale pale suhaila alimpiga picha kelvin
Kelvini aliingia kwenye gari na kupotea ,suhaila alitaka kupiga gari namba zake aliona kabisa hilo gari halikuwa na plot namba.
Leo suhaila aliziangalia zile picha kwa umakini na kumwona huyo mtu aliizoom picha kisha akamwonesha zumra.
Huyu mtu bana kama vile namjua ,ujue huyu mtu aligongaga piki piki flani na kuua watu wawili na nilivyokuwa mdogo wakati wazazi wangu wanauliwa ,pia hii sura ya mtu naikumbuka aliingiaga chumbani kwangu na kunikamata aliniwekeaga kisu shingoni ili anichinje.
Zumra alimuuliza kwahio ikawaje ",nilivyoona hali ya baba yangu kuwa mbaya baada ya kupigwa risasi niliwaambia nendeni kwenye chumba cha baba kuna sanduku lina pesa ,hivyo huyu mtu aliniachia wa kwanza na kukimbilia kiliko chumba cha baba.
Zumra nae aliwaza na kusema ,yawezekana huyo mtu anapenda pesa ,maana lengo lao walitaka kuwaua nyote familia yenu na alivyosikia hela alikuachia na kwenda kulitafuta hilo sanduku.
Basi waliweza kufika hospitalin waliwachukua ,nusra na adinani kisha walienda kituo cha polisi tabata ,ndipo waliambiwa mhalifu wenu amezinduka na sasa yupo sero ,
Zumra aliomba mhalifu aletwe wamuone ambae alitaka kuchoma nyumba moto.
Kelvin aliletwa akiwa amefugwa pingu ,adinani alimwona alishangaa na kushituka mno,aliweza kumtambua ndie aliye mwibia piki piki na kumkata shingo na msumeno na kupelekea adinani kunusurika kifo,pale pale ,nusra aliongea kwa nguvu "kaka huyu mtu ndio alimvunja mudrick mguu na kunipakia mimi kwenye gunia kisha wakatupakia kwenye piki piki ,suhaila kuitizama sura ya kelvin nae alitiririsha machozi ndie aliyehusika na kifo cha wazazi wake ,vile vile anayo picha ambae alishuhudia amewaua watu wawili kwa kuwagonga na piki piki
Je nini kitaendelea?
Mhalifu wa kwanza amekamatwa na amefanya matukio mengi mno
Je atawataja na wenzake?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: