NAITAFUTA FURAHA YANGU 22
Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
---sehemu ya 22---
Tulipo ishia jana, Zumra alivyoona kile kibegi kwa mara nyingine alinyamaza ,na kuniambia naomba kibegi changu.mimi nikiwa natafuna udogo niliangalia mguu wangu ambao unatoa damu.
Gafla niliona kivuli cha mtu akiwa ameshika fimbo kubwa sauti kubwa ilisikika ikisema "nimechelewa sana naona ukenisahau sasa leo nakuonesha vizuri jinsi watoto wanapigwaga.
Babaa usinipigeee baba usinipigeee naenda kuvaa nguo,zumra alipiga kelele baada ya kumwona baba yake ameshika fimbo.lakin baba zumra alivyonitizama mguuni aliona damu kwenye kidonda ,aliuliza wewe mtoto umefanyeje mbona umeumia,kabla sijajibu huyu zumra alidakia na kusema "baba nimemdondokea bahati mbaya hivyo nimemtonesha,
Kwanini unamimbia ovyo ovyo huoni umemuumiza mtoto wa watu?,baba zumra alimgombeza mwanae ,
Basi mie nikiwa natafuna udongo nilimeza na kumwambia bahati mbaya kisha nikainuka ili niondoke ,lakin siku hio mwili haukuwa na nguvu ,nilijikuta na yumba ,baba zumra alinidaka kisha akaita mlinzi nilibebwa na kuingizwa ndani.
Baba zumra alipiga simu daktari alikuja nyumbani alinisafishia kidonda na kuweka dawa ,alivyomaliza ,baba zumra aliwaambia wadada wa kazi waniogeshe niliogeshwa zumra alitoa nguo zake na kunipa nikavalishwa.
Walivyomaliza niliinuka huku nachechemea hadi sebuleni nilimkuta baba zumra akiangalia tv ,nilimwambia "baba asante nashukuru kwa msaada "lakin nilivyotamka neno baba
Machozi yalinidondoka ,maana nilimkumbuka sana baba yangu.
Baba zumra alinitizamaa kisha akaniambia "wewe mtoto si ndo yule ambao tulikukutaga makaburin ukilia ni wewe ama sio wewe.
Nilijibu ni mimi?,akaniangalia kisha akaniuliza wazazi wako wote wamefariki?,nikamjibu ndio huku machozi yananidondoka ,akaniuliza uko unakaa na nani?
Nilimwangalia kisha nikamjibu "toka walivyofariki hadi leo sijawahi kuishi na mtu wala sijawahi kurudi nyumbani wala nyumbani sipakumbuki.
Baba zumra alikodoa macho na kuuliza nyumbani hupakumbuki inamaana umepotea?,nilimjibu sijapotea niliondokaga tu mwenyewe maana nilishidwa kuishi nyumba moja na muuaji.nani muuaji baba zumra aliuliza
Mjomba wangu ndio ameyafanya yote hayo."baba zumra aliwaita wadada wa kazi na kuwaambia wanipatie chakula ,kweli nilipikiwa ndizi na nyama siku hio ,nikatengewa mezani ,kisha nikalishwa na wale wadada ,wakati nalishwa chakula ,zumra alimfuata baba yake na kumuuliza tunaanza safari saa ngapi?.
Baba alijibu saa sita tunatakiwa tuwe tushapanda ndege.
"Zumra akamwambia baba yake "baba siendi huko nataka niende na huyu rafiki ambae anakula nataka niende nae.
Baba alishangaa alimwangalia zumra na kumwambia "tayari tushakata tiketi na huyu mtoto hana pasipoti hivyo hawezi kusafiri ,zumra aliingia chumbami kwake na kusema siendi kamtafutie na yeye tiketi.
Baba alichoka ilibidi apige simu na kuahirisha safari yake kabisa , alikaa wiki nami nikakaa kwenye ile nyumba tukawa tunalala na zumra ,baada ya wiki moja baba zumra nami alinikatia tiket ,pasipot kila kitu ,nikiwa sijui hili wala lile ,zumra aliniambia kesho tunasafiri ,nashukuru nimepata rafiki.
Tukiwa na miaka miine ,nakumbuka asubuhi ilikiwa juma tatu tuliemda airpot tukapanda ndege na kwenda china.kwanza nilikuwa mdogo halafu mie nilijua ndoto zangu zimezimika baada ya wazazi kufariki lakin mungu ni waajabu alinikutanisha na zumra ,basi toka hapo tulianza kujifunza china ,tulisoma masomo ya kawaida ikifika jiono tunaenda judo kufundishwa namna ya kupigana makaratee.
Mimi niliweka jihudi zangu na kujifunza lengo langu siku nikijakumpata juma nimchakaze kabisa nihakikishe roho yake inaishi lakin mwili unakufa.wakati huo zumra ndio alikuwa wa kwanza kujua kupigana ,,watoto wa kichina walitutenga kwa mara ya kwanza maana sie tulikuwa waafrika baada ya kuona uwezo wetu wa kupigana ni mzuri ,kuruka sarakasi ,kucheza michezo mbali mbali ,hapo ndio walijenga urafiki na sisi tulijifunza mambo mengi adinani hivo siwezi kukusimulia yote ni mengi.
Adinani alitabasamu na kuuliza kwahio ninyi mmesoma china toka mkiwa wadogo ,"ndio toka tukiwa wadogo yaani hadi wachina wanajuaga sisi ni mapacha na zumra.adinani aliwaangalia hata mie najuaga ninyi ni mapacha ila kwa sasa nimeelewa.
Adinani alimwangalia sana ,zumra,hadi zumra alijishitukia na kufunika kifua chake alijua huenda adinani anaangalia maziwa yake ,kisha akamuuliza mbona unaniangalia sana?
Adinani alitabasamu na kusema ,"ujue si amini nimeambiwa unajua kupigana asa nikikuangalia haufananii na wapiganaji hata huyu suhaila alinishangaza sana siku ile kituoni sijui aliruka vipi nikashangaa daniel hana jicho moja.
Ha ha suhaila alicheka na kusema "mimi hapo ni cha mtoto huyu zumra unamwona hivi na upole wake anaruka huyu anapaa kama vile kwenye move.
Zumra alicheka na kusema bana mie staki ,kwanza nusra yuko wapi na mudrick ,wote waligeuka na kutizama nje ,walimkuta shangazi amelala .
Zumra aliita "adinani hivi huyu shangazi hanaga jina lake halisi?,maana toka tujuane kila siku tunasikia shangazi tu.
Adinani alitabasamu na kusema "huyu shangazi yetu anaitwa hilda ,suhaila nae akauliza "kwani alizaliwa hivi hivi kipofu au ilikuwaje "?
Adiani aligeuza macho nje na kumtizama shangazi yake alivyolala kisha akawaambia "hata hakuzaliwa hivi,alikuwa anaona vizuri na amesoma hadi darasa la tano ,lakin ilipofika mtihani wa mhula wa pili akiwa kwenye chumba cha mtihani alipewa karatasi ya mtiahani alivyoitizama tu gafla aliona giza ndio hadi leo hakuona tena yaani haoni hata kidogo,
Baba yangu angali yu hai alijaribu kutafuta tiba lakin hakufanikiwa alienda hospitali waliambiwa zile neva za optic zimekufa pia lenzi nae imekufa ,kipindi hicho baba hakuwa na pesa aliacha ,mama nae alijishughulisha kwa tiba za kijadi na za kienyeji hakufanikisha basi ndio ikawa hivyo.
Zumra alitabasamu na kusema "ooh shangazi hilda mbona hilo tatizo ni dogo linaweza kutibika hivyo usijali tuombe uzima tutampelekaga tu china kwa wataalamu.
Suhaila alisimama na kusema "adinani hawa akina nusra si kawaida yao kwenda kucheza nje halafu wakachelewa hivi ,asa leo mbona wamechelewa .ngoja nikawatafute suhaila alitoka na kwenda kuwatafuta akina nusra.
Walibaki zumra na adinani wakiwa wanaongea story za kawaida adinani alisimama na kuchungulia nje ,wakati huo zumra alikuwa amekaa anabonyeza simu yake ,mara mende alitokea ukutani na kumpamdia hadi shingoni
Mamaaaaaa!! Nakufaa zumra alipiga kelele na kuinuka kisha akamkumbatia adinani ,
Adinani alivyomtizama mtoto wa kike aliona mende yupo shingoni akampiga na mkono akadondokea mbali.
Alivyomtizama zumra amelaza kichwa kifuani kafumba na macho halafu amemkumbatia adinani
Adinani alitabasamu ,kisha alianza kuhisi hisia flani ,hivi adinani alitamani kweli zumra angeendelea kumkumbatia lakin haikuwa hivyo "zumra alitoa kichwa baada ya kusikia mapigo ya moyo ya adrano yameenda tofauti ,maana mtoto anakifua laini na kilicho hongoka vichuguu viwili vidogo.vijana wa kileo wanaita saa sita ,zilipogusa tu kifua alisikia raha.
Zumra alifumbua macho na kumwangalia adinani wote walishangaa wanaangalia ,adinani aliwahi na kusema tayari nimempiga huyo mende ameondoka
Ooooh zumra alishusha pumzi na kusema niliogopa eti ujue
Tukirudi upande wa akina nusra leo wakiwa wanacheza walikutana na juma ,juma aliwaita kwa upole kisha akaanza kuwaambia "mudrick na nusra ,mama yenu amenituma amesema mkamwone amewamiss sana,yaani maana amesema niwapeleke sasa hivi?
"Nusra kweli huwa anamkumbuka mama yake ,kwakuwa ashafarikigi ila shangazi yake alimwambiaga ",mama hakufa ila yupo kwenye sanduku anakuombea usome vizuri.
Hivyo nusra alivyoambiwa na juma mama yenu amesema niwapeleke akawaone ,nusra alifurahi na kusema twende unipeleke nikamwone mama yangu.
Mudrick alimwambia mdogo wake "hapana unadanganywa mama shafarikigi wala hayupo duniani ,nusra alimjibu mudrick."hapana mama yupo na kwasasa atakuwa amechoka kukaa kwenye masanduku hivyo naenda kumchukua nimlete nyumbani ,halafu nitamwambia kuwa wewe umeumia mguu unatembea na magongo ,halafu ulikuwaga unalala hopsitalin
Nusra alimshika juma mkono na kumwambia twende unipeleke nikamwone mama ,lakin mudrick alimkataza mdogo wake na kumwambia mama hayupo duniani ashakufa ,ila nusra kwakuwa yeye ni mdogo sana anaamini mama yake yupo hai na aliwekwaga kwenye masanduku wakati anazikwa,hivyo kwa leo anaamini mama amechoka kukaa kwenye masanduku na anataka kurudi nyumbani.
Juma alimwambia mudrick twende ,ila mudrick alikataa ,juma akaona akiendelea kumlazimisha mudrick anaweza akawakosa wote ,juma akatoa chokulete akampa nusra na kumwambia "hii mama amekupa kula ,pia twende ukamsalimie alimshika mkono kisha walianza kupiga hatua na kuondoka eneo lile wakati huo nusra anakula chokuleti aliyopewa na juma.
Hapanaa usiendeee ,hapana usiende nusra ,mudrick alimkataza mdogo wake ila kwakuwa anatembelea magongo ameshidwa kumzuia mdogo wake ,asiende kabisa ,
Wakati huo nusra alimwambia mudrick nisubiri hapo hapo usiondoke hadi nirudi na mama.
Wakaondoka na kutokomea ,mudrick alikaa na kusubiri mdogo wake arudi ,alianza kutembea pole pole kurudi nyumbani baada ya kuona mdogo wake harudi.
Akiwa anarudi huku akionekana mwenye huzuni alikutana na suhaila alikuwa akiwatafuta "suhaila aliita ,mudrickii nusra yuko wapi mbona unatembea peke yako wakati unajua mguu wako umevunjika?
Mudrick alijibu ,nusra amechukuliwa na juma ,amesema anapelekwa kwa mama ,nimemkataza amekataa hivyo nusra ameondoka na juma.
Suhaila kwa mshangao aliuliza nini? Unasemaje ,nusra ameondoka na juma ,mungu wangu!!!!!!!!
Je nini kitaendelea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: