NAITAFUTA FURAHA YANGU ---sehemu ya 24
Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
---sehemu ya 24---
Tulipo ishia jana, Askari walimchukua mke wa juma ili kumpatia huduma ya kwanza wakati huo walikuwa wamesimama kando kando ya barabara ,lakin zumra alivyoangaza macho upande wa pili wa bara bara ,aliweza kumwona juma akiwa amesimama huku anawaangalia
"Zumra alimwambia askari juma yule paleeee,askari aliwasha piki piki upesi ili aweze kumkimbilia juma ,lakin juma nae alikuwa na piki piki aliwasha nae kisha walianza kufukuziana barabarani
Pia askari wengine walimchukua mke wa juma pamoja na mama yusira ,vile vile na zumra walienda moja kwa moja kituo cha polis ,huku ,adinani na askari wawili waliweza kwenda hospitalin kwa ajili ya kumuwahisha nusra akapate matibabu.
Dokta ,alifanya vipimo upesi kwa nusra ,na kubaini amedugwa sindano yenye sumu kali ,basi dokta nae alimchoma sindano ya kupunguza kasi ya ile sumu ,matibabu yaliendelea haraka haraka ,pumzi za nusra zilikuwa zipo mbali sana.madaktari waliweka umakini wa hali ya juu kumtibu.
Taarifa zilisambaa hadi vyombo vya habari ,nakutapakaa kwenye mitandao ya kijamii ,tukio la kutekwa kwa mtoto ,pamoja ,na kutaka kubakwa na mateja,picha za nusra zilisambaa mtandaoni huku watu wakimwombea aweze kupona kutokana na hali yake.
Tukirudi kituo cha polisi ambako daniel amewekwa sero ,mdomo wake ulikuwa umevimba mno ,huku uso umejaa ,baada ya kupasuliwa jicho na kung'olewa meno hakupewa hata panadol ,daniel alilia hadi machozi yakamkauka ,vile vile daniel ,alipata tabu kula ,polisi na wao walimfanyia unyama walisubiri kesi ifike mahakamani akasomewe shitaka ,maana suhaila na adinani walikuja na vithibitisho kamil kuwa yeye ndiye muuaji ,na aliwaua wazazi wake adinani.
Daniel akiwa anahema njaa inamuuma ,kula hawezi hata kidogo ,meno sita yametoka mdomo umevimba ,askari walivyo na makusudi walimpelekea ugali na maharage tena wameyatia pili pili.,daniel alijaribu kutia hata tonge mdomon lakin haliingii hali ni mbaya,
Kwa mikono yake mwenyewe na miguu yake ,daniel akiwa analia kama mtoto alipiga magoti ,mwanzon alikuwa anakataa yeye hajaua .
Alimwita askari na kumwomba ampe karatasi na kalamu
Danile alipewa jinsi alivyoomba ,alikaa chini na kuandika kwa herufi kubwa "MIMI NIKISHIRIKIANA NA WENZANGU TUMEFANYA HAYO MAUAJI KWA MIKONO YETU WENYEWE.
NAOMBENI KAMA KUNAUWEZEKANO MKANITIBU HAYA MAUMIVU NINAYOPATA ,HALAFU MOJA KWA MOJA MNIPELEKE GEREZANI.
daniel alimpa askari ule ,ujumbe ,askari aliusoma kisha akacheka na kumjibu asante kwa kusema ukweli ,ila hatuwezi kwenda kukutibu ,wewe ni mhalifu ,umeua watu yanini tukutibu ,utakaa na majeraha hayo hadi yatakapo poma na subiri hukumu ya kwenda jela tu.
Daniel kuongea ,aliongea kwa shida alitamani amwone adinani amwombe hata msamaha ,lakin akiwaza aliamin hamna mtu atakae msamehe hata kidogo.
Baada ya muda askari alirudi ambae alimfuatilia juma ,akiwa anatiririsha jasho ,alisema yule mhalifu amenipoteza sikujua alikopotelea ila tuimarishe kikosi tuweze kumnasa.
Zilikatika siku tatu ,nusra aliweza kurejewa na fahamu ,na madakitari waliweza kuokoa maisha yake ,adinani alimchukua na kurudi nyumbani pamoja na bibie suhaila.
Tukirudi maeneo ya mlimani city kwenye maegesho ya magari ,zumra alikutana na mchumba ambae baba yake anataka aolewe na huyo jamaa ,mwenye asili ya kiarabu
"Mohamedi sina hisia na wewe na wala sitaki kuolewa na wewe hata baba nimemwambia ,kama anahofia kuvunja urafiki kati ya baba yangu na baba yako basi kupitia mimi nitauvunja.
Sihitaji kuwa na mme mwenye makampuni na mabiashara mengi ,mimi napenda maisha ya kawaida nadhani umenielewa mohamed "zumra aliongea na kutaka kuondoka.
Ila mohamedi alimwangalia zumra kwa jicho kali "kisha akaongea "nimetoka dubai kwa pesa na kuja tanzania kwa ajili yako nakuambia lazima ukubali nikuoe laa sivyo nitatumia nguvu.
Mohamedi aliongea kwa ujasiri kisha akampisha zumra aingie kwenye gari ili aondoke ,zumra nae alifanya hivyo ,mohamedi alikuwa ni king'ang'anizi mno ,alimtuma mpambe wake aweze kumfuatilia nyendo za bibie zumra ili aone ana mahusiano na kijana gani hadi amkatae yeye.
Vile vile nyumbani ,adinani baada ya kurejea alimkuta suhaila anapika ,maana tayari washamnunulia adinani jiko la gesi ,basi mtoto wakike alikuwa akiandaa chakula taratibu.
Adinani anafika alipokelewa kwa ukarimu kisha waliambiwa wapumzike huku nusra alijihisi kuchoka hivyo alipelekwa kulala.
Suhaila alifika sebuleni ile anageuka geuka sijui nani alimwaga maji chini kwenye tails suhaila aliteleza kabla hajadondoka adinani akamdaka vilivyo ,alimshika kiuno pamoja na mkono,ile style jinsi alivyomshika suahila alijihisi kusisimka mwili mzima.
Suhaila alishidwa kujizuia aliupeleka mdomo ili walau abadilishane mate na adinani lakin kabla hawajafanya hivyo,walisikia mgurumo wa gari walisitisha .
Alishuka zumra akionekanika mwenye mawazo.basi suhaila alimwambia "nini mbona unamawazo hivo nani kakukwaza zumra.
Zumra alimwangalia adinani na kujisemea moyoni"sina mahusiano yeyote na adinani ila urafiki wetu ndio unanifanya nihisi tofauti "sijui nikimweleza adinani atakubali sijui hatakubali
Zumra aliwaza "aliongea "adinani samahani naweza kutoka kidogo na wewe ninamaongezi na wewe vile vile ninajambo nataka kuongea nawe.
Adianani alimwambia hamna shaka twaWeza kuongea ,zumra alimwomba watoke nje ,basi walianza kutembea taratibu kwenye bara bara za vumbi.
Zumra alimshika mkono adinani na kumweleza "adinani naomba uwe mpenzi wangu nina shida moja inanikabili nashidwa kuikwepa ,hivyo naomba tuwe wapenzi hapo utaweza kunisaidia mimi kuitafuta furaha yangu.
Adinani kusikia vile alisimama kwanza na kumuuliza zumra kwanini unataka iwe hivyo?,zumra hakutaka kumficha adinani "alimweleza kuwa baba yake anataka kumlazimisha kuolewa na mtu ambae hampendi mtu ambae si chaguo lake.
Sasa zumra hapo sijakuelewa inamana tunakuwa kwenye mahusiano feki na sio ya kweli ,ili kumaliza tatizo lako?,zumra alimwangalia adinani na kumwambia "ndio tunatengeneza mahusiano feki ila mimi na... zumra hakumalizia aliishia kubabaika
Ki ukweli zumra ametokea kumpenda adinani ila anashidwa kueleza hisia zake vile vile adinani ,hivyo inabaki siri moyoni mwake kuwa anampenda adinani.
Adinani nae hakuwa na hisia ya aina yeyote ya kimapenzi kutokana na maisha yake kuwa na misuko suku mingi hivyo ,muda mwingi huwaza lini ataipata furaha ,lini atamkamata mtu aliyefanya mauaji ya wazazi wake.
Adinani alimwambia zumra ,sawa usijali kwakuwa umenisaidia mambo mengi ,kunilipia bili za hospitali ,umekuwa tegemezi kwetu ,unatununulia hadi chakula ,sijui ingekuweje ,usingetokea katika maisha yangu ,kwa upande wangu zumra una msaada mkubwa sana ,hivyo nami niko tayari kukusaidia suala lako naimani litaisha.
Zumra alimwambia adinani "kwa sasa turudi nyumbani maana nishakueleza jambo langu ,walianza kutembea kurudi nyumbani huku wameshikana mikono wakizungumzia jinsi watakavyofanya ili yule mohamedi anae taka kumuoa basi asifanikiwe maana zumra hana hisia nae ila baba yake ndio anataka aolewe na huyo mwanaume.
Nusra umeamka ?,na unajisikiaje?,mudrick alimuuliza swali mdogo wake alipo amka ,tu ,nusra alimwangalia mudrick alipiga magoti na kusema "kaka nisamehe juma alinidanganya naenda kuonana na mama yangu ,lakin alichonifanyia alinichoma sindano mkononi baada ya hapo mwili wangu ulilegea kabisa.
Mudriki alimwambia mdogo wake "nimekusamehe twende anti suhaila anatuita sebuleni
Mudrick na nusra walitoka sebuleni taratibu maana mudrick alikuwa akitembelea magongo.walimkuta suhaila ameendaa chakula
Waooo nusra umepona eee ,basi njoo ukae hapa ule ,suhaila alimwita nusra kwa ukarimu ,wakati huo adinani na zumra nae wanafika nyumbani.
Zumra alivyogeuka nyuma aliona wanaume watatu wako na gari walishuka ,zumra aliwaza na kujisemea moyoni inamna mohamedi ndio amewatuma mnifuatilie ee ,.nishasema sitaki kuolewa na mohamedi.
Zumra alimshika adinani mabeki wakiwa wapo karibu na mlango,zumra aliupeleka ulimi wake ili aweze kubadilishana mate na adinani ,lengo lake ili wale watu waliotumwa na huyo mwanaume wajue kuwa zumra yupo kwenye mahusiano na kijana wa mtaani tu.
Adinani nae hakujizuia ,zumra alianza kunyonya mate na kufanya kila mtu ashangae wale watu waliotumwa kumfuatilia zumra walishangaa walibaki kunyoosha vidole ,inamana anampenzi huyu binti
Wakati huo suhaila alikuwa anatenga chakula sebuleni alivyoangalia nje nae alijionea ,kile kitendo suhaila akashidwa kuvumilia alienda kwa spidi na kumsukuma zumra akadondoka chini.kisha akamkalia tumboni na kuanza kumpiga zumra ngumi za usoni huku akisema
Zumra hapo unanikosea "nishakuambia huyu adinani ni wangu nimetokea kumpenda iweje unataka kumchukua ,huyu adinani ndio alinifanya nisijiue hivyo maisha yangu nimemkabidhi yeye nampendaaaaaa!!! Suhaila alizidisha kumpiga ngumi zumra.
Wakiwa wanapigana gafla gari ilisogea kisha wakashuka vijana sita ,waliwaangalia akina zumra wanavyomgombania adinani hadi kufikia hatua ya kupigana,
Wale vijana waliuliza "mtaa huu kuna kijana anaitwa adinani ?,tunamuulizia kama unamfahamu tunaomba utupeleke. Wale vijana walimuuliza lile swali adinani
Je nini kitaendelea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: