NAITAFUTA FURAHA YANGU 25
Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
---sehemu ya 25---
Tulipo ishia jana, Wakiwa wanapigana gafla gari ilisogea kisha wakashuka vijana sita ,waliwaangalia akina zumra wanavyomgombania adinani hadi kufikia hatua ya kupigana,
Wale vijana waliuliza "mtaa huu kuna kijana anaitwa adinani ?,tunamuulizia kama unamfahamu tunaomba utupeleke. Wale vijana walimuuliza lile swali adinani
Adinani kabla hajawajibu wale vijana ,ilibidi amwinue suhaila chini na kumwambia acha kumpiga mwenzako ,mimi ndio mwenye makosa acha suhaila ,alimwinua suhaila.,hapo ndipo nguvu ya mapenzi ilionekanika ,mapenzi yanaweza kuvunja urafiki mapenzi yanaweza kuvunja undugu.
"Zumra nae aliinuka chini ,alijifuta vumbi ,alimwambia suhaila "ulivyoelewa ni tofauti punguza hasira na uulize kwanini na fanya hivyo mbona siku zote tunaishi mimi na wewe kwa pamoja tunalala chumba kimoja kwanini umeshidwa kuniuliza kistaarabu?,zumra aliongea kwa ustaarabu ndipo suhaila alipayuka kwa nguvu "NAMPENDA ADINANI "
Wale vijana walivyosikia jina adinani wakajua ehee ndio huyu ,mmoja alimsogelea adinani na kumwambia "we dogo inamana umekua hadi kuchukua mademu za watu tena mchumba wa mtu ,ehe hebu niambie wewe dogo.
Ni maneno aliyoongea jamaa mrefu huku akionekana kumsogelea adinani .adinani aliwaza ",ni kweli anatamani kumsaidia zumra kwa suala lake la kulazimishwa kuolewa na mwanaume asie mpenda ,aliwaza atafanyeje ,endapo atakubali yeye ni mpenzi wake zumra hata kama wanaigiza penzi lisilo la kweli bado maisha yake yatakuwa hatarini ,atazidi kuandamwa na juma ,vile vile ataanza kuandamwa na mohamedi ambae anataka kumuoa zumra ki nguvu.
Adinani aliinamisha kichwa na kuona maisha yake bado magumu mno ,atamsaidia vipi zumra ,moyon anatamani kumsaidia akifikiria anaona anazidisha matatizo.
We dogo si naonge na wewe ,wewe ndio unatembea na zumra?
Sauti ya kijana ilimshitua adinani na kumfanya ajibu
Ndio mimi ni mpenzi wake na tunapendana.kisha adinani alimtizama zumra ,kwa mara ya kwanza suhaila akasikia kwa masikio yake adinani anampenda zumra .
Suhaila akaanza kukumbuka matukio ya nyuma jinsi alivyosalitiwa na mpenzi wake ,jinsi mpenzi wake alimwambiaga akarudi dubai na anaenda kutambulisha mwanamke mwingine kwao ili aoe ,leo tena kwa masikio yake akasikoa adinani anatamka anampenda zumra na wapo kwenye mahusiano kwa muda mrefu.
Suhaila hakuongea chochote aliondoka pasina kuaga alianza kukimbia "adinani alivyoona hali ya suhaila hakupenda kumwacha maana anajua hasira zake anaweza hata kujiua
Adinani alimkimbilia suhaila na kumshika mkono.niache adinani nimesema niache ,suhaila aliongea kwa ukali.
Lakin adinani hakuishia hapo "alimshikilia kwa nguvu na kumwambia "ulivyoelewa sivyo unavyodhani ,kama uamuzi uliouchukua kwako unaona ni sahihi ,basi usiniage mimi kama unaondoka ,au kama unaenda kujiua
Ila nusra na mudrick wamekuzoea hata kama una hasira nenda kawaage kisha uchukue uamuzi ulio uchukua.adinani alimaliza kuongea na kumwachia kisha akarudi kwa wale vijana.
Alisimama na kuwaambia "mimi ndio mpenzi wake zumra ,ehe mlikuwa mnashida gani?.wale vijana walimwangalia zumra kwa jicho la kali kisha wakaondoka bila kuongea chochote.waliingia kwenye gari kisha wakawasha gari lao na kuondoka
Adinani alimchukua zumra na kumwingiza ndani wakati huo suhaila ashaondoka kwa hasira ,baada ya kugundua zumra na adinani wanapendana.
"Basi adinani aliuliza "zumra alivyokupiga umeumia sana?,hapana sijaumia mimi suhaila nishamzoeaga maana toka utotoni huwa tukigombana tunapigana halafu hasira zetu zinaisha.
Adinani alijibu sawa "kisha akauliza swali "je zumra unahisi maisha yangu yatakuwa ya furaha ?,
Zumra alitabasamu kisha alikaa kwenye mkeka na kumwambia "adinani mimi nimezaliwa kwenye maisha ya pesa ,ila mimi sitaki kuishi hayo maisha napenda kuishi maisha ya kawaida sawa na kila mtu ,hivyo sitaki kabisa kulazimishwa kuolewa na kijana mwenye pesa ,najua penzi halitakuwa na furaha ,sababu duniani watu wengi ni masikin hivyo ukiolewa na tajiri basi watu wa hali ya chini watajilegeza kwake mwisho wa siku anashidwa kujizuia unakuta mtu mmoja tunashare hio staki kabisa initokee
Kingine yule mohamedi mie sina hisia nae na wale simpendi hata kama yeye ana asili ya uarabu simtaki.adinani naomba unisaidie hivyo tu.
Adinani alishusha pumzi na kumwambia sawa zumra nimekuelewa ila ngoja nikamrudishe suhaila najua ameondoka na hasira anaweza kufanya jambo lolote baya.
Adinani alitoka ili kumtafuta suhaila ,hivyo alimwacha zumra akae na akina nusra pamoja na shangazi yao ,adinani alianza kumtafuta barabarani
Bara bara ya bima kwenye stendi gari ya wale vijana waliotumwa kumchunguza zumra anamahusiano gani au anatembea na nani waliweza kupaki gari kisha waliongea na simu.
Hallo baba zumra ,
Upande wa pili "safi vijana wangu vipi mmeweza kugundua binti yangu anamahusiano na kijana yeyote huko mtaani.
Ndio mzee tumemkuta yupo na kijana flani hivi masikin masikin ,kijana mwenyewe inaonekana ni tapeli maana tumekuta anagombaniwa na wasichana wawili
Baba zumra aliuliza kwa nguvu ",we mussa unasemeaje ,kamata huyo kijana nileteeni haraka nimesema. Mussa alijibu usijali mzee ngoja turudi tukamkamate huyo kijana
Simu ilikatwa wakati huo adinani nae amefika usawa wa ile gari ya akina mussa ambae ame pakiwa ,kijana mmoja aliita ",oya musa dogo mwenyewe si yule pale au .musa alijibu ndio hazikupita dakika tano adinani alikamatwa na kuingizwa kwenye gari kisha safari ilianza moja kwa moja hadi kwa baba yake na zumra.
Adinani aliomba ashushwe ,lakini wale vijana walimwambia tulia ukijifanya mjuaji utaumia sana dogo ,hivyo adinani ikabidi awe mpole ,
Aliweze kufikishwa kwa baba yake na zumra maeneo ya masaki.adinani alivyofika eneo lile alikumbuka ,siku ya kwanza aliendaga kwenye ile nyumba wakati huo akifanya kazi ya uboda boda na alimpelekaga zumra ,siku hio alipewa laki moja .
Adinani kwakuwa hakufugwa macho hivyo alikuwa anaona kila kitu ,aliingizwa kwenye jumba baba yake zumra ,alipandishwa ngazi hadi juu ya gorofa ndipo alimkuta baba yake na zumra amekaa huko huku amekunja sura.
Adinani akiwa amefugwa kamba miguuni na mikononi ,alitupwa kisha aliambiwa amwangalie baba yake na zumra.
Kwa mara ya kwanza anaonana na baba kae zumra akiwa amekunja sura kwa hasira.
Adinani alivyotizama eneo lile la juu kabisa ya gorofa ,aliona kamba ,alivyotizama chini kulikuwa na mabunda ya pesa ,alivyotizama vile vile kulikuwa na kisu ,na kwa pembeni pia kulikuwa na bastola.
Adinani aliamini leo basi ndio mwisho wake wa kuishi "adinani kabla hajaanza kuulizwa swali lolote alikumbuka zumra alimwambia "baba yangu ni mkali na ni mgumu sana kuelewa ,baba yangu akikuchukia anaweza hata kukuua ,hivyo naomba uwe na moyo wa kunisaidia najua adinani nakuweka katika mazingira hatarishi ila naomba unisaidie sitaki kuolewa na huyo mwanaume niliyochaguliwa na baba,
Adinani aliendelea kukumbuka ,zumra alimuuliza ",je utaweza kunisaidia? ,adinani alikumbuka nae alijibu nitakusaidia kwa jambo lolote litakalotokea.
We kijichawa kwanini unanifanya nisumbue akili yangu "huyo binti zumra ukimwangalia jinsi alivyo anaweza kuwa kwenye mahusiano na wewe? Ni swali ambalo baba zumra aliuliza.
Adinani akiwa amefugwa kamba miguuni na mikononi alibaki kimya hakujibu chochote.
Baba zumra aliinuka kwenye kiti na kuongea "hapo kwenye macho yako ,nimekuwekea kamba ya kujinyongea ,nimekuwekea ,kisu cha kujichoma mwenyewe tumboni ,nimekuwekea vile vile bastola ya kujilipua kichwani ,vile vile pesa hizo hapo nadhani unaziona wewe kapuku masikini mkubwa ,vile vile glasii hii hapa ya sumu.
Hivyo vyote ni chaguo lako ,ni kipi utakichukua ambacho utakichukua ,kama hutaki kuachana na binti yangu naomba ujichagulie kitu kinachokufaa kazi ya hiyo.
Baba zumra anae dharau alikaa na kuanza kusoma gazeti.
Alisubiri adinani aseme ,kama anahitaji pesa ,azichukue ili aachane na mwanai ili mwanae aolewe na mchumba ambae yeye anamtaka na si adinani.
Tukirudi upande wa pili maneno ambayo adinani alimwambia suhaila hayakutoka kichwani ,suhaila alitamani ajirushe kwenye bara bara ili agongwe na gari lakin kila akitaka kufanya vile alikumbuka jinsi walivyokuwa wanacheza na nusra ,jinsi nusra anavyopendaga kujifunza kusuka nywele zake.
Suhaila alishidwa kufanya vile ,ndipo aliamua kurudi ili akawaage akina nusra ili aondoke dar es salam na kwenda mbali. Suhaila alikimbia kama kichaa hadi nyumbani na alivyofika alikuta zumra anamvalisha nguo nusra sebuleni
Zumra alitizamana na suhaila kisha akamuuliza ",kwa hio umenichukia mimi na hutaki hata kuniaga suhaila?,kabla suhaila hajajibu simu iliita.
Zumra aliichukua simu na kupokea kisha akaweka loud spika.
Ha ha ha ha ilisikika sauti ya kicheko cha baba yake zumra kisha akaanza kuzungumza haloo mwanangu
"Haloo baba shikamooo
Ha ha ha mzee alicheka na kujibu marhabaa
Zumra akauliza baba mbona leo unafuraha kuna nini?
Mzee alisema unataka ujue na furaki nini ,
Sauti ilisikika upande wa pili ikiamrisha piga huyo ili mwanangu asikie
Ni sauti ya adinani alisika akilia huku akipigwa na fimbo mwilini tena bila hurumaa,huku akiambiwa sema unaachana na binti yangu?
Baba zumra aliongea tena" binti yangu nadhani umesikia "haka kapanya kanachokudanganya kana kupenda mimi baba yako nimekutafutia mwanaume humtaki sasa sikia
"Naona huyu kijana mgumu wa kuelewa nimempa vitu vingi achague ,ili aachana na wewe ataje kiasi cha pesa anachotaka nimpe akuache uolewe na mohamedi eti anajifanya anakupenda sana hataki pesa,
Sasa mwanangu kuhusu huyu kijana msahau kuanzia leo ,hapa nampa dhana ajichagulie ambayo ataona inamfaa kujiua nayo ,
Mzee alisogea karibu na adinani na kumwambia "kati ya kisu ,bastola ,sumu na tukurushe chini ya gorofa unachagua nini?
Adinani kwa maumivu makali aliongea kwa nguvu "nirusheni chini ya gorofa nife ,kisha akasema ,zumra kama unanisikia mimi nakufa hakikisha wadogo zangu wanaishi maisha mazuri wasije kufa kifo kama changu.
Zumra na suhaila kusikia vile ,pale pale kila mtu alitoka nduki wakikimbia kwenda masaki kuokoa maisha ya adini ,kutoka tabata hadi masaki ni mbali ,na suhaila alisahau kabisa kama alimchukia adinani nae alitoka ili akamsaidie. Walikodi piki piki kisha safari ikaanza kuelekea masaki.
Lakin ile tu wanatoka suhaila na zumra kwa mbali juma akiwa amevaa koti lake kubwa na kofia alikuwa anatembea na mtu ambae nae alivaa kofia nae ilizuia usiweze kuzitambua sura zao.,walikuwa wanatembea taratibu taratibu na kuelekea iliko nyumba ya akina adinani wakati huo mudrick ndio wameachwa na mdogo wake nusra pamoja na shangazi yao
Suhaila na zumra wametoka ili kwenda kumsaidia adinani asiuliwe na baba yake ,kibaya zaidi kutoka tabata hadi masaki kunao umbali mrefu mno.
Je nini kitatokea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: