NAITAFUTA FURAHA YANGU 30 (Nwisho)
Story :NAITAFUTA FURAHA YANGU
MWISHO
--SEHEMU YA 30--
TULIPO ISHIA JANA,
Danile aliweza kusimama ile anataka kuongea alishidwa kutokana na pengo lake kubwa ,watu walicheke mno.daniel alishusha pumzi lakin alivyotizama mlango wa kuingilia alimwona mwana mama mmoja akija taratibu huku akitiririsha kachozi.
Danile na jicho lake moja alikodoa huku akiacha mdomo wazi ,yule mwana mama kila mtu aliyekuwa eneo lile aligeuka na kushangaaaa huku kila mtu akishangaa kwa namna yake
Masikin mama huyu!!!,oohh mungu wangu!!!
Watu wote walikaa kimya ,walimwangalia yule mwanamke aliketi uso wake ulikuwa umeungua na moto ,ndio kwanza alikuwa ameanza kupona.si uso hadi mikononi ,pia alionekana kuungua na moto,mama alikaa kwenye kiti akafuta machozi kisha akasubiri kuona mahakama ikiendelea na kesi.
Daniel alinyoosha mkono kwa yule mama aliyeketi huku akionekanika kubabaika ,aliita ma -ma ma maaaa.maaama ,yule mwanamke alifungua mfuko , alitoa kihotipoti kidogo alimwomba askari ampelekee daniel kile kihotipot daniel ,kisha mama akainuka ili aondoke
Alisema mwanangu kabla hujaenda jela ama kunyongwa kula hicho chakula nimepika mama yako ,najua kitakuwa chakula changu cha mwisho kula
Yule mama alitoka na kumfanya daniel alie kwa uchungu,na kuamini siku zote mama ni mama hata ukiwa na matatizo vipi hawezi kukutupa.,yule mama yake na daniel alitoka mahakamani na kuondoka hakupenda kumwangalia mwanae maana anaumia.
Danile alikumbuka ,siku alivyorudi nyumbani ,alimkuta mama akichambua matembele ,alimwambia mama unafanya nini?,mama alimjibu naandaa mboga nikupikie ,daniel alichofanya alizipiga zile mboga teke ,na kumwambia "mama kwanini unanishauri niache wizi wewe ndio utakuwa unanipa pesa za matumizi.
Siku hio danile alichukua kamba alimfunga mama kamba miguuni na mikononi ,alimlaza chini akamfungia chumbani ,daniel alimwaga petroli na kuwasha moto kwenye kijumba ambacho alikiwa mama yake ,alimwambia neno moja kisha akatoka
"Mama hebu ongea na huo moto halafu uniachie uwanja nifanye ninachotaka katika dunia sitaki kelele.zako za kuniambia niache wizi
.mama nyumba iliungua moto ,mdipo moto ulimfikia na kuunguza kamba za mguuni ,kamba zilipokatika ,mama aliinuka ili ajiokoe ,alitoka , lakin tayari moto ulikuwa ushakamata mwilini alifanikiwa kutoka akiwa anawaka moto.
Bahati nzuri watoa huduma waliwakuwa tayari washafika kwa ajili ya kuuzima ule moto. walimchukua mama akiwa ameungua moto ,usoni ,miguuni kifuani na mikononi ,walimuwahisha hospitali wakati huo danile alishaondoka
Siku zote daniel anajuaga mama yake amekufa ,kumbe yupo hai,danile mahakamani alianza kulia kama mtoto,
Ndipo mahakama iliona isipoteza muda iliwasomea mashataka yao na kuwapa hukumu ya kinyongo
Juma pamoja na daniel ,ndipo watu walivyohakikisha hukumu ya mwisho imesomwa ipasavyo watu walitawanyika kisha juma na daniel walisubiri siku yao ifike wanyogwe.
Adinani alirudi nyumbani pamoja na akina zumra ,kwakuwa washamaliza kazi ,mtu ambae alikuwa kikwazo katika maisha yao hatimae sheria imechukua mkondo wake.
Wakiwa nyumbani kwa akina adinani ,ndipo gari aina ya jeep liliingia na kupaki eneo lile ,alishuka bibie hilda alikuwa amevalia miwani vilivyo aliivua na kusema ,hapa ndio wapi ?alitizama macho na kumwona nusra amesimama mlangoni ,kwa mara ya kwanza hilda anamwona nusra kwa mara ya kwanza baada ya kutoka china kutibiwa macho yake.
Nusra aliita shangazi kwa sauti ya juu na kumkimbilia kisha akamkumbatia alimuuliza inamana sasa hivi shangazi unaona,shangazi alijibu ndio naona ,ila kitu hapo ,mlango pale dirisha waya za umeme zile.,
Mara adinani alitoka nae akakumbatiana na shangazi yake ambae ametibiwa upofu wake yuko anaona ,vyema akina zumra na suhaila nao walitoka walifurahi kuona na shangazi sasa ameipata furaha yake ambayo alikuwa anatamani siku zote aipate.
Hilda alikuwa anashape nzuri sura basi kwa umbo lake na hali ya sasa anaona , basi suhaila alimwambia kwa sasa wanaume watapata tabu sana.
Wote walicheka.hilda hakuishia hapo aliingia ndani na kumkumbatia mama mick maana hata yeye alikuwa msaada mkubwa sana katika maisha yao,adinani alimwachia majukumu ya kumlinda.hilda angali kipofu.
Wakiwa wamesimama nje ndipo baba yake zumra alishuka kwenye gari akapiga magoti na kuanza kuongea kwa utaratibu "adinani naomba unisamehe ,najua nimefanya mambo mengi wakati wewe upo kitandani ,kwa upande wako labda unajua najipendekeza kwa kuwa nilikufanyia ubaya.
Adinanani naomba unisamehe nilichukuaga maamuzi mabaya sikujua kama unampenda binti yangu upendo wa dhati.nisamehe
Adinani aliwahi na kumwinua baba zumra ,kisha akamwambia "ulikuwa unahaki hata ya kuniua sababu zumra ni mwanao ,pia kwa wakati ule uliona yule mwanaume ni bora ndio maana ,ulichukua maamuzi.
Kwanini humtaki tena mohamedi?,siku zote hata zumra hajuagi kwa nini baba yake hamuambiagi tena awe na huyo mwanaume ,
ndipo mzee aliwakalisha chini na kuwaelezea "jinsi alivyomkutaga hotelini kitandani amelala na wanawake watatu wakiwa uchi wa mnyama,pia aliendaga hadi nyumbani vile vile kwenye gari alikiwa na mwanamke mwingine.
Suhaila aliuliza swali " baba mbona hatumuoni tena mohamendi ameenda wapi?,baba zumra aliendelea kuwaeleza ,mohamedi nilimtafuta na kumwambia sitaki tena kukuozesha binti yangu kutokana na kuwa na tabia mbaya ,mohamedi alikuwa king'ang'anizi aliniahidi atamtafuta adinani ili amdhuru ikiwezekana ampige risasi.
Alivyoniambie vile mie nilienda makao makuu kwenye ofisi za uhamiaji ndipo nikaenda na ubalozi wa dubai niliwaambia wafute ,passipoti yake ya kukaa tanzania.kweli walinisikiliza alifutiwa kitamhulisho cha kukaa tanzania ,ndipo aliamua arudi dubai hakuwa na namna hivyo ndivyo alivyoondoka tanzania pasina kumdhuru mtu .
Basi baba zumra aliomba msamaha kwa binti yake zumra ,pia na kwa adinani aliomba ,msamaha ,adinani hakuwa na budi alimsamehe pia mzee alimwomba adinani alionesha ushujaa yuko tayari afe ila bado anampenda mwanae
Basi mzee aliomba adinani ampende mwanae na ahakikishe mwanae anampa furaha ,hata yeye anaitafuta furaha hasa akiona mwanae anapata mwanaume ambae anamstahili
Zumra alimkumbatia.adinani kwa mara ya kwanza alisema nakupenda adinani ,jambo lililomfanya hilda nae afurahi kushuhudia adinani anapata mwanamke ambae anampenda na alikuwa anatamani angekuwa na macho amwone adinani akiwa na furaha.
Maana siku zote waliishi kwenye majonzi.baba zumra hakuishia hapo ,alitoa ufunguo wa gari mpya alimwita mama mick kisha alimkabidhi na kumwambia gari lako mpya kutoka japan lipo na hadi sasa lipo bandarini naimani kufikia jioni litakuwa nyumbani kwako,umehangaika sana na hawa watoto ,nimepewa story yote na huyu mwanangu hakika ulikuwa na moyo ,hivyo nakuzawadia gari vile vile nyumba yako unayoishi ,nitaifumua upya na kujenga nyumba ya kisasa.mzee aliongea sababu anayopesa kila kitu kitaenda sawa.
Mama mick alishangaa ,alifurahi na kumshukuru sana baba zumra ,wakaiwa wanaongea nje ,mama joy akiwa peku peku nae alikuja kumwona adinani maana alisikia adinani amerudi baada ya kutoka hospitali.
Basi nusra alivyomwona mama joy ,huwa anamwita mama alimkimbilia na kuita mama.mdogo ,karibu ,baba zumra alivyomtizma chini hana viatu ,alimwambia zumra ,huyu mama mkimaliza mambo yenu ,najua anaundugu na akina adinani mkwe wangu wa ukweli ,hakikisha ukamnunulie ,kuanzia nguo ,viatu kama hana nyumba basi ile nyumba ya sinza ambayo tumeipangisha akaishi huko
Mama mick alizidi kushangaa na kuamini kweli kilio kingi mwisho wa siku kinaangukia furaha., basi baba zumra aliaga anaondoka ,siku hio kwa akina adinani walihisi ni sherehe kwa upande wao.walifurahi .
Jioni ,mama joy akiwa haelewi hili wala lile alipelekwa kwenye maduka ya nguo alinunuliwa kisha akapelekwa sinza kwenye nyumba ambayo amepewa na baba yake zumra.
Walivyomaliza suhaila aliwachukua akina nusra na mudriki pamoja ma shangazi alirudi nao nyumbani ,huku akiwaacha zumra na adinani maeneo ya sinza iliyoko nyumba yao mpya.
Zumra akiwa na furaha ,alimsogelea adinani kwenye sofa na kumkumbatia huku akidondosha machozi yake ya upendo ,chozi lililojaa furaha
Bibie aliita adinani "kwa mara ya kwanza nilomba tuanzishe walau penzi feki ,dhamira yangu nilikuwa natamani uwe wangu ,ila jinsi matatizo yalivyokuwa yamekusonga niliamini huwezi kukubali ,nikueleze ukweli ,najua wewe ulinijuaga mara ya kwanza ulivyonipakiaga kwenye piki piki lakin si hivyo,mimi nilikuonaga magomeni kwenye barabara moja ya vumbi
Kipimdi hicho tulikuwa wadogo ,ulikuwa unacheza na kagari kadogo kando kando ya bara bara ,siku hio nilikuwa na baba kwenye gari
Kwa bahati mbaya ile eneo lilikuwa na dibwi la maji tulivyopita na gari tulikumwagia maji machavu ,nawe hukutukana wala kufanya chochote ulisimama ukatuangalia kisha uliendelea na shuguli zako ukiwa umeloana maji.
Nilikuangalia sana.na kuanzia siku hio mimi nilijawa na roho ya huruma,
Adinani aliona mtoto anaongea sana ,alimsogeza kifuani akapeleka lipsi zikagusana walianza kugombania mate mdomoni taratibu mtoto wa kike akawa anapandisha mguu kwenye sofa wakati huo adinani anapapasa nywele ndefu za bibie
Basi hapo ndio ukawa mwanzo wa penzi zito la bibie zumra na adinani huku baba yake ameridhia kabisa.suhaila hakuwa na wivu hata kidogo ,alifurahia kuona wanapendana ,alishirikiana na wao kila jambo.,
Siku zilizidi kuyoyoma ,adinani alienda makaburi waliko zikwa wazazi wake aliyajengea vizuri , huku akishirikiana bega kwa bega na zumra ,walizidi kuwa na mahaba mazito ,walidumu kwenye mahusiano miaka miwili ndipo
Baba zumra au bwana idrisi ,aliamua kuwafanyia sherehe ya kufunga ndoa ,alimwozesha binti yake kwa adinani ,nusra akawa anamwita zumra wifi na si anti kama mwanzoni alivyokuwa anamwita.
Nusra na wao shuleni wakawa wanasoma vizuri hamna wanafunzi wanawacheka na kuwaambia wao mayatima.,kila siku wanaenda shuleni na gari ,wanarudishwa na gari.mama mick nae alifurahi baada ya kujengewe nyumba mpya ,gari mpya ,aliishi maisha mazuri na kumsomesha mwanae kwa nguvu.
Mick alisoma mno na alipata elimu ya juua ,alivyomaliza alikuja kuajiriwa kwenye kampuni za baba yake na zumra ,wakati huo adinani nae alikuwa miongoni mwa wamiliki wa hizo kampuni
Wakati huo juma na daniel wao waliweza kunyogwa kutokana na mahakama ilivyoamru,adinani na suhaila walijihisi kuwa huru baada ya wabaya wao kuangukia kifo
Siku moja adinani aliwachukua wadogo zake na kwenda yaliko makaburi ya wazazi wao ,wakiwa na maua ,walifika na kuweka maua kwenye makaburi ya wazazi wao.walisoma dua walivyomaliza
Adinani alitoa heshima kwenye makaburi hayo "aliita mama baba nimeitafuta furaha yangu hatimae nimeipata ,nimeitafuta furaha ya wadogo zangu hatimae nimeipata,huko mliko roho zenu ziishi peponi najua yaliyowakuta ndivyo ilivyopagwa.
Sasa tuna amani sisi watoto wenu japo tunatamani mngelikuwepo kwenye hii dunia ,mama uone mke wangu niliyeoa ,mama umwone hilda kwa sasa anaona
Hii ndio furaha tulikuwa tunaitafuta.
------MWISHO---
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: