Story Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU 29





Story Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU


---sebemu ya 29---
      Tulipo ishia jana, Ile mikono ya baba yake ambae amemwona ilirefuka hadi kufika kitandani kwa adinanii na kumshika ,adinani alifumba macho na kupiga kelele hapanaaaaaaaaaaa hapanaaaaaaa
Zile kilele ziliwashitua madaktari na kufanya waingie upesi kwenye chumba cha adinani 
Ile wanaingia adinani alikohoa koho koho kisha akawa kimya alilala na kunyoosha miguuu yake

Wewe ,kaka ,mgonjwaa ,adinani ,ni majina ambayo nesi alikuwa akimwamusha ,adinani alifumbua macho ,kumbe alikuwa yupo ndotoni aliota kama baba yake amemjia hospitali na akimwita .

Adinani aliwaangalia madaktari na kuwauliza ,mimi ni nani?,na kwanini mmeniacha kwenye hichi chumba kidogo hivi.nesi ili bidi ampishe dokta aliamini kabisa kumbu kumbu zake zimeamza kurudi ,dokta alimwangalia na kuchukua vipimo na kumwambia ,"adinani usiwe na wasi wasi utapona ee,dokta alitaka kuondoka ,lakin adinani "alianza kuongea na kumfanya dokta asimame "mama nyumba ipo tena ni nzuri sasa ,nyumba ya amani mama ,mama njooo nikuambie kitu ,"
Ni maneno ambayo adinani alikuwa akiongea peke yake .dokta alishusha pumzi na kuwaza inabidi huyu mgonjwa aletewe watu wake wa karibu .

Dokta alitoka nje na kuwakuta akina suhaila na zumra ,wamekaa nje ,aliwakaribisha wakamuone mgonjwa wao.zumra alikuwa anatembea taratibu kutokana na jeraha lake la tumboni bado halijapona uzuri,zumra alifika kwenye wodi ya adinina ,alikuta adinani yupo kitandani amekaa huku akiongea.

Zumra alienda moja kwa moja na kumkumbatia adinani huku akilia mno "adinani nisamehe haya yote ni makosa yangu ,naitafuta furaha yangu ,adinani nisamehe sikujua kama nitakuweka katika hali ya hatari namna hio ,sikujua kama naweza kukusababishia hadi ukae kitandani wiki zote hizi 

Adinani nisamehe ,wadogo zako umewaacha wapweke ,adinani nusra anakuulizia kila kukicha ,muda mwingine hali ,anahitaji hadi wewe uwepo ndio ale ,adinani nimekupa mtihani mzito mno ambao sikutegemea.

Zumra aliongea maneno mengi mno,huku akilia machozi suhaila aliangalia nae alikaa kitandani alishika miguu ya adinani ambayo ilikuwa ya baridi ,suhaila alikumbuka na yeye kipindi alivyokuwaga mdogo ,kuna siku alidumbukiaga kwenye kisima cha maji nyumbani ,alikuja kuokolewa na baba yake ,na alivyopelekwa hospitali 
Baba yake alimwambia "mwanangu miguu yako ya baridi ,alimfunikaga miguu yake ,basi leo tena suhaila alivyoigusa miguu ya adinani aliona ya baridi alichukua shuka akaifunika ,kisha akamwambia

"Zumra inatosha usilie ,adinani bado hajawa sawa ndio maana anashidwa kukujibu,basi suhaila alimwinua zumra kitandani ili amwache  adinani apumzike kisha wakatoka nje ya hospitali.

Basi adinani alikaa mwezi mzima hopsitali ndipo hali yake ilirejea vyema na kuruhusiwa  kurudi nyumbani ,siku hio alirudi na kukuta ,suhaila ndio anaishi kwenye nyumba ya kwao ,pamoja na wadogo zake ,vile vile mick nae alikuwa akienda siku moja moja  kushida huko basi sikuz akitoka shuleni mapema.
Adinani alirejea nyumbani akiongozana na mama mick ,ndipo alipofika nyumbani nusra alifurahi kumwona adinani amerejea

kaka subiri nikuambie sasa ,huyu anti suhaila alimvunjaga mguu juma ,alidondokaga na gari mtaroni ,akavunjika na mikono eeem.
Adinani alimshika mdogo wake mikono kisha alikaa kwenye sofa ,alikuta nyumba yao imebadilishwa kila ,kitu,kwanza imepigwa rangi kila kitu ,pili ,ndani imewekewa masofa ,kabati yaani kila kitu cha kisasa.

Adinani aliuliza nani amefanya hivi? ,mudrick alitokea chumbani akiwa anachechemea kidogo maana mguu wake tayari ashatoaga like gamba gumu,alimjibu huyo ni baba yake zumra.
Adinani kwa mshangao alimwangalia suhaila ,ni kweli baba yake zumra amefanya hivi?,suhaila alijibu ndio kisha aka uliza  shangazi yakonmbona simuoni hapa au kalala?
Suhaila alijibu pia hayupo hapa tanzania amepelekwa china kwenda kutibiwa macho.

Nani kampeleka huko?,adinani aliuliza akiwa anamshangao,mama  mick alimjibu ,huyo ni baba yake zumra ,pia anaomba umsamehe hakujua kabisa kwamba wewe ni mwema na unampenda binti yake.
Adinani alivyoambiwa hivyo ndio akakumbuka jinsi ilivyokuwa ,alipigwa sana na vijana wa baba yake zumra huku wakimwambia aseme kuwa anaachana na zumra.
Lakini adinani aligoma na kusema hapana simwachi ,alikumbuka alirushwa juu ya gorofa kilichotokea hakikumbuki tena.

Adinani aliomba akapumzike ,ndipo alipo ingia chumbani alikutana na vitanda vya kisasa ,godoro mpya ,adinani alishangaa ilibidi ajilaze kwakua alikuwa anajisikia vibaya.
Alilala, kesho yake asubuhi ndipo 
Adinani alikuwa wa kwanza kuamka ,na alivyotoka nje alimkuta zumra amesimama nje na gari.

Adinani alishangaa zumra anakuja na kumbusu shavuni kisha akamsalimia,adinani alishangaa nae aliitikia salamu ,kisha akauliza kulikoni mbona umewahi mapema?.
Zumra alisema nimewahi nimekuja kuwachukua tuende mahakamani leo tunaenda kusikiliza kesi ya akina juma pamoja na daniel watahukumiwa kifungo ama kunyongwa.

Adinani alijiandaa pamoja na wadogo zake nao aliwaandaa maana walikuwa na wao wanenda kutoa ushaidi ,vile vile suhaila ,nae alikuwepo pamoja na mama mick

Wote walipanda gari hadi mahakamani ,ndipo mida ya saa nne hukumu ilianza kusomwa ,"kwanza daniel pamoja na juma walisimamishwa kizimbani. Japo mguu wa juma ulikuwa umevunjika  na haukupelekwa hospitali hata kidogo mguu ulianza kuoza mahali umevunjika.
Adinani alitoa macho baada ya kuona juma amebebwa juu kama  gogo ,hakuwa na mguu mmoja wala hakuwa na mikono ,juma alikuwa analia tu ,adinani alizidi kushangaa jinsi mwili wa juma ulivyokuwaga amenenepa leo hii amekonda mno ,mifupa inaonekanika,

Juma alilia hadi anatetemeka alivyo simamishwa kizimbani kwanza  ushuzi ulimponyoka ,kile kiendo kilimshitua na kufanya akumbuke tukio la wiki tatu zilizopita.
"Juma alipelekwa gerezanai akiwa vile vile ameumia ,mikono haijapona ,mguu umevunjika ,wanaume ambao wapo gerezani hawakuwa na huruma licha ya yeye kuwa katika maumivu.

Hakuwa na mikono ya kujitetea basi wababe wa hilo gereza walimgeuza mke ,walimwingilia kinyume na maumbile  juma alilia kama mtoto na kujua umuhimu wa dunia inatakiwa uishi vipi.

"Basi watu waliokuwepo eneo lile mahakamani waliosikia hio sauti walicheka mno ,juma yeye alikuwa akilia na kuomba siku akizaliwa tena ,basi atakuwa juma  mcha mungu ,juma mwema juma ambae atapenda watu na kuwajali.

Adinani akiwa na machungu alimwangalia na daniel ,kwanza mdomo wake uliong'olewaga meno ulikuwa mweusi pengo jeusi lishapona ,jicho lake nalo lilikuwa tayari limeanza kupona,

Kesi ilianza kusomwa ndipo  mashahidi walipewa nafasi ya kuonesha uthibitisho ,ndipo suhaila alitoa baadhi ya picha ambazo walipiga  kipindi alivyomgongaga gari la ally baba yake na adinani,

Juma nae alipewa nafasi "juma akiwa analia ,alieleza ukweli wote  ,alianza na mauaji aliyofanya ya wazazi wake suhaila na kueleza  "mimi kwenye hayo mauaji ndio nilikuwa mstari wa mbele ,tuliwaua wazazi wake tulichukua mali ,vile vile nyumba niliimiliki mie ,pesa ziliponiishia niliiuza ile nyumba 

Tukio la pili wazazi wa adinani niliwaua mimi tulikuwa na tofauti ndogo tu na marehemu  ally ,nilimwomba pesa anikopeshe  ili nikanywe pombe ,ila rafiki yangu alinijibu pesa anazo ili amaendamwa  kumlipia ada mwanae ili asome ,kwangu iliniumiza maana mie sikuwa na mtoto wa kusomesha halafu nilikuwa na kiu ya pombe .

Hapo ndio nilichukia na kuamua kumfilisi tulichoma duka lake ,nikamgonga na gari alivyokufa ,ibilisi alizidi kuniandama na kutaka kuiteketeza familia yake ,lakin nimeamini leo binadamu si kitu kwa mwenyezimungu ,hadi sasa tunavyoongea sio juma yule gaidi juma kilema ,si juma wa kusamehewa ni juma wa kwenda motoni ,naomba mahakama bila upendeleo mnipatie adhabu inayostahili kutokana na makosa.

Juma aliongea na kuomba radhi kwa adinani na suhaila ,kisha alimalizia najua hamna atakae nisamehe kwa kuwa niliwafanya muwe mayatima kwa kuwaulia wazazi wenu kwa tamaa ila nikizaliwa upya nitakuwa mwema.

Basi mahakama ilipiga makofi kwa mtuhumiwa na wengine walisema yuko sahihi ,basi daniel nae alipewa nafasi ajitetee ,lakin daniel kila akimwangalia suhaila anakumbuka tukio la miaka kumi na saba iliyopita jinsi alivyompasuaga matiti mama yake .
Danile aliweza kusimama ile anataka kuongea alishidwa kutokana na  pengo lake watu walicheke mno.daniel alishusha pumzi lakin alivyotizama mlango wa kuingilia alimwona mwana mama mmoja akija taratibu huku akitiririsha machozi.
Danile na jicho lake moja alikodoa huku akiacha mdomo wazi ,yule mwana mama kila mtu aliyekuwa eneo lile aligeuka na kushangaaaa huku kila mtu akishangaa kwa namna yake
Masikin mama huyu!!!,oohh mungu wangu!!!

Je nini kitaendelea?


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: