NAITAFUTA FURAHA YANGU. 28
Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
____sehemu ya 28___
Tulipo ishia jana, Akamwambia hatimae leo umekamatwa tena huna mikono ,hebu niambie juma jela utaenda huna mikono ,mmmmmm ,niambie
Juma alitizama chini na kuona mkono wake ulio vunjika ,huku damu inamwagika
Juma alijisemea moyoni,damu ya mtu ukiimwaga ukamuua basi nawe utakufa kwa kumwaga damu ,nini kinaenda kunitokea mimi jumaa.
Juma aling'ata meno alijaribu kurusha teke walau ampige suhaila ,asife pasina kumgusa lakin hakujua kwamba suhaila ni hatari zaidi yake na anamachungu ya kumuulia wazazi wake ,kitendo cha juma kurusha teke ampige kifuani ,pale pale suhalia alikwepa nae alirusha teke kali na kumkanyaga juma mguu ambao alikuwa amesimama nao ,alimkanyaga kwenye goti baada ya hapo kilio tu kilisikika na juma alikaa chini hakuwa tena na uwezo wa kuinuka ule mguu ulivunjwa kwenye goti.
Askari wa usalama barabarani walishangaa na kumwambia suhaila aache hicho anachokifanya ,mara mudrick na nusra walishuka kwenye bajaji ,askari waligeuka na kumwona mudrick akitembelea magongo.
Mudrick alipiga makofi nakusema anti kwa sasa nimekubali ,umemvunja juma mguu ,maana yeye ndio chanzo mimi kuvunjwa mguu,nusra alimwambia juma na yeye "umemuua mama na baba ,sasa na wewe unakufa.
Kitendo cha nusra kusema vile ndio wale askari wa usalama bara barani wakagundua huyu ndie juma anae tafutwa na jeshi la polisi,alibebwa upesi na kupelekwa kituoni.
Wakati huo ,mikono miwili ,imevunjika,mguu nao umevunjika,
Juma akiwa analia alipelekwa sero ,ndipo alivyoingizwa alikalisha ,alishangaa anamwona daniel ,hana jicho,daniel aliita jumaaaa
Pengo kubwa mdomoni lilioneoanekanika,umekuja swahiba wangu.
Hapo ndipo juma alichoka na kuona dunia kweli ni duara ,hakujibu chochote zadi ya kutiririsha machozi
Akijiangalia mwili mzima anahisi maumivu ,
Tukirudi maeneo ya masaki suhaila aliweza kwenda kwa akina zumra baada ya kuhakikisha juma amechukuliwa na jeshi la polisi ,ile anafika alikuta mlinzi yupo nje ya geti ,suhaila aliuliza zumra yuko wapi?
Mlinzi alijifuta jasho na kumwelezea suhaila kila kitu ,kwamba zumra ana hali mbaya na amechomwa na kisu tumboni ambako kilidondoka toka juu ya gorofa vile vile alimweleza kuwa hali ya adinani ni mbaya na wala hadhani kama bado mzima.
Zumra aliwasha piki piki hadi maeneo ya mhimbili kufika alimkuta baba yake zumra anazunguka zunguka huku akionekanika kuchanganyikiwa ,baba nini ulikuwa unafanya ,na zumra anaendelea?
Baba zumra alishituliwa na sauti ya suhaila ,alimwangalia suhaila kisha akaanza kuongea "suhaila nimekulea hadi ukakua nikakusomesha ,umeishi na mwanangu kila mkipita watu wanajuaga ninyi ni mapacha,ila mimi baba yenu nimefanya makosa ,zumra yupo kitandani tunasubiria aamke na yule kijana nae yupo kitandani tena hata bado hali yake haijawa nzuri.
Suhaila alitaka kuingia ndani ya hospitali lakin baba alimzuia na kumwambia "mwanangu kwa sasa zumra yupo kwenye matibabu akipona tu utaenda kumwona,basi mzee alizidi kuchanganyikiwa zaidi
Mara nusra na nurudini walishuka kwenye bajaji ,nusra aliuliza "anti inamana tunarudi tena kuishi huku hospitali kama siku zilizopita ?,maana nusra walivyoumiaga na mudrick walilazwa kwenye hio hospitali na leo alivyorudi akajua anakuja kulala huku.
Suhaila alimsogelea nusra na kumkumbatia na kumwambia "nusra kwa sasa tumwombe mungu ,kaka yako akipona naimani ataishi maisha ya furaha ,juma ashakamatwa na hamna tena misuko misuko sawa ee .nusra alijibu ndio kisha akauliza "nimemmiss anti zumra nimwone tu.
Walikaa hospitalini hadi jion ndipo waliruhusiwa kumwona zumra ,suhaila aliingia pamoja na akina mudrick, walimkuta zumra ametulia anahema taratibu,suhaila alipiga magoti chini akiwa analia.
"Zumra wewe ndio baba yangu ,wewe ndio mama yangu ,wewe ndio kila kitu ,tangia nijuane na wewe sikuwahi kupata shida hata ya shilingi mia mbili ,zaidi ya shida ya mapenzi tu.nikiwa na wewe zumra naishi maisha ninayoyataka ,nachagua ninachokipenda ,
Sitaki kukuingilia kwenye mahusiano yako ,baki na adinani wako ,mfanye aishi kwa furaha ,mfanye mwenye furaha iliyopitiliza na kumsahaulisha kabisa kama amepoteza wazazi wake.
Ni hasira tu ndio zilinifanya nikuambie adinani ni wangu,sikuwa ja mahusiano nae ila nami nilianza kuiljenga hisia za kimapenzi juu yake,sikujua kama ninyi ni wapenzi ,na kila siku nilikuwa nakuuliza wewe na adinani mnamahusiano ,zumra ulikuwa msiri uliishia kunicheka na kuniambia nitulie,
Zumra alimshika mikono suhaila na kumwambia "huna kosa ,kosa ni langu naomba unisamehe nikipona basi kila kitu kitakuwa sawa.muda wa kukaa na mgonjwa ulikwisha kisha waliambia na nesi watoke ,
Suhaila alitoka kisha walienda wodi ya adinani walimkuta nae amelala ,ila waliambiwa hana kumbu kumbu wala hakumbuki chochote maana kichwa chake alivyokigongesha kwenye gari basi ubongo ulishituka ndio maana amepoteza kumbu kumbu
Suhaila aliamza kukaa na akina nusra wiki moja ilipita ndipo zumra yeye alipona na aliruhusiwa kurudi nyumbani ,ila adinani yeye alibaki hospitali ,alikuwa hawezi kusimama ,hawezi kuongea wala hakumbuki chochote ,ile hali ilimfanya zumra kuwa na wasi wasi,
Licha zumra aliruhusiwa kurudi nyumbani ila hakukubali alibaki na alikaa hospitalini ili kuangalia adinani hali yake ,yeye ndio chanzo ,alimwomba wafanye mahusiano feki ili amsaidie aachane na mohamedi lakini adinani aliangukia mateso
Baba zumra nae alizidi kuchanganyikiwa na kujilaumu hafai na sibaba mzuri kwa mwanao ,alimtafutia mwanaume wa kumwoa binti yake.
Huyo mwanaume hakuwa mwaminifu anajirusha na wanawake hotelini kile kitendo kilimuumiza sana baba zumra.suhaila akiwa pembeni ya adinani alianza kuongea kwa hisia huku akilia
"Adinani je utanisamehe?,mimi nimekufanya ulale kitandani kwa muda mrefu,nimekufanya hadi kupoteza kumbu kumbu ,hukumbuki chochote ,kwanini mimi?,amka adinani hebu rejewa na kumbu kumbu zako.
Adinani muuaji aliyemuua mama yako na baba ,amekamatwa ,suhaila ameniambia kwa kinywa chake inuka ukamwone tafadhali adinani zinduka .zumra aliongea hadi alichoka na kujikuta anapitiwa na usingizi wakati nae jeraha la tumboni bado halijapona vizuri
Tukirudi maeneo ya masaki baba zumra alikuwa anatoka na gari ili aende kazin ,ndipo haice ndogo ya kifahari ilisimama nje ya geti ,dereva alishuka ili akamfungulie mlango mtu aliyemleta.
Wakati huo baba zumra nae yupo kwenye gari yake jeep nyeupe
Mlango wa ile haice ya kifahari ulifuguliwa ndipo baba zumra alivyotupa jicho alimwona mohamedi akifunga vishikizo vya shati lake ,lakini kwenye siti ya gari ,kuna mwanamke amejilaza akiwa uchi pia sidiria imetundikwa kwenye siti kwa juu.
Mohamedi alishuka na kumsalimia baba zumra "shikamoo mkwe wangu unaenda kazini?"baba zumra alikuwa anahasira mno ,yaani kijana aliywemwamini na kutaka kumu ozesha binti yake ,kumbe anafanya uchafu na wanawake ovyo hadi kwenye gari ,
Mzee alichunia ile salamu na kumuuliza "ehee umefuata nini kwangu?
Mohamedi alitabasamu na kuuliza "mchumba wangu hajambo?,nimekuja kumwona.mzee kwa hasira alishuka kwenye gari yake na kwenda kuufungua mlango wa haice ,kisha akamwambia unaona huu upuzi wako unao ufanya ,
Yaani wewe pesa zinakupa kiburi unatumia wanawake wawatu vibaya hadi kwenye gari halafu unakuja hapa eti unakuja kuona mchumba.
Mohamedi kuanzia leo basi na sitaki nikuone tena na binti yangu wala sitaki kukuozesha ,ingia kwenye gari kisha ondoka.mohamedi anayomazarau mno,aliegemea gari na kumwambia baba zumra ,
Nilikuwa na hamu ya kulala na mwanamke maana mtoto wako hanitaki ,sio kwamba nimefanya hivi kwa makusidi hapana nilikuwa natuliza haja zangu.
Halafu mzee baba yangu anayopesa hadi anaumwa ,hivyo kubali nimuoe binti yangu ili muweze kufanya biashara na baba yangu.ha ha ha ,mohamedi alicheka na kuingia kwenye gari ,alimwambia mzee "mimi ndio mohamedi huyo binti yako nikikutana nae lazima nilale nae ,
Huwezi kuniita mimi malaya mchafu wakati sijalala na binti ,yako nakuambia iwe kinguvu au kihiyari lazima nilale na binti yako.mohamedi aliongea kisha akaondoka
Mzee aliwaza sana ,huyu kijana anakichaa ama amechanganyikiwa ,nae aliwasha gari ili aende kazini kwake.
Zilikatika wiki tatu ndani ya hospitali ya mhimbili ,moja ya wodi aliyoko adinani ,aliingia mtu ambae alionekanika kuvaa mavazi ya meupe ,alisimama kwenye kona ya mlango alionesha ishara ya kumwita adinani huku akiita kwa sauti ya upole njoooo
Adinani njoooo,yule mtu ameshikilia kibuyu chekundu kilichokuwa kimerebwa vizuri na kuchorwa maua.
Adinani aliinua kichwa ili kumwangalia nani huyo anamwita
Alifunika kichwa kwa kitambaa cheupe "alianza kuzungumza "nyumba ninayoishi inabaridi sana ,hamna mtu yeyote anakuja kunitembelea ,adinani ,unateseka sana njoo kwenye kwenye makazi ninayoishi naimani nafsi yako itapumzika
Adinani alivyomtizama huyo mtu anayeongea miguuni alikuwa na peku adinani aliweza kutizama vizuri aliona ukucha wa kidole cha mguuni ,ulikuwa mweusi ,na huo ukucha alikua nao marehemu baba yake ,adinani alikumbuka siku hadi marehemu baba yake ,aliumiaga alivyokuwa ananyanyua ringi la gari lilimponyoka na kugonga kidole cha mguuni kisha kile kidole kiliharibika siku ile
Adinani akiwa anaangalia vile yule mtu alitoa kitambaa cheupe kichwani ,alikuwa ni baba yake ,baba alinyoosha mkono na kusema njoo kwanangu "adinani nae akiwa kitandani alinyoosha mkono lakin alishangaa umbali aliosimama baba yake mlangoni hadi aliko lala yeye
Ile mikono ya baba yake ambae amemwona ilirefuka hadi kufika kitandani kwa adinanii na kumshika ,adinani alifumba macho na kupiga kelele hapanaaaaaaaaaaa hapanaaaaaaa
Zile kilele ziliwashitua madaktari na kufanya waingie upesi kwenye chumba cha adinani
Ile wanaingia adinani alikohoa koho koho kisha akawa kimya alilala na kunyoosha miguuu yake
Je nini kitaendelea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: