NAITAFUTA FURAHA YANGU 27



Story :NAITAFUTA FURAHA YANGU

--sehemu ya 27 ---- 
  Tulipo ishia jana,Basi vijana wa baba zumra walichukua jukumu la kumtupa chini ,yaani kutoka juuu kabisa ya gorofa ,basi walimwinua adinani akiwa hoi baada ya kuchapwa sana ,tena akiwa amefugwa kamba halafu walimrusha adondokeee chini.adinani alifumba macho na kusema kwa sauti ya nguvu,zumra nakufa kwa ajili yako basi walinde nusra na mudrick
 na uhakikishe wanaipata furaha

Adinani hakutaka kuangalia ni wapi anaenda kuangukia aliamua kufunga macho ,lakin wakati ule adinani anatupwa juu ya gorofa ili adondoke chini ,pia zumra nae alikuwa tayari ashafika nyumbani ,zumra alifunguliwa geti ile anaingia akaona mtu akiteremka toka juuu,zumra aliangalia kwa upesi alikimbia ili akamdake adinani, 
Aliwahi kumdaka lakin hio sehemu kulikuwa kuna gari ime egeshwa eneo lile ,ni kweli zumra alijitahidi kumdaka ila adinani aligongesha kichwa kwenye gari puuuu.
Adinani hakuongea wala kutoa sauti ,yeyote alibaki kimya.

Adinananiiiii,nisameheeeee ,mimi ndio nimekuponzaaa ,adinaniii usifee wadogo zako utawaachajeee, zumra alilia kukua amemkumbatia adinani ,lakini zumra akiwa analia alimlaza adinani chini nae alilala chali huku akilia kwa nguvu mno.

Baba yake alitoka na kumwangalia jinsi mwanae analia alicheka na kusema hio ndio dawa ya watu wabishi,ila nimempenda huyo kijana anmsimamo amekubali kufa kwa ajili ya binti yangu ,basi roho yake iende moja kwa moja peponi ,huo ndio upendo wa kweli.
Baba zumra aliongea na kuingia kwenye gari kisha akaondoka.

Zumra akiwa chali ,juu ya gorofa sijui kisu kiliwekwa vibaya nacho kilidondoka ,zumra akiwa analia machozi yamejaa machoni wala hakuona chochote ,gafla kisu kilienda na ncha kali kisha kikajikita tumboni puuuuuh!!!

Aaaaaaaaah ,ni sauti ya zumra ilisikika kisha akapelekw mikono kwenye tumbo lake alishika mpini wa kisu,zumra nae aliamini anamfuata adinani.
Wale wapambe walio pewa kazi na baba yake ,wanashuka chini wanakuta zumra nae amechomwa na kisu ,hata wao wakashangaa,zumra alijikaza aliwaambia wale vijana ,naomba mtupeleke hospitali na huyu kijana ,endapo mtakataa kunipeleka hospitali nachomoa hichi kisu ambacho kipo tumboni na nikikichomoa tu upepo ukiingia tumbon napoteza maisha.

Baba yangu atajua ninyi mmeniua hivyo nadhani mnamwelewa vizuri wote mtaenda kuozea jela.,zumra akiwa amejikaza aliwaambia vile.wale vijana wanamwogopa mno baba zumra hata hawakubisha waliwapakia wote kwa pamoja na kuwahishwa hospitali.
Zumra hakupoteza fahamu ,hadi wanafika hospitalin ,ile wanapokelewa na madaktari pale pale alipoteza fahamu alipo hakikisha adinani ameingia mikono mwa daktari,
Kisha aliongea neno moja "dokta huyo kijana akifa nami nakufa ,pale pale akazimika.

Wakati huo baba yake na zumra hakupewa taarifa ,yeye alienda moja kwa moja hadi hotel ya serena ,alifika hapo ili kukutana na kijana mohamedi ambae amepanga hotelin,baba zumra alienda moja kwa moja kwenye chumba cha mohamendi aalikijua vizuri alienda moja kwa moja kisha akagonga.

Sauti ya mohamedi ilisikika ndani akiongea huku kuonekana amelewa "nani huyo anagonga mlango ingia ndani mlango upo wazi,basi baba zumra lengo lake la kutaka kuonana na mohamedi ilikuwa kumpa habari kuwa kijana ambae alikuwa kizuizi na kusababisha binti yake kumkataa kabisa mohamedi asimuoe ,basi alikuwa anaenda kumweleza kuwa tayari ashamuua.

Baba zumra alifungua mlango,alibaki ameduaa mlangoni na kushidwa aingie ama arudi. Kijana ambae amemwamini na kutaka amuoe binti yake amemkuta yupo hotelin chumbani ,na wanawake watatu ,wote wapo nchi kama walivyozaliwa ,

Chumba kimejaa pombe za bei mbaya,halafu mohamedi shombe shombe kijana tajiri anae miliki makapuni ya baba yake ,alikuwa akipapaswa kila mahali na wanawake watatu.

Mohamedi aliuliza kwa sauti ya kilevi "wewe nani mbona umesimama na wala huingiii ,au unataka pesa,?,sema kama unashida na hela ,mimi nina pesaaaaa hadi naumwaaa
Warembo nipeni vitu vyote na mkimaliza kila mmoja ataje idadi ya pesaaaa.
Mohamedi akajilaza kitandani ,basi wale wadada wanafanya kumwagia mohamedi pombe mwilini halafu wanaambiwa wazilambe na ulimi hadi ziishe mwilin.

Baba zumra hakuongea chochote alirudishia mlango kisha akaondoka ,kimya kimya,akaanza kukumbuka maneno ya binti yake ,"baba mimi sitaki kuolewa na mtu mwenye pesa ,mwenye makampuni ,huwa hawana mapenzi ya kweli ,huwa wanapedwa na watu wengi wenye tamaa ya pesa .baba akaamin mtoto wake yuko sawa.

Kisha akakumbuka ,jinsi alivyowaamuru vijana wampige adinani ikiwezekana hata afe ,ili akubali kuachana na mtoto wake lakin adinani alikataa kata kata na kusema anampenda zumra.

Mzee alizidi kukumbuka "amempa adinani mamilion ya pesa ili aachane na mwanae lakin adinani aliwaeleza heri afe na si kuchukua chochote ,hapo mzee akaamini ,kweli masikin wanapenzi la dhati ,pia akaamini yule kijana anampenda mwanae na kuamini hatomtesa  wala kumuumiza.

 alikumbuka hali aliyomwacha yule kijana ,alikuwa kimyaa na ametapakaa damu mwili mzima,mzee aliingia kwenye gari mara simu yake ikaita ,alivyoangalia jina aliona ni kijana wake mussa ,alipokea haloo musa

"Bosi samahani sana mtoto wako yupo mhimbili ilitokea emegency amedondokewa na kisu tumboni hivyo kimemchoma na anahali mbaya,mzee aliuliza unasemaaa nini???
Na yule kijana amekufa au yupo hai,mussa alimjibu ,kijana nasikia yupo hai ila nimempa maelezo dokta amuue kabisa  ili tufute ushahidi na kesi tuje tuseme amekufa kwa ajali ya gari.

Baba zumra kwa hasira ,alisema huyo kijana asiuliwe ,fanya ufanyavyo nimkute mzima ,ni heri hata mwanangu afe lakin si huyo kijana ,nimeamini huyo kijana ana umuhimu  ,simu ikakatwa 
Hadi mussa akashangaa imekuwaje boss anasema huyo dogo asife ,kwanini ,basi musaa alikimbia chumba  anachotibiwa adinani ,ili akamwambia dokta asimuue 
Ile anafika mlangoni anakuta dokta anaingia ,mussa akiwa anahema alisema "dokta plz usimuue huyo kijana fanya juu chini apone bosi anasema hadi kufika hapa akute mzima.

Dokta anamjua vizuri baba yake na zumra alivyosikia hivyo basi hapo waliamza kumpa matibabu adinani ,wakati huo zumra kisu kilichomolewa kisha alishonwa sehemu alikokatwa ila kishu kilikuwa kidogo hivyo hakuumia sana.

Zumra baada ya masaa sita kupita, alizinduka alivyoinua kichwa alikuta baba yake amelala pembeni,zumra alishangaa ,aliita babaa baaaabaa je adinani yupo hai?.mzee aliinua kichwa baada ya kulia kwa muda mrefu na kujutia maamuzi yake yaani amemchagulia mwanaume ambae analala na wanawake kwa mara moja zaidi ya watatu.
Vile vile mzee akikumbuka aliamuru adinani auliwe ili asiendelee kuwa na mahusiano na binti yake.

Tukirudi upande  aliko lazwa adinani baada ya kufanyiwa vipimo iliomlnekanika alipata mshituko ,hivyo kumbu kumbu zimepotea hakumbuki chochote ila alianza kuhema taratibu .
Baba zumra alizidi kuwaambia madaktari wafanye juhudi ili huyo kijana apone,

Suhaila na wadogo zake adinani baada ya kumsubiri zumra na adinani warejee nyumbani aliona wanachelewa ,aliamua kuchukua bajaji ili aende masaki akaangalie je amefanikiwa kumwokoa adinani au laa.

Suhaila kila akijaribu kumpigia zumra simu inaita wala haipokelewi akimpigia adinani wala haipatikani kabisa ,suhaila aliwaza huenda wamekubwa na jambo baya.
Suhaila alimwacha mick alinde nyumba kisha akapanda bajaji pamoja na akina nusra na hilda(shangazi),safari ili anza kuelekea masaki.

Lakini wakati  wanatoka nyumbani ,juma hakuwa mbali na eneo lile ,lengo lake juma aliweka ili aondoke dar ahakikishe ,adinani na wadogo zake nao wanakufa.aliamin hao ndio wanamfanya yeye aishi maisha magumu mno.

Juma alikumbuka marafiki zake "daniel ,kelvin na dokuu wote amewapoteza ,wawili wamekufa amebaki mmoja ,juma alizidi kuchanganyikiwa maana alishududia moshi ukifuka kwa mbali wakati dokuu anachomwa moto na wanachi,

Juma alikumbuka, dokuu ndio alimshawishi waweze kumuua  shemeji yake ,baba yake na suhaila ili wapate zile mali.vile vile dokuu alimshauri auze nyumba ambayo baba yake na suhaila alipokufa yeye ndio alirithi kila kitu mwisho wa siku aliuza .

Juma alikuna kichwa chake na kujisemea moyoni "adinani lazima nikuue mimi siwezi kukamatwa na polisi kizebe ,japo unalidwa na hao mabinti wanauwezo wa kupigana,adinani unanini kwanini umekuwa kikwazo kwenye maisha yangu.naitafuta furaha yangu ya mali za zuluma ,adinani lazima nikuue.

Juma aliongea kwa uchungu huku akipiga usukani wa fuso ,alikuwa amepanda kwenye fuso ,alipo waona akina nusra na suhaila wanapanda bajaji basi yeye alichukua fuso aliwaza jambo moja
 .kama alianza kwa kumwaga damu za watu pia kumaliza nao atamaliza kwa kumwaga damu za watu.

Suhaila alimwambia dereva wa ile bajaji mimi naenda masaki ila naomba mimi niendeshe piki piki kisha wewe uwe abiria leo kwakuwa nina haraka basi yule dereva alikubali kisha akakaa siti ya nyuma na akina mudrick safari ilianza kuelekea masaki

Zumra akiwa barabara kuu alishangaa kuna fuso inamfuatilia kwa nyuma ,kila akihama saiti ile fuso nae inamfuata ,basi  
 Suhaila alivyofika relini kwenye bara bara kubwa ,aliwaza nani mwenye hio fuso anamfuatilia basi suhaila alinyoosha na barabara ya ubungo rodi lengo lake kumpoteza yule mtu mwenye fuzo .

Walifika maeneo ya mwanachi barabara ikawa na magari machache basi suhaila alipita pembeni karibu na mtaro yaani akikwepesha kidogo tairi ya kushoto anaingia mtaroni 
Basi juma ambae alikuwa yupo kwenye fuso ,alijisemea hapa hapa hawa watoto naua wote na mwenye bajaji pamoja na bajaji yake.
Juma alikanyaga mafuta akaongeza spidi ili agonge ile bajaji ambayo ipo mbele yake ,hakujua kama kawekewea mtego ,suhaila aliinyoga bajaji na kuingia barabarani vizuri  ile fuso tair za mbele ziliteleza  upande wa mtaroni

Fuso ilipinduka mtaroni tair juuu ,kisha suhaila aliipaki piki piki pembeni na kwenda kuangalia ni nani alikuwa anataka kumgonga,suhaila alienda upande wa dereva alivyoangalia ,aliona mkono upo nusu , alivyoangalia vizuri aliona damu tu .suhaila hakuwa na haraka alisubiri polisi wa usalama wa bara barani walikuja na kufungua mlango walimshusha juma akiwa hatamaniki amedondoka mwenyewe mikono yote miwili imevunjika ,tena mkono mmoja umekatika kabisa na kudondoka.
Miguu ilikuwa mizima ,suhaila alimsogelea juma akiwa analia kama mtoto,
Akamwambia hatimae leo umekamatwa tena huna mikono ,hebu niambie  juma jela utaenda huna mikono ,mmmmmm ,niambie
Juma alitizama chini na kuona mkono wake ulio vunjika ,huku damu inamwagika 
Juma alijisemea moyoni,damu ya mtu ukiimwaga ukamuua basi nawe utakufa kwa kumwaga damu ,nini kinaenda kunitokea mimi jumaa.hatimae juma amekamatwa hana mikono ,kapata ajali

Je nini kitaendeleaaa?



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: