SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)




MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 06



TULIPOISHIA: Patrick aliwapita moja kwa moja bila kusimama Ila Zakayo na Abdul walisimama wakiwaomba wale waliokaa wanyanyuke wakimbie, wakiwa bado wanajilemba lemba mara Wengine viatu vyangu, wengine simu yangu, Wengine begi yangu Ipo wapi huwezi kuamini jeshi la sokwe wenye miili mikubwa mikubwa Kama ishirini hivi ilitia timu, aisee wenzetu ile kushangaa shangaa waliwekwa Kati wote nikimaanisha walizungukwa na sokwe wale. 

SONGA NAYO!

Upande wetu tukiwa tunakimbia bila kujuwa nikipi kimetokea sauti ya Patrick tuliisikia akitusimamisha, nasi tukaona kusimama, alipotufikia Nikamuuliza: kuna nini huko? 

Patrick: sokwe Kama Elfu moja walikuwa wanatukimbiza hivi niongeapo wale wazembe sijui kimewakuta nini huko. 

Mimi na Latina Tulishtuka mno kisha nikasema: kama sokwe ni wengi Sana na bado Sisi hatujaskia kelele za wenzetu basi huko wanachezea kichapo twende kutoa msaada. 

Tulijadiri namna ya kutoa msaada tukapata suruhu, Baada ya muda tulikuja Mimi nilikuwa nimeshikilia tawi la mti uliokauka Ila Kidogo majani yake yalikuwepo huku tawi lile likiwa linawaka moto kweli,  Latina nae vile vile hata Patrick, ndipo tukatokea pale  sokwe na wenzetu walipo tukaja Kama vile tumevuta bangi zisizo za kawaida, kwa kasi ya kufa mtu huku tukipiga ukunga: aaaaaaaahhhhhhhhh. 

Mbio zetu, kujiamini kwetu pia na fujo zetu ziliwafanya sokwe wale waingiwe na uoga ukija kuangalia tulivyokuwa tunakuja na ule moto ndo kabisa sokwe wale wakajikuta wanakosa uvumilivu wakatoka hapo nduki,  na Sisi nyuma tukadata tukawapita wenzetu tuwafukuzia sokwe wale mpaka wakatokomea mbali ndo tukaona kurudi, tulipofika pale tulipowaacha wenzetu huwezi kuamini hatukukuta hata mtu hata mmoja aisee Tulicheka, haraka tukachukuwa simu walizoziacha pia na begi zao kisha tukaanza kuwatafuta.

Tukiwa tunawalalamikia ndugu yangu huwezi kuamini kama vile sasa tunapuliza filimbi ya kuwaita simba huwezi kuamini walitokea mbele yetu simba jike wawili na dume mmoja alioshiba nyama za swala maana kwenye msitu Huo watu adimu sana kuwapata, tumbo ya Latina ilishuka ikawa ndogo Kama mpiga mazowezi vile misuli nayo ikasema tumechelewa nayo ikajituna freshi, Juu yangu kulikuwa mti flani mrefu kiasi, ndugu yangu Latina alinirukia sekunde chache nikashangaa kumuona Juu ya mti ule, ile na geuka kumuangalia Patrick sikujua saangapi kafika Juu ya mti uliokuwa nyuma yangu na muda Huo simba jike mmoja alikuwa Chini ya mti alipokuwa Latina na mwingine kwa Patrick Mimi nikabaki hapo sasa na mzee baba simba dume, macho yangu kwake nayo macho kwangu, Kawaida ya simba ukiwa imara nae anatulia akikusomea lamani huku akinghuruma taratibu ili kukutisha, machozi sikujuwa muda gani yameanza kunitiririka mashavuni, kichwani nikaingiwa na kichaa cha kusema nirudi nyuma tu nikimbie zangu kama kufa tayari Mimi maiti, wee saangapi sijatupa mizigo yote nikaanza kukimbia, nae simba akasema yes wewe wangu, nilipiga kama hatua ngapi simba alikuwa tayari amenifikia na kuushika mtandio wangu kwa nyuma, niseme bahati nzuri au mbaya ile Yeye kanishika mtandio Na mimi nilikuwa nimefika eneo mbaya yenye kishimo chenye Kina kirefu nikajikuta nadondokea humo na simba nikamuachia mtandio tu,  simba alihangaika kuona kitoeo chake kimemponyoka kizembe akaanza kuzunguka zunguka Juu huku akiniangalia vizuri,  muda Huo nikiwa ndani ya Shimo lile  macho yangu kwake kama vile tunaviziana, Dua Za kila Aina wallah niliomba Mpaka nikaanza kuomba msamaha kwa Muumba wangu anisamehe zambi zangu zote,  nikiwa nipo hapo ndugu yangu nilishtuka kuskia mlusi flani karibu na skio yangu, kwanza nikaganda huku nikiskilizia kwa umakini, taratibu nikageuza shingo ili kuangalia je ni nini kinachoendelea! aisee uso kwa uso, macho kwa macho na nyoka Aina ya Kobla, nyoka huyo ni mkali kuliko nyoka wote unaowajuwa, nilijifikiria Imekuwa kuwaje Mpaka Kichwa chake kikawa sambamba na kichwa changu namna hio, taratibu nikashusha mboni tu Hapana kichwa chote wee nilikuwa nimepooza, ile kuangalia Chini ukubwa wa nyoka huyo ulinipagawisha Nikajikuta Napiga ukunga, ile Hali ya kupiga kelele bila kujitambua nilijikuta naipiga mkono nyoka ile sehemu mbaya maeneo ya shingoni nikaibananisha na ukuta wa udongo bila kujuwa, nikaja kushtukia damu inanirukia usoni, sikujuwa nikipi kinaendelea niligeuka kuangalia alipo nyoka Yule, aisee Sikuamini kumuona nikiwa nimemuua ajabu amedondokea Chini,  aisee hapo sikuweza kuvumilia tena nilizimia taratibu. 

Upande wa Latina hata kumkumbuka dada yake alikuwa hakumbuki kwa Muda Huo alijiona Yatima nikimaanisha alizaliwa mwenyewe hivo ndivo hakili zake zilimwambia, isikukute Upo Juu ya mti Chini simba nae katulia Mpaka kulala akikusubiri utoke Juu,  hata upande wa Patrick Ilikuwa hivo hivo,  upande wangu simba dume hakukata tamaa kabisa aliendelea kukaa pale akinisubiri kwa hamu.

Muda Huo mwanajeshi Dominic alifika akatoa bastola mfukoni kisha akapiga lisasi Juu baada ya kuona simba wale, ule mlio uliwashtua Sana wale simba wakajikuta wanakosa uvumilivu wakatoka hapo nduki. 

Dominic aliwashusha Kina Latina ndipo akaanza kuwauliza kuhusu Mimi Ila Hakuna aliemjibu maana hakili nikama zilikuwa zimeruka, Kama dakika nne kupita walianza kujitambua ndipo Dominic akauliza: mwenzenu yupo wapi? 

Wakamuuliza: mwenzetu nani? 

Dominic alimgeukia Latina na kusema: dada yako? 

Latina bila kujielewa akasema: Kwani mi nina dada? 

Dominic aliishiwa na kusema: dada yako Najma yupo wapi? 

Ndipo Latina hakili zikarudi akasema: jamani dada yangu yupo wapi? 

Dominic: ndo nakuuliza wewe. 

Latina alinyanyuka akawa anatafuta huku akisema: mara ya mwisho nimemuona maeneo hayo Sikumbuki nini kiliendelea Kwani kuna nini mbona sielewi? 

Dominic akajuwa Huyu alipagawa Baada ya tukio,  muda Huo Patrick alikuwa kimya hata alikuwa haelewi nini kinaendelea. 

Dominic alipokumbuka Yule simba dume alipo kuwa muda ule akaamua kusogea ili kuangalia pale Yule simba alikuwa amefuata nini, alipofika ndo akaona Shimo kuangalia ndani akashangaa kuniona ndani nikiwa Nimelala na nyoka pembeni yangu Ndo akajuwa basi Mimi tayari nimeshakufa, aliniita kwa sauti ya majonzi ila sikuweza kuzinduka.

Latina aliponiona nimetulia alianza kulia akihisi Labda sipo tena duniani.

Dominic kwa kuwa Yeye alikuwa mwanajeshi alizijua mbinu za kunitoa mle, iwe ni mekufa au bado, alitafuta mti mlefu akaungiza ndani ya Shimo lile akaanza kunitikisa ili kuhakiki je Nikweli sipo tena duniani, ile Hali ya mimi kuguswa na mti ule nilizinduka na kupiga kelele, Patrick na Latina walifurahi sana kuona Mimi bado mzima.

Dominic alinituliza baada ya kuona nimedata, haraka akaenda kutafuta kamba mwishowe wakanitoa ndani ya Shimo lile, tulikumbatiana na Latina kwa furaha ndipo Dominic akatuambia: fanyeni mpango tutoke eneo hili. 

Patrick: wenzetu wapo wapo? 

Dominic: twende huku wametongoja. 

Tulianza safari nilipopiga hatua kama kumi nilidondoka Chini maana muda ule nilipodondokea ndani ya Shimo lile niliteuka mguu, na kutokana moyo ulikuwa bado upo Juu Juu nilivyotolewa sikuskia maumivu yoyote ila kwa kuwa muda ule Nipo sawa ndo maumivu yakaamka. 

Wote walinikimbilia wakaniuliza hali yangu nikawajibu kwa sauti ya maumivu: mguu wangu jamani. 

Latina: jikaze basi. 

Patrick: utaweza kutembea? 

Walinishika mkono nikasimama taratibu, nilipojaribu kupiga hatua tena sikuweza maana maumivu yalikuwa makali ndipo Dominic akachuchumaa mbele yangu na kusema: panda mgongoni. 

Nilishtuka na kumtazama Latina. 

Latina alitabasamu na kusema: panda. 

Nikamjibu: aaahhh! wee! Mwaya mjeda I'm alright. 

Dominic alisimama na kuniuliza: utaweza? 

Nikamjibu: eeeehhh ntaweza mbona. 

Dominic: OK twende.

Ile Kuinua mguu tu nikapiga kelele ndipo Patrick kwa sauti ya hasira akaniambia: si unaona sasa? 

Nikamjibu: ntajaribu. 

Dominic: panda mgongoni usitupotezee muda. 

Wote walinikazia nipande mgongoni, sikuwa na namna nilipanda kwa aibu.

Tulipowafikia wenzetu walipokuwa wametusubiri aisee walikuwa wamepondeka na kichapo cha sokwe wale, Derick aliponiona Nipo kwenye mgongo wa Dominic moyo ulimuuma sana, nilipomtazama niligundua ameumia ila nikapotezea, aliponiweka Chini tu, aisee huwezi kuamini kilitokea kitu juu kikadondoka Chini, watu wote wakapiga kelele huku wakitazama kitu kile......... 


Unahisi nini kitatokea! 
Usikose mkasa huu!


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: