SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)




MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 04



TULIPOISHIA: Rodrigo: vipi kuhusu wazazi wako? Na vipi kuhusu madeni ya baba yako? 

Joyce akadakia: Najma kubali Baada ya zowezi hili tutapata mabilioni ya pesa acha kuwa mzembe. 

Nikamuuliza: sasa Rodrigo itakuwaje mbona Mimi sielewi. 

Rodrigo: tunaelekea huko Kongo ndipo kuna msitu Huo wa Equatorial sema Ndio au Hapana maana hapa hatuna muda je Upo tayari? 

SONGA NAYO! 

Kichwa kiliwaka nikapiga mahesabu ukweli walichokuwa wanakiongea kilikuwa sahihi Licha moyo wangu ulikuwa unasita sikuwa na chaguo nilijikuta nakubali ndipo Rodrigo akasema: kwahio tutajuzana itakavyokuwa. 

Nikamuuliza: Malipo ni vipi? 

Rodrigo: milioni hamsini kwa kichwa cha mtu Kama tutafanikiwa.

Nikamuuliza: ila jamani tutafanikiwa kweli?  Mbona wazungu hili swala hawajalifuatilia Sisi ndo tutaweza? 

Rodrigo: Uliza Kwanini malaria Ipo huku Africa tu huko nchi zilizoendelea Mpaka South Africa Huo ugonjwa haupo na Mbu wapo, Kwanini hio anty Malaria wasituletee? Acha Sisi tufuatilie tusitegemee kila siku kutaftiwa sawa! 

Tulikubaliana hivo tukaagana, Mimi na Joyce tukaenda manyumbani. 

Nilipofika nyumbani nilimueleza kila kitu Latina ndipo akasema: hii bahati hatuwezi kuipotezea lazma twende huko ausio. 

Nikamjibu: wewe haumo utabaki unawaangalia wazazi. 

Latina: dada Acha nije embu fikiria mtu mmoja milioni hamsini tunalipa Deni mwingine milioni hamsini tunapata mtaji tunafungua duka la madawa Unaonaje. 

Nikamjibu: Hapana Latina. 

Latina: please mwenzio nataka kwenda sasa hapa ntabaki nafanya nini Mimi ni mwana science ujuwe! Lazma niende kutalii ili kujiongezea ujuzi zaidi niruhusu. 

Nikamjibu: Nikweli Acha twende wawili tuache tumemwambia doctor amtazame mama baba nae kule yupo Salama. 

Latina: eeeehhh. 

Baada ya siku chache Tulianza kujiandaa ili kuondoka, upande wa Derick alikuwa bado hajarudi wingereza kutokana na tatizo hilo la Ebola lilimfanya asubiri kwanza ajuwe mwisho wake utakuwaje.

Siku yenyewe ya safari yalikuwa ni Majira ya saa tano usiku tulielekea airport ili kuchukuwa usafiri wa ndege tuelekee huko Kongo, Tulifika kwenye chumba maalumu wakatufanyia vipimo ili tusiende na ugonjwa Huo wakatukuta tupo Salama, wenzetu Kama Saba waschana wawili wanaume watano tulisalimiana tukatambulishana, wote hao walikuwa levo ya Juu Sisi tu levo yetu ki science ndo Ilikuwa ya Chini,  mwishowe tulipanda ndege tukapewa siti zetu, maprofesa wa tatu akiwemo Rodrigo Waliingia nao wakakaa, kuna kijana mrefu mwenye weusi wake Wa mng'aro mrefu mwenye bodi kubwa yaani mwili wake alifanana kupenda mazowezi sana, alipotupita alikaa Siti ya mbele yetu ndipo Rodrigo kwa nyuma akanitika na kuniambia: huyo ni mwanajeshi selekali imemteuwa Yeye aje kuimalisha ulinzi wetu. 

Mimi na Latina tukamjibu: ndo maana. 

Watu wote Waliingia na safari ikaanza kimoyo kimoyo nilianza kuwaaga wazazi wangu: I'm sorry mamy and dady hatuna chaguo ila hapa karibu tutakuwa Pamoja na mtafurahi.

Baadhi ya watu walianza kulala,  tukiwa tunazidi kusonga Latina aligeuka kunyuma kumwangalia Joyce ndipo Joyce kwa ishara akamwambie aangalie pembeni Latina alipoangalia pembeni hakuamini kumuona Derick akiwa amekaa huku akisoma gazeti taratibu, Latina macho yalimchomoka akageuka kunitazama ndipo Nikamuuliza: nini? 

Latina: flani. 

Nikamuuliza: nani? 

Latina: Derick. 

Nilishtuka na kumuuliza: Kafanyaje? 

Latina: tupo nae. 

Nikamuuliza: wapi? 

Latina: yupo nyuma yetu. 

Pumzi nusu kukata Baada ya mimi kugeuka nyuma nikamuona amekaa ndipo nikageuka haraka na kuangalia mbele, Latina akaniuliza: tunafanyaje? 

Nikamjibu: usigeuke tena Mpaka tufike.

Latina: subiri jamani Mara moja tu. 

Nikamjibu: Ndo Matatizo yako. 

Latina aligeuka nyuma akamtazama kama sekunde kadhaa akageuka na kuniambia: dada pembeni yake kuna hicho kigoli huwezi kuamini. 

Nikamuuliza: binti mzuri? 

Latina: huwezi kuamini ni kama malaika.

Upande wa Derick  mdada Yule Aliekuwa amekaa nae muda wote alikuwa anamtazama Derick jicho la wizi wizi, Derick alipogundua alitabasamu na kumuuliza: samahani tunaweza kujuwana? 

Mdada Yule akatabasamu na kusema: naitwa Amanda. 

Derick alitabasamu na kusema: Mimi Derick. 

Walianza kupiga story taratibu Amanda akaonekana mcheshi sana na mpenda Utani Amanda alipocheka Derick alimtazama anavocheka aisee binti huyo alikuwa mrembo Sana taratibu Derick akaanza kuvutika nae. 

Upande wetu Usingizi ulituvuta tukalala.

Hatukuchukuwa siku Tulifika katika mkoa uliopo Kongo uitwao Bandundu wana science wa huko walikuja kutupokea tukafikia kwenye hotel kubwa ya kifahari kila mmoja akaoneshwa chumba chake,  Mimi na Latina tulihakikisha hatujajionesha mbele ya Derick maana sikutaka ajuwe kuwa tupo kwenye msafara mmoja.

Kwenye hoteli hio hatukuchukuwa siku mbili tulipewa mwana science mwenzetu wa hapo Kongo ili kutusindikiza na safari ikaanza ili kuelekea kwenye msitu Huo wa pili kiukubwa dunia nzima,  tulipofika kwenye usafiri wa basi watu tulioandaliwa  walianza kusalimiana ili waweze kujuwana kiundani Sisi tukiwa tupo nyuma ya mgongo wa Joyce na Rodrigo Latina alitoka na kusema: aisee hatuwezi kuendelea kujificha mtu ambae tupo nae kwenye msafara mmoja. 

Alisogea karibu kama wengine Na mimi Nikaona isiwe kesi nikaamua kujitokeza, mkaka flani tulietoka nae Tanzania alisema: tuhakikishe tunabeba mafuta ya kutosha. 

Mwingine akamjibu: uliambiwa msitu upo hapa!  Bado safari Ipo tena ndefu kuliko ile iliotutoa nyumbani.

Walitabasamu nilipomtazama Derick Muda Huo Yeye alikuwa bize na Yule binti Amanda mwenye alikuwa na mwonekano tofauti na waschana wote hapo, kijana mmoja alimpa mkono professor Rodrigo na kusema: Mimi naitwa Isaac.

Rodrigo: naitwa Rodrigo. 

Joyce akasema: Mimi Joyce. 

Latina: Latina hapa. 

Nami nikasema: Najma. 

Binti Aliekuwa pembeni yetu akasema: Sofia. 

Mkaka mwingine akasema: zakayo. 

Mwingine: Abdul. 

mwingine: Chande.

Mwingine: Patrick. 

Mdada mwingine: Hamisa. 

Mwanaume mwingine alieonekana kuwa mpole Sana akasema: Jina langu naitwa Joseph. 

Yule mkongo aliekuja ili kutuongoza akasema: naitwa chilunga. 

Abdul: chi! Chi! chi....

Zakayo: utakatika ulimi. 

Tulicheka sote kwa Pamoja. 

Professor mwingine akasema kiutani: naitwa husband (mume).

Tuliangua kicheko Mara dufu ndipo Abdul akamtazama Derick na kumuuliza: samahani mheshimiwa Jina lako Nani?

Derick alitabasamu kama Kawaida yake kisha akasema: naitwa Derick.

Patrick kwa Utani akasema: na huyo wa pembeni jamani! 

Amanda kwa aibu aliangalia Chini ndipo Derick wakaongea kwa kingereza mwishowe Derick akasema: ameskia aibu ntamsemea Mimi Anaitwa Amanda. 

Wanaume wote wakasema: wow!

Walicheka wote hata Derick pia Ila ile Hali ya kucheka huku akiangalia angalia watu maana zilikuwa nyuso ngeni kwake alishangaa kuniona nikiwa bize naangalia Mazingira ya hapo,  macho yalimtoka akataka kunifuata ila Amanda alimshika mkono na kumuuliza: kuna nini? 

Derick akaamua apotezee. 

Upande wetu Zakayo alimtazama Yule mwanajeshi na kusema kwa sauti ya Chini: yule Jamaa nani atamuuliza Jina lake?

Wote Tulimtazama kiukweli Alikuwa anastahili Sifa za kuitwa mwanajeshi maana muda wote alikuwa amekunja uso Kiufupi no shobo. 

Tukiwa tunaendelea kumtazama aligeuka kututazama akashaa watu wote macho kwake ndipo akavua headfone moja na kutuuliza: kuna nini? 

Wote Tulianza kujing'ata ng'ata kwa aibu ndipo Zakayo akaamua aseme: Mimi naitwa Zakayo sijui mwenzangu? 

Mjeda Yule alitabasamu na kusema: Dominic. 

Wote wakarudilia Jina lake: aaahhh Dominic! 

Ndo mimi na Latina tukajuwa Kumbe ni Dominic, tuliangaliana kisha tukatabasamu.

Professor mwingine Kidogo Yeye umri wake ulikuwa umeenda alikuja na dereva kisha akasema kwa sauti ya: let's go! time's money (twendeni muda ni pesa)

Watu walianza kuingia Ila Derick macho kwangu.

Safari ikaanza njiani story za hapa na pale Ila Zakayo na Patrick walikuwa wacheshi sana tulijikuta kwenye safari yetu Hakuna upweke.

Baada ya siku kadhaa Tulifika kwenye msitu ule kupitia usafiri wa boti, ukweli msitu wa equatorial ni msitu unasifika kwa baridi mno, unaambiwa Mvua inanyesha Miezi yote 12, ukweli tulijipanga na Makoti ya kutosha. 

kila mmoja alianza kupiga picha kupitia simu Wengine camera zao, masaa ma nne kupita tulishuka kwenye boti tukaanza kutembea kwa mguu, sikutaka kabisa Mazowea na Derick maana Yeye alitamani tuongee hata kwa dakika mbili Ila Mimi habari hio sikuitaka, Tuliendelea kusonga Mpaka watu Wakaanza kuchoka, Kidogo Mtandao ukakata ndipo professor Rodrigo akasema: Jambo la Kawaida Sana hilo wala msiwe na wasi wasi. 

Zakayo: bado njia ya kunirudisha nilikotoka naikumbuka vizuri. 

Tulicheka sote ndipo Sofia akasema: Ki Zakayo kinaogopa.

Hamisa: walitudanganya eti Mvua haikati huku. 

Patrick: subiri bado hatujazama ndani ya msitu vizuri vizuri. 

Upande wangu Latina alinipa begi yake nimsaidie maana alikuwa amechoka ndipo tukazidi kusonga, nikiwa nipo nyuma ya wote kutokana na mzigo nilijishika kwenye magoti huku nikipumua kwa kasi, ghafla nilishangaa kuona chupa ya mji mbele yangu ndipo nikageuka kuangalia atakuwa Nani kanipatia aisee alikuwa ni Derick, nilishusha macho taratibu kisha nikainua mgongo ili Kutaka kuondoka, Derick akaniambia: maji haya yatakusaidia maana yanaongeza nguvu. 

Nikamuuliza: Kwanini sasa umenipa Mimi? 

Derick: come on Najma! 

Amanda akiwa mbele alishangaa kutuona ndipo akarudi nyuma, alipotufikia alimshika mkono Derick na kusema: wanatuacha Wengine. 

Derick alitabasamu na kuniambia: wahi twende. 

Wao wakaendelea Mimi nikabaki nawatazama tu huku nikijipumzisha ukweli nilikuwa nimechoka sana, juu ya mti niliona kandege kazuri kenye malangi ya njano na mekundu aisee ndege hizo ni adimu sana kuziona kule kwetu Mara nyingi zinapatikana Sana kwenye msitu Huo wa Equatorial, nilichomoa simu nikaanza kukapiga picha huku nikiendelea kukafurahia kanavyotikisa mabawa yake.

 nikiwa nipo hapo sikuweza kuwaona wenzangu tena kama walikata njia nyingine au Waliendelea mbele sikuwaona tena, Kidogo Hofu ikanitawala Nikaona Acha niwafuate Kama nikupumzika nimepumzika vya kutosha, kabla sijapiga hatua aisee huwezi kuamini niliskia mgh'urumo mkubwa ulionifanya nipigwe gazi mwilini nikajikuta Natamani kujuwa nikipi kipo nyuma yangu, taratibu niligeuka huwezi kuamini nili........ 


Unahisi nini kitatokea! 
Usikose mkasa huu!


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: