SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)
MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 05
TULIPOISHIA: nikiwa nipo hapo sikuweza kuwaona wenzangu tena kama walikata njia nyingine au Waliendelea mbele sikuwaona tena, Kidogo Hofu ikanitawala Nikaona Acha niwafuate Kama nikupumzika nimepumzika vya kutosha, kabla sijapiga hatua aisee huwezi kuamini niliskia mgh'urumo mkubwa ulionifanya nipigwe gazi mwilini nikajikuta Natamani kujuwa nikipi kipo nyuma yangu, taratibu niligeuka huwezi kuamini nili........
SONGA NAYO!
taratibu niligeuka huwezi kuamini nilichokiona mbele yangu kilipita kama radi Mfano wake ulikuwa Kama fuvu ya mtu aliekufa muda mrefu, Hofu iliongezeka kupumua nikashindwa nilivyopiga kelele hata sikujuwa nilishtukia nimeguswa begani, nilipogeuka kutazama Sikuamini kumuona Dominic (mjeda) ndie Kaja Baada ya kuskia kelele zangu, kwa dakika mbili niligeuka kichaa bila kujielewa Nilimkumbatia Dominic kwa nguvu huku nikihema vibaya mno mpaka Dominic mwenyewe akashangaa, muda Huo Derick nae alifika maana waliposkia sauti yangu walikuja wanakimbia wakiwa wawili, ile Hali ya mimi kukumbatiwa na Dominic aisee Derick aliumia mno ila hakuwa na chaguo akasogea mpaka pale tulipo, Dominic akaniuliza: kuna nini Najma?
Sikumjibu bali nilimshikilia kwa nguvu, Dominic alimtazama Derick kisha akasema: anaonekana ana hofu nyingi.
Derick alisogea karibu na kichwa changu kisha akaniuliza: Najma it's me Derick, what's problem do you've?
Niliinua kichwa taratibu nikamtazama huku Jasho usoni Ikiwa inazidi kutiririka.
Derick: kuna nini?
Nilimuachia Dominic wala sikutaka kumuambia mtu yeyote kwa kile nilichokiona nilianza kusonga mbele bila kuangalia nyuma, Dominic alisema kwa sauti ya Chini: Labda ana Matatizo.
Derick: nahisi.
Tulipowafikia wenzetu walikuwa wametusubiri kwa hamu, wa kwanza kuja kuniuliza hali yangu alikuwa ni mdogo wangu Latina ila sikuweza kumjibu chochote, wote walitaka kujuwa nikipi kimenisibu Ila niliona iwe Siri yangu tu.
Professor mkuu akasema: jamani tuendelee na safari kuhusu Najma msaidieni hio mizigo Labda atakuwa amechoka.
Walichukuwa Yale mabegi kisha mdogo mdogo Wakaanza kusonga mbele, moyo ulinisunta Nikaona kama ntakaa kimya tukazidi kusonga mbele na tatizo nimeliona Hali ya kwamba tukirudi nyuma Hakuna umbali mkubwa maana tulikuwa bado hatujazama katikati ya msitu vizuri, inaweza kuleta balaa kwangu ndipo nikajikakamua na kusema: msubiri kwanza.
Walisimama ili kunisikiliza, nilipiga hatua kadhaa nikawafikia kisha nikasema: jamani hapa tupo hatarini.
Waliendelea kunitazama ndipo Dominic akaniuliza: una maana gani?
Nikamjibu: nilipokuwa pale Napiga picha ndege flani niliskia sauti yenye kishindo ambacho toka nizaliwe sikuwahi kuskia...
Wote walitamani kujuwa nikipi nilichokiona ndipo nikaendelea kusema: huwezi kuamini nilipogeuka kwa macho yangu mawili wala sio story Hapana hii ni true mwenyewe nimeona fuvu imesimama ghafla ikapotea.
Wote kwa Pamoja waliachia kicheko cha Utani ndipo professor mkuu akasema: sio vizuri Najma kuunda mastory story ya ajabu tukiwa tupo eneo hili.
Nikasema: wallah naapa turudi nyuma kabla ya Matatizo hayajatukuta.
Yule mkongo alietuleta akasema kwa kiswahili chao: usiseme hivo Jolie niko mukukwambia huku kwa hii poli hio mambo ya namna hio haikuwake kabisa mie Nilizani uko mkuzungumzia ma Leopard, ma Antilope, ma Lion Kumbe bitu namna hio vraiment hii poli yetu Iko bien Sana.
Wote walimuamini mawazo yangu wakayapinga ndipo Zakayo akamuuliza kwa kuigizia kiswahili cha kongo: papa eti Jolie Ndo nini?
Akamjibu: Jolie ni mutoto muzuri sana.
Zakayo alinisogelea na kusema: si umeskia mpaka amekusifia embu Achana na hayo mawazo yakutishana atakupa zahabu Huyu Jamaa.
Wote walicheka kisha tukaendelea na safari.
Baada ya siku nne bado tu tunafuata ile lamani tuliopewa iliopo kwenye kikaratasi Kikubwa, Majira ya saa moja tulikaa sehemu tukatafuta kuni tukawasha kisha story zikaanza wakulala wakalala maana mchoko ulikuwa sio wa Kawaida ni ile kupenda pesa tu, nikiwa nipo na mdogo wangu Latina nilimwambia: kwa Yale niliyokwambia bado huwezi kuniamini?
Latina: I'm sorry kweli Sikuamini ila dada unampa wakati mgumu Sana mwenzio embu angalia anavyohangaika kila mara anakuangalia mpaka watu wengine wameanza kugundua.
Nikamuuliza: nani?
Latina: Derick jamani.
Nikamjibu: Yeye si ana mtu wake.
Latina nilipomuambia hivo alinyanyuka akamfuata Derick alipokaa alipomfikia akamnong'oneza: samahani Dada anakuita.
Derick hakuamini alinyanyuka kisha akanifuata nilishangaa kuona anakuja Ila sikujuwa nikipi ameongea na Latina, Derick aliponifikia alikaa pembeni yangu kisha akaniuliza: umeniita?
Watu wote macho kwetu mpaka mwenyewe aibu ndipo Nikamuuliza: nani kakwambia?
Derick: moyo wangu Ndo umeniambia Ila Najma Kwanini unanifanyia hivi?
Nikamjibu: Mimi na wewe Hatuna mahusiano yoyote.
Baada ya Derick kunitazama shingoni na kuona ile cheni alionipa nimeivaa aliniuliza: Kumbe bado unanikumbuka?
Nilipoona ameiona niliishusha Mtandio wangu kisha nikasema: sio yenyewe.
Derick: kosa langu silijui nilitaka siku ile tukae tujadiri namna ya kumtoa baba ila sasa wewe ukakataa angalia tumekuja huku na Yeye bado yupo jela.
Nikamjibu: ulitaka iwe kama siku zote?
Derick: una maana gani?
Nikamuuliza: hata wewe huniamini kwa kile nilichowaambia Muda ule?
Derick: Achana na hizo story.
Usiku Sana Kama saa Sita hivi Usingizi uliniishia nikaamka Baada ya kukumbuka ile fuvu nilioiona jana, nilipoangalia pembeni nilishangaa kumuona Derick kalala karibu yangu bila kujifunika chochote na baridi muda Huo ilikuwa inampiga, nilipojiangalia Mimi nilishangaa kuona nimefunikwa shuka ya kimasai ndo nikajuwa Derick alinifunika Mimi ndo maana anapigwa na baridi, niligeuka kumtazama usoni nikatabasamu na kujisemea moyoni: Nina Hofu sana Derick.
Nilichukuwa kile kimasai nikamfunika vizuri kisha nikakaa huku nikiangalia Mazingira, muda Huo Joseph kijana Aliekuwa mpole kuliko wote alikuwa amekaa huku akiwa anaangalia movie kwenye simu yake pia amevaa headfone maskioni, nilipoona nimepata kampani Nilisogea pale alipo kisha Nikamuuliza: tunaweza kuangalia wote?
Joseph alishtuka kisha akatoa headfone na kuniuliza: bado haujalala?
Nilikaa karibu yake kisha nikasema: Usingizi Hamna.
Joseph: nikweli unajuwa Mimi Sina imani kama tutapata kile tunachokihitaji?
Nikamjibu: yawezekana tukapata.
Tuliendelea kupiga story mpaka tukazoweana Haina Mfano, ukweli upole wa Joseph niliufurshia sana, tukiwa tunaendelea kupiga story Derick aliamka ile kuangalia mbele akatuona mimi na Joseph tukiwa tume share headfone moja huku tukiangalia movie na furaha tuliokuwa nayo Ilikuwa sio ya Kawaida mpaka Derick moyo wake ukaanza kumuuma.
Asubuhi ilipowadia watu Waliendelea kujipumzisha Ila professor Rodrigo alichukuwa begi lake na kusema: mchaka mchaka Unaanza.
Tulianza kuamka taratibu.
Baada ya muda tukiwa tupo njiani tulishtuka kuona kitoto cha simba Kidogo kikipita mbele yetu Nyoyo zilitutoka zakayo kwa uoga akasema: kama mmemuona mtoto wa simba basi kaeni mkijuwa simba yupo karibu, let's go.
Tulianza mbio kama tumewekewa betri kwenye miguu, tulipofika mbele Kidogo tulijipumzisha wakulaani Wakaanza kulaani ndipo professor akasema: Kwani mlijuwa huu msitu hauna wanyama wakali wakali?
Abdul: aisee nilivyokuja huku sikuagana vizuri Na mpenzi Wangu mjuwe.
Patrick: na Mimi na mama yangu.
Dominic alitabasamu na kusema: tupumzike kwanza mengine tutayajuwa kesho.
Tulikaa Amanda akiwa yupo karibu na Derick akamuuliza: wewe specialist mkubwa wa nchi uliruhusiwa vipi kuja huku?
Derick alishangaa na kumuuliza: Kumbe unanifahamu?
Amanda: Hakuna mwana science asiekufahamu wewe.
Derick alicheka kwa furaha kisha akasema: kumbe! Nashukuru.
Mimi nikiwa na Latina tulikuwa tunawatazama wanavyocheka ndipo Latina akasema: Derick nae anaboa!
Nikamjibu: ndo alivyo hivyo.
Upande wa professor Rodrigo pamoja na mpenzi wake Joyce walikuwa zao pembeni huku wakijipiga selfie taratibu.
Mjeda Dominic alikuwa zake pembeni ametulia, akiwa yupo hapo akakumbuka nilivyomkumbatia siku ile alipogeuka kunitazama kwa bahati mbaya muda Huo na Sisi tulikuwa tunamuangalia Nikajikuta nimegonganisha nae macho bila kutarajia aisee Nilipigwa shoti ya umeme machoni nikaamua kushusha macho taratibu.
Tukiwa tupo hapo tulishtuka kuona, Zakayo na Abdul Pamoja na Patrick wanakuja wanakimbia kwa kasi, ile Hali ya wao kuja wanapiga kelele nikaunganisha ile fuvu nilioiona siku ile aisee nilivomshika mkono Latina na kuanza kukimbia nae sikujuwa, watu hapo kutokana na ile yao ya kutokuamini kila kitu Waliendelea kuwatazama kwa mshangao, Patrick aliwapita moja kwa moja bila kusimama Ila Zakayo na Abdul walisimama wakiwaomba wale waliokaa wanyanyuke wakimbie, wakiwa bado wanajilemba lemba mara Wengine viatu vyangu, wengine simu yangu, Wengine begi yangu Ipo wapi huwezi kuamini jeshi la sokwe wenye miili mikubwa mikubwa Kama ishirini hivi ilitia timu, aisee wenzetu ile kushangaa shangaa waliwekwa Kati wote nikimaanisha walizungukwa na sokwe wale.
Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu!
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO


No comments: