SIMULIZI: HOUSE GIRL WA KITANGA 23
SIMULIZI: HOUSE GIRL WA KITANGA
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA
SEHEMU 23
ILIPOISHIA
Maneno yale ya Fadhili yaliufanya mwili wangu usisimke utafikiri sijui nilikuwa nimemwagiwa kitu gani. Nikamtazama machoni kwa umakini zaidi kuona kama kile alichokuwa anakizungumza hakikuwa na masihara.
“Kwani tatizo liko wapi?” nikahoji kwa umakini.
“Tatizo lipo Tumu!” alizungumza huku akitafuta kipande cha mkate.
“Niambie sasa, tatizo ni nini?” nikaendelea kuhoji.
“Tatizo mimi sikuelewi Mwantumu”
“Kivipi?”
“Kwanini Imran akinikuta na wewe ananimaindi?” Fadhili akahoji.
“Kwa kweli hata mimi sielewi”
“Basi mimi nafikiri jamaa ameshakula zigo” alizungumza Fadhili huku akiachia tabasamu na macho yake akinitazama kwa kuniiba.
“Hakuna bwana Fadhili, mimi humu ndani sitakuja kutembea na mwanaume yeyote yule na nimeapa hivyo” nikazungumza kwa msisitizo.
“Mnh hata mimi?” Fadhili akahoji kwa mtego.
“Sijui labda wewe…lakini sijui kama itawezekana pia” nilijikuta nikizungumza kwa kigugumizi. Nilishindwa kumpa jibu la kuwezekana kwasababu tayari nilikwisha amua kuwa na Endrus peke yake.
“Kwanini isiwezekane, au ndio hunipendi siku hizi” Fadhili akazungumza kwa sauti ndogo lakini iliyokuwa ikikoroma kama redio mbovu.
ENDELEA…
“Mbona mimi nimeshawahi kukuambia kama nakupenda, wewe tu ndo umenikataa” nikazungumza kwa sauti ya kudeka.
“Kwahiyo vipi bado unanipenda au?” Fadhili alihoji huku akifuta mikono yake kwa kipande cha tishu.
“Mi sijui, we mwenyewe mkali huko” nikazungumza huku nikichukua vyombo vichafu alivyokuwa ametumia Fadhili.
“Sio hivyo Mwantumu, unajua mambo mengine yanakera sana!” Fadhili alizungumza huku akijiinua kutoka kwenye kiti.
“Mambo gani?” nikahoji kwa sauti ya kubana.
“Ngoja niende, leo nitarudi mapema nije tuyajenge” Fadhili alizungumza huku akivuta hatua kuondoka.
“Fadhili..” nikaita kwa sauti ya wasiwasi.
“Enhe..” akaitika na kugeuka kunitazama kwa makini.
“Kuna kitu nataka nikuombe” nikazungumza kwa ile sauti yangu ya mashaka.
“Nakusikiliza endelea, au unataka twende wote kazini?” Fadhili akazungumza kwa masihara.
“Sijui utanikubalia lakini” nikazungumza huku nikijiuma uma vidole na kuzunguusha miguu safafuni.
“Ndio uongee sasa”
“Unajua kukaa ndani pekeyangu kunachosha sana” nikazungumza kwa mtego.
“Umeshaanza hivyo, haya kajiandae basi twende wote dukani kwangu” alizungumza Fadhili.
“Sio hivyo Fadhili bwana”
“Kumbe unatakaje, au nisiende kazidi tubaki wote wawili hapa ndani” Fadhili aliendelea kuhoji kwa masihara yake.
“Sina maana hiyo bwana Fadhili”
“Haya ongea basi”
“Naomba nikimaliza kazi za hapa ndani niende nikajichangamshe kule kwa dada Bupe” nikaeleza.
“Dah! Tumu mdogo wangu, hivi unamjua Bupe vizuri?” Fadhili akazungumza kwa mashaka.
“Nitakuwa makini Fadhili, hakika hatothubutu kunifanyia kitu kibaya” nikaeleza kwa upole na sauti ya kubembeleza.
“Unaniachaje?”
“Abee..”
“Unaniachaje ili nikuruhusu?” Fadhili akazungumza kwa masihara.
“Nitakuapa chochote kile utakachokitaka” nikaeleza.
“Mnh! Je nikitaka nini…?
“Nini ndio nini?” nikahoji huku nikiachia tabasamu la mahaba.
“Sawa nenda lakini uwe makini kwelikweli” Fadhili alizungumza kwa msisitizo.
“Kweli Kaka Fadhili?” nikazungumza kwa furaha huku nikiwa siamini kwa kile ambacho kilikuwa kimezungumzwa na Fadhili.
“Nawewe hadi uwe na shida ndio unaniita kaka, mbona siku zote unaniita jinalangu” Fadhili alizungumza kwa yale masihara yake.
“Basi kuanzia leo nitakuwa nakuita kaka” nikazungumza kwa sauti ya kujidekeza.
“Lakini sikia nikwambie kitu” Fadhili alizungumza kwa sauti ndogo lakini iliyokuwa na msisitizo.
“Enhe….?”
“Nenda lakini naomba utambue kuwa mimi ninawivu kuliko unavyonifahamu” Mnh jamani nyie Fadhili alizungumza maneno ambayo yaliniweka njia panda. Siku zote nilikuwa nafahamu Fadhi hanipendi na alikuwa amenichukia, sasa cha kuniambi heti anawivu ni kipi? Au alikuwa anamaana gani? Sasa kama alikuwa anamaanisha ya kunionea wivu mimi ingekuwaje maana tayari nilikuwa nimekwisha ukabidhi moyo wangu kwa Endrus.
“Mnh Fadhili wewe!” ikabidi nijichekeshe chekeshe.
“Haya msalimie Bupe” Fadhili alizungumza huku akianza kuondoka na kuniacha nimesimama.
“Nimwambiaje?” nikazungumza kwa bashasha baada ya kuruhusiwa kwenda kwa dada Bupe.
“Mwambie simpendi” Fadhili akazungumza na kuondoka akiniacha pale mezani nikipaweka sawa kwaajili ya watu wengine kupata kifungua kinywa.
Mazungumzo baina yangu na Fadhili yalikuwa yamenifurahisha sana siku hiyo. Sikuweza kuamini kama siku hiyo ningeweza kukutana kwa mara nyingine na mpenzi wangu Endrus. Nampenda jamani mwanaume yule mnh! Niacheni tu nideke.
Nikiwa naendelea na maandalizi yale pale mezani alifika kaka Imran na kuketi kwenye kile kiti ambacho alikuwa amekikalia Fadhili.
“Jamani mtoto mzuri upo?” Kaka Imran alizungumza huku akinitazama usoni.
“Shikamoo kaka Imran”
“Mahaba!” kaka Imrani akaitika kwa utani.
“Mahaba ndio nini sasa?” nikahoji huku nikiwa nimevaa lile tabasamu langu la siku zote.
“We si umeniamkia, nami nimeitika mahaba” Alizungumza kaka Imran.
“Kwahiyo sio marahaba bali ni Mahaba?”
“Kwani wasambaa kule kwenu wanaitikiaje? Si mahaba”
“Mnh haya bwana”
“Njoo basi uninawishe” kaka Imran alizungumza huku akinikodolea macho.
Nilisogea na kuinua jagi la maji na kuanza kumnawisha mikono kaka Imran.
“Nisugue basi mbona unaniachia mwenyewe” kaka Imrani alizungumza.
“Mnh jamani…” nilizungumza na kuingiza mikono yangu kwenye bakuli na kuanza kusugua mikono ya kaka Imran taratibu huku nikimtupia jicho la wizi usoni. Nakwambia mtoto wa kiume alikuwa kama vile ananawishwa kwa maji ya tindikali kwa jinsi alivyokuwa akisisimka mwili.
“Jamani Tumu una mikono mitamu kiasi hiki?” Alizungumza kaka Imran nilipokuwa nikimsugua mikono.
“Kaka Imran muongo, mitamu kwani umeila?” nilizungumza huku nikimsugua kidole cha kati.
“Unafikiri utamu hadi uonje kwa mdomo?”
“Sasa utajuaje bila kuonja?”
“Hata macho yanatosha kuonja na kukufanya uhisi utamu au uchahu”
“Mnh kaka Imran wewe” nikajizungumzisha huku nikimalizia kumnawisha mikono mwanaume yule aliyekuwa amejaa vituko na matendo magumu.
Nilipokuwa namalizia kumnawisha mikono, tulishituliwa na sauti ya mtu mwingine akitusemesha.
“Jamani hayo nayo yameanza lini?” ilikuwa ni auti ya mama ambaye alikuwa akitokea chumbani kwake akielekea pale dining room kwaajili ya kujipatia chochote kabla ya kwenda kazini.
“Karibu mama” Fadhili alizungumza kwa kujishebedua mara baada ya kubaini mama alikuwa ameshuhudia kitendo kile.
“Huo ubwenyenye wa kuoshwa mikono umeanza lini?” mama alihoji huku akivuta kiti na kuketi.
“Aah mama bwana, mbona kawaida tu” kaka Imran alizungumza kwa kujiamini.
“Kawaida kumtesa mtoto wa watu awaoshe hadi mikono, mbona ni mambo ya kikoloni hayo” mama alizungumza huku akiweka sukari kwenye kikombe chake cha chai.
“Sio utumwa mama, haya yanaitwa MAHABATI” alizungumza kaka Imran maneno ambayo hayakuwa yameninogea hata kidogo.
“Mahabati ya kitanga ndio haya?” mama alihoji huku akiamini kaka Imran alikuwa akizungumza kwa masihara kumbe mwenzake alikuwa anamaanisha.
“Nakwambia hata maji ya kuoga yatiwa hiliki ati” alizungumza kaka Imran huku akiiga lafunzi yangu ya kitanga na kumfanya mama kuangua kicheko huku akinitazama kwa macho ya uchokozi.
“Heti Tumu ni ya kweli hayo?” mama alihoji huku akinitazama na kuniachia tabasamu.
“Sijui…” nikazungumza huku nimeziba uso wangu kwa viganja vya mkono kwa aibu.
“Mama mimi naoa huyu mtoto” alizungumza kaka Imran na kuuma kipande cha mkate.
“Mwantumu hawezi kukubali kuolewa na mwanaume ana gubu utafikiri kitu gani” alizungumza mama.
“Hamna mama, mimi sina gubu. Hata Tumu mwenyewe anaelewa, muuleze” alizungumza Kaka Imran kwa kujiamini.
“Heti Tumu utakubali kuolewa na Imran?” alihoji mama kwa utani.
Mama alihoji huku akiamini mazungumzo yale yalikuwa ni ya masihara masikini ya Mungu. Hata hivyo kabla ya kutoa jibu la swali lile kulisikika mtu mwingine akinijibia swali alilokuwa ameuliza mama.
“Wala hakuna atakaye olewa hapo” ilikuwa ni sauti ya baba mzee Sekiza akizungumza akiwa anatokea chumbani kuelekea pale mezani kwaajili ya kifungua kinywa.
“Mnh disco limeingia Mmasai” kaka Imran akazungumza kwa sauti ya chini.
“Enhe hebu niambieni ni nani anayetaka kumuoa Tumu?” alihoji baba huku akijiweka kwenye kiti.
“Mwanao naona amekufa ameoza kwa binti wa kitanga” mama aliendelea kuchombeza akiamini yote yale yalikuwa ni masihara ya wanafamilia.
“Nani huyo?”
“Si huyo Imran”
“Pumbavu, hebu wacheni upuuzi wenu!” baba akazungumza kwa sauti ya kukoroma.
“He mwenzetu kwani vipi?” mama akahoji kwa mshangao baada ya kuona mume wake akikasirika kwa vitu visivyo na msingi.
“Mama acha!” kaka Imran akazungumza kwa sauti ya chini baada ya kubaini mazungumzo yale hayakuwa yamemnogea baba.
“Makubwa basi” mama alizungumza kwa mshangao huku akiwa haelewi kilichokuwa kinaendelea kichwani mwa baba.
“Mmejiachia wenyewe mnazungumza masuala ya kuolewa kwa mtoto mdogo hamuoni hata aibu” baba aliwachana live kaka Imran na mama yeke.
Mama alitaka kuzungumza kitu lakini kaka Imran akamkanyaga mguuni kumzuia asizungume neno lolote.
“Haya bwana, na yaishe” alizungumza mama huku akiosha mikono yake na mdomoni akimalizia kutafuna.
“Sitaki kusikia tena ujinga ujinga wenu” alizungumza baba kwa sura ya ukauzu.
Mama alitazamana na Kaka Imran na kupeana ishara ya kuondoka. Wote kwa pamoja walianza kuondoka wakituacha mimi na baba.
“Haya kwaherini” mama alizungumza wakati wanatoka na kaka Imran.
“Na muende moja kwa moja wala msirudi tena” alizungumza baba kwa msisitizo kuashiria alikuwa amekasirishwa na yale mazungumzo ya Mama na kaka Imran.
Baba alinitazana na kuangua kicheko kwa sauti ambacho sikuelewa kilikuwa kimetokea wapi.
“Nimewakomesha!” baba akazungumza huku akipeleka kikombe kinywani na kupiga funda la chai.
Mara zote nilikuwa nakwepa sana kukaa na baba tukiwa wawili tu kutokana na vitendo vyake alivyokuwa akiniletea mara tu anapopata fursa kama hiyo. Wakati mama na kaka Imran walipokuwa wakiondoka na mimi nikawa navuta miguu taratiibu kumuacha baba pekeyake mezani.
“Wewe unakwenda wapi?” baba alihoji baada ya kubaini nilikuwa nataka kumtoroka.
Niliposikia vile nikajikuta nguvu zikiniishia na kugeuka kumtazama baba kwa macho makavu yaliyokuwa yamekosa nuru ya amani.
“Vipi ndio unakwenda kuleta mwiko nini?” baba akahojikwa masihara.
“Nilikuwa naenda kuwafungulia geti wakina mama” nikajieleza.
“Wachana na mageti watafungua wenyewe” Baba alizungumza huku akisogeza kiti nikae pembeni yake.
“Lakini baba…” nilitaka kujitetea.
“Lakini nini au unataka kuleta habari zako za kufukuzana na miko” baba alizungumza huku akiendelea kukata kipande cha mkate na kukituma mdomoni.
Nilivuta pumzi na kuziachia kwa nguvu, sikuelewa mzee yule nimfanye nini ili asiendelee na mpango wake wa kunitaka kimapenzi. Mbonamimi nilikuwa kama mtoto wake tu ndani mle? Wazee wengine wa mjini sijui wapoje?
“Unaogopa nini njoo ukae, leo hakuna cha mwiko wala mashetani lazima kieleweke” baba akazungumza kwa msisitizo baada ya kuniona sikuwa na mpango wa kumpa ushirikiano.
“Lakini baba unachelewa kazini” nikajibaraguza mtoto wa kike baada ya kuona maji yalikuwa yanaelekea kunifika shingoni.
“Nimekwambia hakuna cha kazini leo, lazima utamu tupeane” alizungumza baba kwa msisitizo pasipo kunitazama usoni.
Mtoto wa kike nikahisi siku hiyo nilikuwa nimepatikana. Nilipomtazama usoni mzee yule nikabaini alichokuwa anakizungumza hakikuwa na masihara. Sikuwa na namna nyingine maana mbinu zote zilikuwa nimemaliza. Ikabidi mtoto wa kike nijilainishe mwenyewe kwa baba.
“Baba…” nikaita huku nikiketi kwenye kile kiti kilichokuwa jirani yake.
“Enhe nakusikiliza”
“Mbona ule mshahara wangu haujanipa?” nikahoji huku sauti nimeilegeza mtoto wa kike na macho nimerembua kimahaba utafikiri nilikuwa na mpenzi wangu Endru kumbe nilikuwa na Mzee Sekiza.
“Sasa ningekupaje wakati kila nikitaka kukupatia unanisumbua, tena hadi tunapigana miko ya kugeuzia mbona” alizungumza baba baada ya kuniona nimelainika mrembo wa kitanga.
“Basi nipe leo…” nikazungumza kwa kudeka huku nikiegemeza kichwa changu kwenye bega la baba.
Huhuuu! nakwambia baba alijisikia kama vile alikuwa peponi. Hakutegemea kama kitoto kisirani kama mimi ningeweza kujibebisha kwake kiasi kile. Nikapeleka mkono wangu wa kusho kifuani kwake na kuanza kumpapasa taratiibu.
“Tu..tu..tumu” baba aliniita kwa sauti ya kukatakata kama vile ana kigugumizi.
“Abee..” nikitika kwa ile sauti yangu ya kudeka.
“Nimekwambia nitakulipa kiasi gani vile kwa mwezi?” baba akahoji kwa sauti nzito huku akizunguusha mkono wake wa kushoto kwenye mabega yangu.
“Si ulisema unaniongezea Laki moja kila mwezi jamani baba umesahau?” Nikazungumza kwa kudeka huku nikijiweka vizuri pale kifuani kwa baba. Masiki ya Mungu mzee wa watu alizidi kuchanganyikiwa na toto la kitanga.
“Hapana Tumu umekosea” baba akazungumza kwa sauti ya kukoroma.
“Kumbe uliniambia kiasi gani?” nikahoji huku nikimtazama usoni na kupeleka mikono yangu kwenye kidevu hake na kuchezea ndevu za baba yule.
“Mimi nilikwambia nitakuongezea laki tatu kila mwezi” baba alizungumza kwa kunibembeleza huku akiutoa mkono wake kwenye mabega na kuuweka juu ya paja langu la mguu wa kulia.
Itaendelea
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: