Simulizi: KAHABA (01)
Simulizi: KAHABA (01)
“Hivi baba Careen, unajua mimi sikuelewi kabisa siku hizi?”.
“Kwa nini hunielewi?”. Nilimjibu mama Careen.
“Eti eeeeh! Unajifanya huelewi”. Mama Careen aliongea huku sasa akiwa amekishika kiuno chake kwa mikono yote na kunitolea macho pima.
“Hapana naelewa”. Nilijibu kwa kifupi.
“Unaelewa nini?”. Mama Careen alibandika swali jingine.
“Ninaelewa kwamba hunielewi siku hizi?”. Nilimjibu kwa nyodo.
“Haya bwana, wewe jifanye una misemo kama waswahili wa pwani”. Mama Careen alinichambua kama mchele.
“We mwanamke hebu acha kuniharibia siku. Yaani ndiyo kwanza kunakucha lakini ushaanza kuupepeta mdomo pe pe pe peeee! Mithili ya chiriku”. Nami nilimzodoa mama Careen kwa maneno ya dharau na kashifa.
“Sawa bwana mshindi wewe. Lakini mi nakwambia mbio za sakafuni huishia ukingoni”. Mama Careen aliniasa.
“Acha maneno yako bwana. Hayo ni maneno ya kuku tu wala hayamtishi mwewe”. Nilimjibu mke wangu kwa dharau huku sasa mikono nikiwa nimeiweka mfukoni na mguu mmoja nikiusugua chini.
Mama Careen hakujibu kitu bali alimnyanyua Careen ambaye alikuwa hajui ambacho kilikuwa kinaendelea kwa wakati ule kutokana na umri wake na kuelekea ndani chumbani.
Mimi nikampuuza mwanamke huyu ambaye niko naye katika ndoa mwaka wa kumi sasa. Nilimwona ni mwanamke wa kawaida ambaye hakuwa na jipya zaidi ya maneno mengi mithili ya chiriku kila uchao.
Nilitoka nje ya sebule na kuanza kufanya utaratibu wa kuelekea kazini. Mwanamke huyu kwa kweli alikuwa amenichafua kabisa asubuhi hii ya leo. Roho yangu ilikuwa nyeusi na sikuelewa nitaimalizaje siku.
Nilitamani nighailishe kuelekea kazini lakini nikaona huo utakuwa si uamuzi wa busara hata kidogo. Haikutakiwa mafarakano ya nyumbani yaharibu utaratibu mzima wa kazi. Nilijua namna nzuri ya kumdhibiti mwanamke huyu.
****************
Ilikuwa ni majira ya jioni wakati mimi nikitoka kazini kuelekea nyumbani kwangu. Nilikuwa sipendi kabisa kurejea nyumbani kutokana na maneno ya kero ya mke wangu. Ndiyo kwangu mimi yalikuwa ni maneno ya kero ingawa ilikuwa ni haki yake kuongea kutokana na kusikia tetesi za kwamba nilikuwa nikitoka nje ya ndoa.
“Unajua Juma mimi nina tatizo moja kubwa sana ambalo linanikera sana”. Nilimwambia Juma rafiki yangu ambaye tulikuwa tukifanya kazi katika ofisi moja.
“Tatizo gani bwana Mayanja?”. Juma aliniuliza huku akinitazama usoni na wakati huohuo tukitembea kuelekea majumbani kwetu.
“Unajua huyu shemeji yako amekuwa kero sana siku hizi”. Nilimweleza bwana Juma.
“Ki vipi bwana Mayanja?”. Aliniuliza bwana Juma.
“Yaani siku hizi amekuwa akiupepeta mdomo kama wale wanawake wa uswahilini. Yaani yeye muda wote ni manenomaneno tu”. Nilimwambia Juma huku uso wangu nikiwa nimeukunja.
“Ha ha ha ha ha haaaaaaaa!”. Juma aliangua kicheko kikubwa sana kitendo ambacho kilinishangaza sana.
“Yaani Juma, mimi nina matatizo makubwa nyumbani kwangu halafu wewe unanicheka. Ina maana unanidharau?”. Nilimwuliza Juma kwa ghadhabu sana.
“Siyo kwamba nakudharau rafiki yangu ila unanifurahisha sana Mayanja”. Juma aliongea.
“Sasa ni nini ambacho kinakufurahisha hapa?”. Nilimwuliza Juma huku nikiwa dhahiri nimeghadhibika.
“Mwanamke hawezi kukusumbua hata kidogo. Mwanamke hatakiwi kukuendesha hata siku moja bwana Mayanja”. Juma aliongea.
“Lakini yule ni mke wangu Juma”. Niliongea.
“Hata kama! Unatakiwa utende kiume!”. Juma aliongea huku akinipigapiga mgongoni.
“Sasa nifanyaje Juma?”. Nilimwuliza Juma.
“Sasa hilo ndilo swali bwana Mayanja”. Juma aliongea huku akiniangalia usoni.
“Ndiyo unijibu haraka sasa, maana mimi nimechoka kabisa”. Nilimwambia bwana Juma nikiwa nina munkari wa kutaka kujua suluhu ya tatizo hili ambalo lilikuwa likinikabili.
“Tulia bwana Mayanja, mambo yako yatakuwa safi kabisa”. Juma aliendelea kunipooza moyo wangu ambao kwa sasa ulikuwa ukichemka sana.
“Kwa hiyo tunafanyaje sasa rafiki yangu?”. Nilimwuliza bwana Juma.
“Mwanamke hatakiwi kukuendesha hata kidogo. Jambo la kufanya ni wewe kwenda kuondoa stress”. Juma aliongea.
“Sasa hizo stress nitaziondoa wapi na nitaziondoa vipi”. Nilimwuliza bwana Juma kwani maelezo yake sikuyaelewa hata
kidogo na yalizidi kunichanganya.
“Wewe subiri wala usiwe na mchecheto. Mimi ndiye kamanda wako katika hili na nitakuelekeza kila kitu na mambo yako yatakuwa fresh kabisa.
Maongezi yetu yalitupeleka mpaka kituo cha daladala. Tulipanda ndani ya daladala ambayo ilitupeleka mpaka katika mtaa wa Mbazi ambako ndiko yalikuwa makazi ya bwana Juma.
Juma alinikaribisha katika nyumba anayoishi kisha yeye akaingia chumbani. Sikufahamu alienda kufanya nini kule chumbani lakini baada ya muda wa kama sekunde thelathini alirejea pale sebuleni. Alinikuta nikiwa nimejipumzisha katika sofa mojawapo pale sebuleni. Naye akaketi katika sofa mkabala na mimi.
“Bwana Mayanja, kama nilivyokueleza hapo awali, ni kwamba tatizo lako leo litakwisha kabisa na utairejelea furaha yako kama hapo zamani”. Juma aliongea huku akichukua rimoti na kuwasha Tv iliyokuwa pale sebuleni.
“Lakini bwana Juma wewe unaonekana una maneno mengi kama chiriku”. Nilimwambia Juma.
“Kwa nini wasema hivyo Mayanja?”. Juma aliniuliza huku akinitazama usoni.
“Una maneno mengi lakini vitendo hakuna. Sasa toka umeanza kuniambia kwamba tatizo langu leo litafika suluhu ni muda mrefu sasa lakini sioni vitendo”. Nilimwambia Juma.
“Tulia bwana Mayanja kwani mambo mazuri hayataki haraka. Muda bado haujafika. Kuwa na subira kidogo na baadaye utafurahi mwenyewe na roho yako”. Juma aliongea.
Huyu Juma mimi namfahamu vizuri kwani amekuwa ni rafiki yangu kwa muda mrefu sana. Tatizo la huyu jamaa ana maneno mengi utafikiri mwanasiasa lakini vitendo mara nyingi huwa ni sifuri kabisa.
Ni mwaka wa saba sasa Juma amekuwa rafiki yangu mkubwa. Tumekuwa tukishirikiana katika mambo mengi sana ya huzuni na yale ya furaha. Katika kipindi hicho chote cha urafiki wetu kuna jambo moja limekuwa likinishangaza juu ya Juma.
Mpaka sasa hivi Juma ni kijana ambaye anaishi maisha ya ubachela ingawa umri na uwezo wa kuoa anao. Kila ninapomuhoji juu ya hili basi amekuwa ni mtu wa kupiga danadana za hapa na pale.
************
Mambo ndiyo kwanza yanaanza. Ungana nami katika sehemu ya 02 ya kisa hiki. BONYEZA HAPA KUPATA MUENDELEZO
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: