Simulizi: KAHABA (02)
ILIPOISHIA
Mpaka sasa hivi Juma ni kijana ambaye anaishi maisha ya ubachela ingawa umri na uwezo wa kuoa anao. Kila ninapomuhoji juu ya hili basi amekuwa ni mtu wa kupiga danadana za hapa na pale.
SASA ENDELEA
Ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku, mimi na Juma tulikuwa tumetinga katika mtaa wa Pinto. Mtaa huu ulikuwa ni mtaa maarufu sana jijini Kano. Ulikuwa ni moja ya mitaa ambayo imechangamka sana. Muda wote iwe mchana au usiku watu walikuwa wakishughulika utadhani hawalali.
Jambo ambalo liliufanya mtaa huu uwe maarufu sana ni biashara ya ufuska. Biashara hii ilikuwa maarufu sana hasa nyakati za usiku katika mtaa huu. Akina dada wengi walikuwa wakionekana wakiinadi miili yao kwa lengo la kuwavutia wanaume ambao wangekwenda kulala nao na kuwapatia pesa.
“Sasa bwana Mayanja hapa ndipo penye suluhu la matatizo yote yanayokukabilia katika ndoa yako”. Juma aliniambia huku akinyoosha kidole kunionyesha jengo la Grand Cassino.
“Mbona sikuelewi bwana Juma? Yaani kunizungusha kwote kule umeamua kuja kunileta huku ambako kumejaa laana na ushetani wa kila aina!”. Niliongea huku nikimshangaa bwana Juma.
“Ushetani? Ushetani uko wapi?”. Juma aliniuliza huku akinitazama usoni.
“Ina maana wewe huna macho? Angalia wanawake wale makahaba, yaani wako uchi kabisa”. Nilimwambia Juma huku nikimwonyesha wanawake ambao walikuwa wakijiuza nje ya Grand Cassino.
“Kweli wewe bwana Mayanja naona umeanza kuchanganyikiwa. Ile ndiyo tiba halisi ya matatizo ya ndoa yako ambayo unasema kila kukicha inakuchanganya kichwa chako”. Juma aliongea maneno ambayo yalinishangaza sana.
“Una maana gani Juma?”.
“Nina maana ya kwamba, inakupasa uende ukachague mrembo mmoja wa nguvu ambaye atakuondoa mawazo na huzuni ulizonazo na kukufanya uwe bwana Mayanja kamili”. Juma aliongea.
“Juma rafiki yangu sasa naona umeamua kunipotosha kabisa”.
“Sasa nakupotosha nini Mayanja?”.
“Hivi wewe huoni badala ya kupunguza matatizo ndiyo nitakuwa nayaongeza matatizo kwa kumsaliti mke wangu?”. Nilimwuliza Juma.
“Mimi siwezi kukupotosha hata kidogo rafiki yangu. Wanawake wa hapa hawana stress. Unamchukua unalala naye na kisha unamlipa ujira wake kidogo halafu mnaachana. Mimi miaka yote ndipo mahali ambapo huwa najivinjari na mwenyewe waniona sina presha kabisa katika mambo ya mapenzi”. Juma aliongea.
Kwa mbali nilianza kuona kama maneno ya Juma yalikuwa na ukweli ndani yake. Kwa nini nimbembeleze mwanamke ambaye habembelezeki? Mimi siyo mtumwa wake kabisa. Yaani namlisha, namvisha, akiugua namtibu na bado nimbembeleze? Aaaaaaah! Haiwezekani hata kidogo.
“Ok, sasa ndiyo nafanyaje?”. Niliamua kumwuliza Juma maana mimi nilikuwa mgeni kabisa katika mambo yale.
“Kwanza shika hizi kondomu. Pili unaenda pale na kumchagua mrembo unayemtaka baada ya hapo mnaenda gesti na kumalizana. Gesti haziko mbali. Utaniangalia mimi ninavyofanya”. Juma aliongea huku akinikabidhi mipira ya kiume.
Baada ya hapo tukaondoka kuelekea nje ya Grand Cassino ambako kulikuwa kumejaa wanawake wengi warembo makahaba.
“juma nenda na mimi. Cheki ninavyolipa”. Mwanamke mmoja alimwambia Juma huku akiyatikisa makalio yake.
Kumbe Juma alikuwa maarufu sana katika maeneo haya. Kila mwanamke kahaba alikuwa akimfahamu. Ama kweli waswahili walisema tembea uyaone .
Macho yangu yalitua kwa mwanamke mmoja mrembo ambaye alikuwa akija kwangu kwa mwendo wa maringo sana. Alikuwa na uzuri ambao ulikuwa ni ngumu sana kumithilika na uzuri wowote duniani. Moyo wangu uliingiwa na ganzi na mdomo wangu ulishikwa na kigugumizi. Nikatokea kumpenda ghafla kwa mahaba mazito.
“Twende zetu”. Mwanamke yule mrembo aliniambia huku akinishika mkono.
Nami mithili ya mwanakondoo aliyekuwa akielekea machinjoni nilimfuata yule mrembo. Nilikuwa nimeshikwa na wehu wa ghafla.
Tulipata gesti na kisha nikachukua chumba. Tukaingia ndani huku nikiongozwa na yule mwanamke ambaye alionekana ni mwenyeji sana maeneo yale.
“Vipi mbona unaonekana mwoga sana?”. Yule mrembo kahaba alinihoji kwa sauti moja tamu sana.
“Mh! Hapana. Niko safi kabisa”. Nilimjibu kwa sauti iliyokuwa imejaa kigugumizi.
“Ok, umebeba
kondomu?”. Aliniuliza.
“Yes! Ninazo”. Nilimjibu huku nikizitoa zile kondomu na kuziweka juu ya meza ambayo ilikuwa mle ndani.
“Sawa. Fastafasta ni shilingi elfu tano, saa moja ni shilingi elfu kumi na tano na mpaka asubuhi ni shilingi elfu thelathini. Sijui wewe ungependelea huduma ipi kati ya hizo?”. Yule mrembo kahaba aliniuliza.
“Saa moja”. Nilimjibu yule mrembo.
Yule mrembo alianza kutoa sketi yake fupi na laini na kubaki na tight ambayo ilizionesha vyema hips zake. Akaitoa blauzi yake na kubaki na sidiria ambayo iliyabeba matiti makubwa kiasi yenye mvuto sana.
Baada ya zoezi hilo kuisha alikuja na kunikumbatia kisha akanipa busu moja mwanana katika sikio langu. Busu lilile lilinifanya nisisimkwe na mwili na kuirekebisha vyema akili yangu ambayo ilikuwa mbali sana. Mjomba naye alisisimka na kuanza kujitutumua ndani ya suruali yangu mithili ya chatu aliyemwona mwanambuzi.
Yule mrembo alinichukua na kunikalisha taratibu juu ya kitanda na kisha akanikalia katika mapaja yangu na kuanza kufungua vifungo vya shati langu huku macho yake ya huba yakinitazama.
Baada ya sekunde kadhaa akafanikiwa kunifungua shati langu na kulitupia mbali. Baadaye sasa akaja katika suruali yangu ambapo aliutoa mkanda wa suruali na kisha kuifungua zipu ya suruali taratibu na wakati huo wote mjomba aliendelea kututumka mle ndani ya mkwego utadhani amelishwa hamira.
************
Tukutane katika sehemu ya 03 kwani itakuwa na mengi sana ya kuyafahamu juu ya kisa hiki chenye
BONYEZA HAPA KUPATA MUENDELEZO
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: