SIMULIZI: NAITAFUTA FURAHA YANGU 02





Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU


    Sehemu ya 2
 ____HII STORY INAFAA KUSOMWA NA WATU WA RIKA ZOTE
INAYO ,SIMANZI NA MAJONZI YALIYOKITHIRI___

  Tuendelee pale tulipo ishia jana,Mara rafiki yake mama adinani alisikika akilia kwa uchungu huku akisema mama adinani kwanini umefariki mapema,naa hawa watoto wako nani atawalea kwanini mmefariki mapema ,mama adinani jamani, nini kimewasibu mbona mmeondoka mapema?
Hakika rafiki yake marehemu ,alilia nakugara gara chini.
Ndipo adinani,mudrick nanusra waliuliza kwa pamoja mama na baba wamefariki? kisha wote wakamwangalia askari kwa mshangao.

Askari aliwaangalia na kuongea ,kweli baba ba ba yenu na mama wame.. Alibabaika mno ,ndipo alijikaza na kusema amefariki kwa ajli ya piki piki.adinani alimsogelea askari na kumuuliza ,ni kweli baba na mama wamefariki ?,askari alijibu ndio wamefariki,
Masikini adinani alikuwa tayari ashavalia nguo za shule alijiandaa kwenda shule ,alijikuta akishuka chini taratibu huku akilia kwa uchungu.

   Nusra alikuwa ni mdogo sana hakuelewa vizuri ila mudrick yeye alielewa basi walianza kulia kwa uchungu ,huku wakiita baba ,mamaaaa ,vile vile mama joy ambae ni rafiki yake mama adinani nae alilia ,ndipo majirani walivyosikia vilio waliamka na kukimbia kusikiliza kuna nini.
Wakati huo aliyesababisha vifo vya bwana ally na mke wake alikuwa anatabasamu kisha akajisemea moyoni.

"Urafiki ni wa kwenye shida tu ,ila ukipata neema tunatemana ,kapumzike salama rafiki yangu ,ally tulishirikiana vyema kutafuta pesa ila hio.pesa imenifanya nikugeuke."
Basi juma nae alisogea kwenye msiba huku akijifanya hajui kitu chochote yaani.

Alimsogelea askari na kumuuliza swali la kizushi ni kweli rafiki yangu ally amefariki?,huku akitiririsha machozi ya unafiki.askari alimjibu ndio amefafiki ila gari iliyowagonga hatujafanikiwa kulinasa na gari linaonesha halikuwa na plot namba,hivyo hatujafanikiwa .kutokana na utandawazi wetu duni basi hatujafanikiwa kumnasa ama kuwatambua aliyesababisha hio ajali.

Askari aliomba ndugu wa marehemu wa bwana ally na mkewe wajitokeze ili wakaoneshwe miili yao.basi juma alikuwa mstari wa mbele na alisimama kama rafiki na mtu wa karibu wa familia ya bwana ally.
Adinani na wadogo zake walilia hadi sauti zikakauka kabisa.basi waliweza kuoneshwa miili ya marehemu na ilikuwa imeharibika mno.taratibu za mazishi zilifanyika ndipo  waliweza kuwazika bwana ally na mkewe. Ulikuwa msiba mkubwa ,pigo kubwa kwa watoto wao alio waacha .
 *****************
             Baada ya mazishi kumalizika ndipo juma alikaa kikao na majirani  wanaoizunguka familia ya marehemu ,hapakuwa na ndugu wa damu upande wa bwana ally ,ila kwa upande wa rahma alikuwepo shangazi yao ambae alikuwa ni kipofu.
Hakuwa msaada maana haoni chochote,duka ambalo lengewasaidia watoto walio baki nalo liliungua na kuteketea kila kitu ,walichobakiwa ni nyumba tu.

Kwenye kikao juma yeye alikuwa kiongozi mkuu " ,alianza kuongea "ndugu majirani wa karibu wa marehemu ally pamoja na mke wake,hamna asiyejua kabisa kama mimi ni rafiki yake. Ni rafiki ambae nilisaidiana nae mambo mengi mno.

Kuna mambo ambayo ninyi hamyajui ila rafiki yangu ally alikuwa akiniambia kila jambo analolifanya,tumekusanya michango kwenye msiba na watu wamechangia ,ni kweli marehemu wameacha watoto watatu kama mnavyo waona ,adinani ndiye mkubwa lakin ndio bado alikuwa kidato cha tatu hana uwezo wa kuendesha familia hatoweza kuwalea wadogo zake.

Pia kipindi cha uhai wake marehemu ally tulikopa pesa benki milion saba ,kisha tuligawana ,yeye alijaza bidhaa zake dukani ,ambako huko dukani nae maafa yamempitia duka lote limeungua,tofauti na mkopo tulio kopa vile vile nilimkopesha milion tatu .na tuliandikishana kabisa.mwenyekiti nadhani yupo hapa na mjumbe maana hawa ndio walikuwa mashahidi wetu.

Juma alitoa mikataba ambayo waliandikishana ,haikuwa mikataba ya ukweli bali aliwahonga pesa mwenyekiti na mjumbe kisha wakaandika mikataba ya uongo.basi mwenyekiti na mjumbe aliitikia ni kweli ilikuwa hivyo juma.

Basi juma aliendelea ,michango iliyopatikana kwenye msiba milioi nne ,nitazichukua na kwenda kulipa deni pesa tulizo kopa nisipo fanya hivyo inamana hii nyumba itapigwa mnada na watoto wake watakosa mahali pa kukaa ,sidhani kama kuna jirani anapenda kuona watoto wamarehemu wakiranda randa mtaani.

Watu kwenye kikao walijadili na kuona ni heri pesa zilizopatikana wakalipe deni ili watoto wasikose mahali pa kuishi.basi juma alifuta ndevu zake kisha akashika karatasi yake na kuendelea kuongea.
Kwakuwa rafiki yangu nilimkopesha milion tatu na tuliandikisha hivyo katika hii nyumba yake ,nitapangisha vyumba viwili na sebule,hivyo watoto watakaa kwenye chumba kimoja nafanya hivyo si kana kwamba napenda hata mimi naumia sana ,(hapo juma alijifanya mwema na mwenye kujali) ila hio pesa niliyomkopesha mimi mwenyewe nilipewa na kaka yangu nae ananidai.

Watu walikataa hilo wazo na kusema "jamani kwanini mnafanya watoto wa marehemu kuishi maisha ya tabu kwanini,hio hela usiidai ufanye kama umeisahau.ndipo mama joy alisimama akiwa anatokwa na machozi " baba yangu juma usiwafanyie hivyo watoto wataishije ningekuwa na pesa mimi ningekulipa ndio hivyo mimi mwenyewe sina hata senti tano."

Mwenyekiti aliongea nae"jamani tuelewe nae alikopa pesa hivyo tutamwachia akodishe hivyo vyumba  viwili na sebule ,akisha maliza na kupata pesa yake basi ataacha nyumba si kana kwamba nyumba inauzwa.

Watu walitafakari ilibidi wakubali maana mwenyekiti na mjumbe wote wanamuunga mkono juma hivyo wao hawakuwa na nguvu ya kuongea.adinani alimwangalia juma kisha akamwambia "hayo madeni mie siyatambui hivyo siko tayari kupokea wapangaji nyumba ya baba yangu.
Juma alicheka na kusema basi kama hutaki ,basi iuzwe tulipe madeni ya watu.ilibidi Watu walimshauri adinani atulie haya ni mapito tu muda ukifika kila kitu kitabaki salama,adinani alikubali ki shingo upande.
Kikao kilifugwa hatimae watu kutawanyika.adinani alibaki na wadogo zake,pia na shangazi yao ambae ni kipofu.
Nusra kila muda alilia huku akimlilia mama yake na baba.

__________________________________________
Wiki mbili zilipita tu baada ya msiba kumalizika ndipo juma alileta mpangaji ambae alipanga vyumba viwili na sebule.adinani hakuwa na kipingamizi kwakuwa alikuwa mdogo ,ndipo walihamia kwenye chumba ambacho walikuwa wanakitumia  marehemu baba na mama yake.
Ilibidi walale wanne,adinani ,na wadogo zake wawili vile vile na shangazi yao.

Maisha yalizidi kuwa magumu ,maana pesa zilizopatikana kwenye msiba ,juma alichukua na kusema anaenda kulipa deni ,vile vile ,nyumba imepangishwa hakika adinani alihisi yupo jehanamu hakuwa na furaha kila mara alimkumbuka baba na mama.

Kutokana na pesa kuwa ya shida adinani aliamua kuacha shule kabisa maana alikuwa kidato cha tatu ,aliamua aingie mtaani ili kutafuta pesa aweze kuwahudumia chakula wadogo zake.

Juma yeye pesa zote alizozichukua kwa ally alinunua piki piki kumi na kuwapa vijana wafanye kazi kwa siku wanampelekea elfu kumi,aliajiri boda boda wengi.
Ndipo alimfuata adinani na kumwambia

" adinani sitaki uishi maisha magumu wewe ni kama mwanangu ,baba yako alikuwa fafiki yangu sana ,najua unajua kuendesha boda boda ,na ulikuwa ukiendesha sana piki piki ya marehemu baba yako ,basi twende nyumbani nikakusainishe mkataba nikupe piki piki uingie kijiweni ufanye kazi ,
Vile vile boda boda inayopesa sana.na utaweza kuwapatia mahitaji wadogo zako watasoma bila shida hata pesa ya chakula utapata kupitia hio piki piki.

Adinani masikin  alivyoambiwa hivyo hakuwaza na kuwazua kutokana na ugumu wa maisha pia hana pesa na wadogo zake wanamtegemea yeye,asipo pata pesa basi hawali chakula basi. 

Adinani kwa kuwa hajui dhamira ya juma ,wala hajui juma moyoni anapanga njama gani ,kwakuwa hana kazi na wadogo zake wanamtegemea ilibidi akubali kupewa mkataba na juma ili ampe boda boda.

Basi juma alimwita mwinyekiti ,kisha alimwandikisha adinani mkataba na kumkabidhi piki piki ,adinani aliingia kijiwe cha tabata bima rasmi na kuanza kufanya kazi ya uboda boda.

Ilikuwa ni kazi ngumu mno kwa adinani maana ni mara ya kwanza ,hakuwa na abiria wengi ,alihangaika siku nzima anapata elfu nane ,basi alirudi nyumbani amenunua unga na mboga mafuta ,aliwapikia wadogo zake kisha wakala na kulala.

Usiku kabla usingizi haujawachukua "nusra aliita " kaka inamaana mama na baba kwanini wamefungiwa kwenye sanduku kisha wakafukiwa chini?,inamana huko kwenye masanduku hayo wanaenda kufanya nini?
Lile swali lilikuwa gumu mno, lilimfanya adinani machozi yamdondoke ,mara shangazi alidakia "alimwambia nusra huko wameenda kusali na wanakuombea wewe ukue vizuri ,utakuwa unaendesha gari ,pia usome vizuri .

Nusra aliuliza tena " mbona wanafunzi shuleni wakati tunatawanyika shuleni wananicheka sketi yangu imechanika wananiita mimi yatima.kweni yatima ni nini shangazi.
Yale maswali yalizidi kumchoma sana moyo adinani ilibidi aamke kisha akatoka nje ili akapunge upepo asiweze kusikia chochote maana anaumia sana.
Shangazi kwakuwa yeye ni kipofu ila anasikia vizuri alimkumbatia vizuri nusra kisha akamwambi"
Nusra yatima ni binti mwenye akili nyingi darasani hivyo wanakuambia hivyo sababu wewe unaakili sana ,sawa eee.

Nusra alisema sawa shangazi kisha akamfunika vizuri ili walale
Wakati huo adinani baada ya kutoka nje alikaa sehemu moja ilikuwa na ua kubwa na palikuwa na giza ,mara alimwona 
Daniel ambae ni mpangaji kwenye nyumba yao ,vile vile danieli aliletwa na juma kisha akampangishia ,

Danieli alitoka kisha alienda kusimama kwenye ukuta wa jirani yao Hazikupita dakika nyingi juma nae alifika na kumsalimia danieli
Mambo vipi jembe langu la kazi
Danielei akiwa na bukta tu ,juu hakuvaa kitu ,alijibu poa huku akipiga mbu wanao mng'ata miguuni.
Walianza mazungumzo yao huku adinani akiwaangalia na kusikia kila kitu.

Juma aliuliza "vipi huyo mtoto adinani kalala au bado yupo nje?,danieli alibonyeza simu yake kisha akajibu amelala huyo si unajua wanalala chumba kimoja wanne.ha ha ha wakome sasa muda wao wa mateso ,maana baba yao tayari nimemfilisi na kumuua kabisa.
Adinani kusikia vile alikaa vizuri na kusikiliza  ni umbea ganj au wanadajili ninj usiku huu.

Juma aliuliza " hebu niambiee ulifanya vipi siku ile dukani ulivyoenda kuchoma lile duka magomeni.daniel alishusha pumzi na kusema .haa kule mbona simpo tu .kwanza tulimtumia mlinzi malaya mmoja akajilegeza bure,yule malaya sisi situlimpa pesa kisha tukampanga akajipitishe kwa mlinzi na ajirahisishe na mlinzi akijilamba midomo na kumtamani basj ajilegeze akubali hata bur, basi yule mlinzi  nae sijui alikuwa na njaa zake upesi alimtamani yule demu kisha alimpeleka demu chemba ili wakafanye yao,halafu mimi nilipata upenyo,nilitoboa dirisha kisha nilimimina 
Petroli ,.
Juma aliuliza ulimimina vipi sasa hio petroli,ha ha ha daniel alicheka na kusema ,nilichukua mpira nikawa namimina kidogo kidogo sasa petroli si ikamwagikia ndani.
Nilivyomaliza tu nilipiga njiti nikadumbukiza kwenye like tobo nilio toboa dirishani  kisha nikaondoka zangu kwahio moto ulikamata mbaya.

Ha ha juma alicheka na kumwambia basi freshi kesho kuna dili moja nitakupa ,adinani akitoka  nataka uingie chumbani  cha kwao ukanitafutie hati ya hio nyumba.
Danieli alitabasamu na kusema usijali mkuu.
Basi juma aliaga na kuondoka huku danieli nae aliondoka na kuingia ndani.

Adinani akiwa nje ndio akapata picha ,inamana duka la baba  limechomwa na mtu ambae wanakaa nyumba moja,tena nyumba ya baba yangu inamana juma ndio anafanya hii kazi.
Adinanani aliwaza nimfuate juma nikamwambie ukweli lakin nafsi ikasita akajiwazia ,kama amemuua baba na akitambua kuwa mimi najua hii siri ataniua je wadogo zangu wataishi vipi?
Adinani alijikuta anamtihani mkubwa alianza kutiririsha machozi.

je nini kitaendelea?


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: