SIMULIZI: NAITAFUTA FURAHA YANGU 03





Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU

********************

         Sehemu ya 3
   Tunaendelea tulipo ishia jana,Adinanani aliwaza nimfuate juma nikamwambie ukweli, lakin nafsi ikasita akajiwazia ,kama amemuua baba na akitambua kuwa mimi najua hii siri ataniua je wadogo zangu wataishi vipi?
Adinani alijikuta anamtihani mkubwa alianza kutiririsha machozi.

Adinani alikumbuka ,baba yake alikuwa anamwamini sana rafiki yake ,walikuwa wana share kusaidiana kujenga nyumba imekuwaje juma akawa msaliti,alijiwazia mno hatimae akachoka na kuondoka hakutaka kulala nyumbani ,
Adinani aliondoka hadi kwa rafiki yake aligonga mlango ,ngo ngo ngo!!!!,hazikupita dakika mbili rafiki yake alifungua ,

Aaah adinani vipi usiku tuna amshana nini shida?,adinani alipitiliza hadi kitandani kwa rafiki yake alijilaza ,huku akilia kwa uchungu mno baada ya kugundua mtu aliye muua baba na mama yake.rafiki yake ambae yeye anasoma ,alikuwa ameweka vitabu mezani bila, shaka alikuwa anasoma nyakati za usiku.

Alimsubiri hadi hasira za adinani zilipo pungua alimuuliza kulikoni mbona unalia?,adinani alimwangalia rafiki yake na kumwambia ,shukuru sana  baba na mama yako wako hai. Siku wakifariki utakuja kunitafuta na kuniuliza kwa nini nakuambia hivi.rafiki yake alimwangalia kisha akauliza kwanini unasema hivyo?
Adinani alikaa vizuri kitandani kisha akavua viatu "alianza kuongea " mick rafiki yangu tulikuwa tunaenda shule wote ona gafla shule nimeshidwa kuendelea,pesa nitapata wapi ya kusoma ,duka la baba limeteketea hilo ndio alikuwa analitegemea kunisomesha,ila nakushauri soma sana rafiki yangu miki.

Vp wanafunzi hapo skonga wanasemaje?,mick alishusha pumzi na kusema ,hawana usemi ila  dayana ,joseph hao ndio walikuulizia ,adinani alitabasamu na kuuliza ,dayana hajambo ?je john bado anamfukuzia?
Mick alicheka na kusema ,ndio anamfukuzia sema dayana anakupenda ila hajakuelezaga tu.

Adinani alishusha pumzi na kumwambia mick ,endelea kuwasalimia mie shule sirudi tena.basi walipiga story zao hadi paka kucha.

Asubuhi adinani aliwahi kudamka na kwenda nyumbani alikuta ,mudogo wake mudrick ameamka amekaa nje analia,
Unalia nini mudrick"adinani aliuliza"
Anko danieli kanichapa kaniaambia nisikae sebuleni ,sebule ni yake ,sababu kapanga vyumba viwili na sebule ,hivyo sisi tunakaa kwenye chumba chetu wala tv yake tusiangalie.

Adinani nae machozi yalimtoka ni kweli inauma mno.mpangaji ametawala nyumba,kinachomuuma adinani amegundua  kuwa daniel anashirikiana na juma ,na ndie aliyechoma duka la kwao.
Adinani alimnyamazisha mudrick kisha alimogesha na kumvalisha nguo zake za shule vile vile nusra nae alimwogesha na kumvalisha nguo kisha akawapaka na mafuta.
Adinani yeye ndiye baba,mama kaka kila kitu ,alivyomaliza walibeba mabegi yao ya shule kisha aliwapakia kwenye piki piki hadi shukeni.

Alivyofika aliwapa mia tano tano kila mmoja.kisha alimshika mkono nusra alimwambia "nusra usome sana ee ,halafu ikifika saa nne ununue kachori ule sawa ee hio mia tano nimekupa kisha alimwangalia na mudrick nae aliwasihi wasome maana ndoto zake za kusoma hazijatimia.
Basi aliondoka na kurudi kwenye kijiwe chake alianza kupiga kazi yake ya boda boda.

Tukirudi nyumba aliyopanga daniel baada ya adinani kwenda kazini na watoto kwenda shuleni ,alianza kunyata kuelekea chumba cha akina adinani wanako kaa,alimkuta shangazi yao kalala tu,aliwaza ataingia vipi ili akatafute hio hati ya nyumba.

Aliwaza kisha alimwita shangazi,masikin shangazi pasina kuelewa chochote aliitika naam daniel

Daniel aliwaza jambo ,kisha akasema ,nimepewa hela na juma,amesema ukanunuliwe nguo zako ,hivyo kuna bajaji nje inakusubiri.shangazi kusikia vile alifurahi kwakuwa yeye ni kipofu basi alimwomba danieli aweze kumsaidia kufunga chumba kisha ampe funguo ,danieli alicho fanya alibadilisha funguo na kumpa kisha akamshika mkono na kumwambia twende  ukapande bajaji ,shangazi alitembea taratibu kisha alipanda bajaji ,kweli danieli aliongea na dereva ampeleke buguruni akamnunulie nguo ,nia yake apate mwanya aweze kupekua chumba cha akina adinani.

Kweli shangazi aliondoka ,ndipo danieli aliingia na kuanza kupekua chumbani ,alitafuta kila mahali kwenye mabegi ya marehemu ,ally na mke wake ,mabegi ya watoto ,begi la adinani ,alitafuta hadi akachoka.hakuipata hati ya nyumba,alivyomaliza alifunga nyumba,
Alimpigia simu juma na kumweleza kuwa hajafanikiwa kuipata,juma alimjibu usijali kuna dili lingine nitakupa.

Basi muda ulisogea shangazi alirudi na kukaa nje maana alikuta hamna mtu.tukirudi maeneo ya tabata shuleni mahali wanako soma mudrick na nusra.tayari ilitimiea mida ya saa nne,ndipo  nusra alinunua kachori ili aweze kupata kifungua kinywa.lakin watoto wenzake walikuja na kumnyang'anya kachori zake.

Katoto kamoja kalimshika mkono nusra na kumwambia" we yatima unakula kula nini hizi kachori tunazila sisi halafu hatuchezi na yatima sisi.watoto watatu waliondoka.
Nusra akiwa na njaa alianza kulia na kumtafuta kaka yake mudrick  alizunguka ndipo aliona kundi la wanafunzi wanashangilia 
Piga huyo ,piga kichwani piga ema,mpige mudrick hana lolote huyo,yalikuwa maneno ya wanafunzi wapambe ambao walichochea ugomvi,
Nusra kufika alikuta kaka yake amepigwa tena amekaliwa tumboni anapigwa ngumi za usoni.

Nusra bado mdogo sana ana miaka mitatu alimsukumu mwanafunzi ambae alikuwa anampiga kaka yake akadondokea huko ,ndipo mudrick alinyanyuka ,shati lake likikuwa limechwanwa chanwa vile vile usoni manundu huku damu zinamtoka.
Mudrick analia ,nusra nae analia wanafunzi wengine walianza kuwazomeaa ,waone watoto yatima wanaliaaaa uwwooooooo waonee

Ndipo kengele iligongwa na wanafunzi kutawanyika,nusra alimchukua kaka yake na kumpeleka bombani a alimnawisha uso  alivyomaliza alivua sweta yake na kumwambia kaka vaa hii sweta maana shati lako limechanwa.mudrick alivaa hakuwa na namna.

Saa sita ilivyotimia adinani aliwafuata wadogo zake shuleni na kuwakuta hawatamaniki mudrick kavimba uso hatari
Aliuliza "mudrick nani kakupiga na kwasababu gani?

Mudrick akiwa na hasira alisema ,emmanueli alininyang'anya mia tano yangu ndio nikapigana nae,adinani alitikisa kichwa kisha akamuuliza nusra,na wewe pesa yako umepeleka wapi?

Nusra alimshika kaka yake mkono kisha akaangalia chini alimjibu" kaka nilinunua kachori wanafunzi walininyang'anya hivyo sijala
Adinani alichoka basi aliwapakia hadi nyumbani alivyofika walimkuta shangazi amekaa nje.adinani aliuliza "shangazi mbona umekaa nje halafu hizo nguo umetoa wapi?.

Shangazi alipapasa mti ili ajishikize aweze kusimama ,kisha akamjibu adinani" hizi nguo kaninunulia juma.adinani alivyosikia jina juma ,aliyakumbuka maneno aliyoyasikia usiku

"Nakupa kazi utaingia chumba cha adinani ukatafute hati ya nyumba,adinani aliwaza na kujisemea kwakuwa sina uhakika nani amewaua wazazi wangu na wala sina uthibitisho ila naimani mungu yupo nitafahamu tu.
Adinani alifungua mlango kisha ,aliandaa chakula  walikula alivyoshiba alirudi kijiweni na kufanya kazi ya uboda boda.

Ilivyotimia jioni adinani alienda tena kwa rafiki yake micki alikuwa anahati ya nyumba alimwomba rafiki yake aitunze sana hio hati .rafiki yake alipokea kisha waliendelea na story zao za kawaida.

Siku zilijongea hatimae miezi mitatu ikakatika ,adinani alimlipa juma pesa ya boda boda vizuri kabisa ,adinani nae aliipenda kazi ya boda boda ikawa kila wiki anamkabidhi juma elfu sabini ,huku na yeye akijimudu kuwatunza wadogo zake pamoja na shangazi
Maisha yaliendelea.

Ni siku ambayo ilikuwa imechangamka sana ijumaa ,adinani akiwa kijiweni maeneo ya tabata bima ,ndipo gari aina ya prado ilishuka eneo lile ,kuna binti mzuri aliyopitiliza ,akiwa amevalia nguo za kisasa kimin kimepanda kidogo juu ya magoti ,nywele zake alizosuka hadi mgongoni.

Basi yule binti alishuka kisha ile gari iliwashwa na kuondoka,boda boda kama kawaida yao walimkimbilia na kuuliza dada wapi waenda ,wengine wanasema ,boda boda hii hapa yaani kama vile uber.
Dada yule alikuwa ameshikilia simu kubwa ,mdomoni kaweka lipstick ambayo ilimkaa vyema.
Aliwaangalia sana boda boda,wengine walikuwa wachafu wachafu na alikuwa anahitaji boda boda.

Aliangalia sana huku dereva wa boda boda wakimsumbua sana wapande kwenye piki piki yao.yule dada aliongea "hey jaman nina uhuru wa kuchagua piki piki ninayoitaka mimi,hivyo tulieni msiwe na wasi wasi.
Boda boda kusikia vile walitulia wengine wanamsifu jinsi alivyomrembo wengine wanaomba namba zake basi ni kelele za boda boda.
Yule dada alitizama kwenye mti flani aliona kijana amelala kwenye bodaboda aina ya boxer kalala juu.aliuliza " jamani ninyi mnamakelele why? Mbona yule kalala anaumwa ama,
Alikuwa si mwingine bali ni adinani ,alikuwa amejipumzisha tu .

Boda boda walimjibu"huyo  hajui kuendesha atakudondosha mara wengine wakasema ,kalala kwa mchepuko kacheza sebene usiku kucha,
Yule dada alisogea hadi iliko piki piki yaa adinani alimwangalia"siku hio adinani alionekanika msafi,kavaa nguo zafi chini kavaa viatu ,
Alimuuliza wewe kaka unaumwa?

Adinani alishituka na kusema hapana siumwi nilitoka kuosha piki piki ndio maana unaona nimetulia hapa.dada alimwangalia adinani na kumwambia nataka unipeleke masaki sasa hivi.
Adinani alisema usijali twende zetu elfu hamsin andaa tu.adinani alitania huku akicheka.
Boda boda wengine walidakia jamani mimi nakupeleka bure.
Basi yule dada alikuwa akicheka tu.
Adinani aliwasha piki piki kisha safari ilianza kuelekea masaki.waliweza kufika masaki na huyo dada aliingia kwenye jumba la maana alimwambia adinani nisubiri utanipeleka tena sinza nabeba kibegi tu kidogo.

Basi adinani alikaa nje ya geti alimsubiri abiria wake baada ya muda ,yule bibie alitoka akiwa na kibegi kidogo mgongoni ,alipanda tena piki piki hadi maeneo ya sinza .
Alivyofika yule dada alitoa pochi alihesabu pesa,laki moja na kumpatia adinani,kisha alimwambia.

Ulisema kutoka tabata hadii masaki elfu hamsini na masaki hadi sinza elfu hamsini haya pesa yako hii.adinani alishangaa kisha akacheka na kumwambia "dada hapana mie nilitania tu elfu hamsini nilikutania yaani pesa ya kunilipa elfu ishini na tano tu.na si laki moja.

Dada yule alimwambia asa kwanini ulinitania mie nikajua labda bei yake,adinani alimwambia nisamehe nilitania tu.
Yule dada alivua elementi kishaa akamwambia sio vizuri kwakua nishaitoa hii laki moja chukua tu ,maana mie sijui bei zenu za tanzania.

Adinani aliguna na kuuliza kwani wewe sio mtanzania kabla yule dada hajajibu geti lilifunguliwa mdada mwingine alitoka aliita zumraaa waooo umekujaa karibu  ndani.

Adinani akiwa ameshangaa yule dada. Ambae anaitwa zumra aliweka ile laki moja kwenye elementi ambayo adinani alikuwa ameishikilia mkononi,kishaa aliingia ndani ya geti .
Geti likafugwa wala hakumuaga adinani.

Adinani alirudia kuhesabu ile pesa alikuta laki moja,adinani aliwaza agonge geti amrudishie pesa yeye abakiwe na elfu 25 tu.mara mlinzi alitoka na kumwambia yule dada uliyemleta kasema asante maana kasahau kukuaga.
Kisha mlinzi alirudishia geti .

Je nini kitaendelea?


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: