SIMULIZI: NAITAFUTA FURAHA YANGU 05
Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
____sehemu ya 5____
Tulipo ishia jana ,baada ya Kelvin alichochea gia na kutokomea huku akimwacha adinani mtaroni,watu waliweza kufika mahali adinani kadondokea ,walishangaa kuona damu inaatoka kama bomba la maji shingoni baada ya kukatwa na msumeno shingoni
Watu kwa mshangao waliogopa huku wakisema "masikini wamemchinja mkaka wawatu
Anakufaa shingo yoote amekatwaa
Adinani hakujitambua tena kadondokea mtaroni kichwa chini miguu juu halafu shingo imekatwa na msumeno
Adinani alijikaza mno na kudumbukia vizur mtaroni hakuumia kichwa sababu alikuwa amevaa element ,adinani akiwa hoi aliikamata shingo yake na mikono miwili,ili kuzuia damu isitoke kwa wingi.
Kumbe hakukatwa shingo yote ila alijeruhiwa sana .watu walianza kujaa na kumwangalia pasina kutoa msaada ,boda boda wa ununio na bahari beach walipata taarifa kuwa boda boda mwenzao amenusurika kukatwa shingo yote na kuporwa piki piki basi walikusanyika eneo lile.
Ki ukweli boda boda wana umoja walikodi bajaji na kumuwahisha adinani hospitali maana hali yake ilikuwa mbaya ,yaani hajitambui.
Dereva wa ile bajaji aliuliza tumpeleke hospitali gani ambayo atapata matibabu haraka.waliwaza kisha wakasema tumpeleke massana maana huku ununio hamna hospitali kubwa ,
Boda boda walishirikiana hadi hospitalin ,lakin walipitia kituo cha polisi na kupewa kibali cha kwenda kumtibu.adinani wakati anaingizwa hospitali ya massana kwa bahati nzuri abiria zumra ambae alishawahi kumpeleka masaki kisha akampeleka na sinza ,ndipo bibie zumra alimlipaga adinani laki moja.
Basi wakati adinani anashushwa kwenye bajaji ,zumra nae alikuwa anapanda kwenye gari yake akiwa na rafiki yake.
Zumra alishituka na kusema jaman ,nimesisimka mwili mzima aaaah.
Rafiki yake akauliza ,kwani umeona nini hebu endesha gari bana tuondoke,zumra alimwangalia rafiki yake na kusema ,suhaila ,yaani nimeona kijana rika letu kaingizwa hapa akiwa amejaa damu sijui kapata ajali.
Suhaila alimwambia zumra ,we kama hutaki kuendesha gari pisha njoo kaaa huku mie niendeshe.,zumra alishusha pumzi kisha aliwasha gari ili waondoke.lakin gafla alikanyaga break na kusema ,we suhaila hebu subiri huyu kijana aliyopitishwa hapa mbona sura yake sio ngeni machoni mwangu sijui nishawai kumwona wapi ,
Zumra alifungua mlango wa gari kisha alishuka na kuingia tena hospitali ya massana ,alienda moja kwa moja hadi chumba cha watu mahututi ile anafika mlangoni hakuona chochote dokta alifunga mlango na kusema ,kwa sasa tunaomba uvumilivu tunamtibu huyu mgonjwa.
Basi zumra hakutaka kumsumbua dokta alitoka kisha aliwasha gari wakaondoka na rafiki yake suhaila.adinani alipoteza fahamu kabisa madaktari walianza kumtibu na kutoa damu kisha kumshona mahali alikokatwa shingoni.
Tukirudi maeneo ya tabata nako kulitokea tibwili ,baada ya daniel kufumwa na mke wake akimbaka kipofu ,shangazi .
daniel alizidi kuonesha ubabe alimpiga mke wake hadi kuzimia.
Lisaa lizima lilipita ndipo mudrick na nusra walirudi toka shule
Nusra alifika mlangoni akashangaa kumkuta mke wa daniel amelalala ,nusra aliita shangazi na wewe umelala na shangazi yetu?,lakin mke wa daniel alikuwa bado kazimika.mudrick ambae yeye alikuwa mkubwa alifungua dirisha ili apate mwanga ndipo alikutana na shangazi akiwa uchi huku amefugwa kamba ,
Mudrick alichukua shuka na kumfunika shangazi yake kisha akatoka hadi kwa mama joy alifika na kumkuta anafagia uwanja wa nje,maana kutoka wanapoishi na kwa mama joy hapakuwa na umbali.
Mudrick huwa aanamwita mama mdogo japo si wa kweli ila jina ndio walilolizoea kutokana na urafiki waliokuwa nao ,na marehemu mama yao.
Mama mdogo twende ukaone nyumbani ,nimekuta shangazi amefugwa pia shangazi mwingine amelala wala haongei.ni maneno aliyoongea mudrick.
Mama joy aliachia ufagia na kuuliza unasemaje mudrick ,huku akianza kutembea kwa upesi ili kuwahi ni kitu gani kimemkuta shangazi,kweli alifika alikuta hali mbaya ,
Alianza kumfungulia kamba shangazi kisha akamtolea matambara mdomoni alimuuliza shangazi kitu gani kimekusibu nani kakuingilia kimwili?
Masikin kipofu alianza kulia na kusema nimebakwa na mtu sijamsikia hata sauti aliingia na kuanza kunichania nguo,basi mama joy alimkalisha shangazi chini kisha alianza kumburuza mke wa daniel na kumtoa nje alivyogundua amezimia.
Alianza kumpepea kwa kanga ,zilikatika dakika kumi na tano ndipo mke wa daniel alizinduka
Ki ukweli alikuwa hajielewi ndipo alinyoosha shingo yake na kuuliza ni kitu gani kimetokea?,mama joy alimwangalia sana mke wa daniel na kumuuliza
"Hebu niambie nimewakuta chumbani ,wewe umezimia na shangazi wa hawa watoto amebakwa ni nani amefanya hilo tukio?,kabla mke wa daniel hajamalizia daniel alirudi na upanga mpya alimnyoshea mama joy na kumwambia
" wewe mwanamke jiangalie ,umetoka kwako na kuja huku kufanya nini ,hicho unataka kudadisi jiangalie usije ukapoteza shingo yako kwanza ondoka hapo.
Mama joy alimwangalia daniel ambae ni mrefu wa wastani aliyejazia kimazoezi ,aliona akiongea chochote anaweza kulambishwa panga,mama alichukua ndala zake ,alivaa taratibu na kuondoka.
Daniel hakuishia hapo aliingia ndani na kutoa mabegi ya mke wake,na kutupa nje,kisha akamwambia "haya sepa nenda kwenu,ndio mimi umenifumania tena nafanya mapenzi kwa unguvu ,hivyo sitaki kukuona ondoka.
Ki ukweli nyumba ilizidi kuingia mkosi ,mke wa daniel alitimuliwa na kuondoka ndipo daniel alibaki peke yake.,moyon akajisemea mambo si ndo haya sasa,adinani amekufa sasa huyu kipofu nitakuwa nafanya huu mchezo kila siku,halafu hivi vitoto nitavipakia kwenye gunia nikavitupe mbagala huko .maana wanatia vizuizi.
Basi daniel aliingia chumbani kwake.mudrick na nusra walimshika mkono shangazi yao na kwenda kijiweni anako fanya kazi kaka yao adinani waliulizia na kuambiwa adinani alipeleka abiria ununio ila hajarudi hadi sasa.shangazi aligoma kurudi nyumbani ndipo walikaa kijiweni ili kumsubiria adinani pasina kujua adinani nae amekubwa na majanga mazito.
Jua lilizama pasina adinani kutokea ,watoto walianza kuhisi njaa ndipo ,nusra alimshika shangazi mkono na kumwambia " shangazi nasikia njaa ,mudrik alimshika mdogo wake na kumwambia "shangazi ni kipofu hawezi kupika tumsubiri kaka arudi ili akapike.
Masikin walisubiri hadi saa mbili usiku adinani hakutokea ndipo mudrick alimwongoza shangazi na kurudi nyumbani,walifika nyumbani ,mudrick ilibidi awashe jiko la mkaa ili aweze kumpikia mdogo wake nusra maana alianza kulia baada ya njaa kumwandama.
Mudrick kwa umri wake kupika alikuwa bado hawezi kutokana na maisha kuwa magumu kila kukicha basi alihangaika kusonga ugali ,ukiwa umejaa mabuje mengi.
Aliepua ,hawakuwa na mbonga walimsubiri kaka huenda atarudi alete mboga lakin. Masaa yalizidi kusonga hadi saa nne,
Mudrick ilibidi achukue ugali na chumvi walikula ,japo ugali ulikuwa hujaiva basi walikula hivyo hivyo wakanywa na maji.
Walilala baada ya kusubiri kaka hakutokea.
Usiku huo huo ndipo juma,kelvin na daniel walikutana maeneo ya kinyerezi mahali anakokaa juma,
Kelvin aliwaambia " piki piki mlio nipa kazi niibe ndio hii hapa kwahio pesa yangu nataka.juma alicheka "
Ha ha ha we kelvin kweli kiboko ehe imekuaje huko hadi ukaichukua ,basi kelvin aliwaelezea kila kitu na kuwaambia
Yule dogo niliona analeta ubabe nikampitishia msumeno shingoni sasa sijui kadedi au mzima,juma alitikisa kichwa na kusema safi sana kama amekufa haina shida aana shida yangu nilikuwa naitake ile nyumba.
Juma aliwaambia ,hii piki piki ni yangu,nilinunua kwa pesa yangu ,nikampa mkataba adinani ,kwakuwa mmeiba na mimi ndio nimewatuma mfanye hivyo ,mie nawapa laki saba saba kila mtu ,halafu hii piki piki nitauza kwa watu wengine au mnasemaje .
Kelvin na daniel waliitikia sawa hamna shida mkuu tunakusikiliza wewe,juma alitulia kidogo kisha akawaambia "kama itatokea huyo adinani akapona basi nitamfungulia kesi kapoteza piki piki yangu ,najua hana pesa hivyo hawezi kulipa lazima atoke kwenye ile nyumba.
Ha ha ha wote walicheka kisha daniel alimwambia juma " kweli wewe ni mtu wa faida yaani madili yako yanakuwaga na faida .
Basi waliagana usiku huo kila mtu alirudi kwake.
Asubuhi pana kucha,nusra na mudrick ambae ni wadogo walienda kijiweni huku wameongozana na shangazi yao ambae ni kipofu ,walienda kuulizia kijiweni "walimkuta hasani dereva wa boda boda ,walimuuliza " kaka hasani ,umemwona kaka yetu leo? Maana jana hajarudi nyumbani naomba umpigie simu.
Hassani aliwaangalia wale watoto na kuwaambia nyie watoto na kipofu wenu hebu tokeni bana msinitie nuksi asubhi hii simu yangu haina vocha.
Mudrick alimwambia samahani kaka ,
Alimshika shangazi mkono kisha akamshika na mdogo wake waliongozana hadi kwa rafiki yake adinani amabe anaitwa mick.
Mudrick aliamini leo juma pili basi mick atakuwa nyumbani.
Kweli walifika maeneo anakokaa micki walimkuta nje ya nyumba yao akisikiliza mziki kwenye simu.mick alivyowaona
Aliita aaah,nakuona mudrick mnaenda wapi asubuhi hii?,mudrick aliuliza ,kaka hajaja nyumbani toka jana,vipi alilala kwako?.
Kabla mick hajajibu chochote ,,nusra alishika tumbo lake na kusema shangazi tumbo laniuma.
Tumbo lilianza kumuuma nusra maana jana walikula ugali ambao haujaiva tena walikula na chumvi.aaaaah tumbooo nusra alizidi kulalamika.
Mick alisema ngoja nimpigie simu yake ,kweli mudrick alipiga simu,simu iliita haikupokelewa.alijiuliza "inamana atakuwa wapi?
Akapiga tena mara sauti ya kike ilisikika ikisema
" halloo
Za asubuhi dada mick alisalimia.
Safi samahani kama wewe ndugu ama unamjua kijana mwenye hii simu tunakuomba ufike mbezi beachi hospitali ya masana ,huyu kijana ameletwa jana akiwa hoi hadi sasa hajazinduka.
Mick aliuliza amefanyeje?
Pale pale simu ilikatwa,
Mudrick aliuliza kaka yupo wapi?
Mick kabla hajamjibu alimwangalia nusra ambae amechuchumaa chini huku amekamata tumbo lake kwa mikono miwili akilalala linamuuma sana halafu kapata taarifa rafiki yake yupo hospitali na hajazinduka.
Je nini kitaendelea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: