SIMULIZI: NAITAFUTA FURAHA YANGU 06
Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
______SEHEMU YA 6____
TULIPO ISHIA JANA,Mick alisema ngoja nimpigie simu yake ,kweli mudrick alipiga simu,simu iliita haikupokelewa.alijiuliza "inamana atakuwa wapi?
Akapiga tena mara sauti ya kike ilisikika ikisema
" halloo
Za asubuhi dada mick alisalimia.
Safi samahani kama wewe ndugu ama unamjua kijana mwenye hii simu tunakuomba ufike mbezi beachi hospitali ya masana ,huyu kijana ameletwa jana akiwa hoi hadi sasa hajazinduka.
Mick aliuliza amefanyeje?
Pale pale simu ilikatwa,
Mudrick aliuliza kaka yupo wapi?
Mick kabla hajamjibu alimwangalia nusra ambae amechuchumaa chini huku amekamata tumbo lake kwa mikono miwili akilalala linamuuma sana.
Mick alikuwa rafiki wa karibu mno na adinani ,hivyo anaumia kuona watoto wadogo wakiranda randa mitaani. ,kwa kumkosa kaka yao,kwa akina mick maisha sio mabaya sana ni ya kawaida.mick alifungua geti na kuwakaribisha ndani watoto pamoja na shangazi yao ambae ni kipofu.
Aliwaingiza ndani ndipo mick alimkuta mama yake akimwagilia ua ambalo lipo karibu na mlangoni.
Mama mick alisimama na kuuliza ,huu msafara wa watoto asubuhi kuna usalama hapo?.
Mick alimwambia "mama najua nakupa kazj nzito sana ,rafiki yangu adinani yupo mbezi hospitali nimeambiwa kalazwa toka jana na hajazinduka ,huezi amin hawa watoto na shangazi yao wamelala peke yao ,asaiv unavyowaona ndio walikuwa wanamtafuta kaka yao.
Mama aliwaangalia watoto ndipo akamwona ,nusra akishika tumbo,mama mick aliuliza ,huyu mtoto mdogo mbona kashika tumbo?,mick alishusha pumzi na kusema msaidie tu hamna namna hawa ni malaika hawajui chochote ,wazazi wao wangekuepo wala usingepata shida ila wewe waangalie ngoja nami niende mbezi nikaone adinani amekubwa na nini.
Basi mick aliwakabidhi watoto kwa mama yake ,kisha yeye alitoka na kuelekea mahali aliko ambiwa rafiki yake kalazwa,basi mama mick alimpeleka nusra moja kwa moja hadi uwani na kuwakaribisha ndani ,ndipo aliingia jikoni na kuwatengenezea chakula aliamini kabisa hawajala.
Alimpatia na nusra dawa za tumbo ,kisha akamkorogea na ngano,basi aliwapatia chai na chapati walianza kula ,huku mudrick akimpozea chai mdogo wake.vile vile anamshikisha shangazi yake chapati kisha anakula.
Mama mick aliwaangalia jinsi watoto wale wanavyoishi machozi yalimtoka ,inauma sana,asikuambie watoto kukosa malezi ya mama mzazi hakika wanateseka mno.
Mick alifika hospitali na kuulizia adinani yuko wapi ,ndipo kuna nesi mmoja alikuja akiwa ameshika simu ya adinani alimuuliza,wewe ni ndugu yake ,ama rafiki.
Mick alijibu mimi rafiki yake,ness aliuliza wazazi wake wapo wapi?,wazazi wake wote wamefariki hata mwaka hujaisha ,anaishi na shangazi yake,vile vile shangazi yake ni kipofu.
Nesi aliguna na kuuliza hana kaka zake wakubwa ama kaka zake.
" mick alimwangalia nes na kumjibu"ana wadogo zake yaani mmoja miaka mitano mwingine mitatu.
Nesi alichoka na kumwambia haya twende ukamwone.
Waliongozana hadi wodi ambayo adinani alikuwepo ile mlango unafunguliwa mick aliangalia upesi na kuona bandeji kubwa shingoni.mick aliingia na kukuta adinani akihema tu huku amefumba macho.
Aliuliza "inamana hajazinduka toka jana?,nesi alijibu ndio ila aliletwa na bajaji moja wamesema wamemwokota mtaroni amechinjwa na jambazi kisha akaporwa piki piki.
Mick aliuliza sasa tutafanyeje?
Mara dokta aliingia na kuwaomba watoke afanye vipimo kwa mgonjwa.
Mick alitoka nje kabisa na kuwaza ,kama adinani amelazwa hospital inamana pesa inahitajika ,na piki piki imeibiwa je adinani atakuwa na pesa ya kumkomboa hospitalin? Mick aliwaza ,siku hio alikaa hospitalin hadi jioni adinani alikuwa hajazinduka ndipo dokta alimwambia
Nenda nyumbank kesho uje na wadogo zake waje wakae nae hapa huenda fahamu zake zitarejea,basi mick hakuwa na kipingamiz alirudi nyumbani.
Aliwakuta mudrick ,nusra na shangazi yao wapo macho wanamsubiri,
Ile mick kurudi nyumbani " nusra aliuliza "mbona hujarudi na kaka yuko wapi?,mick kabla hajawajibu watoto alienda hadi jikon ndipo alimkuta mama yake akiosha vyombo alimwelezea kila kitu jinsi alivyokiona hospitali
Mungu wangu" inamana huyo mwizi alitaka kumua adinani kisa piki piki?
Ndio alitaka kumuua "mick alijibu.
Lakin mama dokta ameniambia niwapeleke wadogo zake hospitali huenda atarejewa na fahamu.
Mama mick alishusha pumzi na kusema sasa hii ni kazi nyingine,inabidi kesho usiende shule ,uwapeleke mimi nitaenda kukuombea ruhusa vike vile nitapitia hapo tabata shuleni nitawaombea ruhusa na hawa akina mudrick.ila usiwaambie kama anahali mbaya hawa wadogo zake.
Basi mick alirudi na kuwaambia " mudrick ,nusra na shangazi twendeni nikawaoneshe kitanda mlale leo hamtaenda kwenu kulala sababu adinani hayupo sawa ee.
Mudrick aliuliza "kaka yuko wapi?,
Mick alitabasamu na kusema ,kaka yupo kesho hamna kwenda shule inabidi niwapeleke mkamwone sawa ee
Watoto waliitikia sawa.basi walienda kulala.
Tukirudi kwa daniel ,mke wake amemfukuza ,basi alisubiri shangazi yao akina mudrick arudi ili aje amwingilie kimwili usiku lakin alikaa hadi saa sita hakuwaona ndipo alimpigia simu juma
"Hallo daniel" sauti ya juma ilisikika,
Juma yaani nyumba nahisi nishaiachiwa sasa hawa watoto na kipofu wao wameondoka sijui wamepotea hapa hapa dar ,ila sina uhakika ,sasa sinilikuambia ninampango wa kumfaidi huyu kipofu sasa hayupo mkuu.
Ha ha juma alicheka na kusema sasa ndio unatakiwa uishi kibabe mke. Ushafukuza lala tu.
Lakin juma ,kwenye chumba cha hawa watoto kuna flatscreen kubwa ya tv ambayo hawaitumii sijui niibe nikauze,maana wameacha chumba wakija kuniuliza nitawaambia mie mwenyewe sijalala hapa.
Juma alicheka na kusema hao watoto hawaweze kukuambia chochote ,kelvin si alikuambia kuwa yule kijana amepitisha msumeno shingoni,we unahisi huyo bado yuko hai.chukua kauze upate pesa ya kununua bangi.basi waliagana na kukata simu.
Daniel aliinuka na kusukuma mlango wa chumba anachokaa adinani alichukua ile tv kisha aliondoka zake na kwenda kuuza.
Basi siku inayofuata mick aliwapeleka watoto hospitalin ndipo mudrick alivyomwona kaka yake amelala huku bandeji kubwa imewekwa shingoni alilia huku akiita kaka ,basi nusra nae akiona mudrick analia nae aanalia ,walilia lakin mick aliwanyamazisha kisha akawaambia ,kaka amelala tu ataamka muda si mrefu.
Basi walinyamaza ,nusra alisogea kabisa karibu na kaka yake alimshika mkono alianza kuongea kwa hisia kali."kaka mbona umelala tu hauamki ona leo hatujaenda shule sababu wewe umelala huku kwa watu ,kaka nimemiss uniendeshe kwenye piki piki unipeleke shule.kaka. amka uone mudrick alivyoungua na moto alivyokuwa anapika ,kaka. Amka basi.
Kaka jana hatujalala nyumbani tumelala kwa mama yake mick,kaka nimejua kuhesabu vizuri ngoja nihesabu vidole vyako.
Nusra alianza kuhesabu vidole vya kaka yake ,1,2,3..hadi tano.
Jinsi nusra anavyohesabu na kushika vidole vyake.
Adinani taratibu alianza kutiririsha machozi ,adinani alitamani kuongea ila alikuwa hawezi alihisi maumivu makali shingon
Nusra aliinuka na kusema kaka sihesabu tena ,hutaki kuamka ile nusra anataka kuondoka ,adinani alimshika mkono,
Mick alishuhudia alivyoona vile alitoka upesi na kumwita dokta alimwambia mgonjwa ameamka amemshika mdogo wake mkono.kweli dokta aliwahi na kumkuta adinani ameshika mkono wa nusra huku machozi yanamtoka.
Nusr aliongea"sasa kaka wewe unanishika mkono unalia kimya kimya hutaki kuamka halafu unalala kwa watu siongei na wewe niache.masikin nusra anaongea hivyo pasina kujua kama kaka yake anahali mbaya kwakuwa ni mtoto.
Basi aliondoka na kumshika mkono mudrick na kumwambia ,mudrick kaka hataki kuamka ananishika tu mkono twende turudi nyumbani,
Mudrick alimkumbatia mdogo wake na kumwambia "kaka anaumwa ndio maana haongei basi mudrick alimfuta kaka yao machozi kisha wakatoka nje.
Dokta alifanya matibabu ,hadi jioni adinani alianza kuongea kwa mbal aliongea kwa shida maana shingo bado ilikuwa inauma.
Basi zilikatika siku tatu ndioo adinani aliweza kuongea kidogo kidogo huku shingoni ameshonwa nyuzi,adinani ilibidi akae hospitali hapo ili apate matibabu,aliendelea kutibiwa huku mudrick wakiendelea kukaa kwa akina mick .
Mick ikawa kila siku anawapeleka shule kisha nae anaenda shule.
Mwezi mzima ulikatika ,ndipo adinani aliruhusiwa kwenda nyumbani,mama mick alijitolea kumlipia pesa za matibabu sababu adinani hakuwa na mama wala baba.
Ile adinani anarejea nyumbani alipokelewa na wadogo zake kwa furaha ,alikuwa bado. Ana kidonda shingoni ila alikuwa anaongea vizuri, adinani aliwachukua wadogo zake ili warudi nyumbani,
Kweli walirudi walikuta chumba kipo na kigodoro kimoja, yaani magodoro mawili ,daniel ameuza ,tv ,kabati zote ameuza.
Adinani alivyoona vile vitu havipo alirudi sebuleni na kumkuta daniel alimuuliza " daniel wewe ni mpangaji kwenye hii nyumba ,ni nani ameiba tv,godoro na kabati ,au umevihifadhi wapi?
Daniel aliinuka na kumwagia maji adinani usoni "we kichaa nini kwahio mimi ni mlinzi wa hii nyumba?,ulivyoondoka vitu vyako ulimkabidhi nani we bwege nini halafu dogo usniniulize maswali ya ajabu nitakutia vibao sasa hivi.
Je nini kitaendelea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: