SIMULIZI: NAITAFUTA FURAHA YANGU 07
Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU
____SEHEMU YA 7_____
TULI
PO ISHIA JANA, Daniel aliinuka na kumwagia maji adinani usoni "we kichaa nini kwahio mimi ni mlinzi wa hii nyumba?,ulivyoondoka vitu vyako ulimkabidhi nani we bwege nini halafu dogo usiniulize maswali ya ajabu nitakutia vibao sasa hivi.
Danie aliongea na kuzima tv kisha akaondoka,adinani hakumkabidhi mtu yeyote vitu vyake ,alirudi ndani kwenye sanduku lake ,ambalo kahifadhi picha ya marehemu baba na mama ,aliangalia ile picha ambayo wamepiga wakiwa wawili ,akiwa ameiangalia mara mudrick aliingia ndani na kuuliza " kaka tunaenda kumsalimia mama mdogo joy tunarudi muda si mrefu,adinani alimwangalia mdogo wake ,kisha akamwambia sawa nenda mkamsalimie maana muda mrefu hajawaona ila mrudi haraka,
Mudrick alitoka na kumwacha adinani peke yake,
Aliishika tena ile picha kisha akaanza kuongea na ile picha "baba ,mama aliita!
Hebu oneni mateso haya ninayopitia ,mama ona shingoni nimenusurika kifo ,kwanini baba na mama hamtaki nami niwafuate ,maisha yanazidi kuwa magumu kadri siku zinavyojongea ,tv uliyonunua baba ona imeibiwa ,godoro limeibiwa nini kinaenda kutokea baba ,niambie
Adinani alilia sana ,alivyochoka aliirudisha ile picha kwenye begi lile akatoke nje.
Lakin ile anafika mlangoni alikutana na juma ,akiwa ameongozana na askari wawili.juma alimsalimia adinani ,habari za masiku kijana mbona hatuonani?
Adinani alikaa kimya alivyowaona polisi alishituka mno ,na kukumbuka siku polisi walikuja kutoa taarifa kuwa wazazi wake wamepata ajali ,leo tena polisi wamekuja wakiwa wameongozana na juma.
Adinani alijibu salama ,shikamooni ,maana walikuwa wamemzidi umri,
Juma alicheka kwa dharau ha ha ,kijana mwezi mzima hujaniletea pesa yangu ya piki piki ,tena umeondoka pasina kuaga ,hivyo nataka piki piki yangu.
Pale adinani alihisi duniani ana mkosi ,alimwambia ,juma inabidi tutafute muda tuongee maana yaliyonikuta nimakubwa ,ki ukweli,
Juma alitabasamu na kujisemea moyoni ,we mtoto huwezi kushindana nami
Juma alinyoosha mkono kuashiria anahitaji pesa za mwezi mzima ambazo adinani hajapeleka hesabu.adinani alijibu
" sina pesa unavyoniona jana ndo nimetoka hospitali"
Juma aliongea kwa nguvu "we adinani piki piki yangu iko wapi nauliza?,
Adinani ilibidi amshike mkono ili waongee pembeni amweleze kuwa ,piki piki imeibiwa ,lakin juma alikataa na kusema polisi kamateni huyu kapoteza piki piki yangu ataenda kujieleza kituoni.
Adinani alichukuliwa pasina kuwaaga wadogo zake na kupelekwa kituo kidogo cha tabata shuleni,,juma nae alienda kituoni ili akapewe piki piki yake,lakin juma huyu huyu ndie alimtuma kelvin akaibe hio piki piki kisha akamrudishia juma ,
Na tayari juma anayo na ameamua kumzunguka tena,basi turudi nyumbani mudrick ,nusra na shangazi ile wanarudi nyumbani ,hawamuoni kaka waliita lakin hawakumwona.
Ilibidi warudi tena kwa mama mick ,kweli walimkuta mama mick anafua,
Nusra aliuliza " mama mick ,kaka amerudi tena huku?maana nyumbani hayupo.mama alimwaga mapovu na kuwajibu "jamani nusra wangu hata hajaja ngoja nimpigie simu.
Mama mick alibonyeza simu na kuweka sikioni.
Wakati huo adinani alikuwa kituoni na alikuwa anakabizi simu ili awekwe sero asubiri kuhojiwa,kabla hajamkabidhi askari simu, ndipo simu iliita na kumwomba askari apokee cm walau dakika moja.
Haloo mama mick" adinani aliitikia
Upo wapi mbona nusra na mwenzake wanakutafuta?
Nipo kituo cha polis hapa tabata shule,adinani alijibu
Mama mick aliuliza kwa mshangao nini tena kimekusibu?
Sauti ilisikika ikisema"kata hio simu dakika moja imeisha na uingie sero,adinani hakuwa na pingamizi alikata simu na kukabidhi kwa askari ,alivua mkanda na kumkabidhi askari.
Mama mick alishusha pumzi na kuwaambia akina mudrick,inabidi mkae tena hapa nyumbani ,kaka yenu ametoka kidogo baadae nitaenda kumleta sawa ee.
Basi aliwapa akina nusra matoi ya kuchezea kisha shangazi yao alimpeleka sebuleni akakae ,aliwapikia alivyomaliza alienda kituoni ili kusikikiza ,nini kimemsibu adinani,
Alijiuliza maswali mengi pasina majibu.
Tukirudi kituo cha polisi adinani alianza kuhojiwa "piki piki umepeleka wapi?" Nimeibiwa piki piki na kujeruhiwa nimeripoti polisi kituo cha mtongani kunduchi mwezi ulio pita ,na walinipa ruhusa ya kwenda kutibiwa?
Juma alisema mimi sitaki kuelewa chochote askari hawa watoto wa siku hizi wajanja ,ukimpa mkataba wa piki piki anafanya miezi michache halafu anauza piki piki anakuja kukuambia nimeibiwa ,hio habari sitaki kusikia.
Adinani alijitetea ,anaomba apewe ruhusa ya kutoka kituo cha polisi na piki piki yake atamlipa kidogo kidogo,juma alimwangalia adinani na kumwambia hakuna cha kulipwa kidogo kidogo ,kwanza utanilipa nini huna kazi,huna wazazi ,ndugu wenyewe huna ,msaada niliokupa piki piki ujishikize uweze kuwalisha wadogo zako ,eti unaniambia piki piki umeibiwa ,haingii akilin nahitaji piki piki yangu ,huna piki piki lete hati ya nyumba ,ile nyumba yenu uiache.
Wakati mahojiano yanaendelea mama mick nae alikuwepo na alisikiliza ,alitamani amsaidie adinani ila hakuwa na pesa ,pesa alizokuwa nazo ndio alimlipia hospitali na nyingine kulipia ada ya mtoto wake mick.
Mama alimwangalia adinani na kumwambia "haina namna ,kama juma ambae tunamjua alikuwa rafiki mkubwa wa baba yako marehemu ndio anakudai piki piki kwa nguvu ,mwanangu usiumie sana ,tuweke mzamana wa hati ya nyumba kwa mwezi mmoja tusipo pata hio pesa ,
Basi hio nyumba utaichukua wewe ,na tukipata hizo pesa tutakulipa,
Juma alicheka na kusema,staki mwezi mmoja nawapa wiki moja ,mkikosa yaani akikosa hio pesa nyumba naichukua ,sina mjadala,.polisi walikubali makubaliano yao ,ndipo adinani alienda kuchukua hati ya nyumba na kuipeleka polisi ,ili ajiwekee mzamana ,kwa wiki moja asipo pata nyumba inakuwa ya juma.
Basi zilikatika siku mbili huku adinani hajui wapi pesa atapata,pesa ya kula anasaidiwa na mama mick ,adinani hakupenda kukaa hivi hivi aliamua kutoka na kutafuta kibarua ndipo alienda kuomba kufanya kazi kwenye banda la chipsi kwa mama amina.
Kibanda chao kilikuwa jirani na baa ya kb ambayo ipo maeneo ya tabata ,alianza kufanya kazi hapo akiwa analipwa elfu nne kwa siku moja,kwa adinani ilikuwa pesa kubwa ,alichojali ni kununua unga ili kuwapikia wadogo zake chakula.
Kwakua. Alikuwa anaenda kwenye banda la chipsi saa mbili basi alikuwa anaamka mapema na kuwapikia wadogo zake chakula ili wakirudi shule wapate chakula na kama watakuta kimepoa basi mudrick anawasha jiko kisha anakipasha kisha wanakula,alifanya kwa siku sita ndipo ilibaki siku moja ,ya saba kama adinani atakuwa hajapata pesa ,basi nyumba inakuwa ya juma.
Siku hio adinani alienda kazini akiwa anawaza ataipata wapi hio pesa ,ndipo mama mick alimpigia simu na kumwambia nimepata milion mbili ,nimekopeshwa na ndugu yangu ,hivyo tutawalipa na hio laki nusu iliyobaki tutawaomba siku tatu watuongezee ili tuitafute sawa ee adinani.
Adinani alijibu huku machozi yakimdondoka ,yaani anampa mzigo mama mick ,kukopa kwa ajili yake,adinani aliumia san ndipo aliendelea na kazi ya kumenya viazi vya chipsi.
Tukirudi kwa daniel walikutana na juma kisha walianza mazungumzo"umesema una uhakika ,adinani ataipata milion mbili na nusu?,juma aliwaza na kusema "ninawasi wasi aanaweza kuipata kwasababu ,yupo karibu na mama mmoja hivi anaitwa mama mick ,huyo mama anaweza kumpatia hio pesa ,tusipo tumia akili nyumba inaweza kurudi mikononi mwao.ni maneno aliyoongea juma,wakati huo daniel anasikiliza kwa makin.
Daniel aliwaza na kumshika bega juma " sikia ni kuambie ,huyu mtoto mdogo hawezi kuendesha akili zetu ,sasa sikia hawa wadogo zake ,nataka niwawekee sumu kwenye chakula ,maana naonaga adinani anapika asubuhi kisha anaweka kwenye hotpot halafu hivi vitoto vikirudi shule vinakula ,mi nataka niwawekee sumu hata wakifa potea mbali ,kwani tumeanza kuua leo ,.
Juma alicheka na kusema kweli daniel una akili hebu kafanye hivyo kabla hawajarudi ,daniel aliangalia simu yake na kukuta saa nne aliagana na juma kisha akaenda moja kwa moja hadi chumba cha adinani ,shangazi alikuwa hayupo siku hizi huwa anaenda kushinda kwa mama joy.
Daniel anaufunguo bandia,alifungua kisha akaingia aliangalia kwenye kameza kadogo aliona hot pot alifungua na kukuta wali ,daniel alitabasamu na kujisemea "watoto sasa inabidi muende aliko mama yenu na baba yenu ,alitia sumu kwenye chakula kisha alifunga mlango na kuondoka.
Siku hio mick alitoka shuleni mapema alipitia shule wanayo soma mudrick alikuta wameruhusiwa ,aliwachukua na kuwapeleka nyumbani kwao kisha aliwapatia chakula wakala ,walivyomaliza aliwaogesha na kuwaambia walale leo watashinda nyumbani hadi watakapo rudi jioni ,
Vile vile mick alienda kwa mama joy alimchukua shangazi ambae ni kipofu kisha akampeleka kwao ,nae alimpatia chakula na kumwambia " nimeota ndoto mbaya usiku hivyo leo msiende nyumbani,
Shangazi kwakuwa ni kipofu aliuliza ,ndoto gani umeota micki?,
Mick alishusha pumzi na kusema ,leo nimetoroka shule sababu ya hii ndoto,na mimi ninakawaida nikiota ndoto lazima itokee kweli sasa leo nataka kuizuia isitokee.
Jana nimeota kuna mtu kawateka ,akina mudrick walivyotoka shule kisha aliwapeleka kwenye jengo moja akawachinja.
Shangazi alicheka na kusema kweli ndoto yako yauongo bana,mick aliguna na kusema shangazi "sikia sasa saa nane usiku nikaota tena kuna mtu kawawekea sumu kwenye chakula ,sasa nusra na mudrick wakala hicho chakula wakafa hapo hapo.
Shangazi aliguna na kusema huenda ikawa kweli je huyo mtu kwenye mdoto ulivyoota sura yake unaijua?,
Mick aliikumbuka ile ndoto na kusema hapana ,alikuwa amefunika uso sijamfahamu.
Tukirudi mida ya saa nane mchana ndipo daniel alienda nyumbani akiamini wale watoto tayari ashawaua na sumu ,ile anafika alikuta mlango umefugwa ,ndipo alizunguka nyuma ya nyumba alikuta dirisha lipo wazi.daniel alichungulia kwenye meza ,alishangaa kuona nyau wawili wakubwa wamekufa hapo ,na ile hot pot ipo wazi bila shaka wamekula kile chakula chenye sumu kisha wakafa.
Danile aliogopa ndipo aliondoka eneo la nyumbani upesi wakati huo mick alienda mahali adinani anafanya kazi ya chipsi alienda kumsaidia .
Oi mick naona umerudi shule mapema leo,mick alicheka na kusema kweli nimerudi mapema nimewachukua akina mudrick na shangazi yao wapo kwetu.
Adinani alisema ni vizuri umewachukua maana leo juma mosi hapa wateja wanakuwaga wengi kwahio kurudi nyumbani saa nane usiku alafu nakuwa na hofu watalalaje wenyewe.
Mick alimwambia basi we fanya kazi zako fresh leo watalala kwetu ,halafu kesho utawachukua ,.
Adinani alimwambia fresh ndugu yangu mick ,umekuwa ukinisaidia vitu vingi sana.
Basi mick nae alishiriki kumsaidia kumenye viazi hapo huku wanapiga story za huko shule.
Mida ya saa tano usiku baa yaa kb ilijaa watu ,kwakuwa ni wiki end basi watu walilewa kweli.chipsi zilinunuliwa kwa wingi ,mishikaki ,kuku ,basi siku hio adinani alifanya kazi sana.
Lakin gafla kuna mdada alitoka kwenye hio baa akiwa anakimbizwa na vijana watatu ,mdada alikuwa akilia na kusema "kuanzia leo sipendi tena yaani hamis unanisaliti na malaya wa baa kwanini unidanganye mimi?
Yule dada alilia huku akigara gara chini yote sababu amekuta mpenzi wake yupo hio baa na mwanamke mwingine,
Wale vijana watatu ,mmoja alisikika akisema" oya yasin kamata huyu demu tumnyang'anye ufunguo wa gari halafu tuondoke nae maskani si unajua kalewa hajielewi halafu mpenzi wake hamtaki wala nini.
Yule dada alisogea karibu na banda la chipsi ndipo kijana mmoja alirusha chupa ya bia ili ampige huyo dada lakin adinani aliona akiruka na kuikinga ile chupa ya bia kwa bahati mbaya zilikuwa zimerushwa mbili nyingine ilimpata adinani maeno ya shingoni tena jeraha lilikuwa halijapona ambalo alikatwaga na msumeno.
Kijana mmoja mwenye rasta alitaka kukwapua mkoba aliokuwa nao huyo dada lakini adinani alijikaza kwa maumivu aliukamata mkoba na kuukumbatia
Lakin yule dada alipigwa teke la mgongoni na kudondoka chini ,kisha wale vijana wakamwambia we muuza chipsi unajifanya mwema unamsaidia huyu dada unamjua?
Adinani aliwaangalia na kuwaambia hata kama simjui nyie nawafahamu vizuri ni vibaka wa eneo Hili kila siku nawaona mnawapora wadada simu wakilewa sasa huyu dada leo hampati kitu.
Gafla wale vibaka walipiga kabati la chipsi puuuu likapasuka paaaaa ,mmoja akarusha kisu ili amchome adinani .
Gafla walinzi waeneo lile walifika ndipo wale vijana wakakimbia
Mdada akiwa amechoka hoi anahema akaangalia ni nani kamsaidai?
Je nini kitaendelea?
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: