SIMULIZI: NAITAFUTA FURAHA YANGU. 09




Story ;NAITAFUTA FURAHA YANGU


_________sehemu ya 9___
      Tulipo ishia jana,Mama amina,mama mick na watu waliokuwa eneo lile waliwaangalia wale wasichana ambao walionekana maisha yao ni mazuri ,zumra alimgusa adinani shingon na kuita kaka amka acha kulia.

Wakati huo suhaila alifungua buti ya gari waliokuja nayo ,kulikuwa na kabati  la chipsi kubwa na mpyaaaa ...
Suhali aliuliza jaman nani mmiliki wa hichi kibanda cha chipsi maana sisi ndio chanzo hadi kabati kuvunjwa ,huyu kijana anae lia ndio alitusaidia na kusababisha vibaka kuvunja kabati.

Adinani kusikia vile aliinua kichwa kuangalia ni akina nani hao,ile anainua kichwa tu alishangaa kuona mkono lain wa bibie zumra ameunyoosha kwake huku ameshikilia kitambaa kidogo.
Aliita kaka naomba upokee hichi kitambaa ufute machoz na uache kulia ,
Adinani alibaki ameshangaa aligusa jeraha la shingoni ambalo jana alitoneshwa na vibaka ila tayari aliweka dawa,ndipo nusra alikipokea kile kitembaa na kumfuta machozi kaka yake,nusra alisema "dada asante kwa niaba ya kaka yangu ,huyu kaka anamawazo mengi.

Adinani baada ya kufutwa machozi na mdogo wake aliinuka ,na kushangaa kabati kubwa limeshushwa chini,
Suhaila alimwambia adinani " kaka unanikumbuka?

Adinani alitikisa kichwa kuashiria ni kweli anamkumbuka"suhaila aliongea"tunaomba utusamehe umelia kwa ajili ya makosa yetu ,pia jana nilishidwa kukuambia asante jinsi ulivyotusaidia ,
Asante sana pia samahan kwa kuchelewa kuleta kabati la watu.
Adinani aliwashukuru na kuwaambia anawaombea dua kwa mungu maana yeye hana kitu chochote cha kuwalipa ,maana isinge kuwa wao leo hii angepelekwa polisi,adinani nae aliwashukuru pia.

Zumra alitembea huku akiuvuta mguu wake wa kulia maana uliteguka ,jana kisha akauliza "huyu mama analia nini?,alimnyoshea mkono mama mick.

Mudrick alidakia " ameporwa pesa na kibaka ,
Zumra aliinamisha kichwa kisha akaangalia mguu wake ulioteguka alimsogelea mama mick alimshika mkono na kumwambia "mama hata ukilia haisaidii kitu ,pesa zishaporwa ,pole sana ila naomba unyamaze halafu tusogee pembeni tuongee.

Adinani nae alimfuata mama amina na kumwambia" asante mama amina kwa kipindi chote nilichofanya kazi kwako ,pia kabati nimesaidiwa kulipiwa hivyo ,na kibarua naacha ili nikatafute sehemu nyingine.

Mama amina aliongea kwa jeuri" mwanaharamu wewe mitoto isiyokuwa na baba wala mama huwa inajeuri acha kazi tu kwanza kunawatu wengi wanalilia kazi ,nakuambia wewe adinani nakuchukia tena ondoka eneo hili upesi.

Adinani aliwashika mikono wadogo zake kisha alianza kutembea mdogo mdogo kuelekea nyumbani,wakati huo mama mick wamesimama pembeni ya gari na zumra kisha walikuwa wapo kwenye mazungumzo.

Umesema umeporwa pesa ,ilikuwa kiasi gani na ulikuwa waenda wapi na hizo pesa,mama mick alipangusa machozi yake na kitenge kisha akajibu"ilikuwa milion mbili na nusu tulikuwa tunaenda kituo cha polisi na yule kijana yule ambae kawashika watoto mikono 
Zumra aligeuka na kumtizama adinani kisha akauliza huko kituon mlikuwa mwaenda kulipa nini au hizo pesa zilikuwa zinaenda kutumika vipi.
Mama.alishusha pumzi na kumjibu zumra" aah yule kijana unae mwona anaenda nyumbani na wadogo zake alipoteza piki piki ya watu hivyo tunadaiwa ,hivyo ndo tulikuwa tunaenda kulipa.

Zumra alimtizama adinani hadi alivyopotelea kwenye upeo wa macho yake ,alivuta kumbu kumbu za nyuma ,alikumbuka "adinani alishawai kumbeba na piki piki ,kisha alimlipa laki moja,na alikuwa anaendesha vizuri anazingatia alama za bara barani.

Kisha akakumbuka jana alivyomwinua chini na alimpiga kibaka alivyochukua simu yake,akakumbuka alimsaidia rafiki yake suhaila ambae alitaka kuny'ang'anywa funguo ya  gari na vibaka.
Zumra alimaangalia mama mick ,na kumuuliza kwani huyu ni mtoto wako?.
Mama mick aliinuka na kumjibu si mtoto wangu ,ila kwasasa namlea kama mwanangu maana hana msaada kokote zaidi yangu .
Zumra aliendelea kuuliza " kwani huyu kijana hana wazazi?
Ndio hana wazazi ndio "
Zumra aliwaza kisha alimwomba mama mick apande kwenye gari waende wote kituoni ili waone kama wataweza kumsaidia adinani kulipa hilo deni.

Mama akili yake ilikuwa imechoka sana ,alipanda gari kisha walienda nyumbani na kumchukua adinani safari ya kuelekea kituoni.

Tukirudi upande wa pili ,kelvin baada ya kukwapua ile pesa kwa mama mick alimpigia simu juma "
Mkuu tayari pesa ipo mkononi hivyo nipo kwako ukitoka kituoni utanikuta nyumbani,wakati huo juma anapokea ile simu tayari alikuwa ashakaribia na kituo cha polisi

Ha ha ha alicheka kicheko kikubwa na kusema hapo babukubwa ,sasa namaliza mchezo ,fanya hivi ili huyu adinani ahame eneo hili akaishi mbali nasi na asiweze kugundua ni akina nani waliwaua wazazi wake.
Hivyo ngoja nikapokee hati ya nyumba.juma alikata simu.

Mama mick alienda hadi tawi la bank na zumra kisha zumra alitoa milion tano na kumkabidhi kisha alimwambia "mama kuwa makin nimejitolea kusaidia kulipa deni huyu kijana inaonekana anateseka sana,ila asije akaishi maisha kama aliyoishi rafiki hangu huyu suhaila unae mwona hapa anaendesha gari.
Nae hanaga wazazi kuna jambo zito lilimpitiaga.
Kila lakheri sijui unaitwa mama nani 

Mama mick alimtajia jina zumra kisha waliagana kisha wakaondoka,wakati huo adinani aliachwa kituoni na alikuwa ameshika bahasha yenye hati ya nyumba.hakujua kabisa kama zumra amejitolea kumlipia hilo deni,kwakuwa alijua dhahiri mama mick ameibiwa pesa kwa ajili yake hivyo aliamua ampe nyumba juma halafu ataangalia namna ya kuishi.

Mama mick aliingia kituoni akiwa ameshika mkoba ,alimkuta adinani amemsubiri ,wakati huo juma nae alikuwepo pamoja na mwenyekiti ambae alikuwa shahidi wao kwenye mkataba walio andikishana kwenye piki piki.

Juma alimtizama ,adinani na kuona amebeba bahasha juma alitabasamu na kujisemea moyoni" adinani kwisha habari yako sasa nyumba naimiliki kiulaini.

Askari aliwakaribisha ndipo , adinani alimwangalia mama mick ,adinani akiwa mnyonge alifungua bahasha ili atoe hati ya nyumba akabidhi tena juma akiwa anaona lakin.,mama mick alimshika adinani mkono kisha akamnong'oneza "adinani usitoe hio hati nimepata pesa hivyo namlipa.
Adinani alishangaa na kuuliza umepewa na nani?
Mama alimwambia adinani

Ni wale wadada walio tuleta hapa kituoni na gari,basi mama alitoa maburunguti ya pesa na kuwakabidhi polisi ilikuwa jumla milion tano.

Mama mick alianza kuongea " hii hapa milion tano ,tunalipa piki piki iliyopotea ,vile vile tunamlipa tena juma ,kuna deni alikuwa anamdai marehemu baba yake adinani milion mbili ambazo zimebaki na alikuwa amepangisha mpangaji.
Hivyo pesa yake tunamlipa leo na mpangaji aondoke leo leo pesa tushalipa.

Juma alishangaa alichokitegema kimeenda tofauti ,yeye alijua atapewa hati ya nyumba lakin amelipwa pesa za kununulia piki piki mpya hadi na deni pia akalipwa,

Juma alitoa macho akajikuta anaropoka haiwezekani haiwezekani mi nataka hati ya nyumba.alijisahau na kuongea hivyo ,ndipo adinani aliinuka na kumjibu juma "unasemaje unataka hati ya nyumba inamana pesa zako huzioni?,vile vile adinani alikumbuka maongezi ya juma na daniel alisema "yeye ndio amehusika kuwaua wazazi wake ,na daniel kuchoma duka.adinani alikasarika ila hana ushahidi wowote hivyo hawezi kuwashitaki .

Juma alitulia tuli ,alipokea zile pesa kisha akaambiwa huyo mpangaji aondoke leo leo. Juma alizidi kuchanganyikiwa waliruhusiwa kuondoka  kituoni 

Adinani aliweza kuikomboa nyumba tena na mpangaji daniel pia anatakiwa aondoke pesa ishalipwa.adinani wakiwa njiani na mama mick ,ndipo mama alimwelezea adinani pesa alizopewa na akina zumra ,adinani alitoa hadi machozi maana hao wasichana wamekuwa msaada wake mkubwa ambayo si rahisi kuulipa fadhila.

Basi upande wa pili juma ,alienda moja kwa moja hadi nyumbani ambako walikutana watatu ,juma,kelvin na daniel ,
Juma alimuuliza kelvin " nikweli umemwibia mama mick pesa ?
Kelvin aliuweka mkoba wa mamamick mezani na kusema "mie siongeagi naoneshaga vitendo mkoba huu hapa pesa hizo hapo.

Juma alifungua kweli alikuta pesa ,pia akawaambia imewezekana vipi huyu mama kamlipia adinani pesa zote tena hadi madeni ,na kasema daniel uhame leo leo ,pesa zangu nishalipwa .
Danile aliuliza kwa mshangao " unasemaje juma nihame?
We si ulisema unafanya mpango hio nyumba itakuwa yangu ,sasa imekuwaje nihame leo.

Juma alishusha pumzi kisha akawaza sana ,alimwambia daniel hama tu kwenye hio nyumba ,sasa inabidi hio familia tuue wote maana washatia nuksi ,
Nimesema huyo adinani tafuteni leo leo afe .

Je nini kitaendelea?


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: