SIMULIZI: RAHMA 13
.
Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher
👉NAMBA 13
Tunaendelea ......
Yule mtu aliyekanyaga begi alichomoa kisu akashika shingo la rahma alihitaji kumuangamiza rahma ili kufuta ushahidi pia walikuwa wanalihitaji sana lile begi alilokuwa nalo rahma yule mtu aliponyanyua kisu juu ili kumchoma rahma, Rahma alipiga kelele kali kelele zile zilimfanya mbwa mmoja aliyekuwa ameshikwa na kiongozi wa hao majambazi kukata mnyororo na kukimbia sehemu aliyokuwepo rahma akiwa ameshikwa shingo.
Kabla mbwa hajafika rahma alichomwa kisu maeneo ya uti wa mgongo yule mbwa alifika na kuanza kupambana na yule mtu ( Jambazi ) rahma alisimama tena baada ya kuona mbwa anapambana na yule jambazi rahma alianza kukimbia na lile begi japo alikuwa anamaumivu makali sana. Hussein akiwa nyumbani alipatwa na wasiwasi Mkubwa mno akamfuata kaka yake:-
"" Kaka kwanini leo rahma kachelewa sana nina wasiwasi mkubwa sana.
"" Hata mimi sifahamu lakini sio kawaida yake kuchelewa hivi.
Hussein wasiwasi ulizidi katika moyo wake akashindwa kuvumilia akamwambia kaka yake waenda kumtafuta rahma kwani sio kawaida yake kuchelewa kiasi hicho .
Rahma alikimbia sana aliishiwa nguvu ikabidi akae chini ili apumzike, baada ya kukaa chini alihitaji kutoa kile kisu kilichokuwa mgongoni lakini hakuweza kukifikia kwa sababu kilikuwa mbali mkono wake ulikuwa haufiki akiwa katika maumivu makali ghafla yule mbwa alitokea akiwa ametabakaa damu mwili mzima. Yule mbwa akajilaza karibu na rahma , rahma alipomkagua yule mbwa aligundua kachomwa na kisu zaidi ya mara moja kwa sababu vidonda vilikuwa vinatoa damu nyingi, rahma aliingiwa na huruma akachana sharti lake la shule akamfunga yule mbwa wakati anamfunga aliona kovu katika mguu wa yule mbwa ndipo alipogundua kuwa yule mbwa ni mbwa wake aliyekuwa anaishi naye nyumbani kule kijijini kwao rahma alilia sana.
Yule mbwa kutokana na kutokwa na damu nyingi alipoteza maisha mikononi kwa rahma , rahma aliumia sana akatafuta majani akamfunika yule mbwa alafu akaendelea na safari kurudi nyumbani kwako. Alitembea kwa muda mrefu alipokaribia nyumbani kwao aliishiwa nguvu kabisa akawa anajivuta kwa kutumia mikono ili afike nyumbani alifanya hivyo hadi alipofika nyumbani alianza kuita kwa sauti ya uchungu :-
"" Baba nisaidie baba yangu nakufa , baba Mkubwa , mama Mkubwa nisadieni nakufa , Martin kaka yangu nisaidie nakufa mimi Ewe mollah wangu nisaidie kama siku yangu imefika nichukue kwa kunipinguzia maumivu nateseka sana mollah wangu *
Rahma baada ya kukosa msaada wowote alijivuta akaingia ndani , alipofika ndani aliweka lile begi ufunguni ( chini ya kitanda ) kisha akahitaji apande juu ya kitanda ili alale ghafla alidondoka chini akapoteza fahamu papo hapo. Baada ya dakika kumi (10) Hussein, baba na mama Martin pamoja na Martin walirudi nyumbani, Hussein akiwa ana mawazo sana kwani walikuwa wameenda kumtafuta rahma lakini hawakumpata. Hussein aliingia ndani ili ajipumzishe alistajabu sana kumkuta rahma ndani na akiwa na kisu mgongoni pia amelala chini Hussein alianza kulia huku akimwita rahma, mama martin alistuka kusikia Hussein akilia akaingia ndani baba martin alimwambia Hussein wampeleke rahma hospital haraka .
Haraka haraka usiku huo huo walimkimbiza hospital walipofika madaktari waliomba karatasi kutoka police , Hussein akambeba rahma haraka haraka akaenda kituo cha police akarudi tena hospital. Daktari alipopata lile karatasi alianza kutoa huduma, Wakati huduma zinaendelea Hussein na wenzake waliambiwa wasubiri nje. Baada ya muda daktari alimaliza kazi yake akatoka nje akawambia wasubiri kwanza mtoto apate fahamu. Baada ya dakika ishirini kupita rahma alipata fahamu, daktari alikwenda kuangalia hali yake kisha akatoka nje akawaita ofisini kwake :-
"" Mtoto yule ni wa nani ?
"" Yule ni mtoto wangu vipi hali yake nimeona amepata fahamu daktari vipi atapona haraka nataka nirudi nae nyumbani sitaki mwanangu akae mbali na mimi .
"" Taratibu usiwe na haraka kiasi hicho, mtoto wako hajambo kwa sasa lakini nasikitika kusema Mtoto wako amepata #Stroke ( kupalalaizi ) kutokana na kile kisu kilimchoma sehemu mbaya sana kiligusa uti wa mgongo kwahiyo kuanzia kwenye kiuno kushuka chini hata kuwa anahisi chochote pole sana kijana lakini usikate tamaa kama ukimpeleka nje ya nchi anaweza kupata msaada zaidi.
"" Daktari unasema !!!! haiwezekani nasema haiwezekani ina maana mwanangu hatotembea tena haiwezekani daaah .
"" Usivunjike moyo kijana yote mipango ya mungu nendeni nyumbani saa hizi ni usiku sana kesho mtakuja kumuona mgonjwa pia jaribuni kutafuta pesa ili apelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi huenda mungu akamsaidia poleni sana.
Hussein alitoka katika chumba cha daktari akiwa na mawazo akaenda hadi sehemu aliyokuwa amelazwa rahma, Hussein alifika akakaa katika kitanda alichokuwa amelala rahma akiwa anatoa machozi rahma alimuuliza :-
"" Mbona unalia baba yangu Mimi nitapona baba yangu mungu atanisaidia .
"" Hapana Mtoto wangu nalia kwa sababu nakuona umeumia lakini usijali utapona sawa mama yangu.
"" Sawa baba yangu umekula ?
"" Hapana nilikuwa nakusubiri wewe si unajua siwezi kula bila wewe Mtoto wangu kipenzi usijali lala mwanangu ili upone haraka sawa eeeh.
Hussein alilala hapo hapo, asubuh na mapema Hussein aliamka na alihitaji kwenda nyumbani kwa ajili ya kuandaa chakula cha rahma mlangoni aligongana na mdada mmoja aliyekuwa anaingia ndani alafu yeye anatoka nje , Hussein aliomba msamaha akaokota
vitu vya huyo dada vilivyodondoka Hussein alimpomtazama huyo Dada ili ampatie vitu vyake alimuona ni fatuma. Hussein alipogundua ni fatuma alimshika mkono akaenda nae mbali kidogo na hospital akamwambia :-
"" Samahani kwa kilichotokea pale hospital naomba nikuambie ukweli leo hii.
"" Ukweli gani kwanza Kwanini siku ile ulinikimbia na hapo hospital ndipo ninapofanyia kazi niambie huo ukweli Hussein ?
"" Fatuma naomba nisamehe sana nilikuwa natafuta hii nafasi muda mrefu sana naomba unisamehe mimi ndio niliyekufanyia ule unyama siku ile usiku kijijini bitale nihukumu utakavyo hata kuniua itakuwa vyema zaidi kwa sababu hapa natamani nife tu kwa yanayonikuta nimeona ni bora nikwambie ukweli mapema kabla sijafa nisamehe sana sana sana.
"" Nini !!!? unasemaje kwahiyo wewe ndio uliyenibaka ? haiwezekani siwezi kukubali.
Hasira zilimtawala fatuma ghafla furaha ilitoweka fatuma akamsukuma Hussein alafu ......
___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: