SIMULIZI: RAHMA 12






Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

👉NAMBA 12

Tunaendelea ......

  "" Hii cheni umeipata wapi ""

Rahma alimshangaa Hussein kwa kubadirika ghafla rahma alisema:-

"" Alinipa marehemu mama lakini wakati anafariki aliniambia yeye sio mama yangu mzazi sikumuelewa kwa sababu kila mwanakijiji huko kijijini kwetu walisema  yeye ndiye mama yangu mzazi na hata Mimi najua marehemu mama yangu ndio mama yangu mzazi labda kwakua hali ilivyozidi kuwa mbaya ndio maana alikuwa anasema  maneno ambayo alikuwa hajui anaongea nini rohoo iliniuma kusikia mama yangu anasema Mimi sio mtoto wake daah nimemkumbuka sana mama yangu 😭

"" Basi mama yangu , basi mtoto wangu mzuri mzuri usilie baba yako nipo hapa nisamehe kwa kukufanya ukumbuke maumivu nyamanza mtoto wangu. 

Hussein alijitahidi sana kumbembeleza rahma na kujiuliza moyoni mwake :-

     "" Mbona hii cheni inafanana sana na cheni niliyompatia fatuma kama zawadi au sio hii lakini zinafanana na Sabrina anasema mama yake ameshafariki mmmmh nahisi zitakuwa zimefanana tu kwa sababu fatuma yeye yupo hai  hajafa .

Hussein alijiuliza maswali mengi mno kichwani mwake lakini baada ya muda akayapuuzia akamchukua rahma wakaingia ndani. Siku iliyofuata rahma kama kawaida yake asubuhi na mapema aliamka na kujiandaa kwenda shule , Alifika shule mapema na baada ya masomo kilipofika kipindi cha mapumziko rahma alikwenda chini ya mti mmoja uliokuwepo hapo shuleni akawa anajisomea vitabu, Nyuma ya mti huo alisikia sauti ya mtu akilia rahma alisogea ili afahamu nani anayelia nyuma ya mti  huo. Alimkuta kijana mmoja akiwa analia sana rahma alistajabu akamsogelea akamuuliza :- 
  
"" Heeeeeeh unalia nini chini ya mti huo alafu upo peke yako ?

"" Kila shule ninayokwenda kusoma walimu na wanafunzi wananicheka kwa sababu ninakigugumizi, Mimi sisomi tena naachana na elimu.

"" Hapana usikate tamaa lazima usome ili kujenga msingi mzuri wa maisha yako wafanye hao wanaokucheka leo siku na waowalie waumie kama unavyoumia wewe.

"" Nitafanyaje ili na wao watoe machozi nikawapige sio ?

"" Hapana njia sahihi ni kusoma kwa bidii ukifanya vizuri katika masomo yako wote wanaokucheka watakuheshimu mno na wataumia kwanini uwashinde katika masomo.

"" Kweli sasa kuanzia leo nataka nifanye hivyo ahsante kwa ushauri wako jina langu Othuman naomba kuwa rafiki yako .

"" Jina langu Sabrinah karibu napenda sana marafiki wema. 

Othuman alifurahi kupata rafiki wa kwanza hapo shuleni, rafiki ambaye aliyemfariji na kumpa matumaini. Siku baada ya siku urafiki  wao ulikuwa kwa kiasi kikubwa sana na hata alama zao shuleni zilikuwa juu zaidi kwa sababu walikuwa wanashindana katika masomo ilifika hatua wote wanatoka namba moja darasani. Othuman na rahma (Sabrina ) walipata sifa nyingi sana hapo shuleni , Walimu na wanafunzi wote waliwapenda na kuwaheshimu sana watoto hao.

Rahma pamoja na kusoma sana lakini hakusahau ahadi aliyompatia baba yake wa hiari ( Hussein) alimuahidi atamtafutia mtaji, rahma baada ya kutoka shule alikwenda kufanya kazi za kusafisha vyombo ili kujipatia pesa ambazo anahitaji kumpa baba yake wa hiari ( Hussein). Siku moja rahma alikawia sana kurudi nyumbani hadi majira ya saa moja na nusu usiku alikuwa bado hajamaliza kazi ya kuosha vyombo. Baada ya muda kidogo rahma alimaliza kuosha vyombo akaanza safari ya kurudi nyumbani kwao baada ya safari ya muda mrefu kandokando ya barabara alimkuta mwanaume mmoja akiomba msaada rahma alisogea ili kutoa msaada kama ataweza.

Rahma alisogea karibu zaidi ghafla yule mwanaume akamshika mguu rahma alistuka mno akapiga kelele baada kuona ameshikwa mguu lakini yule mwanaume alisema :-

  " Usipige kelele binti yangu watakuja kukuangamiza na wewe nakuomba chukua hili begi alafu kimbia nalo ni bora waniue lakini wasipate mzigo huo kimbia binti yangu , kimbia mbali kimbiaaaaaaaaaaaaa .

Rahma akiwa bado amezubaa na kutojua afanye nini alisikia mlio wa kitu kikubwa ( Milio wa risasi ) lakini rahma hakujua kama ni mlio wa risasi isipokuwa ule mlio ulimtisha rahma akachukua lile begi akaanza kukimbia nalo, wakati anakimbia alisikia mlio mwingine  alipogeuka aliona watu watano wakimuua yule mwanaume aliyemwambia akimbie na begi , Baada ya kuona wale watu wamemuua yule mwanaume rahma alidondoka chini alipotaka kusimama ili akimbie lile begi lilikanyangwa na mguu yule mtu  aliyekanyaga begi alichomoa kisu aka..........

___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: