SIMULIZI: RAHMA 11



Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

         
👉NAMBA 11

Tunaendelea ......

  "" Hakuna cha lakini hapo sasa nasema hivi kwakua unampenda kuanzia muda sihitaji chochote toka kwako naomba mfuate si unampenda ?

"" Hapana mume wangu sio kwamba nampenda hivyo unavyofikiria wewe tafadhali naomba linda heshima yangu Mimi sio msichana wa aina hiyo nakupenda wewe mume wangu.

"" Vizuri sasa olewako nikusikie tena unamtaja huyo kijana umenielewa.

Suleyman baada ya kusema hayo alimwita Othuman akamwambia jiandae nikupeleke shule sasa hivi , Fatuma alihitaji kuondoka na mume wake lakini Othuman hakuhitaji kuondoka na mke wake alimwambia abaki nyumbani. Hussein akiwa bado yupo njiani amembeba rahma haraka haraka alimkimbiza hospital kwakua Hussein hakuwa na pesa yeyote alijitahidi kukimbia ili afike mapema hospital kwa sababu hela ya kupanda gari hakuwanayo.

Safari ilikuwa ndefu kiasi kikubwa lakini kwa uwezo wa mungu alifanikiwa kufika hospital kwa bahati njema alipokelewa vizuri pale hospitalini akaomba msaada kwani hakuwa na pesa yeyote daktari msaidizi alimuonea huruma mtoto aliyekuwa ameumia kiasi kikubwa, yule daktari alijitolea na kutoa huduma bure baada ya huduma Daktari alimshauri Hussein kuwa inatakiwa mtoto alazwe ili achunguzwe vizuri lakini Hussein alikataa kwa sababu pesa ya huduma zaidi hakuwa nayo, yule daktari alimuelewa akamruhusu waende nyumbani .

Suleyman alifika shule na mtoto wake Othuman akabahatika kupata nafasi katika shule hiyo , Suleyman alimshauri na kumsisitiza sana mtoto wake asome kwa bidii zote ili kujenga msingi bora wa maisha yake kisha wakarudi nyumbani. Hussein akiwa amembeba rahma mgongoni taratibu taratibu wakirudi nyumbani, wakiwa njiani rahma alisema :-

"" Nisamehe baba yangu nakutesa .

"" Unasemaje !!! Mimi si ndio baba yako kuanzia leo usitamke maneno hayo tena umenisikia sawa?

"" Sawa baba yangu nakupenda sana lakini baba wewe ni dini gani ?

"" Mimi muislam kwanini umeuliza hivyo  ?

"" Kwa sababu baba sijakuoa unasali siku hata moja juzi nilisikia rafiki zangu wanasema sisi wanadamu tunatakiwa tujiulize maswali manne ambayo ni :-

#Mimi__ni__nani ?

#Ninafanya__nini ?

#Tukifa__Tunakwenda__Wapi ?

#Na_Kwanini_wanadamu_tunakufa ?

Walisema ukijiuliza maswali hayo bila shaka lazima umuabudu mungu , lakini mimi sijui ni muislam au mkristo kwa sababu baba na mama walikuwa hawasali.

"" Wewe mwanangu jina lako nani baba yako nimesahau jina lako  hahahaha ?

"" Hahaha uyooo hata hunijui mtoto wako umeshazeeka baba yangu jina langu SABRINAH .

"" Woooh kumbe nilikupa  jina zuri mno binti yangu mpendwa bila shaka utakuwa muislam kama Mimi baba yako kuanzia kesho tunaanza kusali sawa ''

"" Sawa baba yangu ahsante sana nakupenda baba.

"" Sawa acha kuongea unaumwa nakupenda pia binti yangu mpendwa mungu akusaidie uwe na upeo nzuri na binti mwema kama hivyo  mwanangu.

Baada ya siku tatu rahma alifanya juhudi zote pale nyumbani kwao  hadi wakawa wanasali wote, rahma akaanza kujifunza Qur'an kwakua alijitambua yeye ni binti wa kiislamu ,  Siku baada ya siku rahma alizidi kuwa binti mwema mwenye upendo na hekima. Rahma alikuwa anakusanya watoto wenzake wa pale mtaani kwao alafu anawafundisha Qur'an pamoja na masomo ya kidunia alifanya ivo kila jioni baada ya kumaliza kazi za nyumbani kwao .

Siku moja rahma akiwa anamfundisha baba yake ( Hussein) Qur'an wakiwa wanacheka sana kwa sababu Hussein alikuwa na ulimi mzito sana wakati anatamka Qur'an, rahma alizidisha kicheko hadi akalala chini akisema tumbo linamuuma kwa kucheka sana , Hussein akiwa anashikashika tumbo la rahma kwa kumtania ghafla Hussein aliona cheni shingoni kwa raha akaishika ile cheni kisha akamuuliza rahma akiwa na mshangao mkali :-

   "" Hii cheni umeipata wapi ""

Rahma alimshangaa Hussein kwa kubadirika ghafla rahma ali.......

___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: