SIMULIZI: RAHMA 10




Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

         
👉NAMBA 10

Tunaendelea ......
   Hussein aligeuka na kukamata shingo ya fatuma akataka kumpiga ngumi lakini kabla ya kumpiga aligundua msichana huyo ni fatuma aliishiwa nguvu na kushusha mkono kisha akaanza kurudi nyuma akiwa na hofu na wasiwasi uliopitiliza , Fatuma alistajabu mno baada ya kumuona kijana aliyekuwa anapigana na mume wake akirudi nyuma na akimuogopa sana hali ile ilimfanya fatuma ajiulize maswali mengi zaidi kichwani mwake. Suleyman alisimama akashika mkono wa mke wake fatuma kisha akasema :-

"" Tuondoke mke wangu huyu si binadam kidogo aliuwe leo duu.

  Suleyman alimchukua mke wake akawa anampeleka kwenye gari lakini Fatuma aligoma akasema:-

"" Mume wangu huu sio ubinadamu lazima tumsaidie huyu mtoto huenda kaumia kwa ndani anahitajika  akafanyiwe vipimo vya X-RAY ili kulinda afya yake zaidi tafadhali mume wangu msaidie huyo mtoto hana hatia wewe ndio umemgonga.

Suleyman alikubali ombi la mke wake alisogea sehemu alipokuwa rahma lakini kabla hajafika Hussein alijitokeza mbele yake kitendo kile kilimtisha suleyman akarudi nyuma. Hussein alimfuata rahma akamchukua na kuondoka Hussein alipiga hatua chache akageuka akamwangalia sana Fatuma kwa muda kiasi kisha akasema :-

""" Umekuwa mkubwa FATUMA .

Fatuma alistajabu sana baada ya kusikia Hussein anataja jina lake , fatuma alimtazama hussein kwa makini sana kisha akasema:-

"" Wewe ni nani na umelijuaje jina langu ?

"" Mimi ni kijana ninae kufahamu sana na ninakufahau kuliko unavyojifahau wewe nimekutafuta muda mrefu lakini sikufanikiwa kukupa leo hii namshukuru mungu nimekuona natumia nafasi hii kusema #NISAMEHE sana kwa mabaya makubwa niliyokufanyia .

"" Sijakuelewa umenikosea nini na sura yako kwangu kama naifahau lakini sikumbuki nilikuona wapi , Hebu nambie ukweli ili nielewe .

"" Umebadirika fatuma kwa sasa umependeza sana hakika kweli niliyokuwa nawaza kichwani mwangu kipindi nilipokuwa nakuona kijijini #Bitale yapo sawa. Unajua nilitabili siku moja utakuwa mrembo na mzuri kama ninavyokuona leo hii. Kitu kimoja naomba unisamehe mno pia ukweli bado nitaendelea kukueleza kwamba nilikupenda na hadi leo hii bado nakupenda sana japo nilikukosea sana nisamehe .

""" Daaah unanichanganya bado sijakufahamu nieleze wewe ni nani ?

"" Sikia muuza MATUNDA ukikubali nikuoe nitakununulia shamba kubwa lenye miti ya matunda mingi alafu wewe utaitwa "MAMA wa MATUNDA"

Hussein baada ya msemo huo aliondoka  na kumuacha fatuma njia panda. Fatuma alifikiria sana maneno ya mwisho aliyozungumza yule kijana baada ya muda kidogo ghafla Fatuma aligundua kuwa yule ni HUSSEIN mteja wake mkubwa wa matunda kipindi akiwa kijijini anauza matunda, Hussein alikuwa anatumia maneno hayo kila siku alipompelekea matunda, fatuma baada ya kupata kumbukumbu hizo alijikuta kasema kwa sauti ya juu :-

  #HUSSENIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII ..

Wakati huo Hussein hakuwepo tena maeneo yale  Fatuma alichanganyikiwa alijikuta akianza kumtafuta Hussein huku akimwita . Suleyman alizidi kutuwaa kwa hali aliyonayo mke wake baada ya kuzungumza na yule kijana , Suleyman alimfuata fatuma akamshika mkono na kurudi kwenye gari Wakati huo fatuma alikuwa anasema Hussein , Hussein. Suleyman alikasirika sana akasema 

  """" Nani Hussein hapaaaaaa ! 

Sauti ile ya ukali ilirudisha akili ya Fatuma na kumuangalia mume wake alimuona anaingia kwenye gari akiwa amechukia sana Fatuma akamfuata Suleyman wakarudi nyumbani badala kwenda shule. Walipofika nyumbani Suleyman alikuwa anahasira sana akamuuliza mke wake :-

"" Naomba niambie ukweli yule kijana uliyekuwa unamwita Hussein sijui ni nani ?

"" Alikuwa mteja wangu wa matunda kule kijijini hakuna kingine mume wangu tafadhali punguza hasira.

"" Fatuma usinigeuze mimi mtoto kumbuka Mimi si mtoto sawa nieleze ukweliiiiiiiii kabla sijafanya ninachotaka kufanya fatuma ?

"" Basi mume wangu acha tu nikueleze ukweli Hussein ni kijana wa kwanza kupendwa na moyo wangu na nilimpenda sana japo alikuwa anasifa mbaya, alikuwa muhuni , mkorofi na mvuta bange lakini moyo wangu ulimpenda sana sikumweleza hisia zangu juu yake kwa sababu nilihisi ataniona Mimi muhuni lakin sikufanya chochote na yeye hadi leo hajui kama nilikuwa nampenda ni hivyo tu mume wangu .

"" Et eee sawa na kule kuchanganyikiwa na kutaja jina lake Mara kwa Mara ulikuwa unamanisha nini bado unampenda sio ?

"" Ni kweli lakini ....

"" Hakuna cha lakini hapo sasa nasema hivi kwakua unampenda kuanzia muda ........... 

___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.




  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: