SIMULIZI: RAHMA 09





Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

👉NAMBA 09

Tunaendelea ......

"" Umembaka naniii ???

"" Daaah kaka nilimbaka binti mmoja huko kijijini nilikokimbilia kwa jina anaitwa #Fatuma, Nakumbuka  siku ile nilikuwa na rafiki zangu majira ya saa mbili usiku tulikuwa tumekunywa sana pombe na tabia yetu ilikuwa mbaya huko kijiji tulikuwa tukishalewa basi tukikutana na binti au mama yeyote tunambaka. Sasa siku hiyo tulikutana na dada huyo tulimpiga kitu kichwani akaanguka chini kwa nilivyokuwa sikuweza kumchunguza nilimwingilia kimwili yule msichana bila huruma, baada ya kumaliza kutendo kile niliona damu nyingi sehemu zangu za siri ndipo nilipogundua yule msichana alikuwa ni bikra. Nilijilaumu sana kwa unyama huo ikabidi nimtazame usoni ooooh mungu sikuweza kuamini kama ni fatuma binti aliyekuwa rafiki yangu kipenzi na alikuwa ananiuzia matunda sana, wale rafiki zangu walitaka na wenyewe  kumbaka niliwazuia tukapigana bahati nzuri akatokea kijana mmoja hivi akiwa na mtoto tulipomuona tulijua ni askari tukakimbia nisamehe kaka yangu.

"" Nikusamehe nini mjinga wewe 😣   Hivi wewe hussein hiyo akili ya kijinga uliitoa wapiiii eeeh ? Na umepata faida gani kwa kuharibu maisha ya binti huyo , nini faida yake daaah hakika kwa kosa hilo toka kwangu sikuhitaji kabisa ondokaaaaa .

"" Nisamehe kaka yangu sirudii tena nitaenda wapi mimi kaka yangu  nimegundua kosa langu nitaenda kijijini huko kumtafuta ili nikamuombe msamaha yule msichana kaka yangu.

Hussein alimuomba sana msamaha kaka yake, Baba martin ilibidi amsamehe mdogo wake. Siku iliyofuata majira ya asubuhi rahma na martin walitoka ndani ili waende shule wakamuona hussein amekaa nje ya nyumba akiwa hana furaha. Rahma alipotaka kumsogelea Martin alimziwia akamwambia   """ Usimfuate baba mdogo hapendi watoto alafu mkorofi sana usimsogelee "" Rahma alifikiria kidogo kisha akamsogelea hussein alipomfikia alimsalimia alafu akamuliza  :-

"" Baba mbona una mawazo kiasi hicho unafikiri nini baba yangu ?

"" Mh nawaza maisha ni magumu sana na nimefanya makosa makubwa  katika hii dunia pia umri unazidi kwenda alafu sina hata mtoto najuta.

"" Hapana baba hutakiwi kukata tamaa mimi hapa nimeokotwa na baba martin na sina baba wa mama nichukue mimi niwe mtoto wako pia nitakutafutia pesa ufanye biashara sawa baba yangu eeeh ?

"" Hahahaha wewe mtoto unavituko sana nashukuru umenipa faraja kidogo kwa sababu sikutegemea kama nitafurahi kiasi hiki, sawa kuanzia leo unaweza kuniita baba lakini hizo pesa Hahahaha sijui utazitoa wapi kama Mimi nimezikosa na ni mwanaume na ni kijana Mkubwa sana hahaha aya nenda shule mwanangu .

Rahma na martin waliondoka kwenda shule , Rahma alipokuwa shule alisoma kwa bidii zote na bidii zake zilimfanya afanye vizuri katika masomo yake, Walimu wote pamoja na wanafunzi katika shule aliyokuwa anasomea walimpenda mno. Rahma aliongeza bidii zaidi akawa anawafundisha wanafunzi wa darasa la pili , tatu had la nne wakati yeye akiwa darasa la kwanza kutokana na uwezo huo mkubwa aliojaliwa na mungu mwalimu mkuu alimpandisha darasa toka la kwanza hadi darasa la tatu.

Ilikuwa furaha sana kwa rahma na wazazi wake lakini ilikuwa huzuni kwa martin yeye kuachwa darasa la kwanza .Rahma kila alipokuwa akifika nyumbani alikuwa anamfuata Hussein akiwa na daftar na kumuonesha haikuishia hapo rahma alikuwa hawezi kila bila kuwa karibu na hussein wakati huo anaimba na kucheza hali ile ilimfanya Hussein ampende sana rahma na katika maongezi yao rahma alisisitiza na kuahidi siku moja atamletea Hussein pesa za kuanzia biashara, Hussein alikuwa anacheka sana kila akisikia kauli hiyo.

Hussein alimwambia rahma awe analala nae chumbani kwake kwa sababu alikuwa anampenda sana rahma hakupinga alikubali , hussein alijisikia faraja sana kulala na rahma , upendo ulizidi mara dufu kila siku, ikafika hatua hussein alikuwa hali hadi rahma afike ili wale pamoja, Rahma kama kawaida yake akawa akitoka  shule anakwenda kufanya kazi hotelin  ili kutafauta pesa aliyomuahidi Hussein , alifanya kazi kila siku na kutokana na ujanja wa rahma alikuwa anapata shilingi 7000 (elfu saba) kila siku na pesa zote hizo alikuwa anahifadhi ndani .

Othuman mtoto wa fatuma alikuwa mkorofi sana, kutokana na ukorofi wake walimu waliwaita wazazi wake wakawambia wanataka kumfuta katika shule yao. Suleyman alimuomba sana mwalimu mkuu lakini haikusaidia kitu, Suleyman na fatuma walimchukua mtoto wao wakaondoka na gari lao wakarudi nyumbani, walipofika nyumbani Suleyman alikasirika sana alimtazama othuman  akamwambia :-

"" Unaona upuuzi wako umefanya ujinga umefukuzwa shule ndio umefurahi sasa eeeh ?

"" Sasa baba mimi nikijibu swali darasani mwalimu na wanafunzi wenzangu wananicheka kwakua ninakigugumizi nilishindwa kuvumilia nikampiga mwanafunzi mmoja ndio walimu wakataka kunichapa nikasema sichapwi Mimi.

"" Mke wangu umesikia maneno ya huyo mwanao mjinga ndio malezi unayompa hayo sio si ninakuuliza ?

"" Eeeh usinikaripie Mimi kosa la mwanao unataka kuniadhibu na Mimi, lakini maji yanafuata mkondo  mbona wewe ulikuwa unampiga mdogo wako juma alipokuwa anakucheka .

Suleyman akiwa anahasira akamwambia Othuman jiandae kesho tunakwenda shule nyingine. Asubuh na mapema fatuma akiwa na Suleyman na mtoto wao Othuman, waliondoka kwenda kwenye shule hiyo. Siku hiyo hussein alikuwa amemsindikiza rahma shuleni katika kona ya kuingia lango la shule rahma alikumbana na gari lililokuwa na mwendo mdogo  likamgonga akaanguka chini Suleyman alistuka baada ya kujua kamgonga mtoto alishuka ndani ya gari ili kwenda kumuangalia huyo mtoto aliposhuka chini Hussein alimvamia Suleyman na kuanza kumpiga. Fatuma alishuka kwenye gari baada ya kuona mume wake anapigwa aliposhuka alimvuta Hussein aliyekuwa juu ya Suleyman. Hussein aligeuka na kukamata shingo ya fatuma akataka kumpiga ngumi lakini kabla ya kumpiga aligundua msichana huyo ni fatuma aliishiwa nguvu na kushusha mkono kisha .....

___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.




  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: