SIMULIZI: RAHMA 08
Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher
👉NAMBA 08
Tunaendelea ......
fatuma alipotaka kuondoka mkononi kwa yule mtoto aliona kitu kilimshangaza sana akamfuata yule mtoto , akasogea karibu zaidi akiwa bado anaushangaa ule mkono kisha akasema :-
"" Yote kwa yote mkono wako unatoa damu hakikisha umepewa tiba ili kuepuka kupata tetenasi, Pia nisamehe kwa maneno niliyokutamkia sawa mtoto mzuri .
Rahma hakumjibu chochote alikuwa anamtazama tu kwa hasira. Fatuma alipo muona yule binti hamjibu kitu aliondoka , rahma alipomuona yule dada kaondoka aliangalia mkono wake kweli aliona mkono unavuja damu, Rahma hakujali hilo akamfuata martin wakaenda kununua vitu walivyoagizwa kisha wakarudi kwa baba yao, wakati wanarudi njiani rahma alikuwa anamawazo sana Martin akamuuliza :- ....
"" Vipi dada mbona hauna raha unaumwa , alafu jina lako nani ?
"" jina langu naitwa Sabrina nawaza mengi mno hivi Martin wewe hupendi au hutaki kusoma ?
"" Napenda kusoma lakini baba alisema hana pesa ya kunipeleka shule kwa sababu baba mdogo #Hussein alimuibia baba vitu vyake vyote akakimbia, Mwanzo kabla hajamuibia baba alikuwa anaishi nyumbani lakini baba mdogo alikuwa mkorofi , mwizi , mlevi na anavuta bangi nilisikia baba siku moja akimkataza kuvuta bangi.
"" Anhaa kumbe una baba yako mdogo sawa sasa Mimi leo nitaongea na baba ili atupeleke shule au unasemaje ?
"" Sawa lakini sijui kama baba atakubali suala hilo .
Rahma na martin walipofika kwa baba walimkuta baba anawasiwasi , Baba alipowaona aliwakumbatia kwa furaha akasema :
"" Nilikuwa na wasiwasi watoto wangu kwani nimewatafuta sana lakini sijawaona nikawa najiuliza kuna tatizo gani limewakuta watoto wangu siku nyingine nikiwatuma msikawie tena sawa .
"" Sawa baba lakini tunaomba utupeleke shule baba.
Baba alishangaa sana akamtazama rahma ( Sabrina ) kwa muda mrefu sana alafu akamwambia :-
""Binti yangu hata Mimi natamani sana nimpeleke shule kaka yako martin lakini nilishindwa kutokana na hali ya maisha niliyonayo, lakini usijali nikipata riziki nitawapeleka shule sawa mama yangu nawapenda sana watoto wangu.
Rahma alifurahi sana kusikia maneno ya baba, Baba alipomaliza kazi walirudi nyumbani. Baada ya wiki mbili kupita rahma alimsumbua baba sana kuhusu kusoma baba alisema bado hajapewa hela yake ya ufundi akipewa tu atawapeleka shule. Rahma alivumilia kwa muda mrefu mno alipomuona baba yake anasumbuliwa kupewa pesa yake , Rahma alifikiri sana ataendaje shule na ili aende shule inahitajika pesa.
Rahma aliwaza sana akapata wazo akaenda sokoni katika migahawa mbalimbali akawa anaomba kazi za kuosha vyombo, baadhi ya wauzaji hawakumpa kazi kwakua alikuwa mdogo lakini wengine walimpa kazi, Rahma akawa anaenda kila siku baada ya kumaliza kazi za nyumbani wazazi walijua anakwenda jirani hapo kucheza na wenzake hawakutambua kama anakwenda kuosha vyombo ili apate pesa ya kwenda shule. Rahma alipopata pesa kiasi kikubwa, Alimfuata mama kisha akamuuliza :-
"" Mama unapenda kufanya biashara ipi siku ukipata fedha ?
"" Mmmh mwanangu natamani sana kufanya biashara ya kuuza maandazi, Matunda na mboga za majani lakini sina pesa kwanini umeniuliza hivyo binti yangu ?
"" Subiri hapo hapo mama nakuja sasa hivi .
Rahma aliingia ndani na kumuacha mama akijiuliza maswali mengi, Muda mchache rahma akatoka na pesa zote akampa mama. Mama hakuamini akamuuliza katoa wapi pesa zile Rahma akamwambia mama kila kitu jinsi alivyopata pesa zile.
Machozi yalimtoka mama alishikwa na huruma sana akamwambia rahma :-
"" Leo iwe mwanzo na mwisho kufanya hivyo sawa kwa sababu mimi mama yako nipo hai pia baba yako yupo kwanini ujitese hivi .
Mama alimsema sana rahma lakini alimshukuru sana mungu kwa sababu alikuwa anatamani kufanya biashara ili asaidie familia yake lakini hakuwa na pesa lakini binti mdogo leo kafanikisha lengo lake. Rahma alimuomba sana mama kwamba anahitaji kwenda shule, mama alimuahidi atajitahidi atampeleka shule yeye na Martin, Baada ya miezi kadhaa kupita mungu alisaidia Rahma pamoja na martin walikwenda shule .
Jioni ya siku iliyofuata Rahma akiwa na familia yake walikuwa wanakula chakula cha usiku ghafla walimuona #Hussein amerudi akiwa amejawa na huzuni na machozi yakimtoka alipiga magoti akamuomba msamaha kaka yake ( Baba rahma) Baba martin hakuwa na tatizo kwakua ni mtu aliyejaliwa roho ya huruma alimpokea mdogo wake wakakaa chini wakati huo Hussein alikuwa bado ana mawazo mazito kaka yake alimuuliza :-
"" Tatizo nini tena mdogo wangu nimeshakusamehe wala usiwe na wasisi mdogo wangu.
"" Kaka najilaumu sana kaka yangu leo nimefanya ujinga Mkubwa sana maskini yule dada anisamehe mno daaah nisamehe mungu wangu .
"" Kwanini au umefanya nini ?
"" Kaka yangu nimebaka.
Baba Martin alisimama na kutoamini alichokisia baba martin alikasirika sana akamuiliza kwa hasira ;-
"" Umembaka naniii mjinga wewe ?
"" Daaah kaka nilimbaka binti mmoja huko kijijini anaitwa ......
___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: