SIMULIZI: RAHMA 07
Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher
👉NAMBA 07
Tunaendelea ......
Rahma alishika ile chini aliyokuwa ameivaa akamchoma kwenye jicho yule mwanaume aliyekuwa kamshika kwa lengo baya la kutaka kumbaka, Yule mwanaume alipiga kelele kutokana na maumivu aliyoyapata akamuachia Rahama , Rahma alipoona kaachiwa alitumia nafasi hiyo kutoka nje na kutokomea msituni pasipo kutambua anakwenda wapi.Yule mwanaume alipomuona rahma anakimbia alimfukuza kwa sababu alitambua rahma akikutana na wanakijiji atasema yote aliyotaka kumfanyia , Rahma akiwa anakimbia alihisi kuna mtu anamfuata nyuma alipogeuka alimuona yule mwanaume aliyetaka kumfanyia ubaya , Rahma aliongeza spidi zaidi lakini mwisho alichoka.
Rahma alipoanza kuchoka alijikwaa akadondoka chini , Rahma alipomuona yule baba anakaribia kufika alisimama akajificha kichakani akaifunga ile cheni yake mkononi. Yule baba alipofika maeneo Yale alipitiliza akaenda mbele zaidi, Rahma alipomuona yule baba kapitiliza alisimama akiwa anatembea taratibu taratibu kurudi alipotoka, Wakati anarudi akiwa amechoka ghafla alishikwa mkono alipogeuka kuangalia aliyemshika alistuka sana kumuona ni yule mwanaume, Rahma alipiga kelele sana yule mwanaume alimziba mdomo kisha akasogea nae mbele kidogo ambapo palikuwa na MTO . Kwakua walikuwa juu yule mwanaume alimtupa rahma katika mto huo, alafu akarudi kijiji kwao.
Rahma alidondokea katika MTO huo na MTO ule ulikuwa na maji yenye kina kirefu sana na yanayotembea, Maji ya MTO yalianza kumsukuma rahma, Rahma alijitahidi kupambana na maji wakati huo akisukumwa baada ya muda kidogo rahma aliona kipande cha gogo kikipita mbele yake alikikamata akawa amepata nafuu. Yale maji yalimpeleka mbali sana , Maji yalimsafirisha rahma hadi mwambao wa mto huo. Rahma alitoka nje ya maji akajivuta japo kwa tabu akafanikiwa kutoka nje ya mto huo, rahma alikuwa anatetemeka Kutokana na baridi kali rahma alijitahidi kusimama akatereza akajigonga kwenye mti akadondoka chini na kupoteza fahamu.
Baada ya muda mrefu kupita alikuja mvuvi mmoja akiwa ndani ya nyumba wake akiwa ametoka kuvua ndani ya mto huo. Yule mvuvi alipofika nje ya MTO wakati anavuta mtumbwi wake nje alishangaa sana kumuona mtoto akiwa amelala nje ya MTO akamsogelea alipojaribu kumwita hakuitika yule mvuvi alitazama mazingira yale yalivyo duuuuh ! Alikosa jibu isitoshe ilikuwa ni majira ya saa kumi alfajiri, yule mvuvi alifikiria sana ikabidi aseme :-
"""mwenye mtoto huyu yupo wapo"""
Yule mvuvi aliita sana alipoona kimya kimezidi alichukua uamuzi wa kuondoka na rahma. Alipofika nyumbani mke wake alistajabu kuona mume wake akiwa na mtoto amembeba pegani , Mke wake alimchukua yule mtoto akamwambia mtoto wake Martin alete mkeka , martin alileta mkeka akamlaza yule mtoto. Baba martin ( Mvuvi) alimueleza mke wake kila kitu kuhusu yule mtoto aliyemuokota. Mama Martin alisikitika sana na kumuonea huruma sana rahma (Mtoto) machozi yalimdondoka kwa huruma. Baba Martin alikwenda kumwita daktari lakini daktari aligoma kuja kwa sababu baba Martin alikuwa hana pesa .
Baba Martin alirudi nyumbani bahati nzuri alipofika nyumbani alimkuta Rahma ( mtoto) amepata fahamu alifurahi sana , Wakamuuliza mtoto ni kipi kilichomkuta , Rahma aliwasimulia walimuonea huruma sana Mama Martin akasema kuanzia leo huyu ndio baba yako , Mimi ni mama yako na huyu ni kaka yako, Rahma alifurahi na kuwashukuru .
Asubuhi palipokucha Martin na baba yake walikwenda kwenye kazi ya ujenzi mbali na uvuvi baba Martin alikuwa fundi mzuri wa nyumba, Rahma nae akahitaji kwenda walimziwia lakini hakukubali na yeye akaenda huko kwenye ujenzi.
Walipofika katika ujenzi Martin na rahma walikuwa wanamletea baba yao matofali, baada ya muda baba alimtuma Martin pamoja na Rahma sokoni wakanunue vitumbua. Walipofika sokono rahma alimuona mtoto wa kiume akiwa analia Rahma alimsogelea yule mtoto akawa anambembeleza ili aache kulia, yule mtoto baada ya muda aliacha kulia ghafla yule mtoto aliitwa :-
"" #OTHUMAN unafanya nini hapo hebu acha kucheza na watoto wa kimaskini watakuambukiza maradhi.
Alikuwa ni #Fatuma akimuita mtoto wake Othuman, Othuman alipomuona mama yake alimkimbilia. Rahma alichukia kusikia kauli ile akamsogelea yule mama mwenye mtoto ( Fatuma ) kisha akasema :-
""" Katika dunia hii hakuna aliyezaliwa masikini isipokuwa riziki yake haijamfikia tuu na maradhi hayakuubwa kwa masikini pekee, hata nyinyi matajiri yatawafikia , Mimi sina ugonjwa wowote je wewe unahisi upo salama ? Jaribu kujichunguza kwanza wewe alafu ndio unaweza kusema hivyo kwa mwingine .
Baada ya maneno hayo rahma aliondoka lakini moyoni hakuridhika alitembea hatua chache kisha akageuka akamwangalia Yule mama wa mtoto ( Fatuma ) kwa hasira sana kisha akasema :-
"" Kwa kauli yako hiyo ninaapa sitokuwa masikini kwa uwezo wa mungu japo mpangaji ni mungu nitamlilia sana yeye ili nitimize hiki nilichoapa leo.
Rahma aliendelea na safari yake, Fatuma alistajabu sana kuona mtoto mdogo kama yule lakini jasili, fatuma alipotaka kuondoka alimtazama sana rahma mkononi kwa yule mtoto aliona kitu kilimshangaza sana akamfuata yule mtoto kisha....
___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: